Rostam - Kuisambaratisha Tanzania (?)

Rostam - Kuisambaratisha Tanzania (?)

"Kwa ugonjwa huu; nitakufa.. Watanzania wale watalia sana.., nitawaombea kwa Mungu"
Ndugu wanaJF nimeona nianze kwa kunukuu sehemu ya maneno ya Baba wa taifa katika siku zake za mwisho pale St Thomas...
Wacha kamba wewe, unadhani si wajinga hapa, ulikuwepo wakati Nyerere anakufa ukanukuu maneno hayo?
 
Mkuu unahakika kama RA si mtanzania? Au kuwa na rangi isiyo nyeusi maana yake si mtanzania, au kuwa na asili ya Iran maana yake ni M-iran? Kama asingekuwa mtanzania sidhani hata kama angekuwa mbunge.

Ni kweli aliingia Tanzania mwaka 1979....baada ya Shah kupinduliwa
 
mmmmh tukileta habari ya umemwaga mboga ...mimi namwaga ugali uchaguzi wa 2010 utakuwa hatari.....sijui tufanyeje maana hatujui mapadri na wakatoliki/wakristo wata react vipi kama kampeni za kishenzi za udini zitaendelezwa
mix with yours
 
Wacha kamba wewe, unadhani si wajinga hapa, ulikuwepo wakati Nyerere anakufa ukanukuu maneno hayo?

Mwaka aliyokufa nyerere ulikuwa umezaliwa? samahani kwa swali langu....kwa sababu kauli hii ilizungumzwa sana na waliokuwepo na baba wa taifa alipokuwa ST Thomas kupitia vyombo vya habari. .....
mix with yours
 
Great thinking Ramos. Hii ndo habari ambayo Watanzania tunatakiwa tuizingatie kwa tahadhari kubwa sana. Uongozi wa CCM ambao pia umeshikilia dola hivi sasa unatumikia matakwa ya global mafia. Katika mazingira ya namna hii tusahau kufanikisha vita dhidi ya ufisadi pia tusahau kabisa kitu kinachoitwa maendeleo ya dhati; tubakie kusikiliza porojo na takwimu za uongo ilihali maisha yetu yakiendelea kuwa mashakani katika kila fani. Tunachotakiwa kufanya ni kuisadia CCM kwa ama kuung'oa mtandao wa mafia toka ndani mwake au kuiondoa CCM toka madarakani na kuushughulikia mtandao wa mafia kikamilifu. Ni vita kubwa hii.

RA ana nguvu ya ajabu na kibaya zaidi ameishika CCM pale pabaya - sidhani kuna mwana CCM yeyote anayeweza kumnyooshea kidole RA mtandao wake, mwalimu angeweza - na kwa hili tutamkumbuka milele.

Solution ni moja tu - kuwaondoa CCM na serikalini hii madarakani mwezi October - NDIYO inawezekana.
 
Nimegundua kumbe adui yetu namba moja kama taifa ni ujinga, na ndani ya ujinga huo kimezaliwa kitu kinaitwa udini. Ninavyofahamu ni kuwa jambo la dini ni suala binafsi kati ya mtu na muumba wake( kama ana amini kuwa yupo) ndiyo maana katiba yetu pamoja namapungufu inaelaza wazi jambo hili, Ibara 3 (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia isiyokuwa na dini..., Ibara ya 19 (2) Kazi ya kutangaza dini,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa jambo huru la hiari la mtu binafsi..... .Leo hii tunapoona watu wanaleta hisia za udini kwa nia ya kuwagawa watz tunashindwa kuwaelewa. Jambo hili naliona ni mkakati mahsusi wa baadhi ya vyombo vya dola , ukiwa na nia ya kuwagawa watz kwa misingi ya dini ili wakose nguvu ya pamoja ya kukabiliana na genge la watawala.Natoa wito kwa wapenda nchi wote wasiingie kwenye mtego huu wa kidhalimu. Hakuna mtu yoyote katika nchi hii anayeweza kunufaika kimaendeleo kwa kuwa tu mtu anayetawala ni wa dini yake, tutapata maendeleo tu kwa kupata viongozi wazalendo wenye uchungu na nchi yetu. Watanzania tuamke tuache ulevi wa mawazo ya udini.
 
Rostam na El wana mpango kamambe wa kumng'oa Sitta Urambo. Sitta analijua hili na linampa hofu sana. Sitta kakalia kuti kavu. Wana Urambo mwokoeni Sitta arudi bungeni
 
Ramos,

Sio Rostam pekee, hata Kikwete anahusika kwenye mpango wa kuisambaratisha Tanzania
 
Mkuu unahakika kama RA si mtanzania? Au kuwa na rangi isiyo nyeusi maana yake si mtanzania, au kuwa na asili ya Iran maana yake ni M-iran? Kama asingekuwa mtanzania sidhani hata kama angekuwa mbunge.
Bongolander,'
Nina habari za uhakika kuwa kampeni ya uraia wa nchi mbili ilianzishwa na Rostum Aziz. Bila shaka huyu bado anayo pasipoti ya Iran.
 
