Ruzuku ya vyama vya siasa haitokani na Wabunge wa Viti Maalum

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,711
218,259
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika.

Kwa mfano, Jumla ya Kura ambazo Chama kinapata kwenye Majimbo yote ndio zinazopigiwa mahesabu ya kujua hata idadi ya wabunge wa viti maalum watakaotokana na chama hicho na kiasi cha ruzuku ambayo chama hicho kitapewa.

Kwahiyo kumbe ule uzushi kwamba Wabunge wa viti maalum ndiyo wanaviletea vyama vya siasa ruzuku unazimwa kama Mshumaa kwenye kipupwe kikali.
 
Sasa ndo mnakubali kuwa uchaguzi ulikuwa halali
Never haukuwa halali. I guess baada ya maridhiano haya, basi ya nyuma mnayaacha na mnasonga mbele katika maridhiano. Kwa andiko la Erythrocyte hili, I can now believe ie it is most likely kuwa Chadema wamechukua ruzuku iliyoandikwa jana!

Kama Samia anakuwa mgeni rasmi kenye sherehe za akina mama wa Chadema, then nadhani chadema imeshafikia kuwa we can work work the government as wapinzani and not enemies as it was during Magufuli's era!

BUT WITHOUT LOSING FOCUS/COMPROMISING THE BASIC DEMAND FOR KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI
 
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika...
SAWA.
Na hili la kutotambua na kushiriki katika mambo yatokanayo na uchaguzi haramu je? Au hayo yalikuwa ni matamshi ya kufurahisha watu tu?
 
Hili ni jambo muhimu sana ambalo wana JF mnapaswa kulifahamu, kwamba ruzuku ya vyama vya siasa hutolewa kutokana na Kura za Jumla ambazo Chama kimepata kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu husika...
Hii kazi unayofanya sasa inazidi kuwa ngumu sana, hasa kwa mtu kama wewe unayeamini chama kwa dhati kabisa.

Ushauri ninaoweza kukupa ili usiharibu hadhi yako kwa sasa, tena kwa haraka sana, ungejipa muda kidogo ili mambo yafumbuke zaidi huku ndani ya chama.

Haitachukua muda mwingi sasa, hapa tulipofikia sasa kwa hali halisi ya chama kujitokeza mbele kila mtu ajue kipo upande gani.
 
Never haukuwa halali. I guess baada ya maridhiano haya, basi ya nyuma mnayaacha na mnasonga mbele katika maridhiano. Kwa andiko la Erythrocyte hili, I can now believe ie it is most likely kuwa Chadema wamechukua ruzuku iliyoandikwa jana...
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Ni sawa na Liverpool 7 Man U 0
 
Back
Top Bottom