Rushwa njenje Arusha mjini ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa njenje Arusha mjini !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by emalau, Sep 23, 2010.

 1. e

  emalau JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Wana JF sasa sio siri tena, mgombea wa CCM jimbo la Arusha mjini anatoa rushwa bila kificho, wafaidika wa kwanza ni wakina mama wa soko kuu Arusha wanafuatia waendesha pikipiki na waendesha mikokoteni. Anachofanya ni kuwawekea mafuata waendesha pikipiki ya 10,000/= na kuwapa fulana ya CCM, wakina mama na waendesha mikokoteni wanapewa 10,000 na jezi. Pia wenyeviti wa vitongoji ndo wanatumika kwenda nyumba kwa nyumba wakigawa mrungula na Tshirt. Inawezekana nchi nzima ndo mtindo unaotumika tuwe macho.
   
 2. h

  hagonga Senior Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kula kwa CCM lakini kura kwa chadema.
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mgombea wa ccm alikuwa ni waziri katika serikali iliyopita, hivyo ni wazi kuwa amechota fedhanyingi sana za wananchi. Hivyo hiyo ni haki yao. Mgombea wa chadema kazi yake nyepesi awahamisishe wananchi hao wachukue hizofedha kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi na kuwapigia kuira wagombea wa chadema.
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  ATM za ccm, bonyeza namba ya siri yenye tarakimu nne - slaa
  , chukua pesa za ccm, tarehe 31/10/2010 usisahau namba ya siri - SLAA
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwambieni huyo mama anapoteza pesa yake bure. Karamagi aligawa mamilioni kwa mamilioni ya pesa wakati wa kura za maoni.
  Lakini kuna vituo ambavyo hata mawakala wake hawakumpigia kura. Ilikula kwake.
  Watanzania wa leo wanaanza kupata uelewa.
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nilipewa taarifa na kaka yangu aliyeko arusha kwamba kulikuwa na mshikemshike leo Arusha town baada ya TAKOKURU kuvamia bonanza ya ugawaji wa fedha ambapo kuna watu wametimka na kuacha funguo zao za nyumba
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Huyu Dr. aliwaambia wana-Arusha 'nikopesheni kura zenu niwalipe maendeleo' nafikiri wana-Arusha hawakukubali baada ya kuona 'kukopa harusi, kulipa matanga'. Sasa ameamua kununua kura, na hapo hakuna malipo ya maendeleo tena. Wana-Arusha muwe macho na uelewa mkubwa la sivyo mtalia kilio cha kusaga meno kwa muda wa miaka mitano ijayo!
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rushwa kwa sasa ni kupoteza pesa ,bora wanaojigaragaza kidogo ,ila senti watu wanakula na kura hupati .talia
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu hii kweli nimeisikia jana Mama Batilda alikuwa anagawa fedha kama njugu kwa akina mama wafanyabiashara ndogo ndogo maeneo ya soko kuu na stend kuu ya mabasi.Inaelekea TAKUKURU wamepewa maagizo maalum kumlinda Mama Batilda afanye atakavyo,hakuna juhudi zozote zinazofanywa na TAKUKURU kumzuia au kumkamata.

  Nimeanza kuamini TAKUKURU ipo kwaajili kundi fulani,juhudi za kupambana na kuzuia rushwa ni aina fulani ya usanii ambao CCM na serekali yake wameufanya either kuwatuliza wafadhili au kuwaghilibu wananchi waione serekali iko imara na makini kuzuia rushwa katika jamii.

  Shime wana Arusha na watanzania kwa jumla tuwakatae wagombea watoa rushwa bila kujali wanawakilisha chama gani.TAKUKURU ni jibwa lisilokuwa na meno ya kung'ata na hata likiwa na meno ya kuuma linachagua wa kumuuma.

  Tafakari chukua hatua rushwa ni adui wa haki [Mahakamani,Polisi,Magereza,Hospital,TAKUKURU,Ardhi na nk bila kutoa rushwa hakuna huduma].Wanasiasa wanaotoa rushwa kamwe hawawezi kuleta mabadiliko badala yake wataendeleza na kulea mfumo uliopo.
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Batilda chaguo la Lowasa yule FISADI WAZIRI MKUU aliyepigwa chini . Hili liko wazi Arusha . Kumchagua Batilda ni kufanikisha ufisadi maana hata hizo hela anzotoa kapewa na huyo boyfriend wake a.k.a HAWARA. Mama Regina Lowasa UPO? Slaa come and come very fast to redeem this collapsing beatuful but hohehahe nation.
   
 11. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi TAKUKURU nao washamaliza kazi mpaka msimu mjao?
   
 12. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Licha ya kugawa pesa, wafanya biashara katika soko kuu la Arusha wameruhusiwa kufanya biashara barabarani (Barabara zinazozunguka soko hilo). Kwa sasa ikifika muda wa jioni utakuta barabara zote zimejaa bidhaa wanazouza zikiwa zimetandazwa chini barabarani, hata magari hayapiti tena. Sijui manispaa wanaliona hili?
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Dr. Harrison Mwakyembe alishasema.

  Akikupa mpunga chukua kula. Siku ya kupiga kura unampotezea.
   
 14. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #14
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cha ajabu takukuru sasa hatuwasikii tena, walikuwa na kazi maalumu ya kuwang'oa akina mwakalebela na kuwachafua akina sita (na wale wote waliojipambanua kama wapiganaji wa ufisadi ndani ya ccm, sasa takukuru ni kama hawapo tena
   
 15. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  (ccm) chukua chako mapema.
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  NI mtaa gani wanakogawa pesa jameni...Emalau na Ngongo, nambieni jamani! Mi kila siku napiga msele town, mbona sipaoni?...wangenijazia japo lita 10 kwenye kitororoo changu si ningepata ushahidi na kuwadhalilisha kwa hasira zaidi SIKU YA KURA?!
   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu habari za uhakika ni kwamba jana TAKUKURU wamewakamata wanaCCM kadha kata ya Baraa akiwemo meya wa Jiji la Arusha.Umoja wa wanawake wa CCM uliandaa mkutano usiku kwaajili ya kuwahamasisha akina mama wamchague mbunge mwanamke mwenzao Dr Batilda katika ya mkutano vijana wa TAKUKURU wakavamia kikao nakwambia wakina mama walitimua mbio viatu,pochi,miwani,mawigi,funguo za magari na baadhi ya akina mama wasiokuwa na mbio wanashikiliwa na TAKUKURU.

  Nitawapa nyeti zaidi naendelea kufuatilia.
   
 18. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Mambo yako wazi kuwa (EL) alimpatia double B, kiasi cha 90m kwaajili ya kampeni.

  Hizo ni fedha za kodi yetu wa-tz, chukueni kuleni na KURA asipewe huyo naye ni FISADI.
   
 19. d

  david2010 JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Waache hao mafisadi wa CCm waturudishie hela zote walizoiba na wakishamaliza watakuwa hawana hata ya kula ndio watujua Mungu aliye juu
  Maana huyu Mbuge mwenyewe hana sera wala hawezi kushinda bali anatapatapa Tusiwape tena kura wala nafasi ya kutumia sisi vijana, wamama wala wanafunzi tusikubali kuwa kama chambo maana wakipata watakuwa au anakuwa kwa mume wake Zanzibar sasa kweli mtu kam huyo hatupaswi kumpa kura maana Arusha ni aibu sasa kwani hata huyo aliyetolewa hakufanya chochote alikwa mtu wa safari za nje kama JK na amejilimbikizia mali , arusha haina barabara nzuri jamu kubwa na ni kivutio cha utalii na inaingiza hela za kigeni kutokana mn hifadhi za wanyama, madini ya Tanzanite ilipaswa ijieudumie kwa kodi inayoishia kwa mafisadi wa CCm mwaka huu Chadema tunawapa kura kuanzia diwani hadi Rais
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  CCM = Chaka Chua Mafuta
   
Loading...