Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Jamani nchi inanuka nilikuwa Blantyre wk iliyopita Nilitafuta gari ya kupakia mzigo kuleta dar walikataa katakata wanasema hajawahi kuona Trafic wengi barabarani namna hiyo na walarushwa wakubwa,anasema ukimyima pesa unalimwa fine, wao sasa wanaenda msumbiji na south africa, Tujiulize tumepotoka wapi?

Mpaka tutakapoanza kuwasifia wachapakazi badala ya wezi
 
Ulanguzi, uhujumu uchumi, ubadhilifu pamoja na kulimbikizia mali wa watu wachache UMETUPONZA malalamiko ya rwanda na uganda km hzo pesa zngekuwa znatumika km ilivyokusudiwa kwa maana kwenda kwenye mfuko wa serikali kamwe uchumi wetu ucngeyumba lkn nchi inabak kuwa masikin na watu wake wanazd kutajirika kwa kupitia lasilmal za nchi...bora wajitoe ieleweke moja
 
Wewe si ndio ulikuwa ukishabikia conflict ya rwanda na Tz,haukuangalia kitakachofuata mbele ilhali uganda na rwanda ni kitu kimoja.
Also tuitangaze bandari yetu kwa kupunguza gharama kama fast jet uone competition.

Mnachanganya mambo, someni vizuri mada. Uamuzi wa kupitisha mizigo Kenya si wa Serikali ni wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili. ambao hapa wanasemewa na mtanzania mfanyabiashara wa kusafirisha mafuta, ambaye anajaribukuibana serikali ihararishe uharamia kupitisha ktk barabara zetu magari yake yakiwa na uzito usioruhusiwa kisheria.

Wadanganyika kutokujua tunashabikia maharamia ambao miaka yote ndio wanapenyeza hela zao chafu kwa watendaji serikalini kuchelewesha mipango ya matumizi ya reli ktk usafirishaji mizigo mizito.

Hawahawapaswi kuchekewa!!!
 
Mkuu naona unajisumbua bure kumuelimisha huyo mtu. Sisi tunahitaji DRC kuliko hivyo vinchi vidogo, nadhani wakishajiondoa kuna haja ya kusaini mkataba wa makubaliano yaushilikiano na DRC kama USA alivyofanya kwa Saudia Arabia ili DRC watutegemee kwa kila kitu.

DRC na Burundi walimtuma Kenyata aende kuchokonoa/kufanya fitna, hili waweze kuwaunganisha kwenye mpango wa pipeline, sijajua wamefikia wapi.
 
Kikwete aliamua kuiua Mtwara Development Corridor ambayo ilijumuisha Msumbiji, Malawi na Zambia na kuwezesha pia Zimbabwe, DRC kutumia bandari ya Mtwara ili iongeze ufanisi wa Dar port kwa mizigo ya Rwanda, Uganda, Burundi na mizigo ya ndani.

Tumeshauri sana kupunguza utitiri wa road-blocks tukapuuzwa, Jerry Muro alionesha rushwa za polisi barabarani akatendwa.

Sasa Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Zambia wameanzisha corridor yao ili watumie bandari za Msumbiji. Sasa ni Mombasa corridor.

Je, tunaihitaji bado bandari ya matrilioni iliyozushwa Bagamoyo? Is there any economic viability to have this Wakwere port alongside Dar, Mtwara and Tanga ports? Au tuachane na elephant project ya Bagamoyo na tujikite kwenye kufufua reli zetu a kuziunganisha hadi mipakani na kununua vichwa na wagons za kutosha ili tuongeze speed ya cargo clearance at the ports?
 
kuna mambo ya ajabu sana kwenye nchi hii, ukiingiza mizigo kupitia bandari yetu dar, ukikwama kuutoa mzigo wako kwa sababu ya mlolongo wa ushughulikiwaji wa taratibu za documents wao wanakutoza gharama za kuhifadhi mizigo yako.
unaweza kukuta ofisa mwenye dhamana ya kuidhinisha mzigo utoke hayopo ofisini, gharama za kuhidhi mizigo yako zinakuangukia,

kuna wakati unalazimishwa ukahifadhi mizigo yako kwenye magodown yao kwa bei za ajabu kabisa.

chadema wameandamana weeeeeee, watoka bungeni mara kibao wakisema nooooooo!! naona sasa na mataifa jirani wameamua kutoka ndani ya bunge kuonyesha kutoridhishwa na upitishwaji muswada kibabe.
 
Watanzania hili ni fundisho,tuachane na fikra za kufikiria kila siku kuliibia Taifa.Unapo mpa tena nafasi ya uongozi Mtu kama Chenge bado ni mwendelezo wa fikra zile zile za kufikiria ni namna gani ya kupora raslimali za Taifa hili kwa ushirika wa Wageni.
 
Kidogo mimi nitatofautiana na wengi kati yenu...Tatizo la Rushwa na utendaji mbovu liko mda mrefu bandarini...Chanzo ni serikali corrupt.Hili ni tatizo ambalo lazima liwe adressed ili tuweze kwenda mbele...Lakini pia maamuzi ya wafanyabiashara wa rwanda na Uganda sio kwamba yamesukumwa na mgogoro wa nchi za Tanzania na Rwanda kama wachangiaji wengi wanavyodai bali ni utendaji mbovu wa taasisi hii ya bandari.Wafanyabiashara wanaangalia maslahi na sio ishu za migogoro inayokuzwa na vyombo vya habari.......Kwa maana hiyo endapo banadri ya Dar itakuwa vizuri hayo mambo ya migogoro sio kikwazo kwa businessmen given mipaka haijafungwa.

