Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,026
- 20,511
KWA NINI CCM WANAENDELEA KUTAWALA WAKATI MADHAMBI YAO YANAJULIKANA?
Chama Cha Mapinduzi CCM kinaonekana kama kitaendelea kushika dola kwa miaka mingine mitano ili hali kikionekana kimeshapoteza mvuto kwa vijana wengi ambao ndio asilimia kubwa ya wananchi. Kuna sababu nyingi ambazo ndio msingi wa mafanikio ya chama hichi tawala na kuonekana miongoni mwa vyama vitatu vilivyoipatia nchi yake uhuru (TANU/ASP) na mpaka leo viko madarakani-pamoja na ANC Pamoja na ZANU-PF.
SABABU 10 ZA CCM KUENDELEA KUONGOZA TANZANIA.
• Daftari la kudumu la wapiga kura.
Leo CCM inashinda urais kwa asilimia 70% kwa sababu vijana wengi hawajajiandikisha kupiga kura, hata mimi sikujiandikisha. Hii inatokana na ukweli wengi wa vijana hao walikuwa na umri wa miaka pungufu ya 18 ili hali wengine Ilitokana na mwamko kidogo kwa vijana kipindi hicho. Suala la muamuko ni tofauti n asana ambapo kila kijana anatamani kujiandikisha ili afanye maamuzi. NDIO SABABU SERIKALI YA CCM HAITAKI KUSIKIA SUALA LA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU, Hata likiboreshwa itakuwa muda mfupi kabla ya uchaguzi kitu ambacho kitaleta vurugu kubwa ikiwa ni pamoja na umwagaji wa damu kupita kiasi, hakuna kijana atakayevumilia siku ya uchaguzi asikute jina lake kwenye daftari.
• UJINGA ULIOKITHIRI KWA BAADHI YA RAIA.
Mtaniwia radhi kwa kauli hii, lakini halina ubishi; Kama leo RAIS anapinga Rasimu ya Warioba iliyotumia zaidi ya 7Billion za walipa kodi kwa kuzunguka nchi nzima, RAIS anaikana hata elimu ya TAKWIMU na kuonyesha wale wanaosoma course kama BA Statistics, Bachelor of Statistics and Mathematics kwenye vyuo mbali mbali nchini-RAIS anasema mnapoteza muda kwani elimu hiyo haitambuliki nchini, wakati huo huo wahadhiri wetu wamekaa kimya bila kuongea chochote, Wajumbe wa bunge maalum la katiba bado wako Ukumbini wakiendelea kujadili kitu ambacho RAIS ameshatoa muongozo kama alivyotumwa na chama chake, Wanachi tunatabasam na kusema hotuba ilikuwa nzuri sana-NINA MASHAKA NA WATANZANIA. Kwa hali hii tutarajie kuongozwa miaka nenda rudi, na kuwa WATUMWA NDANI YA NCHI HURU YA TANZANIA. JULIUS MTATILO NA WENZAKO ONDOKENI DODOMA HAKUNA KATIBA MPYA HUKOOOOOOOO! MNAFANYA NINI??? POSHO TU MNAUZA UTU WAKATI MMESHAONA HAKUNA KATIBA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
• HONGO/KURUBUNIWA KWA MAKADA WA VYAMA VYA UPINZANI.
Hakuna asiyejua hali ya maisha kiuchumi kwa mtanzania ilivyo mbaya, nasema mbaya kwa kufanya simple analysis ya mwanafunzi wa 1yr MBA: Engineer graduate/ Accountant/ Quantity Surveyor na wengine wanaanzia mshahara wa NET: 700,000/= nyumba standard (Dar), 200,000/= kwa mwezi, Utilities 100,000/= kwa mwezi, Nauli 150,000/= kwa mwezi, Chakula 200,000/= kwa mwezi, Nguo/viatu/vidogovidogo 50,000/= kwa mwezi. Huyu mtu hasaidii wazazi, ndugu, hawezi jiendeleza kielimu n.k Ikitokea mtu kama huyu akaingia kwenye siasa na awe na mvuto kwa wananchi, endapo ataahidiwa 2,000,000/= tu kwa mwezi kuhujumu chama chake-atafanya hivyo, akielewa siku akidondoka kwenye siasa-mtaani kugumu! Sishangai kuwaona kina ZZK na wengine wakihujumu upinzani. Ujinga unakuja pale anayehujumu Upinzani anaonekana kimatendo na ushahidi kibao lakini wapambe watakwambia HAPANA YULE NI RAFIKI YAKE TU! WENGINE WATASEMA KWANI KUWA KARIBU NA RAIS NI VIBAYA? Nikiwauliza hao watu, x-boyfriend wa mkeo unaweza kumruhusu asafiri na mkeo? Ni ubinadamu tu unaweza??????? Au wewe mama/dada unaweza kumruhusu mmeo asafiri na x-girlfriend wake??????? Jibu ni moja hapana! Ni rahisi kumrubuni na kusaliti ndoa yako. Leo watu wanashabikia ziara za ZZK na KIKWETE kweli? Ukiwauliza watakwambia ni kikazi tu MY GOD hata hilo watanzania hawalioni????????
• WOGA
Watanzania tunasifika afrika kwa ukarimu, upendo, unyenyekevu na uvumilivu: Mimi nasema SIO KWELI watanzania hatuna sifa hizo hata kidogo. Watanzania ni WAOGA KUPINDUKIA. Ndio sababu hata kama ni mgeni wataongea nae kwa uoga, nje ya nchi waoga, kufanya maamuzi magumu ndani ya nchi yao hawawezi-ukiwauliza watakwambia-Hapa vita ikitoke MSALA. Wakisikia PUUUUUUU Tayari WANAZIMIA, Kwa hali hii ni lini utawaambia Upinzani wachukue nchi wakakuelewa????? Amka watanzania ubora wa maisha yako unaletwa na mfumo imara, mfumo imara unaletwa kwa kubadilisha serikali nzima.
NITAENDELEA KESHO!
Kwa hisani ya Inocent P. Bhivahagumye‎