Rungwe amvaa Makonda, amtaka amalize utata, aache kulia

Rungwe amvaa Makonda, amtaka amalize utata, aache kulia

Daudi bashite atakubali kurudi koromije, huyu atamwaibisha sizonje, ngoja tusubiri bunge
 
Rungwe amepiga kunakostahili, sasa atoke aelezee. Nawashangaa wanaotumia nguvu nyingi kumtetea Daudi.

Maana kamili ya Rungwe naiunga mkono.

ATOE VYETI UTATA UISHE.
 
KWANN ASITOE TU
BASHITE BWANA. WANACCM WANAMTETEA MTU WAO.
Sheria ina macho na imetungwa kwa mtanzania wa chini. Hiz shutuma zingekuwa kwa mwalimu. Sasa hiv angekuwa sero
 
Kantasundwa....... ni methali ya Kifipa. Mzindakaya na Eliakimu Simpasa waliwahi kutumia methali hii Bungeni kumshauri mzee Idd Simba aachie ngazi. Watu wengi wanashauriwa kuhusu jambo hili lakini wako kimyaaaa! Hivi kweli awamu zote mambo yangekuwa yanaendeshwa namna hii amani na upendo tunavyoimba kila siku vingekuwepo? Watu wanaliweka Taifa kwenye tension bila sababu za msingi,, jamani hatutafika popote.

Hata kama ni kweli anatumia vyeti vyake; kwa nini mamlaka ya uteuzi inayolalamikiwa isije mbele na kufafanua vizuri? Kuongoza Taifa inahitaji combination ya vitu vingi, lakini muhimu zaidi ni kuwa na washauri wazuri. Dawa siyo tamu (ni kali na inakera) lakini huwa tunalazimika kumeza ili tupone, Mhe afanyie kazi ushauri anaopewa hata kama unamkera.
 
Pia amemshauri kuacha kulia kwani kulia hakutamsaidia.
Hili jambo si lakumliza mtu
Hivi kama mtu una vyeti unalilia nini? huyu jamaa anashangaza. Mbona kuna watu kibao wamewahi kuachia nafasi nono mambo yalipoenda kombo? huyu mtu ana uhakika wa kustaafu akiwa mkuu wa mkoa? kwa hali ilivyo sasa akijiuzulu atapata heshima kuliko akiendelea na sarakasi zake za kitoto.
 
a5a0589d5647e827691561ae0b4d5d84.jpg

Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni
*
Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu.
Rungwe ametoa ushauri huo leo kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo. "Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi" Amesema Rungwe
*
Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha. "Siku moja nafungua 'ipad' yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa". Alisema Rungwe
*
Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung'ang'ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.
*
Alimaliza Hivyo Ndugu Rungwe.. Nini maoni yako mdau.. Unamuunga mkono Rungwe au unapingana naye???

[https://mushkhani.wordpress.com/URL]

Kuelekea 2020 lazima aongeee nanyi mjue yupo


Ha ha haaaaaaaaaa


Wafata mkumbo mtazidi kumezwa tu.

Makonda oyeeeeee

N.B.
Na nyie mnaoni quote hamchoki? notifications zimefika karibu mamia matatu siwajibu bado mpo tu tena tangu jana asubuhi. Piteni uko sibadili gia yangu ng'ooooooo
 
Hivi kama mtu una vyeti unalilia nini? huyu jamaa anashangaza. Mbona kuna watu kibao wamewahi kuachia nafasi nono mambo yalipoenda kombo? huyu mtu ana uhakika wa kustaafu akiwa mkuu wa mkoa? kwa hali ilivyo sasa akijiuzulu atapata heshima kuliko akiendelea na sarakasi zake za kitoto.
Akijiuzulu humu ndni hakutakalika yaan atadhihakiwa achaa kwaio hapo njiapanda mkuu
 
Yote aliyoongea "wakili msomi" Rungwe hata Magu anayaelewa vizuri sana. Mzee sio dumb kihivyo. Tatizo jipu limekaa katikati ya jicho kabisa na kulitumbua inahitaji ujasiri kidogo maana si misifa ile waliyokuwa wakimwagiana.
 
Back
Top Bottom