Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Hatuitaji sana Rwanda kiivyo, mimi naona inavyofanya kusaidia Congo nisawa kwani Ikija kutulia matunda yake yatakuwa makubwa, kwani investors watamiminika Congo na watatumia bandari Kama unavyojua mineral company wanatumia bandari Zaidi kuliko na wafanyabira wa Kigali na Vikontena kutoka Dubai.
 
Wao watutenge tu kwenye EAC, naamni wakitutenga, mafisadi wetu kwa namna fulani watabadirika na kua wazalendo kwa asimilia kubwa. Naamini kuna kitu kita tigger kwa ubongo wa mafisadi na kubadili calculas nzima.
 
Unavyouliza bandari ya bagamoyo ya nini ndiyo ilivyo kuwa 90s in Dar wakati foleni zilivyoanza viongozi hawakufikiriA kujenga flyovers ndio maana sasahivi watu wanashinda kwa barabara.Tanzania inahitaji new roads, ports and railways.Unachotakiwa kufikiria jinsi gAni tutapata pesa za miradi Acheni majungu kwani sababu Kikwete katokea bagamoyo ndio maana anajenga huko.
 
Trafki nao wamo du kweli hawa jamaa wanatisha kwenye uchumi wa nchi
 
Tatizo sio ufisadi wala rushwa bandarini. Tatizo hasa ni Kikwete kupeleka majeshi DRC kuzuia Wanyarwanda na Waganda kuchukua mali za Congo. Hata zile hasira za Kagame kuanza kumtukana Kikwete tatizo sio ushauri tatizo ni lile lile la Tanzania kupeleka majeshi DRC kuzuia uibaji wa mali za congo ama kutia kiwingu. Ndio maana jamaa wana hasira kwelikweli. Hapo bandarini hata kama kungekuwa na ufanisi 100% na hakuna polisi barabarani jamaa bado wangeiacha bandari maana masilahi yao makubwa ni kongo. Kikwete kama ameenda kutia kitumbua mchanga.

Hata hayo maendeleo yanayoonekana rwanda asilimia kubwa ni kutokana na mali za CONGO, ikitokea majeshi ya TZ yakawadhibiti M23 huko Congo mtaona jinsi uchumi wa Rwanda utavyobuma.

Rwanda: Govt to Tighten Mineral Traceability to Boost Market

http://allafrica.com/stories/201303180213.html

Rwanda wana plan ku export madini wakati hata hawana machimbo.
sure mkuu umenena, walichofanya hapa ni kumwaga mboga baada ya kikwete kumwaga ugali.pia mkuu inasemekana museven ana asili ya makabila ya kitusti, hivyo kuelewana na kagame ambaye ni mtutsi is normal. umeongea kilakitu kwa uhalisia wake.sina cha kuongeza.
am still worying ABOUT KIKWETE vision ON HOW CUNNING HE IS..in order to enjoy economic benefit WITH CONGO THAN EAC. anategemea kunufaikaje kwa kuisapoti congo. kwani Wakenya hapa inaonyesha watanufaika zaidi kiuchumi na EAC(ama uganda na rwanda and including Tanzania). i think congo has a bunch of chaos, we shouldn't attempt that shit. we might end up contaminated with what so called natural resource curse
 
let them go nothing to worry! Kuendelea kulialia na rwanda&uganda kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina bahari chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye gas na italipa tu acha watuondolee jams na usumbufu
. Hii ni hatua sahihi ya wafanyabiashara was rwanda lakini nahisi kuna shinikizo nyuma ya jambo hili. Ule utatu mtakata wa kagame,kenyatta na kaguta utekelezaji unaanza rasmi. Ushauri kwa serkali yetu tuache kuegemea eneo hili la kodi. Kama wao wanaishi kwa bila hizo kodi na wanatoa ,je sisi si bora zaidi kuliko waoambao kamwe hawapati kabisa.
 
Utasema hayo lakini ni maneno ya mkosaji wenzio wanasonga mbele

wanasonga mbele kuelekea wapi? the hague? au msituni ? we subili tu huko kigali akija ingia rais mwingine lazima atengue uamuzi "kichaa" amabao mwenzake aliufanya kwani hauwezi ishi jangwani kisha ukawaretea kwere jirani zako wanoishi kwenye OASIS , hakika utajuta tu siku na kuja kuwomba radhi yaishe.
 
