Rostam Aziz anavyompiga tafu rafikiye Lowassa

Rostam Aziz anavyompiga tafu rafikiye Lowassa

Hata walioiba kwenye richmond, chenji ya rada, epa nao ni masikini

Ndio wanohitajika kwenye Baraza letu la mawaziri.Acha wivu kaka tuachie wenyewe tutakapo shinda tu wale wote waliochota ESCROW lazima tuwasupport.........maana hawa ndiyo wenye nchi wenyewe
 
Lowassa usimwache kijana huyu kwenye safu yako naamini atuhitaji kuongozwa na waheshimiwa maskini ndio maana wakifika kule wanaiba na kusahau kilichowapeleka.
Mkuu utakuwa na mawazo ya kijnga sana hivi kweli mtu mwizi kama Rostam awe waziri wa fedha mtu ambaye hata uraia wake unatiliwa shaka.
 
mtoa post wewe kichaa chako ni cha hali ya juu sana wakina kinjekitile junior hawakufikii

Sasa wewe umetukosea HAKI watanzania,kama RAIS ni wa kaliba ya LOWASSA unategemea tupate MALAIKA wawe team yake ya miavuli?Amesema anachukia UMASIKINI unategemea amweke maskini hapo?Kaka jumlisha tu utapata jibu sahihi.................

Nakusaidia tu ili usipandwe na JAZBA ukapata BAN bure!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni kweli Tunahitaji watu kama Rostam Azziz,Chenge,Karamagi,Nyalandu,Ngeleja.Mzee wetu hakikisha ile team yote ya Richmond,EPA,na ESCROW lazima ziwepo kwenye Jeshi lako la miavuli.Usiwasahau wauaji wa RAIA wasio nahatia pia tutawahitaji sana,hasa yule aliyeua kule Arusha huyo naona akiwa Waziri wa Ulinzi na JKT ataweza kwa uhakika siyo tu kupambana na raia bali kuhakikisha raia wote watakaojifanya kutafuta HAKI zao kupotea tu kwa siri au kwa wazi.

Na hakikisha sheria ya Askari yoyote atakayeondoa MAISHA ya mpinzani atazawadiwa ubunge au Ukuu wa wilaya

Ukiawaacha Watanzania hwatakusamehe kamwe.............:A S 109::A S 109::A S 109::A S confused::A S confused::A S confused::A S confused:
Sure mkuu bila kusahau wale wezi wa arusha na migodini wote wawe sehemu ya serikali yake.
 
Lowassa usimwache kijana huyu kwenye safu yako naamini atuhitaji kuongozwa na waheshimiwa maskini ndio maana wakifika kule wanaiba na kusahau kilichowapeleka.

Kwa hiyo sifa ya kuwa waziri ni kuwa fisadi aliyekubuhu kwanza?
 
Lowassa usimwache kijana huyu kwenye safu yako naamini atuhitaji kuongozwa na waheshimiwa maskini ndio maana wakifika kule wanaiba na kusahau kilichowapeleka.

Mpwa unamaanisha...?
 
Sure mkuu bila kusahau wale wezi wa arusha na migodini wote wawe sehemu ya serikali yake.

Hahahahah:cheer2::cheer2::cheer2::cheer2::whoo::whoo::whoo:😛eace:😛eace: Simiyu ni wewe au?Karibu pande yangu hii.

Yaani wote hata wale wanonyang'anya wakulima ardhi zao wapewe nafasi za uwaziri wa ardhi itasaidia sana kuongeza pato la taifa kwa kuuza ardhi za wakulima.Na nyie wakulima mkatafute nchi ya kuishi sawa eh,msije mkatusumbua baadaye.........
 
mtoa post wewe kichaa chako ni cha hali ya juu sana wakina kinjekitile junior hawakufikii

mknd wako! tetea hoja badala ya kuja kuweweseka hapa kama kuku anayetafuta kiota cha kutagia.
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia namna Channel Ten inavyotumika kumpamba Lowassa kwenye taarifa zake za habari, na kufanikiwa kuunganisha dots kama ifuatavyo:

Siku zote Channel Ten wamekuwa wakiripoti taarifa za Lowassa kwa ustadi wa hali ya juu sana na taarifa zake hupewa air time ya kutosha tofauti na wagombea wengine ndani ya CCM.

Huu ni mpango maalumu wa Rostam Aziz (mmiliki wa Channel Ten) kumpigia debe fisadi mwenzake ili pindi akifanikiwa kuingia ikulu ya magogoni washirikiane naye kuiba rasilimali za taifa.

Mtakumbuka kwamba Lowassa, Chenge na Rostam ni mapacha watatu (utatu wa KIFISADI) ndani ya CCM. Hawa watu hawakukutana barabarani. Wamekuwa wakishirikiana katika shughuli zao za kulihujumu Taifa kwa muda mrefu sasa.

Mtakumbuka hata Nape Nnauye alijaribu kuwavua magamba akawashindwa. Endapo EL atafanikiwa kuingia ikulu mwaka huu, basi elewa kwamba ikulu yetu itageuka kuwa pango la wanyang'anyi. Tuwe makini na mafisadi hawa na kamwe tusiwaruhusu kuisogelea ikulu yetu.

:israel:
viroba ni vibaya sana,bila shaka mwandishi na wewe ulikuwa umevigida vya kutosha
 
Huu ni mpango maalumu wa Rostam Aziz (mmiliki wa Channel Ten) kumpigia debe fisadi mwenzake ili pindi akifanikiwa kuingia ikulu ya magogoni washirikiane naye kuiba rasilimali za taifa.

Mtakumbuka kwamba Lowassa, Chenge na Rostam ni mapacha watatu (utatu wa KIFISADI) ndani ya CCM. Hawa watu hawakukutana barabarani. Wamekuwa wakishirikiana katika shughuli zao za kulihujumu Taifa kwa muda mrefu sasa.

Mtakumbuka hata Nape Nnauye alijaribu kuwavua magamba akawashindwa. Endapo EL atafanikiwa kuingia ikulu mwaka huu, basi elewa kwamba ikulu yetu itageuka kuwa pango la wanyang'anyi. Tuwe makini na mafisadi hawa na kamwe tusiwaruhusu kuisogelea ikulu yetu.

:israel:

Hivi mbona mnadhani kuwa sisi wote ni "mapumbavu" kama walivyo wanachama wa chama chenu? (Chama Cha Mapumbavu aka FISI WENU). Wizi wa rasilimali unaoendelea hamjauona tu mnangojea Lowassa aingie madarakani? Na hao mapacha watatu si ndio wamemwingiza madarakani raisi aliyepo? Au hujui. Ni hujuma gani ambayo wanashindwa kufanya hivi sasa na hata wakati mwingine wowote rais yeyote wa FISI WENU akiwa madarakani? Huu usanii wenu kaufanyieni Lumumba.

Eti ikulu itageuka kuwa pango la wanyang'anyi, igeuke mara ngapi? Madhali FISI WENU wapo madarakani ikulu ni pango la wanyang'anyi, full stop! Au hujui mambo ya Escrow nini? Unadhani kwanini hawakutoa orodha ya waliochukua fedha Stanbic bank mpaka leo? Muulize kiongozi wa Agizo la Chama Tawala. Sasa anadandia walioweka fedha Uswisi wakati zilizochukulia hapahapa kashindwa kusema. Muulize mwenyekiti wa Kamati husika tutajie nani alichukua fedha Stanbic bank, uone atakavyotoka nduki. We acha Manyang'anyi yaliyopo ikulu ni habari nyingine. Tena alipoingiliwa bungeni na mmoja wa hao mapacha kuhusu hoja zake za Escrow, nusura azimie. Hoja zote zikadoda. Mpaka leo kafunga domo.

Halafu unakuja hapa na ujasiri eti ikulu itakuwa pango la wanyang'anyi, liwe mara ngapi ndipo ujue limekuwa?
 
Hapana shaka sasa Rostam Aziz na Hussein Bashe wanatumia kila aina ya propaganda kupitia vyombo vyao vya habari kama Gazeti la Mtanzania na kituo cha Television cha CHANNEL TEN kujaribu kuuaminisha Umma kuwa Swahiba wao mkubwa, Edward Ngoyayi Lowassa hatendewi haki Katika mchakato unaoendelea wa kumpata Mgombea urais wa CCM atakaepeperusha bendera ya Chama hicho hapo mwezi Oktoba Mwaka huu,. Leo katika taarifa ya habari ya Channel ten saa 12:00 asubuhi, huku mtangazaji akiisoma taarifa bila kujiamini alisema: "Habari zilizotufikia ktoka Dodoma zinasema kucheleweshwa kwa vikao vya mchujo ni mizengwe iliyoandaliwa ili kumkata Lowassa na kwamba ameandaliwa Jaji mmoja(mtangazaji hakumtaja jina) kuandaa waraka mzito kuhusu Maovu ya Lowassa. taarifa hiyo pia ipo katika gazeri la Mtanzania kwa kichwa cha habari, MKAKATI KUMUENGUA LOWASSA WAVUJA. Swali la kujiuliza hapa ni kwanini mizengwe hiyo iibuliwe na vyombo vya habari vya Rostam Aziz pekee kati ya magazeti mengi na vituo kibao vya TV? Propaganda hizi zinaweza kuwa na lengo la kuandaa mazingira yafuatayo:
1. Kupata uhalali wa kuandaa vurugu kwa kisingizio cha Lowassa kutotendewa haki
2. Kuandaa wana CCM kisaikolojia kuwa bendera fuata upepo pale lowassa atakapo amua kuhamia chama kingine kwa kisingizio cha kutotendewa haki.

Tabia hii siyo nzuri kabisa, ni hatari kwa amani ya nchi kwani CCM ni chama kikongwe ambacho kina kanuni zake za kumpata mgombea
Siyo tu anayekubalika kwa wanancni kwa kuwanunua bali anayekubalika kwa wananchi kwa hiari yao.
Sasa kwa matumizi haya ya nguvu ya Rostam Aziz, Rostam ambaye alipokuwa akiwaaga wananchi wa Igunga alisem amechoshwa na siasa uchwara ndani ya CCM, Rostam ambaye amelifilisi taifa kwa biashara haramu, makampuni hewa na uchafu Mwingi, ni wazi taifa linakwenda kuangukia kwenye Mikono isiyo salama.
Ni HERI LOWASSA KULIKO ROSTAMA AZIZ, LAKINI JE INAWEZEKANA LOWASSA BILA ROSTAM?
 
mtajua!! lowassa ni wenu tu, na safari ya matumaini lazima muitembee, hamtaki - mnataka!!
 
Back
Top Bottom