Historia fupi
Kwa wasioijua historia ya Tanzania na Rwanda na Uganda na Sudani Kusini, Museveni, Kagame, Garang wamefunzwa Tanzania, na wote wakiwa pale UDSM wakati wa likizo zao walikuwa wakienda ama Farm 17 pale Nachingwea na hata kusonga front katika vile vita vya Frelimo na Mreno Msumbiji.Wakati wa vita vya Uganda Museveni alikuwa mkufunzi wa chuo cha Ushirika Moshi na ndiye aliye"engineer" kwa Prof Yusuf Lule kuwa Rais wa mpito baada ya Idd Amin, baadae Uganda wakaanza kutifuana wenyewe kwa wenyewe ikaanza hiyo Uganda Bush War. Kagame na Garang ni wahitimu pia wa Kansas Military Academy huko Marekani na Kagame amewapeleka pia huko watoto wake
Museveni na Kagame walipigana wote Bush War (1980-86) iliyomuondoa Obote Madarakani, pamoja na Kiiza Besigye ambaye alikuwa daktari binafsi wa Museveni wakajageukana kisiasa. Kagame baadae akawa Mkurugenzi wa Masuala ya Kiusalama katika Jeshi la Uganda. Mwishoni mwa miaka ya 80 choko choko kwa Habyarimana zikaanza Kagame akajitoa jeshi la Uganda akaunda jeshi lake akiwa na mentor wake Rwigamo ambaye baadae alikuja uawa na ndio kilichozidisha ukatili wa Kagame dhidi ya serikali ya Akazu. Yakaanza makubaliano ya mwanzoni mwa mwaka 90 yaliyoruhusu majeshi ya RPF kuwa na base ndogo Kigali na baadaye yale ya mwaka 1994 ya serikali ya umoja wa kitaifa. Hata kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Habyarimana alishaingiwa na hofu juu ya Museveni na Kagame, inadaiwa alikwenda kuomba ushauri kwa Mobutu ambaye pia alitakiwa kuhudhuria makubaliano hayo Arusha lakini akakacha dakika za mwisho. Hivyo Habyarimana akaanza safari ya kuja Arusha akiwa na ndege yake ya Falcon Dusault aliyopewa zawadi na rafiki yake kipenzi Francois Miterrand aliyekuwa rais wa Ufaransa. Rais wa Burundi Ntaryamira naye alikuja na ndege yake Arusha ambayo ilidaiwa kuwa na hitilafu na kupelekea kupanda ndege ya Habyarimana. Hata hivyo kigezo cha Ubovu wa ndege ndicho kilitumika kuwaweka hawa mabwana mpaka jioni na Museveni akashauri waondoke kwa pamoja ili kutovuruga protokali. Lakini jamaa wa RPF pamoja na washirika wao ilikuwa kama wanajua kitu kilichokuwa kinaendelea. Hatimaye Habyarimana akaondoka Arusha majira ya jioni kurudi nchini kwake kilichofuatia ni historia. Kagame akachukua nchi akampa Melchior Ndadaye baadaye akachukua yeye. Mwili wa Habyarimana alisafirishwa Zaire kwa ajili ya kufanyiwa utaratibu wa maziko ambao pia haukuzikwa kutokana na Mobutu kuzidiwa na Banyamulenge na kuuacha ukachomwa chini ya usimamizi wa Singa singa. Hata RPG zilizotumika kutungua ndege ya Habyarimana zina batch ya jeshi la Uganda jambo ambalo watu wanamhisi Kagame ndiye aliyehusika na mauaji yale pamoja na mshirika wake Museveni.Lakini kwa nyakati tofauti jambo hilo limekuwa likikanushwa vikali.
Wakati wa mauaji ya Habyarimana Kagame alikuwa kwenye uwanja wa vita na inadaiwa wakati tukio linatokea, alikuwa akiangalia mechi ya mpira wa miguu kwa sababu wakati huo kulikuwa na na mashindano ya mpira ya Afrika nchini Tunisia. Kabarebe ndiye aliyekuwa wa kwanza kumnong'oneza juu ya mpango kufanikiwa.Kayumba Nyamwasa na Rose Kabuye ndio walikuwa watekelezaji wakuu wa mpango huo na viongozi waandamizi kwa wakati huo.
