Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Ndugu nafikiri kuna visababu ninavyovifikiria kama ifuatavyo: hii yote ni sis TZ kukataa kingiza ardhi kwenye EAC kwani angalia nchi hizi hawana ardhi tena macho yamebakia Bongo. Angalia classic example, utalii wa Kenya unakwenda chini baada ya TZ na other social media sources zinavyoitangaza vivutio vya utalii. Pia Obama, Bush na Clinton kuja TZ yaweza kuwa sababu kwani in future tutakaribisha investment capital itakayotishia uchumi wa hizi nchi.. Pia si maajabu pia kuhusu gas tuiliyonayo na Uranium ndivyo walivyoona wakijua wabong are soon if not now taking off!!!Nawasilisha mie..
Umeongea ukweli mtupu mkuu, kilichobaki hapa nikujitoa tu kwenye hiyo EAC na kuanza kukomaa kuijenga nchi yetu! malumbano ya kisiasa ndani ya nchi na yale ya kikatiba na muungano yasiathiri mambo muhimu ya kitaifa pindi ikitakiwa kufanya hivyo! hawa majirani zetu sio wazuri hata kidogo, ni manyoka tena wale wenye sumu kali ambao wanaumezo wakuua "200 men in one strike"
 
"Ila cha msingi ni kuyafanyia kazi mapungufu ya bandari plus na hii tabia hovyo ya Traffic kuomba hela bila haya."HAYA MANENO NAYO HUKUYAONA?KWA ENGLISH LETS WORK ON OUR SHORTCOMINGS"Labda nipige na Kiitaliano!

Nimesoma bandiko lako lote ambalo ulianza kwa sema kuwa "Bado tutaluwa tuko na Malawi Zambia na DRC plus Burundi," which suggests that pamoja na kuwa customers A na B wametuacha bado tutakuwa na customers C na D.

Hata hivyo, ukajishtukia kuwa hata customerss C na D utawapoteza hivi hivi kama hutashughulikia matatizo ya product yako.

Ni kama vile hutaki kuwapoteza pia customers C na D lakini huna mpango wa kuwarudisha customers A na B.
 
Ni lazima tujiulize kwanini baadhi ya Watanzania bado wanatumia bandari ya Mombasa ikiwemo mimi mwenyewe wakati ya kwetu ipo?? Sijawahi kusikia wala kuona Wakenya wakitumia bandari yetu.
Jibu: Hii ni kwa sababu ya huduma mbovu zilizopo bandari ya Dar-es-salaam kama, ucheleweshaji wa kutoa mizigo, wizi, rushwa iliyo kithiri, ukiritimba, uzembe, ufisadi,longolongo na mengine mengi. I think we are not serious! This is a lesson to learn.. something needs to be done, else we are done.
 
Ndugu nafikiri kuna visababu ninavyovifikiria kama ifuatavyo: hii yote ni sis TZ kukataa kingiza ardhi kwenye EAC kwani angalia nchi hizi hawana ardhi tena macho yamebakia Bongo. Angalia classic example, utalii wa Kenya unakwenda chini baada ya TZ na other social media sources zinavyoitangaza vivutio vya utalii. Pia Obama, Bush na Clinton kuja TZ yaweza kuwa sababu kwani in future tutakaribisha investment capital itakayotishia uchumi wa hizi nchi.. Pia si maajabu pia kuhusu gas tuiliyonayo na Uranium ndivyo walivyoona wakijua wabong are soon if not now taking off!!!Nawasilisha mie..

Wewe naona bado unatafuta mchawi. Nikuulize maswali kadhaaa.

  1. Hao Watanzania kama akina Ngongo na Jean Baptiste wanaotumia bandari ya Mombasa wanafanya hivyo kwa sababu ya Tanzania kukataa kingiza ardhi kwenye EAC?
  2. Hao Watanzania wanatumia bandari ya mombasa kwa vile tuu Obama, Bush na Clinton kuja Tanzania?
  3. Wanatumia pia bandari ya Mombasa kwa sababu ya gesi tuliyonayo na Uranium?

