Rostam Aziz kuvuliwa Uraia?

Rostam Aziz kuvuliwa Uraia?

OBSESSION inatisha sana

Nilikuwa nashangaa mpaka page ya sita kuhusu Rostam bado hujatokea!!!!

Mweingine aliyekuwa anakosekana ni Masatu hata hivyo yeye nilielewa kwa sababu bado anadili na Magufuri aliyeamuru zana haramu za uvuvi ziteketezwe. Kadhia hiyo imemkumba huko ziwa Victoria na Bwawa la nyumba ya Mungu ambako makokoro yake yapato 120 yalinaswa. LOL
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hii mada nimedandia katikati lakini sidhani kama ina uzito wowote. Mkuu wewe na mimi tu ndio hatukubaliwwi kuwa na Uraia wa nchi mbili.. Nakuhakikishia wahindi na waarabu nchini wengi wao ni raia wa nchi mbili.. Utafukuza wangapi!..
Kisha kibaya zaidi ni hiyo sheria ya mzazi kuukana Uraia wao ili upate kuzaliwa Mtanzania.. Wakuu zangu hakuna mwarabu wala mhindi anayeishi Igunga au Ukerewe anafahamu haya..Kisha basi ukitaka kufahamu ukweli Je, unajua kwamba Wairan walikuja nchini toka karne ya kwanza wkifanya biashara za majahazi - hawakuhitaji hata Passport..
Na wangeomba vipi Uraia ikiwa Uhuru wa Tanganyika na sii Tanzania umewakuta wakiwa nchini mibaba mizima yenye watoto..Aukane vipi Uraia wa Iran ikiwa yeye pia alitawaliwa na mkoloni kama wewe, pengine kabila lako/langu ndilo lilihamia Tanganyika likawakuta wamejaa tele..That is the fact mkuu wangu hata kama inauma sana... Mimi nimezaliwa kabla ya Uhuru na nimewakuta waarabu na wahindi kibao tena huko vijijini, watoto wao tumekwenda shule pamoja.. Waukane Uraia Upi ikiwa nchi hii imekuwa nchi wakiwa ndani..

Jamani hizi habari za kumtafuta Fisadi kwa kuogopa kumsema kwa mabaya yake, kushindwa kuweka vitu bayana kwa hofu ya kupoteza kiti cha Bunge ni upuuzi mtupu. Mbona Dr. Slaa huja ktk point bila kupindisha.. Mtikila kapewa fedha na huyo Fisadi Rostam yuko wapi amekaa kimya hazungumzi tena kama shujaa Mengi aliyekwenda naye sambamba..
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu hii mada nimedandia katikati lakini sidhani kama ina uzito wowote. Mkuu wewe na mimi tu ndio hatukubaliwwi kuwa na Uraia wa nchi mbili.. Nakuhakikishia wahindi na waarabu nchini wengi wao ni raia wa nchi mbili.. Utafukuza wangapi!..

Hili sijui lina ukweli kiasi gani. Unaposema "wengi" sijui mkuu unatumia kigezo gani?

Kisha kibaya zaidi ni hiyo sheria ya mzazi kuukana Uraia wao ili upate kuzaliwa Mtanzania..

Hapana labda hujanipata vizuri, siyo mzazi anayetakiwa kuukana uraia bali ni mtoto ambaye amezaliwa Tanzania ambaye wazazi wake siyo Watanzania. Huyo akifikisha miaka 18 anatakiwa kuukana uraia wa wazazi wake ili abakie na uraia wa Tanzania.

Wakuu zangu hakuna mwarabu wala mhindi anayeishi Igunga au Ukerewe anafahamu haya..Kisha basi ukitaka kufahamu ukweli Je, unajua kwamba Wairan walikuja nchini toka karne ya kwanza wkifanya biashara za majahazi - hawakuhitaji hata Passport..

Mzee, Wairan, Washirazi, waarabu, wahindi, wangoni, wazulu, wamakonde n.k waliokuwa katika Tanganyika na uraia wa walikuwa ni raia wa Makoloni ya Uingereza siku ile Tanganyika inapata Uhuru, mara moja walikuwa raia wa TAnganyika. Na wakati Muungano unafanyika 1964 waliokuwa raia wa Tanganyika na waliokuwa raia wa Jamhuri ya Zanzibar walijikuta wakiwa raia wa Tanzania (ndio maana hakuna uraia wa Tanganyika au uraia wa Zanzibar).

