TANZIA RPC wa TABORA ACP Richard Abwao afariki dunia

TANZIA RPC wa TABORA ACP Richard Abwao afariki dunia

Hapa Duniani tunapita.. Tusivimbe kwa kiburi na tusiache kutenda Mema..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao atakumbukwa.

=====

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao amefariki dunia leo Juni 20, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Jijini Dar es salaam wakati akipatiwa matibabu.

Akizungumza na AyoTV, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amesema “Ni kweli aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao, amefariki dunia leo Juni 20, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.”

DCP Misime ameongeza kuwa taratibu nyingine zinazohusiana na msiba huo zitatangazwa baadaye.

RIP Kamanda Abwao.
Nawahurumia ndugu na marafiki wa marehemu, lakini katika Taifa letu kwa sasa polisi kama binadamu wametumika isivyo.
Wananchi wamejenga hisia hasi katika utumishi wao.
Serikali ina mzigo wa kuwatenganisha polisi kiutendaji na siasa.
 
Ni heri yeye aliyefariki mwili wake umeonekana na anazikwa kwa heshima na Taasisi aliyoitumikia, ndugu, jamaa na marafiki. Mimi nawewe hatujui mwisho wetu. Tusiseme tukamaliza na kujifanya ni watakatifu sana kuliko wengine. Anayejua wema au ubaya wako ni Mungu aliyekuumba.🙏
 
Back
Top Bottom