Rostam - Kuisambaratisha Tanzania (?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam - Kuisambaratisha Tanzania (?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ramos, Jul 26, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Kwa ugonjwa huu; nitakufa.. Watanzania wale watalia sana.., nitawaombea kwa Mungu"
  Ndugu wanaJF nimeona nianze kwa kunukuu sehemu ya maneno ya Baba wa taifa katika siku zake za mwisho pale St Thomas...

  Rostam Aziz, wote tunamfaham kama mbunge wa Igunga na kada wa CCM na mfanya 'biashara' maarufu. Lakini naomba nimzungumzie Rostam tofauti kidogo. Nimzungumzie Rostam kama kiongozi mtendaji wa 'syndicate' ya wahaini wa kimataifa wanao-control chumi na siasa za mataifa kadhaa duniani hadi sasa, yeye akiwa anatekeleza majukumu yake hapa Tanzania.

  Mtakumbuka ni kiasi gani hawa jamaa kuputia kwa RA waliwekeza hadi kuhakikisha wamechukua uongozi wa nchi kwa kuweka raisi waliyemtaka wao kwa matumizi yao. Baada ya kushika nafasi hiyo mnaona jinsi walivyofanikiwa kuuweka uchumi na raslimali za Tz mikononi mwao.

  Wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha wanawafitinisha watanzania kwa misingi ya ukabila ili kuhakikisha hakuna kundi tofauti na wao wanaochukua madaraka. Kwa sasa wameingia katika kipengele cha udini bila kujali madhara yake kwa waTz. Mtakumbuka hivi majuzi gazeti moja la RA liliandika ...Dr Slaa kugombea uraisi kwa tiketi ya CHADEMA.. 'ategemea udini wa wakatoliki kushinda'...

  Haihitaji kuwaza sana kugundua madhara ya kauli kama hii kwa kizazi cha sasa na cha baadae...

  Nadhani kazi kubwa tuliyonayo waTZ kwa sasa wala sio kupambana na umaskini wala nn.. Ni kupambana na wahaini hawa...
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :A S angry:
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,583
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  RA si mtanzania, RA ni raia wa Iran, hivyo hana uchungu na nchi hii kwani hata yakitokea machafuko yeye na genge lake la mafia wa TZ wataikimbia nchi.
   
 4. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kauli hii ya kumhusisha Dr Slaa na wakatoliki niliona mara ya kwanza hapa jamvini ikinadiwa na Malaria Sugu! Upesi upesi ikawaka moto na hadi kufikia kuchapishwa na Mtanzania! Inasikitisha sana. Mara ya kwanza niliipuuza nikijua ni malaria imemsumbua MS lakini sasa nadhani kuna haja ya kukaa na kuiwaza hii hoja, ina mbegu chafu ya kutaka kutugawa. Na itakuwa bahati mbaya sana kama mwana-JF atakuwa anatumiwa na hawa wanasiasa uchwara kupandikiza mbegu ya chuki katika taifa letu.
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nani alaumiwe? Wale watanzania wenye matumbo yasiyoshiba waliomkabidhi nchi kwa sababu ya njaa zao, au ni RA mwenyewe!!

  Hata mimi nigekuwa tajiri aje mtu aniambie nipe hela unifanye utakavyo ningempa! Kama kuna mtu aliyeenda kumwomba hela ya kampeni na kumwahidi nchi kuwa mali yake, sioni sababu ya kumlaumu RA, Jilaumu wewe uliyekubali kuongonzwa na mtu huyo!

  MAzingira tuliyo nayo TAnzania ya sasa ni sawa na mtu aliyeamua kumwuza mke wake kwa matajiri ili apate hela ya kula!!
   
 6. R

  Ramos JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haikunichukua mda mrefu sana kabla uchunguzi wangu kubaini kuwa Malaria sugu ni mwandishi katika gazeti la Mtanzania. Najua kuwa amenunuliwa, lakini ipo siku jasho na damu la waTz itamililia...
   
 7. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Nadhani hata Malaria Sugu ni raia wa Irani. Kama siyo basi ni kweli baadhi ya watanzania wenzetu ni hayawani/zumbukuku, kwani wanashindwa kujua nchi ikichafuka watakao dhurika ni wao na siyo RA:A S angry:
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unahakika kama RA si mtanzania? Au kuwa na rangi isiyo nyeusi maana yake si mtanzania, au kuwa na asili ya Iran maana yake ni M-iran? Kama asingekuwa mtanzania sidhani hata kama angekuwa mbunge.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lakini watu wa aina hii huwa hawadumu, tunaona anavyo tumia uwezo wake kipesa kuvuruga kura ya maoni ya CCM anavyopandikiza watu wake sehemu mbalimbali na bado watu hawaelewi lengo lake.

  Leo CCM wanashangilia lakini watakuja kulia baadae kumuachia chama mtu mmoja. Nasema hivyo kwa sababu ndani ya CCM, hakuna mtu yeyote atakayesema kitu juu ya Rostam kuanzia Mwenyekiti, Makamba, Msekwa hata EL wote wako mfukoni.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hana huo ubavu tena..
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Embu tuanze kufikiria maendeleo jamanihii JF mmeanza kuandika kuhusu mafisadi toka lini na nini kimefanyika na kama akuna cha maana embu tuelimishane juhusu kilimo kwanza/ujasiriamali na sisi tututoke jamaa ndio ashaapangau mabwa angani muandike weeeee mpaka JK aondoke atakula kuku embu tufungue macho tena wapendwa
   
 12. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45

  Jamani haya mambo sio ya Malaria sugu wala Rostam mbona tunataka kupoteza mwelekeo? Huu ni ule mpango mzima wa mtandao na mbinu zao chafu za kuwachafua wanaomchalenge mgombea wao. Hii ndiyo ilitumika pia kumjengea fitina SAS 2005 so sasa hivi target kubwa ni hii kwa vile ndani ya chama cha mafisadi hamna challenge yoyote. Hivi kuna mtanzania asiyekuwa na dini? Na elimu ya dini au kusomea vyuo na shule za taasisi za kidini haiondoi sifa ya kuwa mtanzania na kuwa na uwezo wa kuongoza.

  Mabadiliko muda wake unapofika hamna kinachoweza kuzuia, angalia wenyewe wanavyovurugana sasa hivi na bado hakutakuwa na maelewano hatimaye kitavunjika chama chao. Wametuburuza kwa muda mrefu sana sasa wameshikwa pabaya lazima watatumia mbinu zote za kuchafua wagombea wengine wote.

  GO DR SLAA GO......

  Tumesubiri sana mabadiliko na hatuna sababu ya kuendelea kulea huu mfumo unatuletea umaskini kwa genge la watu wachache wanakula kama viwavi jeshi hawatosheki
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,583
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Mbona ubunge kupitia CCM ni bidhaa, mwenye fedha ananunua,na si m-judge kwa rangi yake bali kwa matendo yake. Na pia hakuzaliwa tz, na hakuna mahali ambapo aliukana uraia wa uajemi alikozaliwa.
   
 14. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ..... YES!!! Pamoja na RA ADUI ZETU are among ourselves. You do not have to read between lines to deduce what enemies of TANZANIA are up to. In any order, super sillious Bongolanders will as usual succumb to the undermentioned disinformation innuendos:

  ONE: Dr Slaa is a Northener, in kinship and blood with his fellow CHADEMA Northeners (Chaggas!!!)

  TWO: CHADEMA aims at dethroning Moslems hegemony currently characteristic of CCM and Govt and thus, in its stead, CHRISTIANITY rules OK? Such rubbish is that graffiti you read in places abound with profound stupidity and bad taste, to name a few accolades.

  THREE: Dr Slaa serves Vatican Intelligence Agency (... the......)

  FOUR: Pls add tothe list

  i-th: doubledigook!
   
 15. R

  Ramos JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tufaham kitu kimoja kuwa Rostam Aziz is not an individual. Rostam Aziz ni sehem tu ya taasisi kubwa iliyoshikilia dola nyingi duniani. He has nothing to do with CCM either, pale anapatumia kutimiza matakwa yao ya kukamata dola. They don't care kama CCM inakufa au vipi as long as wanayo dola. Kwa sasa bado wanatumia mbinu baridi kutufarakanisha ili watutawale (devide and rule) lakini ukweli ni kuwa wanayo Power kubwa sana na siku ikibidi wataanza kutoa roho za wote wanaowapa shida. Ikifika wakati huo tusitegemee kuwa watu kama kina Kilango, Slaa, Sendeka wataishi.

  Hivi ulishawahi kuwaza kuwa watu wenye fedha kama kina Bill Gates wanatoa fedha zao kusponsor tafiti na miradi mbalimbali duniani, Je kwa Watanzania wenye fedha ambazo tunahakika hawawezi kuzitumia zote kama RA, unadhani Fedha zao zinaenda wapi?
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa nchi hii ina utawala bora wa kufuata sheria za nchi, huyu RA saa hizi angekuwa jela! Lakini hakuna utawala bora iwapo waziri anayeshughuklika masuala hayo ndo hivyo tena -- hana sifa zozote za utawala bora!
   
 17. R

  Ramos JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  It is very unfortunate kuwa mbinu ya RA kuwatumia watu kama Malaria sugu, Tumain, DoubleOseven na wengine, sio tu kwamba kunahatarisha umoja wa waTz bali kunawaaibisha na kuwadhalilisha waislamu. Mimi sio muislam lakini katika maisha yangu nainteract na waislam kila sehem na kila saa. Ukweli ni kuwa hakuna muislam mwenye mawazo sawa na hawa jamaa. What I think ni kuwa hawa jamaa wala sio waislam bali ni vibaraka wa RA. Waislam wengi wanaotetea dini yao ni watu wenye akili na hawana mawazo potofu kama hao jamaa niliowataja hapo juu...
   
 18. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Jamani naomba kama kuna mkalimani humu ndani anisaide.
   
 19. minda

  minda JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  haya mambo tunajitakia wenyewe watanzania. hivi kuna mweusi yeyote mwenye influence katika nchi kama iran, india, irak, nk na akafanikiwa? nijuavyo nchi kama misri ni wapinzani wakubwa wa ubaguzi wa rangi lakini sheria zao ni za kibaguzi sana lengo ikiwa ni kuhakikisha hakuna wageni wanaojipenyeza na kununua uongozi. tunapokataa ubaguzi hatumaanishi kwamba tuache kila kitu kwa watu wote regardless of color....etc. tunatakiwa kulinda uchumi, utamaduni na identity yetu; vinginevyo baada ya mwaka 2025 ichi itakuwa imeshatawaliwa rasmi na wageni waliochukua uraia kwani bunge litakuwa limejaa waasia watakaopata nafasi kama hizo kwa kununua.
   
 20. R

  Ramos JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I tell you that it is easier for KIKWETE kupelekwa mahakani hata leo!!, kuliko RA kuchukuliwa hatua yeyote ya kisheria. After all nani atamchukulia hatua wakati wote wako chini ya control yake!!?
   
Loading...