Hivyo, uraia wa Tanzania hautegemei rangi au mahali unapotoka bali unategemea uraia wa wazazi wako au ule wa kuomba. Hivyo, kama baba ni mhindi, na baba huyo alikuwa ni raia wa Tanganyika au Zanzibar basi baada ya Muungano baba huyo ni raia wa Tanzania na watoto wake ni Raia wa Tanzania. Hao watoto hawana sababu ya kuukana uraia wa wazazi wao.

Hapa ndio tunajikuta wengi wetu sana (weusi, wahindi, wairan wa Igunga n.k).

Na hapa ndipo TATIZO la Rostam linapotokea. Wazazi wake HAWAJAWAHI kuwa raia wa Tanganyika au Tanzania. Yeye kaupata uraia wa Tanzania vipi?
 
Mzee Mwanakijiji,
Naposema wahindi na waarabu wengi wana uraia wa nchi mbili ni kutokana na kile mnachomshutumu Rostam..Hakuna mhindi wala mwarabu mzawa wazazi wake waliyekwenda kuukana uraia wa nchi ambayo walitoka..Hata Nyerere hakwenda kuukana URwandiz ndipo tukawakubali watoto wake.. wala wazazi wake hawakuukana..
Mzee, Wairan, Washirazi, waarabu, wahindi, wangoni, wazulu, wamakonde n.k waliokuwa katika Tanganyika na uraia wa walikuwa ni raia wa Makoloni ya Uingereza siku ile Tanganyika inapata Uhuru, mara moja walikuwa raia wa TAnganyika. Na wakati Muungano unafanyika 1964 waliokuwa raia wa Tanganyika na waliokuwa raia wa Jamhuri ya Zanzibar walijikuta wakiwa raia wa Tanzania (ndio maana hakuna uraia wa Tanganyika au uraia wa Zanzibar).
Sasa ikiwa hivyo unataka Rostam avuliwe uraia kwa kitu gani?.. kwa maneno ya Mtikila kuwa wazazi wake hawakuwahi kuwa raia?.. Mtikila ambaye hana ushahidi wowote zaidi ya chuki yake binafsi! Sii huyu aliyechukua fedha kwa Rostam!.. inawezekana anachofanya ni blackmail..
Mkuu watu kibao wanaifahamu familia ya Rostam toka enzi..Na kama huniamini mimi basi huu mjadala wala hauna maana zaidi ya kutafuta mchawi kwa ramli...Kifupi nenda kwao kafanye uchunguzi wako acha hizi habari za Ki nzi, fika mwenyewe uzungumze na wazee wa maeneo anayodai kisha rudi tupe ujumbe wa kweli na sii kum quote Mtikila..
Rostam ana makosa yake, rangi yake haiwezi kutumika kama sababu ya kutafuta Uraia wake kwani angekuwa Mmakonde tungeyasema yote haya ya wazazi wake walitokea Mzambique hawakuukana uraia wa huko...Wangapi weusi wamepimwa kwa kipimo hiki kama kweli huzungumzii rangi na asili ya Rostam?

Huu ndio Ubaguzi unaozungumziwa kwani sioni sababu kabisa ya kumtafuta mchawi kwa rangi yake sawa na maamuzi ya kuwaua wazee kwa dhana ya Uchawi..
Na unaposema Uraia wa Tanzania hautegemei kuzaliwa kwako ila kwa wazazi wako una maana gani sikuelewi hata kidogo! je, ikiwa ikiwa mzazi huyo alikuwa akiishi Tanzania kabla ya Uhuru bado anatakiwa kuukana uraia wa wapi?..
Mkuu wangu kama ulivyosema hapo juu, Uraia wa mtu unaanza na siku ya Uhuru... kuzaliwa kwa wazazi wako sii sababu kabisa ikiwa walizaliwa nje au laa maadam wazazi hao walikuwa wakiishi Tanzania kabla na baada ya Uhuru moja kwa moja wanakuwa ni raia wetu unless wao waukane wa hapa kutokana na sheria inayowakataza kuwa na uraia wa nje. Na hata wakija ukana uraia wetu baada ya kuamua kurudi kwao, mtoto aliyezaliwa wakiwa hapa na kabakia hapa ni raia wa Tanzania..
 