Wacha kamba wewe, unadhani si wajinga hapa, ulikuwepo wakati Nyerere anakufa ukanukuu maneno hayo?

OK. Wenzako wanalipwa kuwasapoti mafisadi. Angalie usije ukawa unajitolea...
 
Nimegundua kumbe adui yetu namba moja kama taifa ni ujinga, na ndani ya ujinga huo kimezaliwa kitu kinaitwa udini. Ninavyofahamu ni kuwa jambo la dini ni suala binafsi kati ya mtu na muumba wake( kama ana amini kuwa yupo) ndiyo maana katiba yetu pamoja namapungufu inaelaza wazi jambo hili, Ibara 3 (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia isiyokuwa na dini..., Ibara ya 19 (2) Kazi ya kutangaza dini,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa jambo huru la hiari la mtu binafsi..... .Leo hii tunapoona watu wanaleta hisia za udini kwa nia ya kuwagawa watz tunashindwa kuwaelewa. Jambo hili naliona ni mkakati mahsusi wa baadhi ya vyombo vya dola , ukiwa na nia ya kuwagawa watz kwa misingi ya dini ili wakose nguvu ya pamoja ya kukabiliana na genge la watawala.Natoa wito kwa wapenda nchi wote wasiingie kwenye mtego huu wa kidhalimu. Hakuna mtu yoyote katika nchi hii anayeweza kunufaika kimaendeleo kwa kuwa tu mtu anayetawala ni wa dini yake, tutapata maendeleo tu kwa kupata viongozi wazalendo wenye uchungu na nchi yetu. Watanzania tuamke tuache ulevi wa mawazo ya udini.

Ndugu yangu Douglas Sallu, moja ya mambo magumu kuyajadili na yenye utata, malumbano, kelele na hisia tofauti ni pamoja na dini kuhusianishwa au kutohusianishwa na siasa.Ingawa ni wazi sana kuwa siasa za sasa duniani zinatawaliwa sana na kile kinachoendelea mashariki ya kati. Kubwa katika hilo ni uhusiano wa wa waizraeli na waarabu amboa kila mtu anatetea imani yake, na utetezi wa imani hizi umevishwa sura ya siasa.Mfumo wa maisha ya mtu ni pamoja na imani yake;ukisiakia kwa mfano hawa ni wazee wa kisukuma, ujue ngosha hawa ni wazee wanoshikilia matambiko na miiko ya kisukuma.Tofauti inayojitokeza ni viwango vya kuamini na kuishi sawa sawa na matakwa ya dini husika.UDINI HAUZALIWI NA UJINGA, WENYE UDINI WANAJUA WACHOKIFANYA.

Siyo sahihi na busara kilipuuza hili, wenye udini hupiga kelele kuonyesha watu wengine ndiyo wenye udini, mwizi kila wakati huogopa kuibiwa, mwnaume kiwembe huwa anamashaka juu ya mkewe hapendi atembee tembee kuhofia atemegwa kirahisi kama yeye anavyomega wanawake wengine.

Hawa wanaoandika wenzao kuwa wanategemea watu wadini zao, mfano katoliki iwachague, ndio wenye udini mioyoni mwao ndio maana waliopsikia Dr Slaa anagombea cha kwanza kutoka kwenye mawazo yao kikawa dini, ili wajaribu kuziba wanachokifanya wao.Mwenye macho haambiwi tazama!!!!
 
Mkuu unahakika kama RA si mtanzania? Au kuwa na rangi isiyo nyeusi maana yake si mtanzania, au kuwa na asili ya Iran maana yake ni M-iran? Kama asingekuwa mtanzania sidhani hata kama angekuwa mbunge.

