Rupia: Hazina ya Mjerumani

Mwaka 2014 tulikuwa na mradi kule mpwapwa sehemu inaitwa kiboriani kuna mission Moja ya waanglican ilisemekana ilijengwa na mjerumani aliyeenda kujificha hapo baada ya Vita kupamba Moto.
Wajukuu zake wakaahidi kuja kujenga hapo kituo wakatuma hela Kwa askofu chiwanga ili majengo yaanze kujengwa.walipofikia kupaua wakaja wenyewe na kuonyesha mahali pa kuchimba usiku wakatoa bati za kutosha kupaua kile kituo baada ya kupaua wakaondoka na mpaka Leo kile kituo hakijamalizika.
 
Labda zipo kwel
Ila mikoa kama sumbawanga na shinyanga(gambushi) wangeshatuambia maana wale ndio wakubwa wa hayo mambo
 
hii kitu haina ukweli wowote kaka yangu alianza hizi mambo toka nipo shule ya msingi mpaka leo miaka saba toka nimalize chuo hajafanikiwa chochote. mwaka 2014 walimwingiza baba nae kwenye hii mambo wakakaa maporini mwaka mzima wakarudi watupu huu niuongo mtu matumaini makubwa mafanikio sifuri kila siku wanaahidiwa mapadre wa morovian ndo wanajua kutoa kwasababu wamefundishwa ujerumani lakini wapi

kaka ashakata tamaa baada ya miaka kama 16 hivi ya kusaka hizi mambo saa hii analima tumbaku

ila kuna historia tamu sana ukikuta wenyewe wanahadithiana
 
kwa hisani ya chakarikamkopo. ( huyu bwana mara ya mwisho kuonekana hapa JF ni tarehe 23 July 2013)

Binafsi nimeshiriki sana kwenye hiyo biashara......kuna ukweli fulani lakini sehemu kubwa ni utapeli kwasababu ya ujinga na kukosa elimu kwa watu wengi. Watu wengi wanangaika kutafuta hivyo vitu lakini ultimately hakuna mtu anayemtaja mnunuzi wa uhakika...wanunuzi wote ni wa kufikirika.
Uzoefu wangu: NI kweli kuna hazina nyingi sana ambayo Wajerumani waliaacha Tz....wakati ule Msuya akiwa Waziri Mkuu katika ziara yake moja Ujereumani aliomba apewe ramani za sehemu ambazo wajerumani waliacha hazina ili zifukuliwe na zigawanywe. Jibu alilopewa ni kuwa hazina nyingi zilikuwa za watu binafsi wanaweza kushirikiana kwenye hazina za nchi ambazo nyingi zina vitu vya serikali....silaha, nk.

Hazina ya serikali pale Mbeya Tukuyu ipo jengo la mkuu wa wilaya...hata kwa macho ukiangalia ile ofisi imejengwa juu ya mlima wa kutengenezwa kule chini ni shimo kubwa sana. Mlango wa kuingilia upo ofisi ya afisa utamaduni wa wilaya. hata ukitembea kwenye ofisi utaona kuna hali ya kuonyesha chini kuna mtikisiko wa uwazi. Mlango mwingine nadhani uko nyumba aliyokuwa akiishi OCD. Miaka kumi iliyopita shirika la moja la Ujerumani waliomba kukarabati boma la mkuu wa wilaya na waliomba ukarabati uanzie ofisi ya utamaduni. Watu wakamshtua aliyekuwa RAS wa mkoa Mbeya (name withheld) akazuia ukarabati huo

Kule kijiji kwa akina Kapteni Komba kuna wageni wajerumani walichimba mashimbo kanisani na kwenye baadhi ya majengo ya kanisa hayo mashimo yalikuwepo hadi mwaka 2006 nilipopita hapo

Kuna kijiji kimoja cha akina Joyce Mhaville (wa ITV) nimekisahau kule Njombe baada ya Isoliwaya kabla hujafika Mfriga kuna binti wa kizungu alikuja kama kama volunteer akakaa baada ya miezi kadhaa akawaita wanakijiji wamsaidie kuchimba shimo fulani akawaambia mkifika sehemu ngumu muache ili nililete vifaa vingine usiku huo akaenda peke yake akachukua cha kuchukua asubuhi wakakuta shimo tupu na binti akatoweka hadi kesho.....sehemu inaitwa Lupembe

Kuna sehemu Mbeya inaitwa Ileya....pale kuna mzungu alikuwa tajiri sana yeye pia alificha mali zake jirani kabis na kanisa la Moravian hata alama za mawe alizoweka kuelekeza alipoficha mali zipo sema vile ni muda mfupi alama hizo zinapotea unapoingia kwenye vichaka. Baada ya kanisa la RC chini ya ''mtafutaji'' mashuhuri retired Afisa Usalama (name withheld) kushtukia hiyo dili waliamua kununua eneo lote hilo ili baadaye waanze kutafuta hizo mali wenyewe.