Mzee Mwanakijiji,
Naposema wahindi na waarabu wengi wana uraia wa nchi mbili ni kutokana na kile mnachomshutumu Rostam..Hakuna mhindi wala mwarabu mzawa wazazi wake waliyekwenda kuukana uraia wa nchi ambayo walitoka..Hata Nyerere hakwenda kuukana URwandiz ndipo tukawakubali watoto wake.. wala wazazi wake hawakuukana..

Mzee naona haujanipata vizuri. Nyerere hakuhitaji kuukana uraia wa Rwanda (kama alikuwa nao) kwani alikuwa ni raia wa Tanganyika kama Koloni (la uangalizi) la Mwingereza. Vivyo wote watu wote (wahindi na wengine) waliokuwa ndani ya koloni hilo wakiwa raia.

Nimefafanua kuwa sheria ilitangaza kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika wale wote waliokuwa raia wa Koloni la Tanganyika (maana yake ni raia wa Uingereza na Makoloni yake) wanakuwa raia wa Tanganyika. Hii ina maana kwa makusudi sisi tulikataa kuangalia uraia kwa sababu ya rangi au mahali mtu anatoka! Uraia ulikuwa very defined.

Sasa ikiwa hivyo unataka Rostam avuliwe uraia kwa kitu gani?.. kwa maneno ya Mtikila kuwa wazazi wake hawakuwahi kuwa raia?.. Mtikila ambaye hana ushahidi wowote zaidi ya chuki yake binafsi! Sii huyu aliyechukua fedha kwa Rostam!.. inawezekana anachofanya ni blackmail..

Hapana, Mtikila alisema kitu hicho Juni mwaka jana! Katika uchunguzi wetu pembeni ndio tumekutana na jambo hilo hilo na ndio tukarudia kuangalia alichosema Mtikila. Tulichojengea hoja ni kuwa sheria ilifuatwa kumvua uraia Ulimwengu na yule mwandishi wa Zanzibar kwanini isifuatwe kuhusu Rostam?
Mkuu watu kibao wanaifahamu familia ya Rostam toka enzi..Na kama huniamini mimi basi huu mjadala wala hauna maana zaidi ya kutafuta mchawi kwa ramli...Kifupi nenda kwao kafanye uchunguzi wako acha hizi habari za Ki nzi, fika mwenyewe uzungumze na wazee wa maeneo anayodai kisha rudi tupe ujumbe wa kweli na sii kum quote Mtikila..

Mzee hilo wala halina mjadala. Familia ya "Rostam" inafahamika Igunga na ndio nimefuatilia vya kutosha kabisa. Sisi siyo wa kwanza kuhoji hili kwa sababu unaposema "familia" ujue tunanzungumzia nini. Mtu huwi raia kwa sababu familia yako ina "historia" ndefu. Hapana, unakuwa raia aidha kwa kuomba, ndoa, au ya kawaida zaidi kwa uraia wa wazazi wako. Kama kuna mzungu ambaye alizaliwa tanzania, na wazazi waliokuwa Watanzania, mtoto huyo haitaji kuukana uraia wa wazazi wake, yeye ni Mtanzania!

Lakini kama kuna Waingereza wanaoishi Uingereza, halafu mtoto wao alikuja mdogo Tanzania na akakulia Tanzania, akazungumza Kiswahili n.k.. haina maana mtoto huyo ni Mtanzania!

Rostam ana makosa yake, rangi yake haiwezi kutumika kama sababu ya kutafuta Uraia wake kwani angekuwa Mmakonde tungeyasema yote haya ya wazazi wake walitokea Mzambique hawakuukana uraia wa huko...Wangapi weusi wamepimwa kwa kipimo hiki kama kweli huzungumzii rangi na asili ya Rostam?

Mzee hili la rangi ni wewe unalileta. Kuweza kuelewa anachofanya RA kinahusiana moja kwa moja na uraia wake; siyo nje ya hilo. Kama Jenerali (mweusi) alivuliwa uraia, kama Premji (mhindi) alivuliwa uraia, kama Ali Nabwa (mcomoro) alivuliwa uraia wake, kwanini iwe suala la rangi inapokuja Rostam?

Unataka kuniambia kuwa tusiguse uraia wa Rostam kwa sababu ni Muajemi? Yaani tuangalie sura yake kwanza kabla ya kusema si "raia"?