Kwa ujumla hali ya siasa nchini Rwanda ilichochewa kwa kiasi kikubwa na kwanza Wakoloni kuwabagua Wa hutu, Wanasiasa kuweka visasi, na ile hali ya Watutsi kujiona na kujisikia wao ni bab kubwa dhidi ya wengine. Wale Interahamwe, FDLR na wauaji wengine walikimbilia kwa Mobutu na kufanya pango lao la kujificha wengine Tanzania na Afrika Kusini kama wakimbizi hali hiyo inamtia hasira Kagame na kumtuma kibaraka wake Nkunda na wengine kufanya choko choko Kongo DRC ili Rwanda iwe salama pamoja na yeye mwenyewe. Wengine wanadai kwamba ni akina Kagame walio "engineer" mauaji ya Laurent Kabila baada ya kukiuka makubaliano yao. Kimsingi hawa viongozi wetu wa Afrika Mashariki hawana tofauti na Ma mafia.
Nadharia za Kimafia katika siasa za Maziwa conspiracy theories and connecting the dots yourself
Tanzania kwa upande mwingine inalaumiwa katika kashfa ya uuzaji wa silaha kwa waasi. Ikumbukwe Tanzania ilikuwa ni kitovu cha ukombozi kusini mwa Afrika, silaha nyingi za wapiganaji anzia Msumbiji, Angola, Namibia na Afrika ya Kusini zilipita hapa na kusafirishwa kwa wahusika kwa njia ambazo Mwalimu Julius alikuwa akizijua na akina Brigedia Hashim Mbita. Baada ya Mandela kuachiwa na kuvunjika kwa Jamhuri ya Sovieti na Kuuawa kwa Nicolae Causescu na mkewe huko Romania, kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin,kuisha kwa vita baridi, mambo mengi yalibadilika na vita hivi vikawa vimesimama na baadhi ya wahusika kupata muafaka. Tanzania ilikuwa na kiasi kikubwa cha silaha ambacho sio chake na hakikaguliwi. Hapo ndipo wajanja walipopata mwanya wa kupiga hela. Na inadaiwa kulipuka kwa maghala ya Mbagala na Gongolamboto ilikuwa ni namna ya kupoteza ushahidi na inaelezwa kulikuwa na wakaguzi wa Zenji ambao waliombwa watoe ushirikiano yaishe lakini hawakutoa, na haikuwapo jinsi ingine zaidi ya hiyo. Ripoti za Tume zimepigwa kapuni kwa kigezo cha Usalama wa nchi.......Mambo ni mengi sana ukielezwa unaweza ukaogopa....Na wengi wanaweza wakadhani ni habari za kubashiri lakini ndio hali halisi...Kuna utata wa kifo cha Dr Omar Ali Juma na kwa nini Museveni hakuhudhuria na kumtuma Makamu wake Dr Specioza Kazibwe, na kwa nini Museveni alichelewa katika dhifa na kiti chake kukaliwa na Dr Omar Ali Juma na kuvuruga itifaki...matukio ambayo watu wanashindwa kuunganisha undani na kifo chake...Ujio wa Joseph Kabila wakati huo huo...na kadhalika. Nadharia hii bado haijakamilika "conspiracy theory" ila watu wanahisi vingenevyo ama foul play ama double agencies kwa baadhi ya maafisa wetu. Museveni alisepa siku hiyo hiyo hakukaa tena bongo na akapokea taarifa za msiba kwa mstuko mkubwa........
Turudi kwenye bifu la JK na PK.
Kitendo cha JK kusema mbele ya Ban Ki Moon na Nkosazana Dlamini Zuma na viongozi wengine wa Kiafrika jijini Addis kwamba jamaa akafanye mapatano na FDLR na Interahamwe ilikuwa kama tusi kwa Kagame na embarassment ni kama kauli hiyo haikuwa mahali pake na wakati haukuwa muafaka kwa JK kusema hivyo pengine kauli hiyo ingetolewa katika vikao vya ndani. Hali hii ndiyo imechochea uhasama mkubwa wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Tanzania ambao nadhani utamalizwa pia kidiplomasia. Tanzania na Rwanda zimeingiliana kwa kiasi kikubwa kwa makabila hivyo kitendo cha JK kutoa amri ya kuwafukuza watu ambao wana asili ya Rwanda ilikuwa pia kama hatua ya kulipizana kisasi wataalam wanaita " Ping -Pong diplomcy". Hali hii inaendelea na kumekuwa na kutokuaminiana.
