bushman
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,412
- 747
chenge kichwa wewe acha kuwaza kima------
unazumgumzia andrew chenge au chenge mwingine???huyu kichwa wapi kaja na kodi ya simu imegonga mwamba!!!!!!!!! Kilaza tu huyu.
chenge kichwa wewe acha kuwaza kima------
let them go nothing to worry! Kuendelea kulialia na rwanda&uganda kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina bahari chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye gas na italipa tu acha watuondolee jams na usumbufu
Una mawazo finyu sana ya kuona mambo kwa mapana yake, kama Rwanda wa njia mbadala wa kuingiza mizigo yao hatuna jinsi la ni kufuata yale madai yao ya msingi katika kufanya nao biashara ama tutegemee kuathirika kibiashara wakienda bandari ya Mombasa.
Jamani naombeni msaada. Binafsi ninfahamu umuhimu wa bandari za Dar na Tanga. Kwa sababu hiyo zikipanuliwa nitaelewa. Sasa bandari ya Bagamoyo itakuwa ina-serve maeneo gani na umuhimu wake ni upi?
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
......................TUJIKUMBUSHE..................
![]()
Transport and Infrastructure Cabinet Secretary Michael Kamau, Kenya.
If the Tanzanians were not people that they are; Mombasa port would have died a long time ago. Fortunately, with their Ujamaa thinking, they are not able to develop things very fast, said Mr Kamau.
nijuavyo mimi ni importer (mmiliki wa mzigo) ndiye anaamua mzigo wake upitie bandari gani lakini hii haiondoi ukweli kuwa mlengo wa sera za nchi husika unachangia katika kuwashawishi wananchi wake waamua nini kuhusu mizigo yao. Na pia haina maana kuwa kama nchi iko strategical positioned au advantages zingine basi haina haja ya kufanya bidii kuvutia wateje kwa kuamini kuwa 'watakuja tu'.Kijoigraphia...nchi za EA zinaifanya iwe tegemezi kwa Tanzania....
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....
1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?
Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???
Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!
Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
![]()
Na Raymond Kaminyoge,
Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam, alisema Hanspope.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.
Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.
Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.
Kamati ya Bajeti
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.
Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi, alisema.
Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.
Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo, alisema.
Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.
Umoja wa nchi tatu
Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.
Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.
Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.
Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.
Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.
Mlishangilia kufukuzwa kwa wanyarwanda, ni sawa wanyarwanda walitakiwa kuondoka lakini si kuwashtukiza leo nchi ile inahangaika kuwahifadhio kwa kuwa hatuwaarifu mapema na wao wameamua kumwaga mboga come 1st september, hakuna mizigo kupita DARPORT.
- Bajeti ya mgimwa majanga,
- clearing and forwarding companies majanga ina maana itabidi kupunguza wafanya kazi
- wenye malori ya kusafirisha mafuta majanga no cargo to haul
- baadhi ya vitengo TRA vitapunguiza wafanyakazi
- Consumption ya fule nad lubricants kwa malori itashuka na hivyo kuathiri, sector ya nishati
- Kwa ujumla yako mengi haya yote ni kukosa uvumilivu ktk kuamua, kazi tunayo
Yaani sasa tutaitegemea zaidi Zambia labda na Burundi tu katika kuitumia bandari ya Dar es Salaam.
Malawi nao huitumia bandari hiyo lakini nadhani itafifia sana.
Ni mara kumi sisi tufunge mkanda kuliko kuwaandalia wajuku zetu M23. Kama DRC wangewafukuza miaka ile leo kusingekua ni kikundi kinachoitwa M23 kikidai kumegewa sehemu ya DRC. Kwanza siku zijazo tunategemea kuanza kusafirisha nikel tani milion tisa kwa mwaka kitu ambacho bandari ya Mombasa haiwezi kufikia.
Hapana sio JK! ni sisi wenyewe tumejifikisha hapa na ni sisi tutakaojikwamua kutoka hapa....
Mimi sidhani kama kagame anaweza kuwahakikishia urahisi wa biashara wafanya biashara wake kiivyo. Ni kwamba hapo mwanzo kilichowafanya wakawa wanatumia bandari ya Dsm ni kitu gani? Sasa wajidai wanajitoa, kiukweli hakuna mfanya biashara anaehitaji ucheleweshwahi wa bidhaa zake, kilichopo ni nchi yetu kuimarisha ufanisi bandarini.
Pili hao wakina Poppe ni waongo sana, ukiona mtu anakazania vitu kama mzani vitolewe ujue huyo ninmwizi, hayo jamaa wanazidisha kupita kiasi kiwango chao chakubeba mzigo. Hata wakati huu ambao kuna mizani nyingi wanazidisha vile vile. Hakuna mwizi anaetaka vituo vyapolisi viweke kila kona.
Nimesikia baadhi ya vyombo vya habari vikisema eti ni hujuma! Come on! Tumerogwa?![/QUOTE
nimeangalia news sasa hivi ntv kenyata yupo china...wamezungumzia usumbufu uliopo bandari ya dar...wanasema wao mziigo hautachukuwa siku tano kufika kigali toka ulipofika port msa