Rukwa: Polisi Waua tena Mwananchi!

Rukwa: Polisi Waua tena Mwananchi!

wakati wenzako wanaomboleza wewe unafanya utani kwa nini mazoezi hayo hawajamfanyia mama yako?

Punguza Jazba BADO MMOJA! huu ni aina nyingine ya uandishi wa kufikirisha, btw toka lini kukawa na mazoezi ya kulengashabaha na kuua raia wasiokuwa na hatia isipokuwa bongo tu? wenzetu huwa wanatumia risasi za bandia ikibidi lakini hapa kwetu tumeshuhudia wananchi wakiuawa as if sheria inaruhusu...Tatizo Mfumo mzima umeoza Mkuu... Tena kwa taarifa tu, Said Mwema amesaidia sana kupunguza makali kiasi kwamba wasaidizi wake wanamuona nyoronyoro! Imagine Mahita angekuwa ndo IGP sasa hivi hali ingekuwa vipi...Hofu yangu ni kuwa soon Polisi nao wataanza kuwindwa maana action n reaction ziko sawa...
 
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?

kwa hiyo polisi wanaruhusiwa kuwatwanga watuhumiwa risasi?
 
Mbna polisi akiuawa hampanui mijidomo yenu hyo kama Diamond..
 
Raia ni muda wa kujihami vinginevyo hawa majambazi watatumaliza ..tutumie kanuni ya Newton kupambana
 
Matukio mengi ya polisi kuua wananchi kwa madai kuwa ni wahalifu yamebainika kuwa si kweli.
Tunakumbuka sakata la zombe. Hivi karibuni ameuwawa na polisi mfanyabiashara mmoja mjini Geita ambaye imekuja kubainika baadae kuwa walimpora shilingi milioni 350 baada ya kumuua.

Bila ushabiki ni lazima jeshi la polisi libadilike na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Kama kweli ni wahalifu wafikishwe mahakamani ndipo wahukumiwe hata kama ni adhabu ya kifo itakuwa vizuri.
 
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?

Polisi wanatembea na mahakama au ni kuwashika wahalifu na kuwafikisha kwenye mhimili wa mahakama sheria ichukua mkondo wake. Acha kutetea unyanyasaji wa polisi.
 
mimi nadhani hili jeshi la polisi linatakiwa lisafishwe kabisa
Kuna hitajika reformation ya hali ya juu sana katika hili jeshi,rushwa,maadili,kulindana,intelijensia duni,ubabe na umimi vimeota mizizi na kumea.
 
sasa kama hao polisi walimpora huyo mfanyabiashara ili kupoteza ushahidi si ilibidi wamuue kabisa! kwani wale wafanyabiashara wa madini wa Mahenge waliouawa jijini Dar ishu yao ilikuwaje...si hivyo hivyo! hao ndio zao!
 
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?

Kumbe majukumu ya Polisi yamebadilika siku hizi? Watuhumiwa wanauawa badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki itendeke? Watu wanaosemekana kuwa na hasira kali wanapofanya hayo yaliofanywa na polisi mbona wanakemewa? Polisi ni nani wasikemewe? Mtuhumiwa atahesabiwa kuwa na hatia pale itakapothibitika pasi na kutia shaka kwamba kahusika katika kile anachotuhumiwa, na wenye mamlaka ya kufanya hivyo ni mahakama!
 
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?
Iwapo polisi wanamkamata mhalifu na kisha wao ndio wamhukumu kifo, mahakama zina kazi gani? Utawala wa sheria uko wapi Tanzania??? Kwa hiyo unataka polisi wapendwe kwa lipi?
 
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?
Sumu. .....ukituhumiwa wizi ndio tukutwange shaba??
 
Last edited by a moderator:
Taarifa imesema alituhumiwa kwa wizi, hiyo ya kudai polisi wanawamaliza wananchi wasio na hatia huku wahalifu wakijivinjari bila wasiwasi inatoka wapi tena? Au unataka kujenga chuki kati ya polisi na wananchi? Wananchi wakilichukia jeshi la polisi wewe utafaidika na nini?
Sasa kama ni mtuhumiwa inakuwaje polisi wamuue? Mtu kafuatwa nyumbani na hakufanya purukushani yoyote ya kupambana na polisi inakuwaje polisi wanamuua badala ya kumpeleka mahakamani?
 
Mbona maelezo ninayoyaona humu na nilivyoyapata humu ni tofauti?
Kuna mtu alieko sumbawanga, kanambia askari walikwenda nyumbani kwa huyo jamaa kwa ajili ya kumkamata lakini kutoka kwake alitoka na panga na kumpiga Askari 1 na kumjeruhi mkononi, ndipo askari walipotumia nguvu na kumpiga mguuni, kisha wote walipelekwa hospitali bahati mbaya mwananchi huyo amefariki kwa kupoteza damu nyingi. Na askari anaendelea kupata matibabu baada ya kupata fructure katika mkono aliopigwa panga na mwananchi huyo.
Kwa hivyo wananchi wenzangu pamoja na madaktari wenzangu tujaribu kueleza kwa kutokana na uhalisia na tusimuonee aibu mtu, chama au serikali ikiwa kumetokea kosa lisemwe ili tuweze kuishi kwa amani na usalama.
Na wasimamiaji wa sheria wajaribu kwenda kama sheria inavyotaka.
 
Policcm hao mauaji hayata isha mpaka tutakapo chukua nchi yetu
 
Nakuunga mkono Dokta, hata na mimi nilisikia hivyo hivyo ila sikupata tu ufafanuzi na nilisikia Askari yuko Mahututi sijui kweli au ni propaganda tu kama hizo zinazotumwa na hao wengine.
 
Back
Top Bottom