Tuache siasa. Customers service Tanzania ni mbaya kupita kiasi. Tunaringia sana tulivyonavyo lakini ukiambiwa orodhesha faida ya kuwa na hivyo ulivyo navyo ni almost zero.

Tunapenda sana kujisifu kwa sababu zisizo za msingi.
 
Kama ni msafiri wa barabara ungekuwa ushajiuliza swali hili siku nyingi... ,Kuna msururu mrefu kwenye mizani ukianzia kibaha, michese, morogoro, dodoma, shinyanga, katika mizani zote hizi lazina lori ipoteze zaid ya dakika arobaini na tano.. (muda unaopotea kwenye mizani tuu ni zaid ya masaa matatu kwa gari moja) ni masaa na bado kuna trafiki katika mkoa mmoja tuu kuna trafiki check poin zaidi ya sita na kila moja ina poteza muda wa dakika kumi (muda unaopotea kwenye hiz check point ni zaidi ya saa moja kwa gari)..

Total time cost per year goes up to billions of money... Kiukweli hatuko kibiashara na viongozi wetu wamekosa vision labda kwa sababu hawayaoni haya na waliochini yao wanafaidika na huu urasimu.. na rushwa..

Hii ni moja kati ya maeneo ambayo wachumi wetu wangefanya utafiti na bila shaka hukosi PHD katika eneo hilii...
Badala ya kuwa objetive na kujiuliza kwanini Rwanda na Burundi wanakimbia bandari zetuu sisi tunachukulia kila kitu personal and subjective.. kwa akili hizi hatuwezi kutoka hapo tuliopo tutakuwa nchi ya laana kina mtu analalamika, hakuna mwenye majibu wote ni lawama na kujihamii tuuu

Mimi sio msafiri wa barabara bali ni mtumiaji mzuri wa bandari ya Dar na Mombasa for exports.
Ninaoperate kutokea Kampala, Dar na Mombasa.
Wengi mnaongea ubovu wa bandari ya Dar es salaam na hakuna anayesema ufanisi wa Mombasa port ni upi....

Hivi ni sahihi kudhani kwamba Uganda itatumia bandari ya Dar (over 1600km) wasiende Mombasa (about 1100km) iwapo huduma inakaribiana!

Kigali is almost the same distance from Mombasa/Dar....1400km on average. Kwa hiyo endapo huduma za Mombasa na Dar zinakaribiana a slight advantage may swing the balance.

Kuna mapungufu kwenye bandari yetu lakini haimanishi Mombasa are good performers....
FYI, Importers wa magari Zimbabwe wanatumia bandari ya Dar maana sheria yetu inaruhusu kuendesha gari iliyo on transit (SA inabidi ubebe gari yako).

Narudia tena kina Hans Poppe na wengine tuwekeeni takwimu linganifu....sio maneno tuuuu!!!
 
Ni lazima tujiulize kwanini baadhi ya Watanzania bado wanatumia bandari ya Mombasa ikiwemo mimi mwenyewe wakati ya kwetu ipo?? Sijawahi kusikia wala kuona Wakenya wakitumia bandari yetu.
Jibu: Hii ni kwa sababu ya huduma mbovu zilizopo bandari ya Dar-es-salaam kama, ucheleweshaji wa kutoa mizigo, wizi, rushwa iliyo kithiri, ukiritimba, uzembe, ufisadi,longolongo na mengine mengi. I think we are not serious! This is a lesson to learn.. something needs to be done, else we are done.

