Rwanda yamkataa Balozi wa Tanzania

Rwanda yamkataa Balozi wa Tanzania

Kilbark maelezo yako yamenigusa sana, naomba unisaidie zaidi, kwa kumbukumbu zako, imewahi kutokea huko nyuma kwa barozi wetu kukataliwa na nchi aliyokuwa appointed kwenda, na kama tayari, Je ilikuwa ni kwa sababu za kiusalama kama hizi za Kagame.

Naendelea kuamini kwamba serikali yetu imekuwa dhaifu sana chini ya uongozi wa huyu Jamaa.

Rwanda kumkataa balozi wa nchi jirani kwa sababu za kispy siyo dalili nzuri, kwani ni mara chache sana kumkataa balozi mteule kwa sababu za kispy hata kabla hajafika. Wangeweza kukaa naye na kumwangalia nyendo zake kwa makini na iwapo wangejidhihirishia kuwa kweli ni spy basi wangefikia kumwambia aondoke baada ya hapo.

Sababu pekee za maana ambazo wangeweza kutumia kumkataa kabla hajafika ni za kisiasa, kwa mfano iwapo wana ushahidi kuwa mtu huyo aliwahi kuwa na negative attitude dhidi ya Rwanda au viongozi wake, basi wangeweza kumtakaa kwa madai kuwa kutokana na msimamo wake hawataweza kufanya naye kazi kwa ufanisi.

Lakini kudai kuwa wana wasiwasi atakuwa ni spy, ni dalili za kutojiamini na pia ni manifestation ya sense of self-guilt kuwa mabalozi wao ni maspy huko waliko. Wametengeza mazingira mabaya kuwa mabaloazi wao nchi za nje kwani watachukuliwa na wenyeji wao vivyo hivyo, na kuanza kuangaliwa mienendo yao kwa makini sana, na possibly kuishi maisha restricted sana.
 
Zile siraha zote kwa sasa hakuna kiwanda hata kimoja kinacho unda, Uganda wana Ndege bora kabisa kutuzidi


uganda wana hii SU-30 kutoka Urusi,

Acheni kubeza. Wake M23 wamekula kipigo cha mbwa mwizi na Rwanda walikuwa nyuma yao kwa kila kitu. SU 30 kitu gani! Our air defence is impenetrable equipped with state of the art ant air missiles. Rwanda is a very small country geographically and that poses a huge disadvantage incase a war between the two countries erupt. Kukosoana tukosoane humu ndani but linapokuja suala la nchi nyingine kutuchezea? Tanzania forever.
 
Hahaahah jeshi lenyewe kula kulala wanashindwa hata kuuwa mbu wanaoneza homa ya dengu

Ewe mvivi wa kufikiri. Umeona kuuwa mbu wa dengu ndo kazi ya Jeshi? Jeshi letu kula kulala? Mipaka iko salama. Huyo Kagame na mama Banda hapo malawi wanajua uwezo wetu fika ndo maana wamekuwa wapole. Dont take the army for granted my friend. Waulize M23kilichowapata ndani ya muda mfupi ajabu. Kagame si alikuwa anawadaidia kila kitu? Mbona walichemsha wakaufyata. Wakati mwingine kuwa smatt kidogo katika ku-comment.
 
Rwanda kumkataa balozi wa nchi jirani kwa sababu za kispay siyo dalili nzuri, kwani ni mara chache sana kumkataa balozi mteule kwa sababu za kispay hata kabla hajafika. Wangeweza kukaa naye na kumwamngalia nyedo zake kwa makini na iwapo wangejidhihirisha kuwa ni spy basi wangefikia kumwambia aondoke baada ya hapo.

Sababu pekee za maana ambazo wangeweza kutumia kumkataa kabla hajafika ni za kisiasa, kwa mfano iwapo wana ushahidi kuwa mtu huyo aliwahi kuwa na negative attitude dhidi ya Rwanda au viongozi wake, basi wangeweza kumtakaa kwa madai kuwa kutokana na msimamo wake hawataweza kufanya naye kazi kwa ufanisi.

