RPC Mwanza: Heche na Msigwa walitakiwa kutoa taarifa kwangu kuwa wanaingia Mwanza na watafanya shughuli zao hapa

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
RPC-Mwanza, SACP Ramadhan Ngh'anzi anasema John Heche na Peer Msigwa kuwa walipaswa kutoa taarifa kwake kuwa wanaingia Mwanza na watafanya shughuli zao hapo. RPC hajui lolote kuhusu "uhuru wa mtu kwenda atakako" (ib.17) katiba ya JMT, sheria ya 1984, Na. 15?

Au Mwanza siyo Tanzania?
 
LOoo, imekuwa hivyo tena?

Hii ni kwa viongozi wa CHADEMA pekee, au vyama vyote vya siasa?

Nchi hii sasa inaelekea kwenye mlipuko, maana 'pressure' inazidi kuongezeka tu kila mara!

Hii 'pressure' ni lazima ipate njia ya kutokea, haiwezi kuongezeka bila mwisho wake kutokea.
 
1626574164920.png
 
Ni pale vigezo vya ukatili na kuvunja katiba, sheria na haki vinapotumika kumpa askari cheo matokeo yake ndip hayo.
rpc mwanza.png

Sasa fikiria huyu afande ni RPC, je tutegemee nini kutoka kwa makoplo na vyeo vya chini huko polisi? Yeye apewe taarifa kama nani na kwa sheria ipi?

Nani anawapa hawa vyeo vinavyowazidi kimo, je ni CCM? Hii ndiyo sababu kubwa kwa nini madai ya Katiba ni ya msingi kabisa ili tuutokomeze huu ujinga!
 
Kuna maRPC wana akili za kitaahira.

Yaani watu wanaenda Mwanza kwa shughuli zao binafsi halafu wampe yeye taarifa ili iweje?

Huyo RPC alijua wakina Msigwa na Heche wako Mwanza, alitaka nini tena?
 
RPC mpuuzi sana ,yaani anataka kusema ni lazima uombe ruhusa kwa ma RPCs ukitaka kwenda mkoa wowote ndani ya TZ?
 
Mkuu: " ebana fanya ufanyavyo mkutano huo usifanyike .

RPC:" lakini mkuu wana haki ya kufanya mkutani, hata mama analijua hilo nawaambiaje wananchi"

Mkuu:" we naona kazi imekushinda ni eidha unafanya au tutengue huu uteuzi wako!!"
Baadae
"John Heche na Peer Msigwa walipaswa kutoa taarifa kwangu kuwa wanaingia Mwanza na watafanya shughuli zao hapo" RPC
😁😁
 
Back
Top Bottom