You are missing the point. Wengi wa wanaoshabikia CCM wanafanya hivyo kwa sababu binafsi na si kwa sababu wanaamini jamii kwa ujumla wake itanufaika. Mimi naamini kuwa society is worse off
kwa kuwa na chama kimoja tu kinatawala miaka yote au tunapokuwa na mazingira ambayo asilimia zaidi ya 80 ya wabunge ni kutoka chama kimoja. Our political situation is unhealthy, working against us, and voters/society as whole (and not individual political parties, Mbowe, Slaa, Lipumba, Mbatia, Yericko etc.) is the ultimate loser. And the whole point of multiparty democracy is to enable society create the needed checks and balances. Nakubaliana na mleta mada kuwa kwa sasa huu uwiano haupo kwa sababu, pamoja na mambo mengine,ya ujinga (ignorance) wa wapiga kura. Wapiga kura hawajaweza kutumia sanduku la kura kama fimbo ya kuwachapa wanaofanya vibaya na kuhakikisha kuna uwiano bungeni kwa maslahi mapana ya jamii. Tumeendelea kuchagua wezi na mafisadi kwa kuwa tu wanatoka CCM. Hata kama upinzani ni dhaifu kama inavyodaiwa, ni muhimu kuhakikisha kuna uwiano. CCM pia ina mapungufu mengi tena ya kutisha na inaendelea kutawala kutokana na uoga wa wapiga kura na wananchi kwa ujumla. Watanzania wangekuwa na tabia ya kuuliza maswali magumu, CCM ingekuwa chama cha upinzani wakati huu. Mambo mengi ya hovyo yanafanywa na watawala na yanatuathiri moja kwa moja lakini tuko kimya. Tunasubiri Mbowe, Slaa, Mnyika, na Lipumba watusemee. Na hata wakisema, hatuwaungi mkono. They cannot do it themselves. Na hata kama CCM ingekuwa haina mapungufu yeyote, bado jamii ingeathirika mno kwa chama kimoja kutawala bunge na wagombea kuendelea kushinda chaguzi kwa asilimia 79 au 80. Kwa kifupi, mahali penye demokrasia ya kweli, chama kimoja kutawala miaka 50 is unheard-of.