Lakini pia hata kama waganda na wanyarwanda wataacha kutumia bandari yetu...Na endapo tu tutakuwa efficient katika bandari yetu Population ya watanzania inatosha sana kupata pesa ya Kutosha bandarini....Tuondoe watendaji wabovu tu.

Tujenge viwanda,Tutoe ajira kwa watu wetu...Tuna population kubwa hivyo cost of labour itakuwa ndogo...Tuzalishe bidhaa at a relatively low cost compared to jirani zetu......Tuondoe Rushwa TRA na Uhamiaji.....Tujenge reli kuunganisha hadi kwenye mipaka yetu...tuache kutegemea barabara kwa usafirishaji.....Tufanye agressive advertisement ya utalii wetu....LET US BE AGRESSIVE katika kila kitu....Watanzania ufike wakati sasa tujiamini kwamba we are the best in the region...and we can do wonders katika Uchumi wetu na kuwa Giant of Africa........Lastly Tupate Uongozi bora wa kutuwezesha kuyafanya hayo hapo juu.
 
Mkuu hoja yako imekaa vizuri hasa kuhusu uimarishaji wa Reli ya kati.

Bila usafiri mathubuti wa reli tusitegemee ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam kuongezeka!

Kwa mfano treni moja inaweza kubeba hadi tani 1200 kwa wakati mmoja, ambao ni mzigo wa lori 30 zenye uwezo wa kubeba tani 40. Mzigo wa treni 5 tu kwa siku ni sawa na lori 150.

Bandari inaweza kuhudumia malori mengi kiasi hicho kwa siku? Na barabara zinaweza kuhimili malori mengi kiasi hicho kwa siku bila usumbufu kwa watumiaji wengine wa bara bara?

Wengi waliotoa maoni wanamantiki. Uzuri ni kwamba tunaendelea na jadi yetu ya kulalamika bila kuchukua hatua.Hatua muhimu kuliko zote ni kuimarisha reli zetu. Mambo ya mizani yatakwisha, maana inaonekana hata hizi barabara kila siku zinaharibika (ulaji huu) pamoja na kuwa na mizani nyingi. Je zikipunguzwa si ndio itakuwa balaa? Nahisi reli haziimarishwi ili hawa wenzetu waendelee kununua malori kwa malori na kujitajirisha. Hebu fikiria diesel ya TRC inasafirishwa kwa malori wakati shirika hilo hilo ndio linamiliki reli. BP sasa hivi Puma ilijenga kituo cha kupokelea mafuta kwa TAZARA kule Makambako kwa maana mafuta yote yanayokwenda mikoa ya kusini yapakiliwe pale, kimefanya kazi kwa muda mfupi na kilichotokea God knows.
 
loh tumekwisha......
sisi ni wapumbavu sana
 
Jamani naombeni msaada. Binafsi ninfahamu umuhimu wa bandari za Dar na Tanga. Kwa sababu hiyo zikipanuliwa nitaelewa. Sasa bandari ya Bagamoyo itakuwa ina-serve maeneo gani na umuhimu wake ni upi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kwa staili hii uchumi wetu utakuwa kweli!! Wadau hebu tulijadili kidogo hili.
 
Tumeyataka wenyewe, bandarini kuna urasimu wa kipumbavu sana, rushwa nje nje!
 
Waende tu tutabaki na SADC yetu hawawezi kuishi bila sisi hao bora waende ili ardhi yetu ipone na mabepari hawa Wakenya wote wanaojifanya kufundisha English medium warudi kwao haraka tunawajua wamejaa hapa Bongo wanataka kuolewa.
 
Tusirukeruke tutafute chanzo cha yote haya ni nini ??????halafu tutafute suluhu ya tatizo hilo sio badala ya kutafuta mikakati ya kujenga uchumi imara sisi tunahangaika tu kutengeneza mikakati ya kuiua CHADEMA kucha kuchwa,ngoja na zanzibar ijitenge kabisa labda tutajifunza.
 
wewe kweli ni krapu

hebu niambie unalinganishaje matumizi ya bandari ya watu wa rwanda na wilaya ya ilala au temeke??

if we lose DRC, then tutaumia zaidi, ila si rwanda (kama unavyodhani

Uganda sio watumiaji wakubwa wa Dar, they have been using Mombasa for ages

fanya homework yako wewe imbechili kwanza... hatuangalii bendera tunaangalia numbers

nalaabuk wahed

Yes Mkuu...Spot on.....Waganda ni wateja wa Mombasa Port...Hata Rwanda yenyewe kwa population yake haina impact kubwa sana ingawa ipo.......Ishu kubwa ni kama tukiipoteza DRC.The issue here tukomae kuanzisha uhusiano na DRC ambao utakua beneficial zaidi.....
 
chenge.jpg

Na Raymond Kaminyoge,



Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.



Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

“Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi,” alisema.


Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

“Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo,” alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.



Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.

Kila mchuma janga hula na wa kwao sasa haya tena majanga
 
Pamoja na mbwembwe zote za mwakyembe kujitapa kuwa ameboresha bandari ya dar,kumbe ni bure kabisa!
 
katika maisha, ukishindwa kuzitambua faida za umuhimu wako inabidi uoneshwe na kuzijutia gharama za kuupoteza umuhimu huo. hivyo basi hilo litakuwa fundisho kwa tanzania japo viongozi watajisafisha kwa kuwaponda rwanda na uganda ila ukweli utabaki palepale na nilazima itatugharimu.
 
Back
Top Bottom