Rostam Aziz: Slaa ni mpotoshaji

Rostam Aziz: Slaa ni mpotoshaji

Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.

Rostam alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi, alipozungumza na vyombo vya habari kuelezea mambo kadhaa zikiwamo sababu za kujiondoa ndani ya Chadema.

Dk. Slaa alidai kuwa mwaka 2009 baada ya kutaja orodha ya mafisadi 11 nchini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam, Rostam alimpigia simu na kumtishia maisha.

Dk. Slaa pia alidai juzi katika mkutano wake na vyombo vya habari uliorushwa na vituo vitatu vya runinga kuwa Rostam anaifadhili Chadema.

Katika taarifa yake jana, Rostam alisema: "Nilimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa alipokuwa akizungumza katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

"Kwa mara nyingine kama ilivyo hulka yake miaka yote, Dk. Slaa kathibitisha pasipo na shaka kwamba yeye ni mbinafsi na mpotoshaji mkubwa."

"Nimesikitishwa na kushtushwa japo sikushangazwa hata kidogo na hatua ya Slaa ambaye sasa anaonekana kukubuhu kwa uzushi kutoa matamshi ya namna hiyo.

"Sijapata hata mara moja kuwa na mawasiliano na Dk Slaa wakati wowote. Madai yake kwamba eti nilimtisha ni ya kupuuzwa na yasiyo na msingi hata kidogo," alisema Rostam.

Rostam alieleza kuwa ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa watu wanaomfahamu Slaa kwamba anaweza kumtishia maisha na yeye akakaa kimya bila kuchukua hatua ya kwenda polisi na kumshitaki halafu anakaa na jambo hilo kwa miaka yote hadi juzi ndipo alisema hadharani.

"Ili kuthibitisha madai yake hayo, namtaka Dk. Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wa jambo hilo," alisema Rostam.

Huu ni uongo mwingine wa dhahiri. Namtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi pia katika madai yake haya.

"Ni huyu huyu Dk. Slaa ambaye mwaka 2010 alizusha kwamba eti mimi, tukiwa na Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa tulikutana katika hoteli ya La Kairo, Mwanza na kupanga njama za kumuibia kura zake za urais," alisema na kuongeza:

"Wakati Slaa akitoa madai hayo ya uongo, mimi nilithibitisha kwamba wakati huo nilikuwa Afrika Kusini na Rais Kikwete akiwa Lindi huku Lowassa akiwa Arusha. Ni wazi kwamba tusingeweza kukutana La Kairo kama alivyodai yeye."

Kwa mujibu wa Rostam, Dk. Slaa kuna wakati alimzushia hadi Rais Kikwete alipodai kwamba alisafiri kwa usiku mmoja kwenda China kumtoa mwanaye aliyekuwa amekamatwa na vyombo vya usalama, kisha kurejea Dar es Salaam usiku huo.

"Ni Slaa huyu huyu ambaye mwaka 2010 wakati wa kampeni alifikia hatua ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba kulikuwa na malori yaliyobeba kura za CCM ambazo zingesaidia ushindi wa wizi yaliyokamatwa Tunduma. Malori hayo yalipokaguliwa yalibainika kuwa na mizigo ya kawaida," aliongeza katika taarifa hiyo.
 
2009 List of Shame ni typing error au kasema yeye? Kama kasema yeye basi naye mbumbu tu…!!! Alafu iko wazi banah wala hatuitaji kumung'unyaaa maneno kwani yeye si ndie mfadhili wa Lowassa…!!! Sasa kuna.ajabu gani hiyo hela ikitumika pia Chadema? Tunajua Rostam banah wewe na Lowassa pete na.kidole akiingia yeye Magogoni we unavuta chupa ya Wine huna wasiwasi nchi utakuwa ushaitia mfukoni
 
Na akiishika ndugu magufuli? Nchi ataiweka kwapani?
 
Kufadhili Chadema hajajibu, maana yake ni kweli...

Chadema inafadhiliwa na mafisadi...
 
Dr. Slaa, amekuwa na kichwa cha Josephine... sio Slaa tena... chezea Wahaya wewe... mzee kapigwa Ka.t.ere_____HAJUI KITU TENA.... haongei tena, kuanza mapenzi ya ukubwani shida sana
 
Kikwete aliingizwa na Rostam hakuna anayesema biashara zake zote kubwa Kikwete na Rostam washirika halafu munahamisha kesi kwa wengine jamani tuna macho na masikio duh Kinana wachina wa meli za pembe za ndovu wanafadhili CCM Ndogate kapewa pwani yote ya mtwara vijijini atoe fedha za kampeni kwa CCM mupo kimya mukidhani habari hazijavuja yameshatolewa maelezo mengi
 
Dr. Slaa, amekuwa na kichwa cha Josephine... sio Slaa tena... chezea Wahaya wewe... mzee kapigwa Ka.t.ere_____HAJUI KITU TENA.... haongei tena, kuanza mapenzi ya ukubwani shida sana

Yaani ni hiviii... Ukijitunza kuosha viombo ukubwani lazima uvivunje.
 
Attachments

  • 1441806492581.jpg
    1441806492581.jpg
    14 KB · Views: 389
rostamu mnamuoneaga bure huyo jamaa,sijui ndo wivu wa maendeleo....
 
Kufadhili Chadema hajajibu, maana yake ni kweli...

Chadema inafadhiliwa na mafisadi...

Kwa hiyo ni sahihi kusema hata Dr.Slaa anafadhiliwa na CCM??? Maana haieleweki ulinzi na maisha ya ghagla ya kusafiri kama mtalii yameanza lini.Labda unaweza kutuambia fadhili wa Dr.Slaa na Lipumba
 
2009 List of Shame ni typing error au kasema yeye? Kama kasema yeye basi naye mbumbu tu…!!! Alafu iko wazi banah wala hatuitaji kumung'unyaaa maneno kwani yeye si ndie mfadhili wa Lowassa…!!! Sasa kuna.ajabu gani hiyo hela ikitumika pia Chadema? Tunajua Rostam banah wewe na Lowassa pete na.kidole akiingia yeye Magogoni we unavuta chupa ya Wine huna wasiwasi nchi utakuwa ushaitia mfukoni

Rostam yupo ccm na wala hajatangaza kuhamia chadema kosa lake nini
 
Kwani huyu Rostam si alishatoa taarifa yake? Kuna kipi alisahau kujibu?
 
Amtaka Slaa kujitokeza hadharani kuthibitisha kauli zake. Akanusha kuisaidia CHADEMA. Asema Slaa ana historia ya uzushi.

Chanzo: Channel 10

======================

Sheria inasemaje kwa mtu ambae amekuchafua kwa tuhuma zito kama hizo alzo toa Dk slaa dhidi yake..kama kwel ni uongo y asiende Mahakamani!
 
Back
Top Bottom