Rostam acha siasa - Cheyo

Mwenyekiti wa UDP amemshauri bwana Rostam kuachana na siasa na kufanya biashara kwani upepo wa kisiasa nchini kwa upande wake ni mbaya mno, amemshangaa kukaa kimya licha ya tuhuma lukuki zinazomwandama.

Source: Mlimani TV
Maoni yangu
Namuunga mkono Cheyo lakini hata akiacha siasa arudishe pesa zote alizokwiba from his dirty deals na ajisalimishe mwenyewe Polisi.

nilidhani anamshauri aache ufisadi!!!!
 
Mwenyekiti wa UDP amemshauri bwana Rostam kuachana na siasa na kufanya biashara kwani upepo wa kisiasa nchini kwa upande wake ni mbaya mno, amemshangaa kukaa kimya licha ya tuhuma lukuki zinazomwandama.

Source: Mlimani TV
Maoni yangu
Namuunga mkono Cheyo lakini hata akiacha siasa arudishe pesa zote alizokwiba from his dirty deals na ajisalimishe mwenyewe Polisi.

ni sawa lakin namshauri hata yeye mwenyewe cheyo aache siasa maake anaongea utumbo mwingi kuhusu cdm bila sababu za msingi
 
Siyo RA aache siasa tu. bali JK anapaswa amchukulie maamuzi magumu pia ya kufikishwa katika vyombo vya dola.
 
Maelezo ya Mh. Cheyo yanaacha maswali mengi makubwa kuliko majibu.

1. Ni sheria gani Tz inayo kataza wafanyabiashara kuwa wanasiasa, maana nijuavyo mimi kuna wafanyabiashara kibao ambao mi wanasiasa kutoka vijijini hadi Taifani leo nchini Tz, tukianzia na yeye unless tumwombe Mh. Cheyo afafanue Mfanya Biashara ni nani kwa mujibu wa hiyo sheria ninayoisubiri au Kanuni ya Bunge. Aidha ni kwa nini wakati wa kutangaza nafasi za kugombea, sifa ya kuwa mfanya biashara na definition yake isiwekwe waziwazi kuwa ina m- disqualify mgombea? Je anajua kuwa hata kuwekeza katika kampuni fulani au kuwa na hisa au kuchukuwa mazao ya shamba lako na kuuza n.k pia ni kufanya biashara, vitu ambavyo Mawaziri, Wabunge , Madiwani wengi tu wako katika kundi hilo?

2. Anaonyesha kuwa watu (wengine) wana machungu na Rostam; je yeye Cheyo, naye ana hayo machungu (naomba kujua position yake)

3. Ukiendea kwenye media na kusema waziwazi kuwa ungekuwa wewe 'ingekuwa OUT'; sasa tunaomba Cheyo utamke waziwazi makosa ya Rostam na siyo kusingizia uchungu walionao watu wengine au kutunga kosa (maana sijaona sheria mimi ya kukataza kwa mwanasiasa na pia mfanya biashara).

Mtu haukumiwi kwa hisia tu za watu wengine na Cheyo kama kiongozi wa chama Kitaifa hawezi kusema tu 'OUT bila kuwa na uthibitisho fulani wa makosa ya Rostam. Na endapo hilo ndivyo, je pendekezo lake la 'Out' sijui kutoka katika Chama au katika uongozi linatosha? Kwa nini asiseme kuwa angekuwa yeye angemfikisha katika vyombo vya sheria?

Natamani ningekuwa mwandishi wa habari tumrejeshe Cheyo na kumpa nusu saa kwenye Conference ajibu hizi hoja zangu tatu waziwazi! Vinginevyo nitarudi hapa na kutoa tafsiri yangu ya kile alichokuwa anajaribu kukifanya!

Cheyo alifirisika kule Swaziland na viwanda vyake vya nguo vikauzwa. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kurudi TZ. Kwa sasa hana kitu zaidi ya kutegemea ubunge. Enzi za Swazland jamaa alikuwa na majigambo siyo mchezo ndiyo maana hata baada ya kurudi Bongo alikuja na Bez lake na those days alikuwa anatembea na body guard. Sijui kama bado anaendelea na huo mtindo au sasa kisha zoea amani ya Bongo na hahitaji ulinzi kama zamani!!!
 
Si kweli, kwa nafasi ambayo yeye alimteua (mweka hazina CCM) alimtoa tena kwa aibu kubwa, lakini ninyi wananchi mmemchagua kuwa mbunge wenu mlitaka afute ubunge wake? kwa nini mnaruka wajibu wenu? kwa vyeo vyote vya Rostam wananchi wakitaka wanaweza kumtoa.
Na hiyo ya kamati kuu? Ina maana JK kama mwenyekiti hana uwezo huo?
 
hivi Rostam ni mmoja wa wale mafluke wanaopita bila kupingwa?........maana kama wananchi walipiga kura basi wakulaumiwa ni wananchi wa Igunga.
 
SIo aache siasa tu tumfikishe na mahakamani arudishe mali zetu alizotupora

Na kisha tumfukuze nchini kabisa, aende huko Iran au Kanada tumemchoka kwa kweli. Jamaa kateka watu muhimu wote na sekta ya umeme anaihujumu kila kukicha akimtumia waziri aliyemweka pale. Maana sijawahi kumsikia Ngeleja akizungumzia ule mradi mkubwa wa Stiegler Gorge hata siku moja sijuwi nyie wenzangu labda alishasema sikumsikia. Maana huo mradi ndo mwarobaini wa tatizo la umeme nchini. Rubada kuna kipindi (mwaka jana) walisema Wachina walishafika TZ wakiwa na vifaa vyote tayari kwa ujenzi wa mradi huo tena kwa pesa zao lakini serikali ikawawekea mizengwe. Kwanini? Inawezekana ili majenereta ya Rostam yapate biashara huku waTZ tukitaabika na mgao.
 
Kwa Tanzania siasa za ukweli ziko CDM huko UDP na kwingineko ni gelesha tu; hakuna aja ya kuumiza kichwa na maneno ya Cheo. Tusonge mbele tu hadi kieleweke.
 
Kushitakiwa ndio jawabu. Cheyo naye busara iko wapi?

Busara ya Cheyo ilianza kupotea siku nyingi. Anafurahia posho za kwenye kamati za Bunge bila kujali upinzani unaathirika vipi na hilo. Ndo maana Chama Cha Mafisadi wanampenda sana siku hizi.
 
Mzee Mapesa anatumiwa na CCM na Serikali infact kwenye CCM karibia wote wana mwogopa RA, sasa wamemuomba mzee Mapesa amueleze RA ajiuzulu kwa njia hiyo ni kama vile Mwakiembe aliposema EL ajipime. Sasa hapa ni juu ya RA ajipime, kutokana na makashafa lukuki ajitoe, siku si nyingi ataitikia wito huu, utasikia kutokana na kukabiliwa na biashara nk nk najiuzulu ubunge nk nk.
 
Back
Top Bottom