Lakini kudai kuwa wana wasiwasi atakauwa ni spy, ni dalili za kutojiamini na pia ni manifestation ya sense of self-guilt kuwa mabalozi wao ni maspya huko waliko. Wametengeza mazingira mabaya kuwa mabaloazi wao nchi za nje kwani watachukuliwa na wenyeji wao vivyo hivyo, na kuanza kuangaliwa mienendo yao kwa makini sana, na possibly kuwa kuishi maisha restricted sana.

Kichuguu habari za masiku.

Hawa Rwandans wasitusumbue sisi. Tuna matatizo muhimu ya kuona Watanzania wanaondokana na hali ngumu ya maisha. Tatizo tulilonalo sasa hivi ni kwa sababu ya kuwa na rais ambaye anandaa maisha yake baada ya kupoteza muda wa miaka kumi kuwakumbatia mafisadi. Laiti kama rais angekuwa makini ni kuwafukuzia mbali na kufunga balozi yao hapa na kuwarejesha watanzani wanaoishi Rwanda hatuna muda wa kupoteza na serikali ambayo inajulikana iliingia madarakani kwa njia za kikatili bila kufuata utaratibu unaoeleweka. Kagame na M7 are dangerous people period!
 
Acheni kubeza. Wake M23 wamekula kipigo cha mbwa mwizi na Rwanda walikuwa nyuma yao kwa kila kitu. SU 30 kitu gani! Our air defence is impenetrable equipped with state of the art ant air missiles. Rwanda is a very small country geographically and that poses a huge disadvantage incase a war between the two countries erupt. Kukosoana tukosoane humu ndani but linapokuja suala la nchi nyingine kutuchezea? Tanzania forever.

Samahani mkuu, utanishawishi vipi kutetea matendo ya viongozi wangu hasa wanapokorofishasha na viongozi wa mataifa mengine wakati viongozi hao hao wamekuwa na matendo yanayokinzana na ustawi wa taifa langu?
 
Samahani mkuu, utanishawishi vipi kutetea matendo ya viongozi wangu hasa wanapokorofishasha na viongozi wa mataifa mengine wakati viongozi hao hao wamekuwa na matendo yanayokinzana na ustawi wa taifa langu?

Ndugu yangu unajua huu mgogoro ulianza pale JK aliposhauri rwanda kuzungumza na waasi wale. Sasa Kagame ilimkera sana lakini hakuonesha hivo pale mkutanoni hadi aliporejea nyumbani na kutoa kauli za kudhalilisha kw rais wetu. Alisema "WHAT WAS SAID BY KIKWETE IS UTTER NONSENSE" miongoni mwa mengine. Sasa JK naye yalimkera lakini akayameza kiume vinginevyo kingewaka. Kuna makamanda flani wa ngazi ya juu jeshini walimshawash kumchapa jamaa but rais akachomoa. Wakati mwingine mtu anapoku-provoke wewe ukatumia busara tofauti na yeye alivotegemea huwa anapata aibu sana. Hapa JK anastahil credit . Sasa kw upande wa nyumbani iko wazi kwamba kuna madudu mengi yanayostahil kukemewa na kulaaniwa kw namna zote nanayofanywa na watendaji wetu akiwemo mr president mwenywe. But linapokujabsuala la taifa jingne kujaribu ku-undermine dignity yetu hapo ni lazima tushikamane. Ni sawa tu an kwa na baba ambaye ni mlezi mbaya lakini hayo yanakuwa ya nyumbani kwan siku ukimkuta anapambana na wanaotaka kumdhuru nadhani hutawasapot hao watu bali baba yako then mkirud home bifu linaendelea kama kawaida.
 
Sababu ya ugomvi huu siyo kama inavyo elezewa lko nyingine zaidi! hapa vita inatafutwa u shauli tu hauwezi kuleta yote haya.HATUTAKI VITA NA KAGAME.Silaha zilizoonyweshwa zote zakununua hakuna hata moja iliyoundwa Tanzania.
 
