Rukwa: Amuua mjamzito na watoto wawili kwa deni la Tsh. 100,000

kila mmoja kwa imani yake alikumbuke taifa akiomba ,tuombee uchumi wa mtu mmoja mmoja maana ukiangalia chanzo kikuu cha mauwaji ya hivi karibuni ni uchumi ,,,watu hawana hela basi wanakuwa na hasira hasira na kwenye hasira ndipo yalipo makazi ya shetani 😭
 
Hata angekuja humu jf angesema anamdai mjamzito hiyo pesa tungemchangia na ingefika angepata pesa yake.. haya angalia anaenda jera bure kwa ajili ya pesa mbuzi laki moja.. JINGA TU
 
Hizi ni laana zinazolikumba Taifa baada ya kumuua mtu asiye na hatia.
Na bado tusibotubu na kusali ni mengi yanakuja, damu ya mwenye haki kamwe haiendi bure.
Na mbaya zaidi sijawah kumsikia Hangaya a.k.a Simba jike akimtaja Mungu hata kwa bahati mbaya.
Nilipenda toka miaka na miaka Tanzania kumtanguliza Mungu, utasikia Asalaam alyekum,Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristo, na mengineyo mengi. Ilikuwa salamu ya kuleta amani na watu kutambua kuna Mungu. Hata Marekani na ubabe wao, wanamtanguliza Mungu katika chochote utasikia "God Bless America" Ati siku hizi tunajifanya hatuhitaji kumtaja Mungu.

Mungu ni wa ajabu, ni Mungu wa sifa, umtajapo au kumuita tu kuna jambo ufanya. Ukijifanya mjanja Mungu ataondoa amani na kuleta vurugu. Sioni kiongozi mkuu wa nchi akikemea au kuongelea mauaji yanayo endelea. Kuwataka wananchi wafikirie maamuzi yao kwanza kabla ya hatua, na kumtanguliza Mungu mbele. Kiongozi wa nchi akisema jambo ufanya wananchi wake watafakari. Mpaka kufikia 2025 tutashuhudia mengi.
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili.

Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.

Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.

"Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyumbani kwa marehemu na kisha kufanya mauaji hayo na kutokomea," alisema Mallya.

Alisema polisi walipomuhoji sababu za kuwaua na watoto, alijibu kuwa aliamua kuwachinja kwa kuwa watoto hao walimuona wakati anamuua mama yao na pia wanamfahamu kwa kuwa mekuwa akienda katika nyumba hiyo mara kwa mara kudai fedha, hivyo wangemtaja.

Mapema wiki hii, jeshi hilo lilisema tukio hilo linadhaniwa kutokea usiku wakati mama huyo na watoto wake wakiwa ndani ya nyumba yao, kisha watu waliotekeleza mauaji hayo kuingia ndani.

NIPASHE

Mallya alisema mume wa mwanamke huyo ambaye yuko Dar es Salaam alianza kumtafuta mkewe kwa kumpigia simu, lakini ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Alisema alipopiga kwa muda mrefu simu hiyo ilizima, hali inayoonyesha kuwa ilizima kwa kuishiwa chaji na kila alipojitahidi kupiga haikupatikana.

Baada ya hapo alimpigia rafiki yake, Paul Leonard, na kumwagiza aende akaione familia yake na alifika nyumbani hapo saa 2:30 usiku na alishangaa kukuta mlango umefungwa nje kwa kufuli, hivyo aliamua kuwaita viongozi wa kijiji na walipofika na kubomoa mlango na kuingia ndani walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).
IGP Sirro alikwisha sema tuangalie majina tunayowapa tunaowazaa, na hii inathibitishwa natuhumiwa.
 
Nilipenda toka miaka na miaka Tanzania kumtanguliza Mungu, utasikia Asalaam alyekum,Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristo, na mengineyo mengi. Ilikuwa salamu ya kuleta amani na watu kutambua kuna Mungu. Hata Marekani na ubabe wao, wanamtanguliza Mungu katika chochote utasikia "God Bless America" Ati siku hizi tunajifanya hatuhitaji kumtaja Mungu.

Mungu ni wa ajabu, ni Mungu wa sifa, umtajapo au kumuita tu kuna jambo ufanya. Ukijifanya mjanja Mungu ataondoa amani na kuleta vurugu. Sioni kiongozi mkuu wa nchi akikemea au kuongelea mauaji yanayo endelea. Kuwataka wananchi wafikirie maamuzi yao kwanza kabla ya hatua, na kumtanguliza Mungu mbele. Kiongozi wa nchi akisema jambo ufanya wananchi wake watafakari. Mpaka kufikia 2025 tutashuhudia mengi.
Mimi naweza kusema Asalam aleikum au Bwana Yesu asifiwe na nikawa Shetani tuuuuu............
 
Tutangaziwe state of emergency ikibidi tujue maana kinachoendelea ni hatari sana.
Je, hapa tulipo bado ni sehemu salama kuishi?
 
Hizi ni laana zinazolikumba Taifa baada ya kumuua mtu asiye na hatia.
Na bado tusibotubu na kusali ni mengi yanakuja, damu ya mwenye haki kamwe haiendi bure.
Na mbaya zaidi sijawah kumsikia Hangaya a.k.a Simba jike akimtaja Mungu hata kwa bahati mbaya.
nani alimuua...............acha kujitafutia dhambi
 
Back
Top Bottom