Ufanisi wa Bandari ya Dar ni mdogo sana ukifananisha na Mombasa.
Rushwa kwa TZ ni kitu cha kawaida kabisa yaani ndiyo halali yake na halali ndiyo rushwa.
Mizani ni nyingi kwa maana kwamba zinachukua muda mrefu gari kupita kwenye mizani(foleni).
Reli ni suala muhimu sana na hili PK alishamwambia JK kuhusu kuimarisha reli ya kati ms kuiongeza mpaka Rwanda, hii ingemaliza usumbufu wote wa rushwa, mizani, ucheleweshaji wa mizigo, uharibifu wa barabara nk.
Lkn JK &Co. hawataki reli ifanye kazi coz watakufa njaa na malori yao yatakosa kazi, PK ameongea na Museveni&Uhuru wakakubaliana wazo zuri tujenge reli, bandari ya mombasa ina ufanisi mzuri kwahiyo kazi itakuwa nzuri ktk sekta zote.
Haya ni matokeo ya rushwa, unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na serikali ya chama cha majambazi.
 
Kwenye urasimu ktk haka ka nchi ketu kuna ka ukweli,Ila tufahamu kuwa kenya wamekuwa wakikamezea mate kabandari ketu na juhudi zao za kupursuade rwanda,burundi na ug kuacha kutumia hiyo bandari na kuhamia Mombasa zinaelekea kuzaa matunda
 
Ndio madhara ya kutotaka amani na wapinzani wenu......tafuteni amani....na kama wale walioshiriki mauaji bado wapo wafikishwe kwenye vyombo vya sheria........Charles Taylor ni mfano halisi.....mbali na kuwa yeye alikuwa Kiongozi wa nchi



Obviously wale ni Wanyarwanda.......wanatakiwa warudi kwao Rwanda..........ongeeni mkubaliane amani na mjengeane hoja za kufikishana mbele ya vyombo vya sheria.........msituletee unrest kwenye maziwa makuu........




Haiwezekani upande mmoja uka-dictate position ya mazungumzo yanayotakiwa yahusu makubaliano ya pande mbili........huo ni uchizi.....there no way mtapata muafaka kwa mtizamo huo........

NB: kama ulikuwa hujui....kwa taarifa yako.......Wamarekani wanazungumza na Taliban plus Al-Qaida kuhusu mstkabala mzima wa amani mashariki ya kati na maeneo mengine yanayohusu interest za Marekani na wenzake....




....hebu leta evidence ya hiyo kitu.......waliitangaza lini na ilikuwa wapi.......


[h=2]US offers $5m bounty for FDLR's Mudacumura[/h]



The US government has offered US$5 million for information leading to the arrest, transfer and conviction of Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) supreme commander, Sylvestre Mudacumura.
US Ambassador-at-Large for Global Criminal Justice Stephen J. Rapp announced this on Thursday during a tele-press conference.
Mudacumura is wanted by the International Criminal Court (ICC) on charges of crimes against humanity and war crimes, including murder, rape, torture and attacking civilians.
He is the overall commander of the FDLR, a DRC-based militia group largely blamed for the 1994 Genocide against the Tutsi.
Mudacumura's name was added on the list of the most wanted fugitives, which also features several key architects of the Genocide, including Felicien Kabuga, Protais Mpiranya and Augustin Bizimana.
Uganda's warlord Joseph Kony, leader of the notorious Lord's Resistance Army (LRA), is also on the list.


Any more questions?
 
tatizo linalotugharim ni ushabiki usiyokuwa na tija...nimegundua wewe ni muelewa isipokuwa mahaba ulonayo yanakufanya usitumie weledi wako katika kujadili mambo...acha mahaba hili ni swala nyeti sana....hata kama rwanda ni sawa na temeke so inafanya temeke mbili..ikijitoa tutabakiza temeke moja tu economically it has a lot of impact....acha ushabiki
Tanzania ina wilaya ngapi? Je kwa sasa ni percent ngapi ya bidhaa za rwanda zinapitia Dar?

je rwanda inachangiq asilimia ngapi ya pato la bandari ya dar?

Je kuna athari gani hasi za warwanda kutumia bandari yetu kwa sasa? Angalia kwenye matumizi ya barabara na overloads, ukwepaji ushuru (kufaulisha mizigo yao nk.)

Endapo wrwanda controbutes hata asilimia. Saba ya pato la dar basi ntasema kuna loss, so far ni anecdotals tu


btw, hiyo kauli unayotumia ya mahaba, nimeiona hata kwenye ile ID yako nyingine... Naona mnazaliana kama vitoto vya nape
 
Tuwe wakweli usumbufu bandari yetu ni mkubwa urasimu,rushwa na uzembe sio kwa wageni tu hata sie watanzania unatutesa tukubali ufanisi wetu uko chini tuimarishe huduma zetu kuanzia bandari zenyewe mpaka reli waganda na wanyarwanda wenyewe wataona hasara kutumia mombasa tuache kulialia tuchape kazi kwenye sekta hii sawa uamuzi wa rwanda na uganda ni wa kisiasa zaidi lakin na sie tunachangia kwa uzembe wetu tujipange tu kagame na mu7 hawatadumu milele siku wakifa wakiondoka madarakan watakaokuja watarud dar lakin lazima tukiri tatizo lipo katika bandar yetu
 
US offers $5m bounty for FDLR's Mudacumura





The US government has offered US$5 million for information leading to the arrest, transfer and conviction of Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) supreme commander, Sylvestre Mudacumura.
US Ambassador-at-Large for Global Criminal Justice Stephen J. Rapp announced this on Thursday during a tele-press conference.
Mudacumura is wanted by the International Criminal Court (ICC) on charges of crimes against humanity and war crimes, including murder, rape, torture and attacking civilians.
He is the overall commander of the FDLR, a DRC-based militia group largely blamed for the 1994 Genocide against the Tutsi.
Mudacumura's name was added on the list of the most wanted fugitives, which also features several key architects of the Genocide, including Felicien Kabuga, Protais Mpiranya and Augustin Bizimana.
Uganda's warlord Joseph Kony, leader of the notorious Lord's Resistance Army (LRA), is also on the list.


Any more questions?

Yes; are you not stupid?
 
Habari kwamba Rwanda na Uganda zimeamua kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao ni za kusikitisha kama ambavyo ni za kushtua. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta (Tatoa), kilitangaza juzi baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Bajeti kwamba nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo sugu mbalimbali ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakilalamikiwa lakini Serikali ikaamua kutia pamba masikioni badala ya kuyatatua.

Hivyo, tunaposema uamuzi wa nchi hizo mbili ni wa kushtua hatumaanishi hatua hiyo imekuja kwa kushtukiza. Hii ni kutokana na ukweli usiopingika kuwa, nchi hizo pamoja na nchi nyingine jirani, zikiwamo Zambia na DRC, kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikia hasara na kadhia wanazozipata kwa kutumia Bandari hiyo. Sababu zinazotolewa ni pamoja na wizi wa mizigo, yakiwamo makontena na vifaa vya magari kama vile redio; uchakachuaji wa mafuta; urasimu na ucheleweshaji wa mizigo kutoka bandarini; ukubwa wa ushuru wa forodha na barabara; na ugumu wa kufika na kutoka bandarini kutokana na misururu ya magari.

Lakini lalamiko kubwa zaidi la nchi hizo ni kwamba Serikali ya Tanzania haieleweki wala kuaminika pale yanapokuja masuala ya kibiashara na mengine mengi yanayohitaji uamuzi wa haraka. Tumedokezwa kwamba kutoeleweka na kutoaminika kwa Serikali ya Tanzania kunatokana na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na ugeugeu na undumila kuwili kwa kutenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na wakati mwingine kusema ‘ndiyo' wakati ikiwa na maana ya kusema ‘hapana'. Hilo ni lalamiko mtambuka ambalo pia linazungumziwa miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na ukweli kwamba uamuzi wa Rwanda na Uganda ulitazamiwa na wengi kutokana na Tanzania kutoshughulikia malalamiko ya nchi hizo kwa muda mrefu, sisi tunadhani uamuzi huo umelishtua taifa kiuchumi. Kitendo cha mataifa hayo kuamua kutumia Bandari mbadala ya Mombasa ni pigo kubwa kwa Tanzania kiuchumi, kwani pengo lake katika pato la taifa halitaweza kuzibwa kirahisi katika miaka mingi ijayo.

Pamoja na vitendo vya ufisadi na wizi wa mabilioni ya fedha uliopo katika Bandari hiyo, Ripoti ya Benki ya Dunia (WB), inasema bado Bandari hiyo inaweza kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani kwa asilimia kubwa iwapo zitachukuliwa hatua za kuleta ufanisi katika Bandari hiyo. Hivi sasa bado meli zinatia nanga kwa muda mrefu zikisubiri kupakuliwa mizigo na hali ni hiyohiyo kwa mchakato wa kuiondoa bandarini.

Tunachotaka kusema hapa ni kwamba asitafutwe mchawi asilani, kwani mchawi ni sisi wenyewe tuliozilazimisha Rwanda na Uganda kutumia Bandari ya Mombasa kutokana na uzembe na udhaifu wa Serikali yetu. Tayari kuna madai yasiyo na mashiko kwamba hizo ni hujuma za Rwanda dhidi ya Tanzania eti kutokana na hali ya ‘kutoelewana' kati ya marais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.

Hatua hiyo ya Rwanda na Uganda bila shaka itaisukuma Serikali ya Tanzania kusoma maandishi ukutani na alama za nyakati, kwamba isipopiga vita wizi na ufisadi na kuleta ufanisi bandarini, Zambia na DRC pia zitaondoka kama ilivyofanya Msumbiji na sasa Uganda na Rwanda. Tayari Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameanza kuchukua hatua stahiki. Tunarudia kuishauri Serikali imuunge mkono.