Huu ndio Ubaguzi unaozungumziwa kwani sioni sababu kabisa ya kumtafuta mchawi kwa rangi yake sawa na maamuzi ya kuwaua wazee kwa kudhaina ni wachawi..

Hili halina msingi.

Na unaposema Uraia wa Tanzania hautegemei kuzaliwa kwako ila kwa wazzazi wako una maana gani sikuelewi hata kidogo ikiwa mzazi huyo alikuwa akiishi Tanzania kabla ya Uhuru..Mkuu wangu kama ulivyosema hapo juu, Uraia wa mtu unaanza na siku ya Uhuru... kuzaliwa kwa wazazi wako sii sababu kabisa ikiwa walizaliwa nje au laa..

Nadhani hapa tunazungushana kwa jambo jepesi tu: Kuwa Raia wa Tanzania kunategemea uraia wa wazazi wako (haitegemei kama walizaliwa hapa au la). Kama wazazi wako ni Watanzania, wewe ni Mtanzania, na kama una uraia wa nchi nyingine ifikapo miaka 18 unatakiwa kuukana uraia ule mwingine vinginevyo unapoteza uraia wa TAnzania (ndiyo iliyotumika kwa Ali Nabwa).

Wazazi wa Rostam (sijasema familia, wajomba, shangazi, binamu au wakwe) hawajawahi kuwa raia wa TAnzania au Tanganyika. Sasa yeye Rostam kapata vipi uraia? Hilo ndilo swali unisahihishe. Kusema tusizungumzie, au kudai ni suala la rangi ni kukwepa hoja iliyopo mbele yetu.

Kama una habari kuwa RA wazazi wake ni Watanzania au walikuwa watanzania nisaidie tu kwani itazima mjadala huu mara moja! Je wazazi wa Rostam ni Watanzania? tangu lini?
 
Mzee Mwanakijiji,
Unaposema wazazi wa Rostam hawajawahi kuwa raia wa Tanganyika wala Tanzania una maana gani?... yaani umefuatilia na kujua kwamba wazazi wake hawajawahi kuishi Tanzania au?..

Na kama hufuati maelezo ya Mtikila labda nambie wewe vizuri Rostam alizaliwa wapi,... au niulize, hivi Mkandara nilizaliwa wapi, nani humu JF anajua nilipozaliwa!..Nakuombeni fanyeni uchunguzi kama kweli mnayaweza yote haya.. Kuna sheria gani iliyofuatilia uzawa wangu hadi leo kujenga imani kuwa mimi ni Mtanzania na wazazi wangu walikuwa Watanzania/Watanganyika..

Huyo Jenerali inajulikna kabisa ni hayahaya ya Rostam, ndipo naposimama mimi kwamba sheria iliyotaka kutumika kwa Jenerali inatokana na mambo mengine kabisa.. Sii kwamba tunatafuta haki ya uraia wa mtu ila tuna matatizo na mtu huyo kiasi kwamba tunashindwa kumkabiri kwa matatizo yaliyopo tunatafuta Uchawi..
Rostam awe Mtanzania asiwe ni FISADI na ndicho kinachotusukuma sote kutafuta hila za kumweka hatiani..Tofauti na Rostam, Jenerali alikuwa fimbo ya kipofu na wanyonge na wenye nguvu wakatafuta uchawi wa uraia wake kama njia ya kumzima..
Mtu asokuwa raia wa Tanzania atajulikana tu, wala hakuna haja ya kuchimba sana.. hizi nguvu za kutafuta uraia wake tungeziweka ktk kutafuta ushahidi unamfunga ningefurahi sana maanake ndivyo serikali inataka kuwa raia waje na ushahidi na sii kazi ya vyombo vya sheria..
Hivyo mkuu wangu jaribu kitu kingine hii ni majungu matupu wala haina harufu kabisa..Maswala ya Uraia wa mtu siku zote ni roho mbaya.. Hata huku Ulaya kuna Wadanganyika kazi yao kutafuta mtu kwa uraia wake kisha wakamchomee kwa wazee kuwa anaishi chini ya meza..Inahusu nini kama sii kukosa maisha na kazi ya kufanya.. Maisha ya mtu na uraia wake inakusumbua nini!..na uta gain kipi kama mtu huyo ataondolewa nchini..Kusema kweli maswala kama haya hunichefua sana..samahani lakini!
 
