Hakuna asiyefahamu kuwa haya mambo yapo na yapo tangu enzi na enzi. Ukisoma vitabu vitakatifu vya dini ikiwemo Biblia utakuta haya mambo yanazungumziwa ambapo ni ishara kwamba yapo tangu miaka maelfu mia huko nyuma, lakini hoja hapa ni kwamba: hivi kitu kibaya katika jamii huwa kinaelezewa kwa kukemea au kwa kujaribu kukipamba!?
Ukitafsiri maudhui ya kile kipindi, je, kilikuwa kinaikanya jamii kuachana na hiyo kasumba au kilikuwa kinaishawishi jamii kuona ushoga ni jambo la kawaida!? Kwa namna walivyohojiana, ni mashoga wangapi wangejiona wako njia mbaya na wanatakiwa kuacha na ni mashoga wangapi walifurahi na kujiona wako njia sahihi (tena wengine walimpongeza eti amejieleza vizuri na kwa kujiamin)!? Ukijaribu kutafsiri yale mahojiano, unadhani asilimia ya watu waliovutiwa na kuhamasika na ushoga huenda hata kutamani kuendelea au kuingia kabisa inalingana na waliohamasika kuacha!? TAFAKARI