Kifupi ni kuwa Nyerere aliamua kujenga magereza, JKT, Shule sehemu zote ambazo alihisi kuna hazina ya madini au wajerumani waliaacha mali zao

The story goes on and on.................................
Mm n mzawa wa tukuyu uliyoyaongea n ukweli mtupu,,nakupongeza kwa hilo!! Pia kuna kule kunaitwa taraja la Mungu chini ya lile daraja yaani ndan ya maji pia nasikia kuna mali!! Ndio maana lile eneo lipo ndan ya chuo cha magereza!! Fafanua kama unalielewa vizur
 
Ukienda KILWA MASOKO ulizia sehemu inaitwa kisiwani...watakuonyesha sandaku la chuma limepigwa minyororo lipo chini ya maji. Unaliona hata ukiwa kwenye mtumbwi...lakin hamna mtu amewahi lichukua, wameshajaribu sana. Hadi leo lipo
 
MAKOSHNELI mkuu mimi pia naishi hapa jijini mbeya uliyoyaeleza mengi nayajua so mfano bwana Lena, soko la uhindini pia kuna mti kwa babu yangu inasemekana kuna rupia maeneo hayo kikweli hata tukienda kesho ilo eneo wamejaa nyuki na hawajawahi kuhama.
nitakuja kuwaondoa hao nyuki ili tukombe rupia ili tuishi kama malaika maana usawa huu chama tawala kinajua kinachofanya
 
Mali kubwa kuliko ote ni akili yako kichwani. Itumie.

Kuna siku mtu alituletea rupia ya Mjerumani hapa JF, anayo, anataka kuiuza, akifikiri nibutajiri.

Kwa sababu mimi ni mtu ninayetaka kutumia akili yangu, nikataka kuitafuta ile rupia online, nijue thamani yake.

Nilipopata thamanibyake onlins na kul8nganisha na mategemeo nilioata bumbuwazi.

Ilikuwa inapatikana kwa bei rahisi sana.
 
