Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Sasa kama mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ni Andrew Chenge unategemea watu wako serious kweli na serikali hii?
Yaani ktk watu wote mzee wa vijisent ndio amepewa uenyekiti?
Kazi tunayo

Duu hii kali
 
Kwa iyo ile misusuru ya magari mapya kwenda Rwanda hatutaiona tena hapa Singida!!
 
Kwa wingi wa madawa yanavyopitishwa hapa kwetu ni heri hata JKNI nao ususwe mpaka tutakapojipanga
 
Sasa kama mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ni Andrew Chenge unategemea watu wako serious kweli na serikali hii?
Yaani ktk watu wote mzee wa vijisent ndio amepewa uenyekiti?
Kazi tunayo

Duu hii kali, ila nahisi kwa style hii yunayofanyiwa na majirani itatu-cost, juzi kulikuwa kuna kikao kikubwa cha masuala ya fedha pale Arusha kinachotakiwa kiudhuriwe na ncho zoote washiriki asipokuwepo mshirika mmoja hakifanyiki, basi Rwanda wametoa udhuru kwamba hawapo tayari kuhudhuria kwasasa labda siku za hapo baadaye, kutokana na hili imebidi kikao hicho kikubwa kisifanyike. Inaumiza sana
 
NO NEED of KNEEL DOWN but govt must eases and facilitate the all routine objections,let programe the better way so that our service will quickest,fast enough/I DONT NO FOR CORRUPTIVE GOVT& EGOISM AMONG LEADERS god bless tanzania
 
Mimi sidhani kama kagame anaweza kuwahakikishia urahisi wa biashara wafanya biashara wake kiivyo. Ni kwamba hapo mwanzo kilichowafanya wakawa wanatumia bandari ya Dsm ni kitu gani? Sasa wajidai wanajitoa, kiukweli hakuna mfanya biashara anaehitaji ucheleweshwahi wa bidhaa zake, kilichopo ni nchi yetu kuimarisha ufanisi bandarini.
Pili hao wakina Poppe ni waongo sana, ukiona mtu anakazania vitu kama mzani vitolewe ujue huyo ninmwizi, hayo jamaa wanazidisha kupita kiasi kiwango chao chakubeba mzigo. Hata wakati huu ambao kuna mizani nyingi wanazidisha vile vile. Hakuna mwizi anaetaka vituo vyapolisi viweke kila kona.
 
Siku zote hawakuyaona hayo matatizo mpaka wakati huu?
Hizi ni hasara za kuongoza nchi ki-taarabu taarabu.
Tunavuna tulichopanda.
Mungu atusaidie maana itakula kwetu, na huu ni mwanzo tu
 
Everything has a price. Rwanda and Tanzania are losers! Kenya is the most winner. Uganda - neutral!

Ukiacha Kenya na Uganda hao waliobaki wanajidai ni maskini jeuri. Lakini kwa faida ya nani? Unapokuwa kiongozi unahitaji kuwa makini sana linapokuja suala la ujirani mwema. Kuna kitu kinaitwa give and take. Aina yo yote ya ubabe haisaidii.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Tunapoelekea serikali hazitakua na nguvu ya kupanga watumie bandari ipi... ni wafanyabiashara ndio wataamua

so i dont see any problem, Rwanda na Uganda are small countries (kiserikali na kibiashara), nevertheless, wafanyabiashara binafsi wanweza kuwa huru kutumia bandari yoyote kutokana na quality of service

i am not worried na serikali zao kuamua, i am more concerned na ufanisi wa bandari zetu
 
NO NEED of KNEEL DOWN but govt must eases and facilitate the all routine objections,let programe the better way so that our service will quickest,fast enough/I DONT NO FOR CORRUPTIVE GOVT& EGOISM AMONG LEADERS god bless tanzania
Unataka kusema nini? Kama wewe ni Mtanzania andika kwa Kiswahili. What you have written is a group of words with no meaning. Kama wewe ni Mnyarwanda andika kwa Kifaransa wapo wanaofahamu Kifaransa kwenye JF wata-react accordingly.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.



Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

“Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi,” alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

“Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo,” alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.



Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.

Source:Mwananchi
 
mbona hizo mbwe mbwe tu .... atake asitake bado nchi yake ni "land locked country-rwanda" atake asitake.

kwli ni land-locked if u really are learned huwezi argue hivo economically imekula kwetu...na ndo maana umeona bwana PK anatafuta mbadala kabla hakijanuka zaidi...politics is killing us
 
Tunapoelekea serikali hazitakua na nguvu ya kupanga watumie bandari ipi... ni wafanyabiashara ndio wataamua

so i dont see any problem, Rwanda na Uganda are small countries (kiserikali na kibiashara), nevertheless, wafanyabiashara binafsi wanweza kuwa huru kutumia bandari yoyote kutokana na quality of service

i am not worried na serikali zao kuamua, i am more concerned na ufanisi wa bandari zetu

aloooo.....humu jamii kuna vituko...eti nini?well sijajua elimu yako...
 
Haya maneno ni ya kweli wala sio uzushi Tanzania ina vikwazo vingi sana ili watu wachukue rushwa
 
Back
Top Bottom