Rostam Aziz kuvuliwa Uraia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz kuvuliwa Uraia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 5, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwaka Jana mwezi Juni, Mchg. Mtikila alitoa tuhuma ambazo hazikupewa uzito unaostahili. Hata hivyo habari za hivi karibuni na uchunguzi huru uliofanyika unatupa sababu ya kuamini kuwa kuna kitu kuhusu maisha na uraia wa Rostam Aziz (Igunga - CCM) kinafichwa kwa makusudi au kwa kutegemea kuwa hakitaulizwa. Maelezo ya Mtikila aliyoyatoa mwaka jana ni haya yafuatayo aliyoyapa kichwa cha "Hatima ya Mwajemi Sakarir". Soma kijarida chako pia na ufanye uamuzi wako mwenyewe ni nini kinafichwa na kwa nini?

  HATIMA YA MWAJEMI SAKARIR (ROSTAM) AZIZ


  Kiini cha ufisadi wa kutisha na uporaji wa Nchi yetu, unaofanywa kama vile Watanganyika wote ni mataahira, ni kutoweka kwa uraia wa kweli wa kuipenda nchi yetu na kuwa na uchungu nayo wa kiwango cha uhanga kwa ajili yake. Kwa sababu ya 'utaahira' wetu nchi yetu imekamatwa na mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliuofanyika katika Benki Kuu na Hazina ya Nchi yetu, ambaye ni Mwajemi yaani raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.


  Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya 'mataahira' kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la 'Rostam'. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ng?ombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.


  Nilipoanza kuzungumzia uraia wa 'Rostam' Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo, ingawa alisahau kwamba Premji wa Kigoma alizaliwa hapa lakini hakuwa raia kwa sababu wazazi wake hawakuwa wameukana uraia wa kwao, wala yeye Premji hakuwa ameomba uraia kwa mujibu wa Sheria, hata kama aliweza kujipatia Passport ya nchi hii kwa njia za ufisadi kama alivyofanya yeye. 'Rostam' amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli.

  Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya Nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu.

  Kwa ufupi Sakarir alipofika nchini mwetu baada ya masomo yake Uingereza, aliunganishwa na viongozi watatu wa CCM waliokuwa marafiki sana ambao ni pamoja na Rais Kikwete.

  Rostam alipata nguvu ya kisiasa kwa kutumia mapesa mengi ya mfuko maalum wa nchi yao wa 'Iranians in Diaspora', aliyoyapata kama raia mwaminifu wa Iran, aliye na shughuli zenye maslahi kwa nchi yao katika nchi ya nje. Nguvu hii ndiyo iliyomtia Benjamin Mkapa mkononi mwake na kuwa msingi wa uhuni na jeuri yote aliyonayo leo.

  Mafisadi walionufaika na mtaji huo wa Sakarir Aziz ndio waliofanya uhaini wa kumpa Ubunge wa Igunga alipofariki hayati Charles Kabeho. Wazee wa Kiajemi waliolowea hapa, Hussein Heidari na Hassan nduguye ndio waliompokea kijana Sakarir Aziz kule Igunga, kwa sababu wanao uhusiano na mkewe Aziz yaani mama yake Sakarir au Rostam.

  Hawa wazee ndio waliomnadi huyu Mwajemi kwa wazee wa Igunga katika kuiba Ubunge wa Nchi ya watu ambao anawachukulia kuwa 'mataahira'. Sakarir Aziz anao nduguze wa kiume wawili yaani Jahangir Aziz ambaye alipigana kizalendo kabisa ile vita ya nchi yao dhidi ya Iraq, na wa pili ni Akram Aziz.

  Kamati yetu imejitolea kuwasaidia wananchi wa Igunga wanaotaka kufungua kesi dhidi ya Sakarir Aziz na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa kuwanyima uwakilishi Bungeni tangu Mbunge wao hayati Charles Kabeho alipofariki. Kwani Mwajemi wa Jamhuri ya Kiislamu, 'Rostam' Aziz hawajali kabisa wananchi wa Jimbo lile, hata katika maafa kama ya kukosa kabisa usafiri baada ya madaraja ya mto Mbutu kuzolewa na mafuriko, au machafuko yaliyotokana na masuala ya ushirikina.

