Ruvuma: Barabara kuu ya Mangaka - Tunduru yafungwa kwa muda. Ni kutokana na mvua zinazonyesha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Tunduru - Ruvuma

Kutokana na mvua kubwa zinazonyesha ukanda wa Morogoro na Selous, daraja kubwa la Mto Muhuwesi lililoko hapa Tunduru limejaa maji hadi juu ya daraja na kwa hiyo tumechukua uamuzi wa haraka wa kufunga barabara kuu ya Mangaka - Tunduru Mjini kwa muda. Eneo la barabara linalofungwa ni eneo la mto lililo kati ya kata za Muhuwesi na Majimaji.

Magari yanayotokea Mbeya, Iringa, Songea na Mkoa wote wa Ruvuma kuelekea Mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar yanapovuka Tunduru Mjini yapaki na kupumzika kusubiri hali iwe sawa Mto Muhuwesi. Magari hayo yanaweza pia kusimama/kupaki na kusubiria Sisi kwa Sisi au Muhuwesi Kijijini.

Magari yanayotokea mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam kuja Tunduru, yanashauriwa kusimama na kupaki Nakapanya, Namiungo au Majimaji.

Madereva wasilazimishe kuvuka daraja hili kwa sababu wataleta madhara, lakini vyombo vyetu vya usalama vimechukua tahadhari zote, visikilizwe.

Julius Mtatiro
DC Tunduru,
13.02.2024
IMG-20240213-WA0006.jpg
IMG-20240213-WA0007.jpg


======

UPDATES

=======

DARAJA LA MTO MUHUWESI SASA LINAPITIKA 100%

UPDATES ZA ASUBUHI HII - Jtano, 14.02.2024 - Saa 1.00 Asubuhi (0700HRS)


Baada ya maji kushuka, TANROAD wamefanya itifaki ya ukaguzi na kujiridhisha daraja liko salama.

Tangu saa 12 asubuhi ya leo tumefungua barabara hii na magari yanayoingia na kutoka Tunduru yanapita kama kawaida.

Wajulisheni abiria na madereva wote kutoka kokote waendelee na safari na watumie barabara yetu.

Tuendelee kuwakumbusha, mwendokasi unaua, kila anayeendesha chombo cha moto achukue tahadhari za kiusalama.

Karibuni Tunduru!

JSM,
Tunduru.
IMG-20240214-WA0004(1).jpg
 
Nachingwea apa ni kama tumefungiwa kisiwani hakuna kutoka...kwenda masasi barabara haipitiki kwenda Liwale pia barabara haipitiki.
ni kutumia njia za porini na boda boda
 
Bora DC Mtatatiro (Zamani Naibu Katibu Mkuu-CUF) ameifunga hiyo barabra kwa sababu kuna madereva vichwa maji kama hayo maji wangelazimisha kupita hapo na kuhatarisha maisha ya raia.
 
Back
Top Bottom