at last wamebana wameachia. Hii ni theory yangu ya jinsi gani Rwanda walikuwa na wasi wasi na huyo jamaa. There are two scenarios. Scenario ya Kwanza labda wana informant ndani ya serikali ya bongo. Theory ya pili, huyu jamaa hana digital foot print, a typical characteristic of an undercover spy ambaye yupo involved kwenye deep clandestine operations. Jaribu kuse arch information za huyu jamaa kabla ya wiki iliyopitwa he is no where to be found. Ina maana hata Email hatumiii. Hii sio usual. Jamaa naona hofu ikawaingia kuona kwamba wanaletewa an agent who is a ghost lol. Ila naona wamenyosha mikono juu baada ya kuona italeta mfarakano zaidi ha ha ha
 
at last wamebana wameachia. Hii ni theory yangu ya jinsi gani Rwanda walikuwa na wasi wasi na huyo jamaa. There are two scenarios. Scenario ya Kwanza labda wana informant ndani ya serikali ya bongo. Theory ya pili, huyu jamaa hana digital foot print, a typical characteristic of an undercover spy ambaye yupo involved kwenye deep clandestine operations. Jaribu kuse arch information za huyu jamaa kabla ya wiki iliyopitwa he is no where to be found. Ina maana hata Email hatumiii. Hii sio usual. Jamaa naona hofu ikawaingia kuona kwamba wanaletewa an agent who is a ghost lol. Ila naona wamenyosha mikono juu baada ya kuona italeta mfarakano zaidi ha ha ha

Nimependa analysis yako,undercover spy ni threat kwa nchi yeyote bwana.
 
Sina kumbukumbu halisi Sangarara, isipokuwa matukio ya kutokuaminiana yalikuwa makubwa sana wakati wa vita baridi,masuala ya kidiplomasia, hali ya usalama na itikadi ya nchi. Tanzania iliwahi kuvunja uhusiano na Nigeria miaka ya 60 kwa msimamo wake wa kuiunga mkono jamhuri iliyojitenga ya Biafra, Tanzania ilivunja uhusiano na Israel kutokana na msimamo wake dhidi ya uonevu na ukatili dhidi ya Wa-Palestina, kwa Afrika tulikuwa na mahusiano ya kusua sua na Hastings Kamuzu Banda na Mobutu Seseseko kutokana na ukibaraka wao wa kuukumbatia ubeberu. Tanzania ilikuwa haifungani na upande wowote lakini kwa kiasi kikubwa itikadi yake ilikuwa sanjari na ile ya Kisovieti.

Viongozi wenye kaliba ya Nyerere ni wachache na adimu kuwapata Afrika, waliobaki wamekuwa wajinga wajinga na vibaraka wa mabeberu na mataifa tajiri. Afrika haina mwenyewe, Afrika sio huru tena, hata hao wanaopishana PK na JK ni vibaraka wakubwa na wanatumika kwa namna moja ama nyingine katika migogoro hii. Sikumzungumzia Victor Bout kwa sababu ya muda juu ya kuhusika kwake kwa mgogoro wa maziwa makuu, na namna vyombo vya magharibi vinavyomchora "depict" kama mhusika mkuu wakati sio kweli. Kwa ujumla mataifa ya magharibi yameshiriki kwa kiasi kikubwa katika mgogoro huu wa maziwa makuu. Mathalan Mataifa yanayozungumza kifaransa dhidi ya yale yanayozungumza kiingereza.
 
Rwanda imemkataa Balozi mteule wa Tanzania, Mussa Siwa, ambaye alitakia na serikali kwenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo.Taarifa kutoka Rwanda na duru za ndani ya serikali ya Tanzania zimeeleza serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi huyo kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiusalama.

Habari kutoka ndani ya Ikulu ya Rwanda zinaeleza kuwa serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi Siwa, baada ya kumshuku kuwa ni jasusi. Siwa kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa ofisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Tazania kwa sasa haina balozi nchini Rwanda tangu Dr.Marwa Matiko amalize muda wake wa kufanya kazi hiyo. Nafasi hiya kwa sasa inakaimiwa na Francis Mwaipaja,ambaye kabla ya kupelekwa Rwanda alikuwa msaidizi wa katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya Rwanda aliliambia MTANZANIA kuwa viongozi wa nchi hiyo wanachukuwa tahadhari dhidi ya wanadiplomasia wa Tanzania wanaofanya kazi nchini Rwanda , tangu nchi hizi mbili ziingie katika vita ya maneno mwaka jana.