  'Rostam' Aziz anashirikiana katika kupora Nchi yetu na gabachol* mwingine aitwaye Yusuf Manji, ambaye pia si raia wa nchi hii na akibisha ushahidi utatolewa.

  Bilashaka Wabunge safari hii watataka kujua ni nani hasa waliotoa Passports za Tanzania kwa 'Rostam' Aziz, Jahangir Aziz na Akram Aziz na kwa misingi gani.

  Wezi hawa wanaipora nchi hii bila huruma, na ndio wanaowaambia watawala wa CCM cha kufanya ili wakombe mapesa yetu B.O.T na Hazina, na kutumia matrilioni yetu kuwatia viongozi wetu ndani ya mifuko ya makoti yao, ambamo wanalishwa masazo yao na kuchomoza vichwa kuchungulia nje kama vindege kuwasanifu wananchi, na kurudi mifukoni mwao wakidhani wanakula kumbe wanaliwa wao na Nchi yao! Hatutaki Rais wetu wala Wabunge wetu wawe vindege ndani ya mifuko ya makoti ya 'Rostam' Aziz na Yusuf Manji!

  'Rostam' na yusuf Manji wapo Dodoma na shehena ya mapesa ya EPA, kwa kazi ya kuwanunua wabunge wanaowadharau kwamba eti ni mataahira, wawe karatasi ya msalani (toilet paper) ya kuwasafisha uchafu wao halafu na yenyewe itokomee pamoja na uchafu, kwani haiwi safi tena baada ya kutumiwa!

  Tunaitaka Serikali iwakamate hawa wahalifu hatari wa Taifa letu huko Dodoma na kuwapokonya makaratasi yao yote ya kusafiria na kuwaleta kizimbani maramoja kwa uharamia wote walioifanyia Nchi yetu.
  Saa ya ukombozi ni sasa!


  Mchungaji C. Mtikila
  MWENYEKITI WA KAMATI

  26/6/2008

  Maswali:
  Kwanini Rostam hakufungua mashtaka dhidi ya Mtikila ya kumzushia kuwa si raia na kujaribu kumchafua jina lake ukizingatia kuwa tuhuma ya kuitwa "fisadi papa" na ya kuambiwa kuwa si "raia" hiyo ya "papa" ni mtoto tu?

  Kwanini serikali haikumkemea Mtikila na kumpiga mkwara wa kumchukulia hatua n.k )?
   

  Attached Files:

 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  Hayo maneo hapo juu yananitia uchungu sana! Huu ni ukweli kuhusu uhusiano wa hawa mafisadi, CCM na Viongozi wasiokuwa na maadili wala uzalendo, wala akili za kutambua kuwa wanaliwa wao pamoja na nchi yao!

  Hata kama Mchg. Mtikila alituhumiwa kupokea 3m za RA, this man is more patriotic compared to hawa viongozi wengine wa CCM wanaokumbatia mafisadi!

  Sijui hii article ilkuwa wapi siku zote hizi......asante MMM kwa kuiweka hii kitu hapa!
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  -MTIKILA PIA,ameonyesha udhaifu mkubwa sana baada ya KUNYWEA,pale 'papa' alipoweka wazi kwamba mbona mikila pia alienda kukopa hela kwake 'kwa ajili ya kuliendesha kanisa!