Mzee Mwanakijiji,
Unaposema wazazi wa Rostam hawajawahi kuwa raia wa Tanganyika wala Tanzania una maana gani?... yaani umefuatilia na kujua kwamba wazazi wake hawajawahi kuishi Tanzania au?..

Ndiyo maana yake, nisingeweza kuzungumza tu hivyo.

Na kama hufuati maelezo ya Mtikila labda nambie wewe vizuri Rostam alizaliwa wapi,... au niulize, hivi Mkandara nilizaliwa wapi, nani humu JF anajua nilipozaliwa!..Nakuombeni fanyeni uchunguzi kama kweli mnayaweza yote haya.. Kuna sheria gani iliyofuatilia uzawa wangu hadi leo kujenga imani kuwa mimi ni Mtanzania na wazazi wangu walikuwa Watanzania/Watanganyika..

mzee siku ukitaka kugombania uongozi wa nchi au kama tuna sababu ya kufikiri vinginevyo tutauliza tu.

Huyo Jenerali inajulikna kabisa ni hayahaya ya Rostam, ndipo naposimama mimi kwamba sheria iliyotaka kutumika kwa Jenerali inatokana na mambo mengine kabisa.. Sii kwamba tunatafuta haki ya uraia wa mtu ila tuna matatizo na mtu huyo kiasi kwamba tunashindwa kumkabiri kwa matatizo yaliyopo tunatafuta Uchawi..

hili ni kweli, na katika kumkabili mtu huyo tunatumia njia zote zilizo katika uwezo wetu mojawapo ni hiyo ya kisheria.
Rostam awe Mtanzania asiwe ni FISADI na ndicho kinachotusukuma sote kutafuta hila za kumweka hatiani..Tofauti na Rostam, Jenerali alikuwa fimbo ya kipofu na wanyonge na wenye nguvu wakatafuta uchawi wa uraia wake kama njia ya kumzima..

Kikombe kilichopimiwa hawa, chapaswa kupima na yeye. Kwanini kisitumike kwa Rostam?

Mtu asokuwa raia wa Tanzania atajulikana tu, wala hakuna haja ya kuchimba sana..

Nadhani kinyume chake ni kweli.

hizi nguvu za kutafuta uraia wake tungeziweka ktk kutafuta ushahidi unamfunga ningefurahi sana maanake ndivyo serikali inataka kuwa raia waje na ushahidi na sii kazi ya vyombo vya sheria..

Hii ni sehemu ya harakati zile zile siyo nje ya hizo. Huwezi kuelewa anachofanya RA bila kuelewa msingi wa hicho anachofanya. Hivi unajua ni kwanini alitumia majina ya Rostum, Rustom, Rostam n.k kwenye kusajili ATDL ?

Hivyo mkuu wangu jaribu kitu kingine hii ni majungu matupu wala haina harufu kabisa..

Nitawaachia wengine kutafuta kitu kingine, mimi nachagua ninachofanya, mwingine anaweza kufanya vingine. Ukishindwa hili unajaribu lile. Ndio maana ya mapambano, wakati mwingine ili goli liingie inabidi mumminye Kipa!

Maswala ya Uraia wa mtu siku zote ni roho mbaya..

Si kweli!

Hata huku Ulaya kuna Wadanganyika kazi yao kutafuta mtu kwa uraia wake kisha wakamchomee kwa wazee kuwa anaishi chini ya meza..Inahusu nini kama sii kukosa maisha na kazi ya kufanya.. Maisha ya mtu na uraia wake inakusumbua nini!..na uta gain kipi kama mtu huyo ataondolewa nchini..Kusema kweli maswala kama haya hunichefua sana..samahani lakini!

Hli lina ukweli; lakini RA asingekuwa na nafasi aliyopo na nguvu aliyonayo, wallahi uraia wake mimi wala usingenisumbua. Lakini anapokuwa na nguvu hadi ya kutuchangishia fedha za Rais wetu the line has been crossed and pushing back we will and we must.
 
Mzee Mwanakijiji,
Maswala ya Uraia wa mtu siku zote ni roho mbaya.. Hata huku Ulaya kuna Wadanganyika kazi yao kutafuta mtu kwa uraia wake kisha wakamchomee kwa wazee kuwa anaishi chini ya meza..Inahusu nini kama sii kukosa maisha na kazi ya kufanya.. Maisha ya mtu na uraia wake inakusumbua nini!..na uta gain kipi kama mtu huyo ataondolewa nchini..Kusema kweli maswala kama haya hunichefua sana..samahani lakini!

