Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Leo kuna taarifa ya TCRA kuwapa adhabu ya kuwaomba radhi watanzania na watazamaji wa kipindi cha take one kinachorushwa na clouds tv kwa kukiuka maudhui ya utangazaji. Katika taarifa hiyo mkurugenzi wa vipindi wa kituo hicho Bw. Ruge Mutahaba anaonekana kusema kama wameonewa na anasema huenda wakakata rufaa.
Binafsi naona adhabu waliyopewa ni ndogo sana kwani hapa Tanzania hakuna sheria inayoruhsu ndoa za jinsia moja. Kwa walioona yale mahojiano na yule shoga watakubaliana na mimi kuwa ule ulikuwa ni "uhamasishaji" wa ushoga wala sio kupinga jambo hilo.
Yeye anasema jamii haitakiwa kuogopa kutaja jambo hilo hadharani. Lakini kama wangelenga kuifundisha jamii ubaya wa jambo hilo nadhani (na naamini ndo ingekuwa sahihi) wangetafuta mtu aliyewahi kujihusisha na jambo hilo halafu akaachana nalo na hivyo kipindi kizima huyo mtu angejikita kuelezea jinsi tabia hiyo ilivyombaya na kwanini yeye aliamua kuachana nayo, mabaya gani aliyopitia na mazuri gani anayo yaona baada ya kuacha "ushetani" huo. Hapo hadhira iliyokusudiwa huenda ingejifunza kitu kuliko walivyofanya kwa kumpa promo yule shoga na akaongea kwa kujiamini kabisa eti anapenda na mara nyingine anajiuza mwili wake na eti anatamani apewe mfadhili aweze kupandikizwa mimba!.. hivi kweli hapa Bwana Ruge hujaona mlipokosea tuu!?