  -kwa hiyo hata wapiganaji wetu SIO SAWASAWA!njaa zinatumaliza.mtikila pipa sasa hivi HAONGEI TENA JUU YA HUYU MTU,jaribu kuchunguza!jamaa 'alimshika pabaya'

  -tutafika tu lakini
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Mtikila aliingia kwenye mtego wa rostam kijinga kabisa, actually mtikila hakuwa na malengo ya kukopa hela kutoka kwa Rostam, lakini rostam alipoona mtikila kapiga pentagon, alitumia akili ileile ya kitapeli na kutuma wapambe kwa Mtikila na kumwambia jamaa anatoa mikopo kiraisi tu we ngoja tukuungainishe nae ili akupe chochote, lakini bila kujua plan ya fisadi rostam, maskini mtikila na njaa yake akaingia kwenye makono ya rostam na ndio ukawa mwisho wake

  Hili lililomkuta Mtikila hayupo pekeyake, wapo wengi mno, Mtikila kaamua kukaa kimya lakini kuna wengine (Manyerere Jacton) wapo majukwaani kabisa kumtetea huyo jamaa kwa sababu wameshakula cha watu
   
 5. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inaonekana viongozi wetu ni dhaifu, haiwezekani tuhuma nzito kama hizi wanyamaze kimya wakati Mengi kataja mafisadi papa wanaagiza vyombo vya dola vimhoji kunani hapa?

  Uchaguzi ujao wa 2010, mdahalo uwepo ili tuchuje vizuri viongozi wetu. Nafasi ya Urais ni nyeti sana tumeona President Obama anavyoendesha nchi ya Marekani na kupata uungaji mkono duniani kote.

  Nawashauri waandishi tumieni dhima kuu ya kuaminiwa na jamii kulipatia msisitizo jambo hili. Mgombea yeyote atakayejaribu kutafuta visingizio ya kukwepa mdahalo ajengewe mazingira ya kuonekana hafai na dhaifu kwa wadhifa nyeti kama hiyo!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kinachonishangaza ni je utunzaji wa rekodi mbalimbali za wakazi wa Tanzania (siyo lazima raia) ukoje mpaka ishindikane kujulikana mtu katokea wapi na vipi?

  Kwa nini asichunguzwe? Iweje mtu apate passport ya Kitanzania kienyeji enyeji? Basi tuna "watanzania" wengi.

  Kuna maswali mengi ya kuulizwa na yalipaswa yachunguzwe ukweli ujulikane. Mimi naona jamaa analindwa sana maana haya maswali siyo vigumu sana kuchunguza na kupata majibu yake.

  Tanzania tunatia huruma kama hata wageni wanakuja na kutuibia chini ya "mwamvuli" wa utanzania. Na mtu kama huyu akiulizwa defense yake ya kwanza kuwa kuna ubaguzi. Tanzania inatia huruma.

  Nawalaumu hao watanzania wajinga waliokubali kutumiwa ili kumpatia anachotaka.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Unajua hili swala lilimpotezea credibility na moral authority ya kumsema RA. Hata kama alikuwa anasema ukweli baada ya ile scandal ya kukopeshwa ilikuwa ngumu kwa mtu yeyote kumchukulia serious.

  Mtikila naye alifanya kosa ambalo ni kutokujua kuwa for every attack there is a counter-attack. Kabla ya kuweka mabo hadharani alitakiwa achunguze alicho fanya huko nyuma. Pia ali takiwa kujua jamaa lazima ata jibu mapigo kwa hiyo ali paswa kujiandaa kuwa je RA akini jibu hivi mimi nijibuje? He didn't anticipate RA's move thus he was caught by surprise.

  Kwa sasa Mtikila kumsema RA na watu waamini inabidi atoke na very concrete proof isiyoacha any question marks.
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Jun 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wewe una uhakika ameipata kienyeji ? Au unafuata mkumbo tu
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Better safe than sorry. Kama uraia wa mtu una question marks ni bora kuchunguzwa. Kama uraia wake ni wa haki ita gundulika kama siyo nayo ita gundulika.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  sasa mtu siyo raia wa tanzania, je passport ya tanzania amepataje?
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Jun 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuleta vithibitisho ? Usihukumu mtu kama una vithibitisho peleka swala hilo katika vyombo vya sheria sio unachokonolewa tu na wewe unakubali kuchokonoleka
   
 12. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #12
  Jun 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  watu wengi tanzania uraia wao una maswali mengi kutokana na taratibu zilizokwepo
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  taabu ya wa-CCM ndo hii, ukiuliza kitu wanajitetea kwanza "lete uthibitisho". Hata mambo ya wazi mnataka uthibitisho? Niambie wewe RA ni mkurya, msukuma, mhaya au? Na je, katiba ya tanzania uraia wa nchi mbili?