Mwaka 2009 nilipata kibarua ya mda pale ngorongoro, nikazoeana na mwenyeji mmoja wa pale ingawa yeye si mzaliwa wa hapo... Siku moja akanipa wazo tupande mlima moja mrefu ulio pembezoni mwa creta, akanipa data kidogo kuwa wakati wa vita vya pili wajerumani walitumia mlima huo km chimbo lao. Chini ya huo mlima kuna mashamba na majengo yao ambayo yapo hadi leo.... Tulipanda huo mlima tukiwa tumebeba lunch box zetu, tulipofika karibu na kilele tulipita kati ya miamba fulani tukaona maganda ya risasi na vichupa vidogo vya soda vikiwa vimepoteza sura. Tulifika mahali juu kidogo tukakuta kidimbwi ikiwa imezungukwa na miti mikubwa. Mojawapo ilikuwa na kitu kikiwa kimefungwa na mnyororo ambao umezama ndani ya mti yaani mti umekua nao ukameza mnyororo. Tulicheki tukaona ni kisanduku kina kofuli ilopata kutu na kuzeeka sana... Tuliamua tujaribu kuitoa ghafla ukaja upepo tukajikuta tuko chini ya mlima nyuma ya shule fulani ya msingi, hatukuwa na ujanja tukarudi kambini. Baada km wiki mbili tukaazimia kurudi na vifaa ili tushushe lile sanduku... Tulipofika hapo ile tumegusa ule mti mi nikajikuta niko barabara fulani inayoenda kijiji fulani inaitwa endulen, sikujua mwenzangu yuko wapi, nilijaribu kumpigia cm yake ikawa haipatikani. Nikarudi kambini jioni lakini jamaa bado hayupo hadi siku ya pili ndo akapatikana kwenye cm. Akanijibu amejikuta yuko wilaya jirani ya karatu ilimbidi apande basi ili arudi kazini... Tulikoma kwakweli. Miaka chache tena baadae 2014 kuna mzee fulani mwenyeji wa manyara akaniambia nimsaidie kutafuta soko la mali zake fulani ambazo alichimbua ktk pori kilomita kadhaa mashariki mwa hoteli ya ndutu kule Serengeti. Akaeleza kuwa aliona kitu km msingi wa nyumba kimesakafiwa ktk bonde waliamua kivunja ili waone kuna nini. Walifanikiwa kutoa sanduku lakini ghafla akatoka shimoni joka kubwa aina ya chatu akapanda juu ya hilo sanduku. Wakaamua wachukue kondoo moja km kafara kwa joka hilo, baadae likarudi shimoni na wao wakachukua sanduku hilo. Wakafika mahali ikabidi walivunje wakakuta bunduki 2, mawe yanayon'gaa km kilo 3, mikufu 2, binocular 2, nguo za khaki, pesa za rupia sarafu 52 imeandikwa tabora pound, na vitu vidogo vidogo. Bunduki waliamua wazichimbie ardhin, na vingine wakaweka ndani mfuko afu wakachimbia ndani ya boma la tajiri wao wa ngombe... Mwaka ukapita afu yeye akarudi kwao manyara. Baadae yule mwenye boma akawa amemtuma kijanake kumweleza huyu mzee aje aondoe vitu hivo kwake kwasababu vinaleta vitisho vya radi kila siku. Niliposikia hayo nikapatana nae aende mtu wangu moja ili walete, soko si tatizo. Baada ya wiki niliandaa safari yao walipokaribia ile nyumba ghafla mzee akawa km hajielewi anaongea mwenyewe hataki mtu karibu yake. Jamaa akanipigia cm, nikamwambia urudi nae, eti wakati wa kurudi ile wenge imepotea yuko sawa. Na yeye anashangaa mbona tunarudi walikotoka awali? Ikabidi tutemane na hiyo mambo coz kila utakalogusa lina mauzauza....... Simshauri mtu afuatilie hizi mali coz unaweza ukajikuta we ni mganga wa kienyeji au ni mchawi
We jamaa haya ya kweli au story tu?
 
Nilioana documentary moja hawa jamaa walivyohamisha masanduku ya chuma kurudi kwao lakini time wasn't on their hands ilibidi nyingine wazifukie

Kama technology ingekuwa kama ili to leonamandege makubwa wangebeba kila kitu.
Samahani hiyoDocumentary inaitwaje
 
Ukienda KILWA MASOKO ulizia sehemu inaitwa kisiwani...watakuonyesha sandaku la chuma limepigwa minyororo lipo chini ya maji. Unaliona hata ukiwa kwenye mtumbwi...lakin hamna mtu amewahi lichukua, wameshajaribu sana. Hadi leo lipo
Duuu
 
kwa hisani ya chakarikamkopo. ( huyu bwana mara ya mwisho kuonekana hapa JF ni tarehe 23 July 2013)

Binafsi nimeshiriki sana kwenye hiyo biashara......kuna ukweli fulani lakini sehemu kubwa ni utapeli kwasababu ya ujinga na kukosa elimu kwa watu wengi. Watu wengi wanangaika kutafuta hivyo vitu lakini ultimately hakuna mtu anayemtaja mnunuzi wa uhakika...wanunuzi wote ni wa kufikirika.
Uzoefu wangu: NI kweli kuna hazina nyingi sana ambayo Wajerumani waliaacha Tz....wakati ule Msuya akiwa Waziri Mkuu katika ziara yake moja Ujereumani aliomba apewe ramani za sehemu ambazo wajerumani waliacha hazina ili zifukuliwe na zigawanywe. Jibu alilopewa ni kuwa hazina nyingi zilikuwa za watu binafsi wanaweza kushirikiana kwenye hazina za nchi ambazo nyingi zina vitu vya serikali....silaha, nk.

Hazina ya serikali pale Mbeya Tukuyu ipo jengo la mkuu wa wilaya...hata kwa macho ukiangalia ile ofisi imejengwa juu ya mlima wa kutengenezwa kule chini ni shimo kubwa sana. Mlango wa kuingilia upo ofisi ya afisa utamaduni wa wilaya. hata ukitembea kwenye ofisi utaona kuna hali ya kuonyesha chini kuna mtikisiko wa uwazi. Mlango mwingine nadhani uko nyumba aliyokuwa akiishi OCD. Miaka kumi iliyopita shirika la moja la Ujerumani waliomba kukarabati boma la mkuu wa wilaya na waliomba ukarabati uanzie ofisi ya utamaduni. Watu wakamshtua aliyekuwa RAS wa mkoa Mbeya (name withheld) akazuia ukarabati huo

Kule kijiji kwa akina Kapteni Komba kuna wageni wajerumani walichimba mashimbo kanisani na kwenye baadhi ya majengo ya kanisa hayo mashimo yalikuwepo hadi mwaka 2006 nilipopita hapo

Kuna kijiji kimoja cha akina Joyce Mhaville (wa ITV) nimekisahau kule Njombe baada ya Isoliwaya kabla hujafika Mfriga kuna binti wa kizungu alikuja kama kama volunteer akakaa baada ya miezi kadhaa akawaita wanakijiji wamsaidie kuchimba shimo fulani akawaambia mkifika sehemu ngumu muache ili nililete vifaa vingine usiku huo akaenda peke yake akachukua cha kuchukua asubuhi wakakuta shimo tupu na binti akatoweka hadi kesho.....sehemu inaitwa Lupembe

Kuna sehemu Mbeya inaitwa Ileya....pale kuna mzungu alikuwa tajiri sana yeye pia alificha mali zake jirani kabis na kanisa la Moravian hata alama za mawe alizoweka kuelekeza alipoficha mali zipo sema vile ni muda mfupi alama hizo zinapotea unapoingia kwenye vichaka. Baada ya kanisa la RC chini ya ''mtafutaji'' mashuhuri retired Afisa Usalama (name withheld) kushtukia hiyo dili waliamua kununua eneo lote hilo ili baadaye waanze kutafuta hizo mali wenyewe.

Kifupi ni kuwa Nyerere aliamua kujenga magereza, JKT, Shule sehemu zote ambazo alihisi kuna hazina ya madini au wajerumani waliaacha mali zao

The story goes on and on.................................
Mkuu hiyo ya Lupembe ni kweli mbona sijawahi sikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo uvumi pia, kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa nchi (Tanzania) amejenga HEKALU katika moja ya mkoa (Mwambao) chini kuna utajiri wa DHAHABU..

Vipi na tetesi hizi..! Naomba anaefahamu kuhusu hili atujuze..

Nazo zikiachwa, uvumi utarithishwa kizazi na kizazi
Sio Lushoto huko.kwa CHE
 
Kuna mahandaki kibao yalichimbwa na hawa wajerumani. Hasa kwenye makanisa, mfano kwenye kanisa moja wapo Dodoma kuna kanisa lina handaki inasemekana linaenda umbali wa kama KM hadi chini ya mlima flan lkn handaki hilo limwfungwa kwa geri la nondo nene na kufuli lenye uzito kama wa kg 10 ma hakuna mwenye funguo. Kuna wajerumani walienda na camera zao miaka flan wakaendesha ibada kijeruman pale kisha wakapiga picha, wakaondoka.
 
Jamani ivi lupia bado inaitajika na vipi ile pesa yenye trekta kama Ivy League vitu dili nicheki apa 0629159317 call na whatsapp apo
 
Duh nimefatilia sana hii thread no body knows where the actual market is especially in Tanzania or east africa in general ama kweli ni utapeli mimi ninazo rupie zaidi ya moja ila sharti langu unaehitaji nitafute usibip na kama vp nitakuelekeza nilipo
 
Wadau, kama tumewahi sikia kwamba wajerumani waliacha Mali zao walizozichuma hapa kwetu kutokana na kile kinachosemekana ni kuondolewa ghafla na MWL.nyerere kutokana na agizo la UN.sasa ishu inapokuja ni pale ambapo watu wamebaini uwepo wa Mali hizo jinsi ya kuzichukua. Watu wengine hutumia waganga wa kienyeji lkn huambulia patupu, wengine hubahatika, wengine hupata madhara makubwa. Maswali tunaojiuliza ni je hawa wajeruman hatuwawezi?. Mchango wenu wadau.
 
Back
Top Bottom