Kwa sababu anatoka Karatu na Wachaga wanatoka Kilimanjaro, basi wameshakuwa kundi moja?
Una maana kuwa Mwandiga kwa Zitto nako ni Nothern Tanzania?
Hungary (Magyar) ni nchi iliyopo Eastern Europe na imezungukwa na majirani karibu wote ambao ni Slovans. Ila cha ajabu, lugha yao iko karibu zaidi na Finland na hawana uhusiano wowote na hao akina Czech, Slovakia, Bulgaria etc. Kwa mtu kutoka Karatu, hana uhusiano wowote na Mchaga. Pia anayegombea hana uhusiano wowote na Mtei ambaye ni mwanzilishi wa Chama.
Dr. W Slaa kafanya kazi nzito kupata umaarufu wake. Hakubebwa na akina Lowassa au RA kufikishwa pale alipo. Wakati wengine wakimshangilia Rais Kikwete kuweka sahihi sheria ya uchaguzi kwa mbwembwe, mtu mmoja pekee alikuwa anakesha kuhakikisha kama kweli alichoweka Rais sahihi ndiyo hicho na akakuta SI HICHO.
Ndiyo mtu pekee aliyeanza KUFUMUA madudu ya Kifisadi. Wengine tulidhani ni Mzindakaya kumbe yule alikuwa anatumika pale marafiki wawili wanapogombana na mmoja anamshambulia mwenzake kwa kumwaga madudu via Mzindakaya.
Ndiye mbunge pekee aliyedai "Mishahara ya Wabunge ni mikubwa" huku na yeye akiwa mbunge na kusema IPUNGUZWE.
Ndiye aliyefumua list ya Mafisadi na Rais wetu hadi leo akaikalia. Na aliweka hadi ushahidi lakini wapi.
Kuna mengi kayafanya hadi AKAJIJENGEA jina. Huwezi kuja hapa kuanza kumchafua mtu na ukafikiri eti tutanunua. Na kama ni kweli Vatican wangelihitaji kuweka mtu, basi wangeliweka Muislaam. Wale jamaa wa Vatican, hata Wayahudi wanawaogopa. UK, USA na Russia wanafahamu kuwa Ujasusi wa Vatican ni mwisho wa Matatizo. USA walipigana na Wakoministi (Cold War) yakawashindwa. Walipoingia wazee wa kazi kwa kumtumia Papa John Paul II, Mkoministi akabwaga manyanga chini.
Kama ni kweli wanataka kufanya hilo, wangelikuja na njia nzuri zaidi na si kutumia mtu wao wa zamani ambaye mbali kabisa unamuona.
Mlimtukana Malecela mwaka 2005. Mkamtukana SA Sallim mwaka 2005. Safari hii tupo macho. Kumbukeni maneno ya Dr. H. Mwakyembe kuwa "Watanzania siyo mabwege tena". Kimewauma kuwa hadi mwisho hamkufahamu kama Slaa atagombea. Hamkufanya matayarisho mazuri kummaliza. Sasa mnaanza kurusha mawe bila kufahamu adui yuko wapi. Kumbukeni kwenye Biblia imeandikwa "Achezaye kwa upanga, hufa kwa upanga". Msijifanye Watakatifu sana maana watu wakianza kumwaga siri zenu, mhhhhhhhh patakuwa hapatoshi.
Mwisho wa siku wote tutabaki kuwa Watanzania. Tugombane kisiasa huku tukikumbuka kesho. Ona sasa mmeshampoteza SAS, Malecela sijui kama ataendelea kuwasaidia. Fisadi Mkapa anajificha na kutokea kanisani kujisafisha. RA na EL dawa yao inakuja mwakani wakati Slaa atakapokuwa Rais. MAFISADI WOTE anzeni kunyowa......
UKO NA SLAA au UKO NA MAFISADI.
..... YES!!! Pamoja na RA ADUI ZETU are among ourselves. You do not have to read between lines to deduce what enemies of TANZANIA are up to. In any order, super sillious Bongolanders will as usual succumb to the undermentioned disinformation innuendos:
ONE: Dr Slaa is a Northener, in kinship and blood with his fellow CHADEMA Northeners (Chaggas!!!)
TWO: CHADEMA aims at dethroning Moslems hegemony currently characteristic of CCM and Govt and thus, in its stead, CHRISTIANITY rules OK? Such rubbish is that graffiti you read in places abound with profound stupidity and bad taste, to name a few accolades.
THREE: Dr Slaa serves Vatican Intelligence Agency (... the......)
FOUR: Pls add tothe list
i-th: doubledigook!