Tanzania na Uganda zasaini makubaliano kuimarisha ushirikiano wa kimkakati reli ya SGR

Tanzania na Uganda zasaini makubaliano kuimarisha ushirikiano wa kimkakati reli ya SGR

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
421
Reaction score
297
TANZANIA NA UGANDA ZASAINI MAKUBALIANO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI RELI YA SGR

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zimeendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kufuatia kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano (MoU) wakati wa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) uliotamatika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Machi, 2026.

MoU hiyo imesainia kusimika mwanzo wa mashirikiano katika maendeleo ya reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) itakayounganisha Isaka – Lusahunga – Murongo/Kikagati hadi Mpondwe. Mradi huo unatarajiwa kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na abiria kati ya nchi hizo mbili pamoja na kuongeza kasi ya biashara na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kupitia mradi huo wa reli ya SGR, Tanzania na Uganda zinatarajia kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Uganda na nchi jirani, hali itakayochochea ukuaji wa biashara ya kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

Aidha, Tanzania na Uganda zimefikia maazimio ya kuweka mikakati mipya ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo uchukuzi, biashara, uwekezaji na miundombinu.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya Tanzania na Uganda kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na wa kidugu uliopo kati ya nchi hizo mbili pamoja na kukuza maendeleo ya pamoja kwa manufaa ya wananchi wake.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa Serikali na maafisa waandamizi kutoka pande zote mbili.
 

Attachments

  • IMG-20260314-WA0012.jpg
    IMG-20260314-WA0012.jpg
    434.7 KB · Views: 15
  • IMG-20260314-WA0006.jpg
    IMG-20260314-WA0006.jpg
    393 KB · Views: 12
  • IMG-20260314-WA0011.jpg
    IMG-20260314-WA0011.jpg
    450.5 KB · Views: 14
  • IMG-20260314-WA0010.jpg
    IMG-20260314-WA0010.jpg
    395.7 KB · Views: 12
  • IMG-20260314-WA0008.jpg
    IMG-20260314-WA0008.jpg
    388.4 KB · Views: 14
Kuna jambo la muhimu umelisahau

Utafiti wa awali umebaini njia kadhaa zinazowezekana katika mradi huu

Kwa upande wa Tanzania, wapangaji wanazingatia njia za Isaka–Lusahunga–Murongo/Kikagati na Isaka–Nyakasanza–Omurushaka–Kakunyu/Nshongyezi, wakati nchini Uganda njia zilizopendekezwa ni pamoja na Kikagati–Mbarara–Bihanga–Kasese–Mpondwe na Kikagati/Nshongyezi–Ntungamo–Bihanga–Kasese–Kamango.


Mpondwe ni miongoni mwa vituo vya mpakani mwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vyenye shughuli nyingi zaidi. Kuunganisha ukanda huo na Reli ya Standard Gauge (SGR) ya Tanzania kunaweza kuhamishia kiasi kikubwa cha usafirishaji wa mizigo kuelekea Bandari ya Dar es Salaam, ambayo huhudumia zaidi ya tani milioni 18 za shehena kila mwaka kwa ajili ya masoko ya nchi za ndani zikiwemo Uganda, Rwanda, na Burundi.
 
Ndani Haijakamilika Tayari Mnahaha Kwenda Burundi, Uganda ♥️
Uhuni Mtupu
 
Tuliambiwa lot ya SGR Isaka-Rwanda,Leo tena Uganda nao wanaanzia Isaka.

Kwanini mmoja kati yao asiunganishie kwenye line ya mwenzie badala ya wote kuanzia Isaka?

Au Isaka-Rwanda ishaota mbawa?
 
Ndani Haijakamilika Tayari Mnahaha Kwenda Burundi, Uganda ♥️
Uhuni Mtupu
Ya Burundi contractor yuko kazini.

Mpaka Inbestors wameshaanza kwenda Burundi kuchimba NICKEL, kwasasa hauling ni rahisi.
 
Back
Top Bottom