Hizo zote ni sababu za msingi....lazima tukubali kuwa uendeshaji wa taasisi zetu nyingi nyeti ni wa kiwango cha chini sn ukilinganisha na wenzetu....mbaya zaidi sijawahi kuona kiongozi yeyote zaidi ya mwakyembe while it is too late akijifunza na kuja na mbinu mbadala za kuboresha sekta zetu nyeki zikiwemo airport, bandari, reli nk.......WATZ TUSIPOBADILIKA HUU UZEMBE TUNAOURUNDIKA MIAKA NENDA RUDI NDO HUU UNATURUDIA....Dunia ya kisasa mambo yote yanaendeshwa kisasasasa......TICTS haina uwezo ila kwa kuwa ni ya wakubwa akiwemo rais basi haiwezi kuguswa hatimaye ufanisi ndo huo kila siku malalamiko.......Kila mfanya biashara mfano kariakoo anakwambia ananunulia bidhaa zake nairobi....viongozi wapo na wanajua lkn hakuna anayejifunza kwa nn wanaenda nairobi wkt sisi tuna opportunity zaidi ya hao wakenya...." TUKUBALI KUWA NCHI HII IMEKOSA VIONGOZI NA LAZIMA TUFUMUE MFUMO HUU WENYE AKILIMGANDO" OTHERWISE ITAENDELEA KULA KWETU NA TUTAENDELEA KUTAFUTA WACHAWI ILIHALI TUNAWAJUA ILA TUNAOGOPA/TUNASHINDWA KUWACHUKULIA HATUA....HUU NDO UKWELI MCHUNGU NIUJUAO
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!

...Thank You!...........

Hao akina Hanspope ni wa kuangaliwa kwa makini sana hao.........they do not care....wanafuja wana fisadi wakishirikiana na akina Vijisenti..........
 
Hivi haya maoni hapa yanawafikia walengwa na wanayafanyia kazi?
Nachokiona ni kujichosha tu kwa kumwagia jiwe maji ili lilainike na kujilisha upepo. Kama hata robo tu ya mawazo ya wadau hapa yangetumika, nadhani tungekuwa katika nafasi nzuri ya kuwin ktk battle hii. Hebu aulizwe Mwakyembe anampango gani juu ya hili au ndo anataka sifa kwa kufanya kazi za wizara nyingine?
Je, haoni umuhimu wa reli sasa kuliko wakati wote? Mfano bandari ya Kigoma iko taabani kwa kuwa tu reli ya kati imekufa! Tuone aibu jamani! Dah
 
Wengi wanaojadili humu ndani siyo wanauchumi hata kidogo isipokuwa ni wadandiaji tu wa hoja. Uganda na Rwanda wakijitoa wataahiri vipi uchumi wetu? Hilo ndio swali la kujiliza na siyo kuanza kuweka humu chuki binafsi sijui mara hilo ni tatizo la JK sijui huyu ni Mr. dhaifu na kadhalika. Rwanda na Uganda wakijitoa na wajitoe tu na wala hakuna madhara makubwa. Hebu tujiulize hivi sisi tunapata nini kwa Rwanda na Uganda kwa kutumia bandari yetu. Je, hamjui kuwa barabara zetu zinaharibika mno kwa malori makubwa yasiyo ya kawaida? Watakaoaathirika ni wale wafanyabiashara na wafanyakazi wa bandarini ambao huinyima mapato nchi kwa ruhswa zao za kishenzi. Watu wa kawaida kamwe hawezi kuathirika na ujinga uliopo katika bandari ya Dar es |Salaam. Sisi tuimarishe reli na tujenge uchumi wetu kwa kuangalia vyanzo vingine. Sisi tumebarikiwa kuwa na vyanzo vingi. Bandari ni sehemu ndogo mno ya mapato ya Tanzania. By the way waache Rwanda waitumie bandari ya Mombasa kwani watapata hasara kubwa na vitu huko Rwanda vitakuwa na bei kubwa mno na kuleta inastability kwao.
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu, kilichobaki hapa nikujitoa tu kwenye hiyo EAC na kuanza kukomaa kuijenga nchi yetu! malumbano ya kisiasa ndani ya nchi na yale ya kikatiba na muungano yasiathiri mambo muhimu ya kitaifa pindi ikitakiwa kufanya hivyo! hawa majirani zetu sio wazuri hata kidogo, ni manyoka tena wale wenye sumu kali ambao wanaumezo wakuua "200 men in one strike"

Sasa hivi, GDP (PPP) ya Kenya na Tanzania are almost the same. Uganda na Rwanda wala siyo nchi za kuitingishia kifua Tanzania, washindani wakubwa kiuchumi against Tanzania in East Africa ni Kenya, full stop.

Hawa wengine, hawana ufukwe wala maziwa makubwa kama Tanzania, wataishia kumangamanga tu, na sababu kubwa ni siasa zao, M7 na Kagame. Ila they are most welcome any time to use our bandari.

Bandari ya Mombasa ilikuwa ni free port for all east african states after independence, wakenya wakaitaifisha. Leo Waganda na Wanyarwanda wanajifanya Mombasa ...Mombasa, haya, yetu macho sisi.

Tatizo la Tanzania kubwa kwa sasa ni CCM!! CCM imeoza na uongozi umewashinda. Tukiiondoa ccm, hawamajirani watakuwa wanalisikilizia vumbi tu!
 
Ule mradi wa kujenga reli ya pamoja kati ya Tz na Uganda kuanzia Bandari ya Tanga hadi Musoma ndio harijojo?
 
Sasa hivi, GDP (PPP) ya Kenya na Tanzania are almost the same. Uganda na Rwanda wala siyo nchi za kuitingishia kifua Tanzania, washindani wakubwa kiuchumi against Tanzania in East Africa ni Kenya, full stop.

Hawa wengine, hawana ufukwe wala maziwa makubwa kama Tanzania, wataishia kumangamanga tu, na sababu kubwa ni siasa zao, M7 na Kagame. Ila they are most welcome any time to use our bandari.

Bandari ya Mombasa ilikuwa ni free port for all east african states after independence, wakenya wakaitaifisha. Leo Waganda na Wanyarwanda wanajifanya Mombasa ...Mombasa, haya, yetu macho sisi.

Tatizo la Tanzania kubwa kwa sasa ni CCM!! CCM imeoza na uongozi umewashinda. Tukiiondoa ccm, hawamajirani watakuwa wanalisikilizia vumbi tu!
Tufanyeni kadri inavyowezekana kulitatua tatizo la kiuchumi linaloikabili Tanzania, kama ni CCM, ndio kikwazo basi ing'olewe tu tumechoka, kama ni watendaji ndani ya serikali basi wawajibishwe, kila anaehusika na kurudisha maendeleo nyuma aondoke katika nafasi husika! tubakiwe na maadui wa nje tu, lakini itakua ni kioja kama tutakua tunakulana sisi kwa sisi kama samaki au wanyama pori!!!
 
Watanzania tusiwe na wasiwasi kwa hili, ni kweli uchumi utayumba kiasi lakini ukweli utabaki palepale kuwa bandari yetu ndio suluhisho la kweli kwako na watarudi tu, leo PK na MU7 wameungana kwa hili lakini miaka kazaa iliyopita walikuwa mahasimu wakubwa, kwa akili ya PK lazima alikoroge huko mbeleni, na mizigo itakayo hamia huko ni ya serikali tu, kwa upande wa wananchi, bado wataendelea kuitumia bandari ya Dar, wanaweza wakafanikiwa lengo lao kama watamudu kuihamisha tanzania na kuipeleka sudani au botwasana.
 
Haya yote yanatokana na usimamizi mbovu wa rasilimali zetu na kutokujali maslai ya nchi, wenye dhamana wamekuwa wakijali maslai yao2'hata kama tukisema tujiwekeze ktk gesi nk mwisho wa siku kama watawala hawata badilisha fikra tutaendelea kuwa wa mwisho ktk maendeleo kuliko majirani zetu wote' rasilimali zetu zote tulizopewa na mungu ambazo "ni kiasi tu cha kupanga jinsi gani ya kuendesha" ukiangalia madini yetu, wanyama wetu, bandari' badala ya kuwa ni neema kwetu sisi sote imekuwa ni kama mali ya watawala' bado gesi na mafuta, (mwanzo wake tu ni utata mtupu) imefikia sasa ukitambulika wewe ni mtz unatazamwa kwa jicho la 2! Inakera sana nchi hii... Ee..mungu baba wabadilishe fikra viongozi wetu..hata ukiwaua wote tutashukuru mungu'.
 
