Kama siasa ndio hizi, basi hakuna maana ya kujiingiza huko. Mwanzisha thread, nadhani hii ni aina ya siasa za majitaka kutaka kumchafua Ndugai bila sababu ili azma yako ya mgombea fulani wa kiti cha spika apite. Sioni sababu ya kwa nini Lowassa aingizwe kwenye hili zoezi wakati Mzee wa watu keshakubali kwenda kuchunga ng'ombe, Monduli. Kumbukeni tu, fitina za aina hii hazijengi bali huharibu hata lile jema lililopo. Mkishampata speaker kwa fitina kama hizi, mnafikiri walio upande wa upinzani watafurahia? Hamtaweza maliza makundi ndani ya CCM kama tutakwenda kwa style hii. Tafakarini!!