Source: Mwananchi

My take,
Tusiwe watu wa lawama, tukubaliana ya kwamba tunamapungufu makubwa ya kiutendaji na urasimu wa kutisha bandarini pamoja na mipango hewa ya serikali yetu.. Watanzania tubadilike na kuwa wazalendo si wa kusifiwa na kulaumu majirani zetu walifanya mambo kinyume nasi ila ni kwa kujali na kutumia vema raslmali zetu.

Nimeona mtu anasema hii haina athari ila serikali iweke nguvu kwenye gas!! hayo ni mawazo ya mwendawazimu yaani madini, utalii, ardhi na bandari umeshindwa itumia hiyo gas utaiweza vipi??? nahsi tuna laana na si bure
 
sure mkuu umenena, walichofanya hapa ni kumwaga mboga baada ya kikwete kumwaga ugali.pia mkuu inasemekana museven ana asili ya makabila ya kitusti, hivyo kuelewana na kagame ambaye ni mtutsi is normal. umeongea kilakitu kwa uhalisia wake.sina cha kuongeza.
am still worying ABOUT KIKWETE vision ON HOW CUNNING HE IS..in order to enjoy economic benefit WITH CONGO THAN EAC. anategemea kunufaikaje kwa kuisapoti congo. kwani Wakenya hapa inaonyesha watanufaika zaidi kiuchumi na EAC(ama uganda na rwanda and including Tanzania). i think congo has a bunch of chaos, we shouldn't attempt that shit. we might end up contaminated with what so called natural resource curse

As long as tukifanikisha kuzima M23, CONGO itatulia na potential ya kunufaika na CONGO ni kubwa mno kulinganisha na EAC. Wewe utanufaika je na EAC ni kidogo sana. Uganda siku zote walikuwa wanapitishia mizigo mingi Kenya utakumbuka ile vurugu ya kenya ya mwaka 2007 baada ya kung'oa reli jinsi M7 alivyotukana.

Tuna potentials zote, na tuna kila sababu zote za kupiga maendeleo tena bila hata utegemezi wa nchi yoyote. Kinachokosekana ni commitment za viongozi wetu tu. Lakini wakiji commit hata kwa 30% tu hao jamaa wa kaskazini hawatuoni tena kwa mbali sana.
 
NIMEKUBALI WATZ NDIVYO TULIVYO, KILA SIKU TUNAPENDA SANA KUTAFUTA VISINGIZIO HATA KWA MAMBO AMBAYO TUNAJUA UKWELI WAKE. Tatizo kubwa la watz ni dharau na kujiona . wanajiona wao ni matawi ya juu na hawashauriki. Likitokea la kutokea ndo sasa utasikia wanavyochonga na kulaumu, CHANGE IS MANDATORY.
 
Hakuna kupinda pinda hapa,hayo yote yanatokea kwa upuuzi na uzembe wa ccm na huyo ndie mchawi mkubwa
 
Hongera gazeti la MWANANCHI la leo 23 Agosti kwa tahriri yenu nzuri kuhusu matatizo ya bandari ya Dar es Salaam yanayosababisha wafanyabiashara wa Uganda na Rwanda kuazimia kuikacha. Tahriri ilionyesha ujuzi wa taaluma.

Gazeti la MTANZANIA linaonyesha matatizo kwenye taaluma kwa kujaribu kuchochea chuki kati ya Tanzania na Rwanda kwa siku kadhaa sasa. Suala la wafanyabiashara wa Uganda na Rwanda kutaka kuacha kutumia bandari ya Dar es salaam kwa sababu ambazo zimetajwa na Katibu mtendaji wa Chama cha wafanyabiashara wa mafuta Tanzania (TATOA), Bw Zacharia Hans Poppe zipo wazi, zikiwemo urasimu kwenye kutoa mizigo bandarini, wingi wa mizani za kupimia mizigo njiani, askari wa usalama barabarani kudai rushwa.
Mtanzania, jirekebisheni.
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
wa kenya wanaweza kuwa wanatuzidi kwa uwepesi
na haraka ya kutoa mizigo bandarini na pia kwa customer care kwa maana ya kwamba hata kama Trafiki watakuwa wana Kero basi linapokuja swala la maslahi ya taifa wanaweka Kero ama njaa zao pembeni ili kulinda maslahi ya taifa kwamba wanaacha kuwasumbua wageni ili kesho na kesho kutwa wawe na moyo wa kururudi kuja kufanya biashara tena . hivyo kwamba wanawajali wageni hasa wale ambao wana maslahi kwa taifa.tuache siasa katika swala hili na tutafute tatizo liko wapi ili tuweze kurekebisha na tuendelee kupata faida kutoka kwa wanyarwanda na siyo blaablaa kwenye biashara hakuna mtu anayetaka kufanya bila faida ukiona kwamba wanyarwanda na waganda wamehama kutoka bandari ya Dar kwenda Mombasa elewa kuna tatizo.
 
Back
Top Bottom