Rushwa nje nje Dodoma Uspika wa Bunge, PCCB mko wapi?

Rushwa nje nje Dodoma Uspika wa Bunge, PCCB mko wapi?

kisatu

Senior Member
Joined
Jan 16, 2015
Posts
150
Reaction score
95
Hali ya mji wa Dodoma imechafuka usiku huu baada ya mgombea wa UKAWA Edward Lowasa kuamua kuhamishia nguvu zake kwa mbunge wa Kongwa Job Ndugai. Lowassa amechukua uamuzi huo baada ya aliyedaiwa kuwa mgombea anayemuunga mkono ndani ya CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi kuenguliwa na kamati kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM taifa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Uamuzi wa wafuasi wa Lowassa waliobaki ndani ya CCM kumuunga mkono Job Ndugai umefikiwa usiku baada ya kikao kizito kufanyika chini ya mjumbe maalum aliyefahamika kwa jina moja la Peter aliyedai kuwasili Dodoma jioni akiwa na maelekezo maalum ya bwana mkubwa (Lowassa).

Tayari wabunge wameanza kuhongwa pesa kiasi cha kati ya shilingi milioni 1 -2 kwa wabunge wa zamani na milioni 1 hadi laki 5 kwa wabunge wapya.
Pesa hizo zimeanza kugawiwa kwa wabunge wa kanda ya kati usiku majira ya saa 5:40 huku zoezi hilo likipangwa kuendelea hadi alfajiri ya siku ya kamati ya wabunge wa CCM kupiga kura.

Mjumbe huyo maalum kutoka kwa bwana mkubwa anagawa pesa hizo katika hoteli moja maarufu kukaliwa na kambi ya Lowasa iitwayo NAM hotel. Kiasi kingine cha pesa kinagawiwa na mdogo wa mgombea uspika huyo ambaye jina lake halijaweza kufahamika.

Kambi ya Lowassa ndani ya CCM imeapa kuhakikisha kuwa inachukua nafasi ya Spika kwa gharama yoyote ili kukwamisha utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
 
Ccm wazee wa siasa za maji taka nyinyi wenyewe kwa wenyewe ni kuchafuana tu
 
Si kweli kuwa ukawa wanamuunga mkono ndungai bali hizo ni njama za Mzee sita kuchafuana, kwanza Tambua ndungai ni Adui Namba moja wa ukawa hususani Mh sugu na Mh Tundu Lisu ni maadui wa ndungai kutokana na kuwatoa nje mara kwa mara kipindi akiwa naibu spika
 
Ccm wazee wa siasa za maji taka nyinyi wenyewe kwa wenyewe ni kuchafuana tu

Kamati kuu ya CCM wanamtaka ndungai ili awasaidie kuwakandamiza Upinzani Kama alivyokuwa akifanya huko nyuma.
 
Ndungai hachafuki kijinga jinga hivi. Tangu lini Ndungai akakaa na mzee wa kujinyea na mwasisi wa ufisadi Tanzania, fisadi Lowassa!?

#NdungaiForSpeaker
 
Lowasa na Ndungai wapi na wapi? Ukawa hawampendi ndungai kabsa maana wanajua akiwa spika atakuwa akiwachezea faulu nyingi sana.
 
Si kweli kuwa ukawa wanamuunga mkono ndungai bali hizo ni njama za Mzee sita kuchafuana, kwanza Tambua ndungai ni Adui Namba moja wa ukawa hususani Mh sugu na Mh Tundu Lisu ni maadui wa ndungai kutokana na kuwatoa nje mara kwa mara kipindi akiwa naibu spika

Pesa ubadilisha watu

Mbona wengi wa CCM walihamia Chadema

Lolote linawezekana duniani
 
CHADEMA wanahusikaje na mambo ya CCM? Shikaneni uchawi wenyewe!

Kwani nani anaongelewa anayetamani kupata sehemu ya kupumulia bado

Inahuma kukimbia chama na sasa kua hauwezi kurudi.

Lowassa ni Chadema damu damu ...teh teh teeeee
 
Inaweza kuwa jambo jema ili ile katiba ya wariona irejeshwe.
 
Hii ni kawaida ya CCM, lazma watafute mchawi, wampake uchafu mwisho wa siku fitna zisiishe, wamekua kama bongo movie, kutwa kucha ni kutafuta wachawi na wanga kwenye fani

CCM badilikeni kama JPM anavyotaka
 
Mtamalizana mwaka huu mlituaminisha lowassa ndiye tatizo ndani ya CCM ameondoka lkn bado mnaparuana nyie kwa nyie,.... Vp sitta anaelekea mahakamani au?Namba ishas omeka hapo
 
Back
Top Bottom