‘’Viongozi hapa wamekuwa na hofu kubwa na Tanzania na kufanya wawe macho na watanzania wanaoishi hapa na hasa maofisa ubalozi na ndio maana wamemkataa balozi huyo mteule’’. Alisema mtoa taarifa wetu.

Wafuatiliaji wa maswala ya kidiplomasia wametafsiri kitendo hicho kuwa ni mwendelezo wa kutofautiana kati ya serikali za nchi hizi mbili.

Rwanda iliingia katika mgogoro na Tanzania baada ya kuchukizwa na ushauri uliotolewa na Raisi Jakaya Kikwete wa kuitaka serikali ya nchi hiyo kufanya mazungumzo na kundi la waasi la FDLR, ambalo limejichimbia ndani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais kikwete alitoa ushauri huo mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-Moon na Raisi wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, wakati wa mkutano wa viongozi wa ukanda wa maziwa makuu ya afrika uliofanyika mjini Addis Abab, Ethiopia, Mei, mwaka jana.

Ushauri huo ulipokelewa vibaya na Rais Kagame na waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo, Louise, Mushikiwabo, ambao walitoa kauli za kumdhalilisha Rais Kikwete.


Mkataba wa Vienna

Hata hivyo, Rwanda ina uhuru wa kisheria wa kumkataa balozi mteule wa kigeni kama inaona hafai kwenda kuishi nchini humo. Kifungu cha nne cha mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961 unaozungumzia masuala ya kidiplomasia baina ya mataifa,kinatoa uhuru wa nchi kumkubali balozi mteule wa kigeni. Mathalani Tanzania , mwaka jana ilimkataa balozi mteule wa Ujerumani, Margit Hellwig – Boette, ambaye alitakiwa kuja kuwa balozi hapa nchini mara baada ya kumaliza muda wake nchini Kenya.

Sefue asema hana taarifa

Akizungumzia suala hilo, Sefue alisema taarifa hizo hajazipata na kwamba wizara ya mambo ya nje ndiyo inayoweza kufahamu vizuri suala hilo. ‘’Mimi sifahamu chochote kwakweli, nadhani watu wa wizara ya mambo ya nje ndiyo wanajua process (taratibu) hizi ndiyo maana hata jina la huyo balozi aliyekataliwa silijui’’ alisema.

Wizara ya mambo ya nje washangaa

Nae mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mkumbwa Ally, alishangaa na kuhoji kuwa hizo taarifa tumezipata wapi kwani ni habari za ndani.

‘’Hizo taarifa mmezipata wapi, ni taarifa za ndani, chanzo chako cha habari ni nani’’,alihoji ally. Hata hivyo, alipoombwa kuzungumzia swali la msingi alisema suala hilo lipo nje ya uwezo wa wizara yake kwani Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteuwa na kutangaza jina la mteule huyo.

“Kiujumla sijapata taarifa za uhakika kuhusu suala hilo kwa sababu uteuzi wa balozi yeyote ni ‘process’ utaratibu’’ , hivyo hatuwezi kujua jina lake mpaka uteuzi wake ukamilike ndipo tutangaziwe na mwenye mamlaka hayo ni Rais, hivyo siwezi sema chochote ‘’
alisema.

MTANZANIA lilifanya jitihada za kumtafuta Siwa bila mafanikio kuzungumzia suala hilo.

Katika siku za hivi karibuni uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeonekana kusuasua na hata viongozi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakidaiwa kukwepana katika hafla mbalimbali zinazohusu nchi zao pamoja na zile za jumuiya ya Africa mashariki(EAC).

Wiki mbili zilizopita, Rais kagame alikacha kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na zanzibar zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marais wote wanachama wa ( EAC).

Mbali na Kagame kutokuhudhuria maadhimisho hayo, pia aliukacha mkutano wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, lakini alikwenda nchini Kenyana kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaounganishwa na mradi unaoitwa ‘ Northern Corridor Infrastructure Project’. Waziri Mkuu Pinda aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.


Source: Gurudumu la Habari

Chezea JK wewe
Balozi.jpg
 
Rwanda ni nchi ya hovyo sana,inastahili kupingwa na kila mtu popote pale,hovyo sana
 
Back
Top Bottom