Wito: Ibara ya 18 ya Katiba iheshimiwe na wote! Kusifu na kupongeza ni haki, kupinga na kukosoa pia ni haki - si uadui, si chuki, si kinyume!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya Leo
Screen Shot 2022-11-27 at 10.28.54 AM.png

Screen Shot 2022-11-27 at 10.29.38 AM.png

Kwa Maslahi ya Taifa" ya leo inajikita kwenye Ibara ya 18 ya Katiba kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, yetu ya JMT ya mwaka 1977, kuanzia Ibara ya 18 – 24, katiba yetu imetoa haki zifuatazo: 18. Uhuru wa Maoni. 19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo. 20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine. 21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma. 22. Haki ya kufanya kazi. 23. Haki ya kupata ujira wa haki. 24. Haki ya kumiliki mali.

Haki hizi sio hisani sio huruma, sio option, kusema zinaweza kutolewa au laa!, haki hizi ni stahili, zinapaswa kutolewa na kuheshimiwe na Watanzania wote ikiwemo serikali na viongozi, na taasisi zote. Kwa leo nitajikita zaidi kwenye Ibara ya 18, inasema

18: Uhuru wa Maoni Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6"

(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa kutoingiliwa kati mawasiliano yake.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Haki hizi na uhuru huu wa kutoa maoni, unakwenda sambamba na mipaka ya kawaida ya uhuru, yaani hakuna uhuru usio na mipaka, mwisho wa uhuru wako ni pale uhuru wa mtu mwingine unapoishia. Huu uhuru wa kutoa mawazo yako, unapaswa kuheshimiwa na wote, hata kama hukubaliani na mawazo hayo, na wewe pia unapaswa kuheshimu uhuru, maoni na mawazo yaw engine, hata kama hukubaliani nayo

Leo nimejikita kwenye ibara hii, kufuatia juzi kati hapa, kuna mtu ametoa mawazo yake kuhusu jambo fulani, mtu huyo ameshambuliwa kila kona kwa kushukiwa kama mwewe anavyotaka kunyakua kifaranga cha kuku, wengine wakimbeza, wengine wamdhihaki na wengine hata kufikia kiwango cha kumtukana na kumdhalilisha!

Kilichopelekea mtu huyo kushambuliwa, ni kwa sababu tuu amekosoa jambo fulani!. Kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa

Toka enzi za Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete na Rais Magufuli, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki iwe na haki ya kusifu tuu na kupongeza tuu, lakini kukosolewa iwe nongwa, ni kosa, ni dhambi!.

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.



Kukosoa serikali, sio kosa, wala ukosoaji, sio uadui, sio chuki, na sio dhidi ya serikali, ukosoaji wa serikali ni differing opinion ambao pia ni haki ns

na unalindwa na katiba, amlimradi ukosoaji huo uwe ni ukosoaji unaofanywa kwa nia njema ya kuisaidia kujenga nchi, kuisaidia serikali na kuwasaidia viongozi, ambao unaitwa constructive cricism, ukosoaji wenye nia ya kujenga na kusaidia, ambao huendana na ushauri wa njia bora ya kufanya hilo jambo unalokosoa. Ukosoaji mbaya ni ule wa kubagaza, kuzodoa, kutumia lugha za kuudhi, kutukana na kudhalilisha.

Kwenye Freedom of expression ni haki kwa wote,wenye kusifu na kupongeza, wana haki ya kusifu na kumpongeza kwa kuupiga mwingi, na wenye kukosoa wana haki ya kukosoa, hivyo haki ya kusifu inakwenda sambamba na haki ya kukosoa, ibara ya 18 ya katiba inataka haki ya kusifu iheshimiwe na haki ya kukosoa pia iheshimiwe.

Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia zaidi kuliko wanaomsifu kwa kuupiga mwingi!, huku tukiwaomba viongozi wetu, wazidishe kungumusha (kuzifanya ngozi zao kuwa ngumu), ngozi zao kwa kufuata msemo wa kizungu wa “take the bitter with the sweet”, kama wanavyofurahia kidonge kitamu kwenye matamu na mazuri, pia wawe tayari kupokea vidoge vichungu kwenye machungu, ila pia utafiti wa dawa, umethibitisha vidoge vichungu ndio vinatibu homa, ili upone lazima ukubali kumeza kidonge kichungu. Viongozi wetu wawe na ngozi ngumu, kumeza vidonge vyote vitamu na vichungu!, upinzani sio uadui, kusifia sio kosa, sio dhambi na sio kupenda, na kukosoa sio kuchukia, sio uadui sio dhambi!, kuna wanaompenda sana Mama na wanamkosoa kwa mapenzi mema ili asishindwe!.

Wasalaam
Paskali
 
Kwa umri wako unabidi kupambana ili uache Legacy na sio kusifu na kuabudu wanasiasa .

kama umeishi USA
CANADA
miaka kibao na umeshindwa kutoboa don't expect any changes from praise and worship.

50+ ni miaka ya kuhakikisha unaacha athari chanya na sio kufanya Kazi za kusifu wanasiasa with an empty plate.
 
Hana ubora wowote.

Tangu alipopigwa mkwala na Magufuli aliufyata akabaki kupiga mapqmbio tu kwa utawala dhalimu wa Magufuli.

Mbona hakutoka front wakati huo kudai hii haki muhimu wakati ule wa kutawaliwa gizani?
 
Kusifu na kupinga zote ni haki, muhimu haki hizo zizoeleke, watu wasigandishwe kujua kusifu tu kwasababu anayesifiwa ni wa chama chenu, na kuacha kazi ya kupinga ifanywe na wapinzani pekee, huko ni kujidumaza akili.
 
Watu wanatakiwa tu kuwa objective.

Ukisifia onyesha huo uzuri unaousifia na sisi kweli tuthibitishe.

Na ukikosoa onyesha ni kwanini unakosea lakini pia toa ushauri nini kifanyike ili kuboresha.

Shida kubwa ni kwamba, uwezo wa kuwa objective inahitaji mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kufikiria na kuchanganua mambo.

Otherwise kama mtu unakosa kuwa objective halafu hapo hapo unasifia au kukosoa, lazima uonekane ni mwehu
 
Wanao sifu na wanao kosoa wote wako sawa maana katiba iko wazi kabisa mbaya zaidi mambo yote mawili hutafsiriwa tofauti na viongozi wetu.

"Serikali iliyo wekwa na watu na ambayo inawatumikia watu haiwezi kupotea daima"
 
Mimi naona hakuna shida kwani Dkt. Bashiru alikuwa anakosoa namna ya kusifu. Ila kumiminiwa risasi au kufukuzwa kazi baada ya kukosoa ndio kuheshimu katiba? Labda makala hii ingetolewa wakati ule wa tukio la Dodoma na la yule mfanyakazi wa TRC ili kuonesha uhuru wa mwandishi.
 
Mimi naona hakuna shida kwani Dkt. Bashiru alikuwa anakosoa namna ya kusifu. Ila kumiminiwa risasi au kufukuzwa kazi baada ya kukosoa ndio kuheshimu katiba? Labda makala hii ingetolewa wakati ule wa tukio la Dodoma na la yule mfanyakazi wa TRC ili kuonesha uhuru wa mwandishi.
Mkuu Mwanamayu, naomba hilo tukio la Dodoma, ila makala hii ni kuhusu uhuru wa kutoa maoni, mtu akipongeza aheshimiwe, na akikosoa pia aheshimiwe, hivyo huu ni wakati muafaka kabisa kwa makala hii.
P
 
Asante sana Mkuu Lee, nimedhamiria kujikita kwenye utetezi wa latiba na haki za binaadamu, watu watendewe haki na sisi tutendeane.
P
Kama mwandishi mbobezi na Wakili msomi kujikita katika utetezi wa katiba na haki za binadamu ni jambo jema sana na linalo hitaji pongezi.
Tatizo mada uliyo chagua ni dhaifu sana, haki ya kusifu na kukosoa.
Mada dhaifu kama hizo waachie kina Etwege & Co na wewe tafuta mada nzito nzito utuletee

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom