Rostam ni Mfalme na mwamba hapa Tanzania

Sasa Taifa gesi wanakwenda kuwa provider wa energy kwa kila mtanzania masikini na Tajiri. Ila tuwe positive jamani Rostam ni mwamba yeye anafit kwa kila Rais...
Ni mwamba kwelikweli mzee wa dowans/richmond...bado hatujasahau. watoto kama wewe ndiyo hamjui hili
 
Sasa Taifa gesi wanakwenda kuwa provider wa energy kwa kila mtanzania masikini na Tajiri. Ila tuwe positive jamani Rostam ni mwamba yeye anafit kwa kila Rais...
Jamaa hatumii emotions kwenye biashara.
 
Lobbying, ni jambo la kawaida na katiba yetu mpya liwekwe wazi ila sio apendelewe kuliko Lake Gas na wengineo.

Yeye ni Mfanyabuashara anaangalia profit sisi Wananchi nao tunaangalia affordabilty.

Anaewahi ndio hupata, deal hizo haziji kwa bahati mbaya watu wameandika wamelobby zimefiki na fursa waliiona wakaona gap lipo sasa unataka iweje zaidi?

Msianze kulialia tu maana Taifa Gas alijipanga mapema kila wilaya anakituo cha kujazia Gas sasa aliplan muda mrefu afike vijijini na kweli kafika wale uliokua ukisafiri unaona depot za mihan gas na sasa zimebadilishwa zinaitwa Taifa Gas ndio hao hao, cha kufanya serikali imuondolee kodi na imuwezeshe kusambaza nchi nzima na zimamoto kila mkoa na wilaya wajipange kuwaelekeza watanzania jinsi ya kutumia kwa ufasaha Gas ili isilete shida, ili hata Bibi yetu wa kule kigonsera au hanga mwanasteri au mputa au kwenda na kaisho au nyambiti au dareda atumie nishati salama kwa ufasaha na kuokoa muda wake
 
Hii gas inayozungumziwa hapa ni ya majumbani ya kupikia?

Ndio mfano wa hizi.

IMG_0726.jpg

IMG_0727.jpg

IMG_0728.jpg

Ni mfano kama huo hapo
 
Anaewahi ndio hupata, deal hizo haziji kwa bahati mbaya watu wameandika wamelobby zimefiki na fursa waliiona wakaona gap lipo sasa unataka iweje zaidi?...
Ninachojua mimi serikali sio wajinga hawawezi kuifanya Taifa Gas kuwa sole distributor wa gas nchi nzima.

Tunahitaji competition kwenye utoaji wa huduma ili kuongeza ubora wa huduma na price stability

Pili hivi wakimwondolea kodi huoni kuwa makampuni mengine yatakufa kama Oryx gas, Lake gas n.k. Unafikiri serikali itapoteza kodi kiasi gani kutoka kwa makampuni hayo? Na wangapi watapoteza ajira?

Acha kuandika mambo kwa mihemuko
 
Kuna wakati Rostamu alituhumiwa kuwa gamba ndani ya CCM lililotakiwa kuvuliwa...najua chawa humu ndani si rahisi kukumbuka zama hizo. Alipoona CCM haina dira Rostamu mara moja akachukua hatua kuachana na ujinga wa alichodai ni siasa za maji taka. Alisema kaeni na chama chenu hicho na kweli akaachia hadi ubunge!

Huyo ndiye Rostamu. Kuna wakati Pinda mwenyewe alionya bungeni kwamba mafisadi ndani ya CCM wana nguvu za ajabu na wakishughulikiwa nchi itayumba. Je wangapi wanamkumbuka kijana moja wa CCM, Napee Nnauye? Huyo alivalia njuga swala la CCM kujivua magamba matatu...Rostamu, Lowassa na Chenge!

Yaani hapa nilipo nacheka, nikikumbuka Kagoda, Richmond na CCM hiyo hiyo ya Kikwete, Magufuli na King Maker Rostamu! Magufuli alijipima nguvu na Rostamu akajikuta ana nguvu za soda. Haikuchukua muda Rostamu huyo akatinga Magogoni Ikulu na kukakribishwa kama mfalme aliyerejea! Chezea King maker Rostamu!

1667291943372.png
Hakika nawaambia chawa popote mlipo, hamuijui CCM na tuliobahatika kuijua tunakaa nayo mbali kama ukoma. Nguvu aliyorudi nayo Kingmaker safari hii inatisha na kaikuta CCM iko pale pale anapopahitaji. Kakuta gari lipo kama halina dereva, halijui linakotoka wala linakoelekea...masikini Tanzania, tutafika tumechoka sana.

1667292022346.png

Naachia hapo!​
 
Hakika
Tusikubali awe na Monopoly kwenye gas, na pia tusikubali hawa Matajiri waungane dhidi yetu, kama Makampuni haya ya Simu za mikononi yanayotutesa na bei za Bando.


Soko la Nishati liwe huria ili tuwe tunachagua ya bei nafuu.
 
Back
Top Bottom