Museveni ndiye mshirika mkubwa wa Kagame ambaye naye anatajwa kuwa mshirika mkubwa wa Salva Kiir na ndiye aliyehusika na mauaji ya Garang. Ikumbukwe Garang alikuwa na mazungumzo binafsi na Museveni mpaka Usiku wa manane na hali ya hewa haikuwa nzuri. Garang alipotaka kulala Museveni akagoma na akampatia Presidential Chopper ambayo iliripotiwa kuanguka na Garang kupoteza maisha .Inadaiwa kulikuwa kuna ugomvi wa baadhi ya maeneo mpakani mwa Uganda na Sudan yenye Utajiri wa mafuta na Garang akawa kichwa ngumu kuamua ama ni Uganda yenye kufaidika ama la kimsingi huu mgogoro utakuja ibuka tena, Garang kudaiwa kuwadhamini LRA kama proxy army ya kuidestabilise Uganda na kujimilikisha maeneo hayo tajiri ya mafuta yaliyopo mpakani mwa Uganda na Sudani Kusini, Wengine wanadai familia tajiri ya Kimarekani ya Zorros ilikuwa nyuma ya pazia, Waasi wa Kongo kupitisha bomu na kutega kwenye helikopta (haijulikani wametumwa na nani). Madai ambayo Museveni amekuwa akiyakanusha vikali. Ukiangalia mgogoro huu wa Sudani ya Kusini, Kiir amekuwa karibu na Museveni na nchi washirika EAC, mjane wa Garang amekuwa karibu na Machar Riek pamoja na Khartoum.
Hizi ndizo siasa za Afrika Mashariki Rwanda ina idadi kubwa ya mashushu wake ambao kwa asilimia kubwa wako serikalini . Kinachofanyika Dar kinajulikana Kigali wakati huo huo. Hicho ndicho kitu kilichomwumiza kichwa Ben Mkapa mpaka sasa JK. Kimsingi sioni umuhimu wa kutunishiana misuli na nchi ya Rwanda ambayo mwaweza kuidharau kwa udogo wake lakini ukakuta ina uwezo mkubwa wa kiintelijensia, Usalama na Uchumi pamoja na rasilimali watu ambayo inajua nini maana ya kujenga nchi yao. Hata hivyo, sidhani mpaka sasa ( labda wakati wa Mwalimu Julius) Tanzania ni nchi yenye/iliyokuwa intelijensia ya hali ya juu yenye kufuata mifumo ya Kikyuba na Kiisrael. Kwa kiasi kikubwa JK analaumiwa kwa kuvuruga hii mifumo kwa kigezo cha udini na kutozingatia ushauri wa wazee wakati alipoingia madarakani na haya ndio matokeo yake watu wana-temper naye kila kukicha. Mwalimu alikuwa sio mtu wa masikhara, pamoja na umaskini wetu hawa wajinga wajinga hawakuwa wakituchezea anzia kaburu wa Rhodesia, Namibia mpaka Mkaburu mwenyewe, Mmarekani alikuwa anaumiza kichwa ndio maana wakawa wanatumia kigezo cha taasisi zao za kifedha kutubana kiuchumi, lakini ile morali yetu hawakuwezana nayo walituogopa sana na walimwogopa sana Nyerere. Nyerere aliijenga Tanzania Nyerere aliifanya Afrika iheshimike. Hivyo mafahali wawili wakigombana zinazoumia ni nyasi vita ya Kagame na JK ni mateso kwa wana Rwanda na Wa Tanzania wasio na hatia. Tuombe Mungu warudi kwenye mapatano kwa sababu Wanyarwanda ni ndugu zetu na ni damu yetu kama waafrika.