Hapana shaka sasa Rostam Aziz na Hussein Bashe wanatumia kila aina ya propaganda kupitia vyombo vyao vya habari kama Gazeti la Mtanzania na kituo cha Television cha CHANNEL TEN kujaribu kuuaminisha Umma kuwa Swahiba wao mkubwa, Edward Ngoyayi Lowassa hatendewi haki Katika mchakato unaoendelea wa kumpata Mgombea urais wa CCM atakaepeperusha bendera ya Chama hicho hapo mwezi Oktoba Mwaka huu,. Leo katika taarifa ya habari ya Channel ten saa 12:00 asubuhi, huku mtangazaji akiisoma taarifa bila kujiamini alisema: "Habari zilizotufikia ktoka Dodoma zinasema kucheleweshwa kwa vikao vya mchujo ni mizengwe iliyoandaliwa ili kumkata Lowassa na kwamba ameandaliwa Jaji mmoja(mtangazaji hakumtaja jina) kuandaa waraka mzito kuhusu Maovu ya Lowassa. taarifa hiyo pia ipo katika gazeri la Mtanzania kwa kichwa cha habari, MKAKATI KUMUENGUA LOWASSA WAVUJA. Swali la kujiuliza hapa ni kwanini mizengwe hiyo iibuliwe na vyombo vya habari vya Rostam Aziz pekee kati ya magazeti mengi na vituo kibao vya TV? Propaganda hizi zinaweza kuwa na lengo la kuandaa mazingira yafuatayo:
1. Kupata uhalali wa kuandaa vurugu kwa kisingizio cha Lowassa kutotendewa haki
2. Kuandaa wana CCM kisaikolojia kuwa bendera fuata upepo pale lowassa atakapo amua kuhamia chama kingine kwa kisingizio cha kutotendewa haki.
Tabia hii siyo nzuri kabisa, ni hatari kwa amani ya nchi kwani CCM ni chama kikongwe ambacho kina kanuni zake za kumpata mgombea
Siyo tu anayekubalika kwa wanancni kwa kuwanunua bali anayekubalika kwa wananchi kwa hiari yao.
Sasa kwa matumizi haya ya nguvu ya Rostam Aziz, Rostam ambaye alipokuwa akiwaaga wananchi wa Igunga alisem amechoshwa na siasa uchwara ndani ya CCM, Rostam ambaye amelifilisi taifa kwa biashara haramu, makampuni hewa na uchafu Mwingi, ni wazi taifa linakwenda kuangukia kwenye Mikono isiyo salama.
Ni HERI LOWASSA KULIKO ROSTAMA AZIZ, LAKINI JE INAWEZEKANA LOWASSA BILA ROSTAM?