=================================================================
Ukweli ni kuwa huyu nguli wa mafisadi si Mtanzania. Hakuzaliwa Tanzania na wala hajawahi kuomba uraia wa Tanzania. Alifika hapa TZ akiwa na umri unaokaribia miaka 7 hivi na yalibaki ni historia.
Wakati tunasoma naye pale IFM miaka ya tisini niliwahi kumuuliza alipataje kubinafsishiwa viwanda vyote vya ngozi. Ndipo akatamba kuwa Tanzania ukiwa na fweza chochote waweza kukifanya. Akaeleza na historia yake halisi ya alivyokuwa Mtanzania bandia. Wakati huo alinionyesha cheti cha kuzaliwa ambacho alikuwa amekipata kwa njia za kughushi ambacho alikuwa akitembea nacho mfuko wa nyuma wa suruali ili kionekane cha kale. Si mnajua tena ili kionekane ki-Igunga igunga hivi.
Kutokana na fweza alizo nazo sasa na uroho wa wadanganyika kwa fweza, anaweza kuwa na mashahidi hata alfu watakaojitokeza kuwa walikuwepo akizaliwa. Lakini ukweli unabaki palepale si Mtanzania. Kama ana roho za binadamu na nafsi iliyo hai anatambua hilo. Ameishi kwa uongo miaka yote na kwa ushetani huo hawezi kurudi nyuma pamoja na wapambe wake. Kila chenye mwanzo kina mwisho. Sisi sote anaweza kutodhihaki lakini kwa kitambo kwani Mungu hadhihakiwi, chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wapambe wajiandae kuvuna pamoja naye na mavuno yako karibu mno!

Dawa ya mjinga ni kuumia
 
haya mambo tunajitakia wenyewe watanzania. hivi kuna mweusi yeyote mwenye influence katika nchi kama iran, india, irak, nk na akafanikiwa? nijuavyo nchi kama misri ni wapinzani wakubwa wa ubaguzi wa rangi lakini sheria zao ni za kibaguzi sana lengo ikiwa ni kuhakikisha hakuna wageni wanaojipenyeza na kununua uongozi. tunapokataa ubaguzi hatumaanishi kwamba tuache kila kitu kwa watu wote regardless of color....etc. tunatakiwa kulinda uchumi, utamaduni na identity yetu; vinginevyo baada ya mwaka 2025 ichi itakuwa imeshatawaliwa rasmi na wageni waliochukua uraia kwani bunge litakuwa limejaa waasia watakaopata nafasi kama hizo kwa kununua.

Maneno ya busara haya! Inashangaza Waafrika huwa hawaoni huu ukweli..... na wengine wanajifanya ohoo ubaguzi wa rangi.....
 
.

Hivi ulishawahi kuwaza kuwa watu wenye fedha kama kina Bill Gates wanatoa fedha zao kusponsor tafiti na miradi mbalimbali duniani, Je kwa Watanzania wenye fedha ambazo tunahakika hawawezi kuzitumia zote kama RA, unadhani Fedha zao zinaenda wapi?

Asante, umenifumbua macho, aheri wale wenye kuona na kusadiki kuliko wao wenye kuona na kusikia lakini hawasadiki! Manji huwa anatoa kidogo kidogo kule Yanga, kina Bakh..., Men...,Mka.., EL,n.k wanapeleka wapi, mhhhhhhh
 
Asante mkuu, RA atakufa tu kama mnyama na kaburi litakuwa makao yake tu. Waache waendelee kupiga kelele ila watz washaelimika hatukubali kudanganywa tena hata alete udini au ukanda bado hatutakubali. come october 31 watajua kuwa tushaelimika na hatudanganyiki tena!
 
OK. Wenzako wanalipwa kuwasapoti mafisadi. Angalie usije ukawa unajitolea...
so, as long as unachukia mafisadi basi tukuunge mkono kwa kila utakachosema? Wacha kamba, umekiri hukuwepo wakati Nyerere anakufa, wala hiyo nukuu sio well documented, usitupeleke hapa kama gari bovu.
 
kama ni kweli basi kuna watu washakuwa part ya Usalama wa taifa bila hata woo kujijua.

Watu kama hao wanakuwa na siri nyingi sana. Wanakuwa na siri ya viongozi wetu wananunulika kwa shilingi ngapi? Wanaweza kuwa na siri kubwa ambazo hata wakurungezi wa taasisi zetu za usalama hawana. Vipi kama account bandia za Chama au watu fulani wachache ziko kwa majina yao. Ndio maana tunaweza kubaki tunashangaa mbona hakuna kinachotokea. Lakini naamini Tanzani hatujawa na watu kama hawa

Ogopa watu ambao wawekezaji wa nje wanawaamini na kuwatumia kuliko wanvyoamini kituo cha uwekezaji (TIC). Ukiwatumia wao process zinakwenda kwa kasi ya ajabu.????

Mungu ibariki Tanzania
 
Bongolander,'
Nina habari za uhakika kuwa kampeni ya uraia wa nchi mbili ilianzishwa na Rostum Aziz. Bila shaka huyu bado anayo pasipoti ya Iran.
Mkuu naomba uhakika wa habari hii..
Tunamchukia sana RA lakini tusije pandikiza sumu ktk maswala nyeti sana kwa sababu yake hali matakwa ya Uraia wa nchi mbili una malengo makubwa zaidi ya RA.
 
Back
Top Bottom