peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,799
21,396
Sasa nimejifunza na kutambua kauli inayosema ‘ ni kauli za kisiasa’.

MaRPC wa mikoa ya Arusha na kilimanjaro wameamua kupuuza kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mh Kinana kwa kufungulia trafic wa kutosha ndani na nje ya miji.

Idadi ya matrafiki bara barani imezidi tena na mijini wanazunguka kama nyuki bila kujali maeneo muhimu ya kukaa na kukusanya chao mapema na kurudi makao.

Tuliwapigia RPC Arusha na Kilimanjaro kuwaulizia kuhusu kauli ya Mh. Kinana walijibu kwa nyakati tofauti kuwa wao sio wasemaji wa jeshi la Polisi.

Ombi : Jeshi la polisi litii bila shuruti kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CCM. Comred Kinana.
 
Wengi wa Madereva wanaolalamika ni wale wasiofuata Sheria na Taratibu zilizowekwa, ukiwa na gari lililokamilika na wewe mwenyewe umekamilika ikiwemo kuendesha gari kwa kufuata Sheria za uendeshaji hakuna trafiki atakayekusumbua.
 
Kinana ni mwanasiasa, ni WA kupuuzwa.

Idadi ya AJALI nchini imeongezeka sana Hadi Rais amehoji kwann!!!!!

Kama suala ni RUSHWA watafute njia za kuwabana TRAFIC wasipokee RUSHWA .

Kinana apumzike tu kama wastaafu wengine akina Odinga!!!!
 
Kinana hawezi kuelekeza jeshi la polisi jinsi ya kudhibiti ajali za barabarani mbinu hizo ni za jeshi la polisi swala la kupunguza traffic barabarani aliliongea kisiasa kwa hiyo ni wakuupuzwa.
 
Kisheria Kinana hana mamlaka ya kumuagiza RPC

Kinana alitoa Ombi na siyo agizo

Ndio maana alisema "Namsihi IGP apunguze Askari wa usalama........

Sasa hizo nasaha zake Viongozi wa polisi wana uamuzi wa kupima kwanza usalama na kufanya maamuzi sahihi siyo kwa kukurupuka.
 
Hata kama sitopenda trafiki barabarani lakini kauli ilibidi itolewe na serikali. Sio kinana Wala shaka, ccm wajiheshim.
 
Hao jamaa hawako kwa ajili ya kuhakikisha Sheria za Barabarani zunafuatwa,Barabara ni Migodi yao ya kuvuna.

Unakuta Vibao vya 50kph vimeng'olewa na wanajua, hawafanyi juhudi zozote za kurudisha ishara na vibao, ila kazi ni kuwinda Madereva kutishia kuwapiga faini mpaka 'wakunjiwe' Misimbazi.
 
Hao jamaa hawako kwa ajili ya kuhakikisha Sheria za Barabarani zunafuatwa,Barabara ni Migodi yao ya kuvuna...
Kinana ana UADILIFU na USAFI kiasi Gani kuwakemea matraffic??

Kama mizigo yake inakwama kupita atajijua mwenyewe!!!

Kwanza alitoka hadharani na kuomba astaafu, kurudi kwake kazini ni Amejivua gamba kama nyoka,??

Apuuzwe tu!!!!!!
 
Nilikuwa porini huku nilipoona taarifa ya kinana,jana nikaenda wilayan kwetu nilishangaa kuona mpaka huku kwetu trafik wamepunguzwa barabaran,
 
Sasa nimejifunza na kutambua kauli inayosema ‘ ni kauli za kisiasa...
Kikodi cha usalama barabarani ni mradi wa wakubwa huko polisi. Kuanzia chini hadi makao makuu ya polisi.

Kuwapunguza barabarani ni kupunguza mshiko wa wakubwa.

Kwa mikoa iliyo tajwa ambayo nami ni mdau wa mikoa hiyo naungana na mleta mada kwamba trafiki wamerudi barabarani kwa wingi mnooo.

Yaani hutembei mita 500 bila kupigwa mkono.

Shughuli zimerudi kama kawaida. Makusanyo kwa kwenda mbele
Huwezi tenganisha polisi wa Tanzania na rushwa.

Arusha tuna high way ya kutoka Sakina hadi Tengeru na tahadhari zote za waenda kwa miguu na baiskeli hii barabara ilijengwa kwa lengo la kupunguza foleni barabarani, lakini jamaa zetu polisi jujificha kwenye maua kupiga tochi. Yaani maana ya highway tena yenye double road ina potea.

Viongozi wapo wana ona lakini wako kimya.
 
Wengi wa Madereva wanaolalamika ni wale wasiofuata Sheria na Taratibu zilizowekwa, ukiwa na gari lililokamilika na wewe mwenyewe umekamilika ikiwemo kuendesha gari kwa kufuata Sheria za uendeshaji hakuna trafiki atakayekusumbua.
Hivi kama gari imekamilika trafiki ana kosa cha kukuambia? Au nawe ni mtembea na miguu kama mimi?
 
Kinana ni mwanasiasa, ni WA kupuuzwa.

Idadi ya AJALI nchini imeongezeka sana Hadi Rais amehoji kwanini...
Taja mji mmoja ambao ajali zimetokea mjini.!! /acha kutetea mambo ya ajabu.
Kinana hakuongelea magari ya nje ya mji. Bali ali zungumizia mijini.

Huko nje ya miji kuna utaratibu wake. Jaribuni kuelewa mtu akiwa ana toa maoni.

Au nawe ni muathirika wa kuto kupata hongo?
 
Sasa nimejifunza na kutambua kauli inayosema ‘ ni kauli za kisiasa’.

MaRPC wa mikoa ya arusha na kilimanjaro wameamua kupuuza kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mh Kinana kwa kufungulia trafic wa kutosha ndani na nje ya miji.

Idadi ya matrafiki bara barani imezidi tena na mijini wanazunguka kama nyuki bila kujali maeneo muhimu ya kukaa na kukusanya chao mapema na kurudi makao.

Tuliwapigia RPC Arusha na Kilimanjaro kuwaulizia kuhusu kauli ya Mh. Kinana walijibu kwa nyakati tofauti kuwa wao sio wasemaji wa jeshi la Polisi.

Ombi : Jeshi la polisi litii bila shuruti kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CCM. Comred Kinana.
Ni nchi nzima Mkuu, majuzi tumetoka Mbeya kuja Dar, tumesumbuliwa sana njiani na hasa Mafinga hadi Iringa tumesimamishwa zaidi ya mara 6, shida ni kwamba wanatafuta rushwa for 0 offenses
 
Taja mji mmoja ambao ajali zimetokea mjini.!! /acha kutetea mambo ya ajabu.
Kinana hakuongelea magari ya nje ya mji. Bali ali zungumizia mijini. Huko nje ya miji kuna utaratibu wake. Jaribuni kuelewa mtu akiwa ana toa maoni.
Au nawe ni muathirika wa kuto kupata hongo?
Kinana kutetea raia ni hadaa tu, Hana UADILIFU kutetea chochote.

Wangekuwa na Nia thabiti wangeharakisha mchakato wa KATIBA mpya Ili mifumo ifanye KAZI vizuri kuzuia Traffic kupokea RUSHWA.

Mm bado siezi NASA ktk mtego wa kipuuzi kama huo,Eti kinana alete ufumbuzii!!!!!
 
Back
Top Bottom