Shemeji popote ulipo tafadhali rudi home Mzee wako anakuita.
Sasa kama muda muafaka wako wa kutafuta pesa ni usiku, unataka mke wa kukuchungia nyumba ama? Mi nataka uweke hausigelo ili ukirudi unakuta msosi na nguo zako zimefuliwa. No demands. Au unaonaje baba?
King'asti kutafuta kwangu usiku hakuniondolei haki yangu ya "kuoa".
Kurudi asbuhi, mchana, jioni ama usiku ni swala tu la ratiba.
Sasa kilichomuondoa kwako hakirekebishiki. Unamtaka arudi ili akubaliane na hali ama? Let her go, atapata asieyetafuta hela gizani. Na wewe tafuta asiejali kulinda fenicha zako. Simple!
King'asti!!! Wahenga walinena
Mvumilivu hula mbivu. Kwanini asizisubiri mbivu
Mchumia juani hulia kivulini. Kwanini asikisubiri kivuli. Machungu yote yatakwisha.
Kila mwenye mafanikio, kuna magumu aliyoyapitia.
Rudi nyumbani mama. Hizo no changamoto tu.
Hahaha weeh hizo chai za 19kweusi usimuuzie dada wa watu! Nuie mkikamata mkwanja mnashikika sasa? Atakaa hapo juani na wewe ukichuma, saa ya kuvuna unatafuta wasio na sunburn wenye ngozi mororo wa kula nao vinono hehehe. lara 1 njoo umueleweshe huyu.