Ruvuma: Kijana wa miaka 24 ahukumiwa jela maisha kwa kosa la kulawiti mtoto wa miaka mitano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
ce6ba062-e57e-45f4-83b3-5e5a72708422.jpeg
Mahakama ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Oktoba 25, 2023 imemuhukumu kifungo cha Maisha jela, Pius Stephano Mbunda (24) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Tingi Wilaya ya Nyasa baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume (5).

Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya Jinai Na 31 ya mwaka 2023, Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Mh. O. N. Ngatunga alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julay 07,2023 majira ya saa kumi na Moja jioni huko Kijiji cha Tingi - Nyasa na kufikishwa mahakamani tarehe Julay 25.2023 na October 25,2023 hukumu ilitoka na kupatikana na hatia ya kosa hilo.
 
Back
Top Bottom