RPC wa Mbeya Benjamin Kuzaga asema “Pikipiki zilizokabidhiwa Polisi zitumike kwa malengo yaliyowekwa”

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Wakaguzi wa Kata nane wa Mkoa wa Mbeya wamekabidhiwa Pikipiki aina ya Boxer kwa ajili ya kurahisisha na kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao katika Kata zao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki hizo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Disemba 03, 2023 katika Uwanja wa FFU Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutambua umuhimu wa vitendea kazi katika kufanikisha utekelezaji wa kazi mbalimbali kwa wakaguzi wa Kata.

PICHA 02.jpg

PICHA 03.jpg

Aidha, Kamanda Kuzaga amewataka Wakaguzi Kata hao walipata mgao wa Pikipiki hizo kuhakikisha wana kwenda kuzitumia kwa malengo yaliyowekwa na Jeshi la Polisi hasa la utoaji wa elimu ya ulinzi na usalama.

Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rungwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Philipo Mhako amemshukuru kupata Pikipiki mbili ambazo zitakwenda kutatua changamoto ya usafiri kwa wakaguzi kata kutoka na baadhi ya maeneo kutokufikika kwa urahisi.
PICHA 01.jpg

Mkaguzi Kata ya Madibila iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Julius Mongo ameahidi kutumia Pikipiki hiyo kuwafikia wananchi katika maeneo ya vijijini na kwenye vitongoji na kutoa elimu pamoja na kutatua kero mbalimbali za kiuhalifu na kijamii.

Jumla ya Wakaguzi nane wa Kata za Lufilyo na Masuku zilizopo Wilaya ya Rungwe, Kata ya Matema Wilaya ya Kyela, Kata ya Matwiga na Kambikatoto Wilaya ya Chunya, Kata ya Ikukwa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi na Kata ya Madibila Wilaya ya Mbarali wamekabidhiwa Pikipiki awamu hii ya kwanza.
 
View attachment 2832117
View attachment 2832118
Aidha, Kamanda Kuzaga amewataka Wakaguzi Kata hao walipata mgao wa Pikipiki hizo kuhakikisha wana kwenda kuzitumia kwa malengo yaliyowekwa na Jeshi la Polisi hasa la utoaji wa elimu ya ulinzi na usalama.

Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rungwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Philipo Mhako amemshukuru kupata Pikipiki mbili ambazo zitakwenda kutatua changamoto ya usafiri kwa wakaguzi kata kutoka na baadhi ya maeneo kutokufikika kwa urahisi.
View attachment 2832119
Mkaguzi Kata ya Madibila iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Julius Mongo ameahidi kutumia Pikipiki hiyo kuwafikia wananchi katika maeneo ya vijijini na kwenye vitongoji na kutoa elimu pamoja na kutatua kero mbalimbali za kiuhalifu na kijamii.

Jumla ya Wakaguzi nane wa Kata za Lufilyo na Masuku zilizopo Wilaya ya Rungwe, Kata ya Matema Wilaya ya Kyela, Kata ya Matwiga na Kambikatoto Wilaya ya Chunya, Kata ya Ikukwa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi na Kata ya Madibila Wilaya ya Mbarali wamekabidhiwa Pikipiki awamu hii ya kwanza.
Safi kabisa, wamewarahisishia usafiri wa kwenda kusachukulia vimada wao pamoja na kufanya ziara na doria za kukusanya rushwa mtaani.
Hongera kwao.
 
Back
Top Bottom