  Je, Rostam aliwahi kuukana uraia wa iran?

  Unasema vyombo vya sheria? vyombo vya akina Hosea? hata kutafsiri sheria wanashindwa?

  Rostam asubiri tu ni suala la muda na nakwambia na nilisha toa thread siku chache zilizo pita, rostam atakimbia nchi hii muda siyo mrefu.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu hiyo unasema kutokana na utaratibu basi mtu uraia wake ukiwa na mashaka asiulizwe?

  Kumbe unajua kuna watanzania wengi ambao uraia wao una mashaka kwa nini usidai wachunguzwe? Mtu kuchunguzwa au kutiliwa mashaka siyo kuhukumiwa. He is innocent until proven guilty ila ni huo innocence unaotakiwa kuthibitishwa.
   
 15. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #15
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yaani, tumeshindwa kum-nail RA kwa ufisadi wake sasa tunaangalia uraia? What difference does it make?
  Fisadi+Tanzanian, Fisadi+Non-Tanzanian they all deserve to be locked up and the key thrown away.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mkuu hii ni mikakati from uraia tunaweza kabisa kumfukuza huyu jam.bazi nchini
   
 17. c

  chabeby Member

  #17
  Jun 5, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa naamini kuwa CCM na serikali yake ni MATEKA wa MAFISADI!! watanzania tumekosa nini? kufa kwa Mwalimu Nyerere ndio kumewafanya viongozi wa CCM kuwa vipofu namna hii? kinacho wafanya wanamn'gang'a nia FISADI nini? huyu jamaa anaitoa wapi jeuri yake?

  Kwani viongozi wetu wamenunuliwa kiasi gani ili wananchi twenye uchungu na nchi yetu tuchangane pesa tuwarudishie!! Kama mtu ana uraia wa nchi 2 tayari kakosa sifa za kuwa raia wa Tanzania sasa kwa nini mtu huyo anakuwa sehemu ya kutunga sheria wakati tayari yeye kashaivunja kabla hata ya kuingia Bungeni?

  CCM wamerambishwa nini na huyu mtu mwenye kiburi hata cha kutumia chombo cha UMMA (TBC1) kujisafisha kwa maji ya taka? tena huku akiwa katokea ikulu kwenye kikao kilichohusisha viongozi wakubwa wa nchi? Kwani viongozi wetu wamepigwa sindano gani ya ganzi inayowafanya wasizinduke tena kutoka kwenye nusu kaputi iliyowalenya?

  kwa nini huyu Fisadi hashughulikiwi? amewapa nini viongozi wetu?

  NINA HASIRA NAYE SANA HUYU maana ndugu zetu wasio na hatia wanakufa kwa njaa na kukosa madawa ila yote ni kwa ajili ya huyu fisadi papa!!
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  So you agree if he is a fisadi he should be locked up ni matter his citizenry? If you agree then I don't see why you would be against his citizenry to be questioned. If the man is innocent he can walk free.
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji naomba kuuliza, hivi Gen. Kombe alipouawa ni kweli kwamba yeye alikuwa anapinga ufisadi uliokuwa umeanza kujitokeza ndani ya ikulu miaka hiyo?
   
 20. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Rustam Sakarir Chakaar Abdurasul Aziz Rostam "Mchelee"!!

  The King maker! I salute You!, kwa umri ulio nao Mzee umefanikiwa sana.

  Pokea HONGERA kutoka kwangu ya dhati kabisaaaa!

  FP
   
Loading...