Kama rwanda na uganda wanaendesha serikali zao bila mapato ya bandari.. kwann tz tuogope kuishi bila wao??
 
Mimi naona hii bandari tuifunge kabisa na sisi tutumie Mombasa maana ni janga la taifa. Bandari miaka nenda rudi inalalamikiwa na matatizo hayo hayo!
Bandari ni Lango la Biashara Miaka ile kulikuwa na wimbo huo....
 
now tell economy ya rwanda ni ipi, mzunguko wa mizigo/consignments za kuweka impact kwa nchi kama Tanzania ni upi??? mnaagiza kipi na kuuza kipi chenye business volume kubwa kulinganisha ilala au kinondoni???

let me keep quiet... maana naona unachukua habari za hawa local transporters na kuifanya muhimu sana

Myopia at its best

tatizo linalotugharim ni ushabiki usiyokuwa na tija...nimegundua wewe ni muelewa isipokuwa mahaba ulonayo yanakufanya usitumie weledi wako katika kujadili mambo...acha mahaba hili ni swala nyeti sana....hata kama rwanda ni sawa na temeke so inafanya temeke mbili..ikijitoa tutabakiza temeke moja tu economically it has a lot of impact....acha ushabiki
 
Watanzania tusiwe na wasiwasi kwa hili, ni kweli uchumi utayumba kiasi lakini ukweli utabaki palepale kuwa bandari yetu ndio suluhisho la kweli kwako na watarudi tu, leo PK na MU7 wameungana kwa hili lakini miaka kazaa iliyopita walikuwa mahasimu wakubwa, kwa akili ya PK lazima alikoroge huko mbeleni, na mizigo itakayo hamia huko ni ya serikali tu, kwa upande wa wananchi, bado wataendelea kuitumia bandari ya Dar, wanaweza wakafanikiwa lengo lao kama watamudu kuihamisha tanzania na kuipeleka sudani au botwasana.
Naungana nawe mkuu. Hapa ni suala la kujipanga vzr tu. Kwa landlocked countries ni uwendawazimu wa ukubwani kuwekeza kila kitu chako kwa jirani mmoja. Tukumbuke miaka takriban 4 ilopita uhusiano kati ya kenya na uganda ulikuwa shakani hata kupelekea vita baina yao wakigombea kisiwa cha migingo ktk ziwa victoria ambapo jeshi la uganda walivamia kisiwa na kupandisha bendera ya uganda. Kama isingekuwa busara za Kibaki vita ingepigwa. Rwanda na Uganda nao pia uhusiano wao kwa miaka kadhaa umekuwa wa paka na panya hata kuchapana mara mbili ndani ya DRC wakigombea dhahabu za wizi. Hivo itakuwa ni upuuzi kuitenga Tz kwa kudhani wanaikomoa. Akili zao finyu zinawafanya washindwe kutambua kuwa kwa jiografia ya nchi zao ilivo wanafanya kosa la kihistoria na la kiuenda wazimu. Watalazimika kulamba miguu ya wakenya maisha yao yote na midomo ikikauka mate watakuja wenyewe. Hatuhitaji kuwa bembeleza ila watakuja wenyewe tu. Muda na mazingira ya wakati vtawafanya watupigie magoti wakati tukisimama wima. "Ngoma ya kitoto huwa haikeshi" Kuwa na rafiki kama Kagame ni sawa na urafiki wa mbuzi na fisi. We fikiria ka nchi ka Rwanda ukubwa na jiografia kama kiberiti wtatokea wapi kama sio kulamba viatu vya jirani zake? Bora Mu7 anaongoza nchi na sio Kagame sawa na katibu tarafa. Tukipoteza wao wanapotea.
 
Back
Top Bottom