Upupu at its best
 
Rustam Sakarir Chakaar Abdurasul Aziz Rostam "Mchelee"!!

The King maker! I salute You!, kwa umri ulio nao Mzee umefanikiwa sana.

Pokea HONGERA kutoka kwangu ya dhati kabisaaaa!

FP

Utanzania wako wewe unatia shaka,unamsaluti kwa lipi jema alilolifanya,ni kwa kuwaibia watanzania wewe ukuwa mmoja wapo au kwa kuwaweka mifukoni viongozi wa serikali ya Tanzania.Kwa ushabiki huu inawezekana na wewe umefaidika na ufisadi.
 
hahahahaaa... JF bana!!
 
Well I see it this way. Chadema next yr imsimamishe mgombea Igunga, well definetely atashindwa maana hayo mahela ya kifisadi ya RA yatamfanya apite tu. Mgombea huyo atakayeshindwa afungue kesi akisaidiwa na akina Tundu Lisu NA WOTE TNAOIPENDA NCHI YETU kuhoji uraia wa RA........... maybe that will unfold the saga!
 
Kama ubunge atashindwa kwa sababu ya mahela ya RA, hiyo kesi ya kuhoji uraia wa RA atashindaje. Labda hiyo kesi iendeshwe kwenye mahakama ya chi nyingine - definitely not in Tz.
 
Kama ubunge atashindwa kwa sababu ya mahela ya RA, hiyo kesi ya kuhoji uraia wa RA atashindaje. Labda hiyo kesi iendeshwe kwenye mahakama ya chi nyingine - definitely not in Tz.

Lakini don't you see kwamba tutapata nafasi ya kufahamu mengi kuhusu historia ya huyu jamaa ambayo so far inaonekana haijulikanijulikani vizuri! At least he will have to testify on every account including kuwataja au kuwaleta say watu aliosoma nao, watu aliokuwa nao nk.
 
Nitawaachia wengine kutafuta kitu kingine, mimi nachagua ninachofanya, mwingine anaweza kufanya vingine. Ukishindwa hili unajaribu lile. Ndio maana ya mapambano, wakati mwingine ili goli liingie inabidi mumminye Kipa!
.
....teh..teh..Ohhh! i love JF!!
 
Ushauri wa Nyambala unabidi kufikiriwa vizuri sana. Tena hapo ndipo wananchi kule Igunga watapata nafasi ya kutueleza sisi watanzania wenzao mambo mengi. Huyo mgombea wa Chadema angelikuwa na msaada wa kisheria kutoka wadau wengi tu hata mchango wa kifedha kuendesha kiyo kesi tungechangia. Mradi huu U-king maker uleleweke vizuri. Na huenda tungelinusuru hili Taifa letu.
 
sasa mkishaweka mpango wa namna hiyo; RA hatogombea mwakani kwa sababu atakuwa "amechagua biashara na kuachana na siasa".. na hapo mnakuwa mmefungwa goli moja mtungi!
 
mwanakijiji ungekuwa unajua jinsi unavyochukiwa......4 ur information linaandaliwa fungu kukununua......tukikuona kimya tutajua umeshafika bei......
 
The Following 23 Users Say Thank You to Mzee Mwanakijiji For This Useful Post:
911 (5th June 2009), Allien (5th June 2009), andindile (5th June 2009), Bulesi (5th June 2009), Dark City (5th June 2009), Halisi (5th June 2009), jmushi1 (5th June 2009), josm (5th June 2009), LeoKweli (5th June 2009), Mag3 (5th June 2009), Mazingira (5th June 2009), Mpendatz (Today), Msanii (5th June 2009), Mwawado (5th June 2009), Next Level (5th June 2009), Nsaji Mpoki (5th June 2009), Ochu (5th June 2009), Recta (5th June 2009), rmashauri (5th June 2009), semilong (5th June 2009), SteveD (5th June 2009), Waga (5th June 2009), Wambandwa (5th June 2009)

ohhh dear!
 
mwanakijiji ungekuwa unajua jinsi unavyochukiwa......4 ur information linaandaliwa fungu kukununua......tukikuona kimya tutajua umeshafika bei......

hebu tupumzishe..yaani hataka juma tano hatujaingia!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom