Rukwa: Amuua mjamzito na watoto wawili kwa deni la Tsh. 100,000

Hi kitu isipo dhibitiwa itaendelea kuwa hbr za kawaida na hapo tutakuwakama rwnda na burundi watu wanachinjwa vibaya sna sijui watu wametoa wapi hi roho ya nmna hi
 
Wenye roho mbaya na chuki wanamtwisha lawama mkuu wa inchi, yaani haiingii hata akilini,
Chuki zitawamaliza
 
Ni msongo wa mawazo (stress). Kukosekana kwa msaada wa kisaikolojia kwa maeneo mengi, hivyo watu kukosa mwelekeo wanapoingia ktk changamoto
 
Najuuuuta kuisoma hii habari, imeniuma na imeniliza, nammuwazia huyo Mume jamani,

Eeeh Mola wangu tunaenda wapi sisi waja wako, tumekua makatili kuliko ukatili wenyewe
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawil
Huyu atakuwa wa Moshu akahamia huko kiutafutaji Mana jamaa huwa hawachezi na pesa Yao.
Yaani mchaga akikudai afu akachoka siku akija anataka tu roho yako hata Kama unamlipa Mara Mia ya anachokudai anakikataa yeye anataka roho yako tu na si mengine.
Big up sana sio wa kuwachezea ujue.
Hata hapa new York Kuna hotel moja kubwa inaitwaa kimario anayeijua aseme.
Sie acha tuchunge ng'ombe na kucheza ngoma. Marehemu pumzikeni kwa amani peponi.amina
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili.

Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.

Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.

"Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyumbani kwa marehemu na kisha kufanya mauaji hayo na kutokomea," alisema Mallya.

Alisema polisi walipomuhoji sababu za kuwaua na watoto, alijibu kuwa aliamua kuwachinja kwa kuwa watoto hao walimuona wakati anamuua mama yao na pia wanamfahamu kwa kuwa mekuwa akienda katika nyumba hiyo mara kwa mara kudai fedha, hivyo wangemtaja.

Mapema wiki hii, jeshi hilo lilisema tukio hilo linadhaniwa kutokea usiku wakati mama huyo na watoto wake wakiwa ndani ya nyumba yao, kisha watu waliotekeleza mauaji hayo kuingia ndani.

NIPASHE

Mallya alisema mume wa mwanamke huyo ambaye yuko Dar es Salaam alianza kumtafuta mkewe kwa kumpigia simu, lakini ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Alisema alipopiga kwa muda mrefu simu hiyo ilizima, hali inayoonyesha kuwa ilizima kwa kuishiwa chaji na kila alipojitahidi kupiga haikupatikana.

Baada ya hapo alimpigia rafiki yake, Paul Leonard, na kumwagiza aende akaione familia yake na alifika nyumbani hapo saa 2:30 usiku na alishangaa kukuta mlango umefungwa nje kwa kufuli, hivyo aliamua kuwaita viongozi wa kijiji na walipofika na kubomoa mlango na kuingia ndani walikuta mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane akiwa amechinjwa pamoja na watoto wake Milliam (8) na William (4).
Nimecheka utafikiri mazuri,ila aisee bila kuanzisha vitengo vya councelling na elimu ya saikolojia ,watu wengi watakufa na wengi kuishia jela..

Hapa ni mwanzo tuu tukiwa kama Nigeria ndio mambo yatazidi,watu wanaongezeka kwa Kasi na ugumu wa maisha unashika Kasi..

Rest in peace mjamzito .
 
Ndio umuue MKUU
Kila kinacho tokea kinatakiwa kiwe funzo kwetu tunaobaki ili kuepusha madhara, haiwezekani wewe unikopeshe kwa wema kabisa tena pengine baada ya Mimi kulia sana alafu siku unakuja kunidai nakukibu eti "sikukutuma unikopeshe" hilo ni jibu baya sana na kila mtu ana kiwango chake Cha mwisho Cha uvumilivu ukikutana na mvumilivu anaweza kutumia busara ila ukikutana na mtu asie mvumilivu unaweza hata kuuwawa kama ilivyo mtokea huyo dada.

Sawa alicho kifanya jamaa siyo kitu kizuri lakin pia wakopaji wajifunze kauli nzuri maana hujui mtu alitafuta alicho kukopesha kwa tabu kiasi gani na hujui muda aliokuja kuchukua chake ana shida kiasi gani alafu unaanza kumjibu kiduwanzi
 
Kila kinacho tokea kinatakiwa kiwe funzo kwetu tunaobaki ili kuepusha madhara, haiwezekani wewe unikopeshe kwa wema kabisa tena pengine baada ya Mimi kulia sana alafu siku unakuja kunidai nakukibu eti "sikukutuma unikopeshe" hilo ni jibu baya sana na kila mtu ana kiwango chake Cha mwisho Cha uvumilivu ukikutana na mvumilivu anaweza kutumia busara ila ukikutana na mtu asie mvumilivu unaweza hata kuuwawa kama ilivyo mtokea huyo dada.

Sawa alicho kifanya jamaa siyo kitu kizuri lakin pia wakopaji wajifunze kauli nzuri maana hujui mtu alitafuta alicho kukopesha kwa tabu kiasi gani na hujui muda aliokuja kuchukua chake ana shida kiasi gani alafu unaanza kumjibu kiduwanzi

Fact MKUU
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom