Rombo: Mchungaji ashikiliwa kwa kumbaka muumini

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo katika Kijiji cha Manda Chini wilayani Rombo, Amani Upendo kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wakati akimfanyia maombi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema tukio hilo lilitokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo alipokwenda kwenye maombi, baada ya familia yake kuzunguka kwa muda mrefu kumtafutia tiba ya ugonjwa wa kuanguka uliokuwa ukimsumbua.

“Huyu mchungaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumbaka mwanafunzi, aliyekuwa na ugonjwa wa kuanguka, baada ya familia kujaribu kumtibu hospitalini pamoja na sehemu nyingine ikashindikana.

“Hivyo wakaamua kumpeleka kwenye maombi, kwa hiyo akiwa kwenye maombi ndipo mchungaji alipofanikiwa kumbaka," amesema Kanali Maiga.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, Mwenyekiti wa Kijiji Manda Chini, Ernest Mrosso amesema siku hiyo wakati tukio linatokea binti huyo alikuwa ametumwa kusaga mahindi aliporudi nyumbani alijiandaa kwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kwenda kuombewa.

"Alipofika nyumbani aliacha ule unga akawa amekwenda kwenye maombi na alikuwa na wenzake ikafika mahali mchungaji akawaambia wale aliokuwa nao waondoke yeye ataendelea kumwombea binti huyo.

"Wakati akimwombea huyu mtoto alidondoka chini ndipo mchungaji alipomchukua na kwenda kumfanyia unyama huo aliofanya, hatimaye mtoto alipokuja kuzinduka ndio akakuta tayari amefanyiwa unyama huo ndipo alipochukuliwa na kupelekwa hospitali," amesema Mrosso.

Mwenyekiti huyo amelaani kitendo hicho huku akisema ni unyama ambao haufai kabisa kwa kiongozi wa kiimani kufanya tukio la namna hiyo na kusema ni kitendo ambacho kimeichukiza jamii.

Chanzo: Mwananchi
Hi dini wepesi Sana kumuamini mtu, yaani wao mtu akitokea tu from nowhere akisema yeye nabii tayari washamuamini, mtu yupo tayari amruhusu mkewe usiku akalale kwa mchungaji hili aombewe, halafu walivyo wajinga wakiambiwa kweli hasira zao wanamalizia kwa Waislamu
 
Mbona hata huko kuna baadhi ya mapadre, maparoko ambao wamekuwa wakikutwa na tuhuma kama hizi, na wakati mwingine hadi kulawiti watoto wa kiume...

Huu ushetani kwa sasa hauna cha dhehebu wala dini, tuwalinde watoto zetu...
Ni kweli, hayo ni matatizo ya mtu mmojammoja binafsi, so watu wasitumie kuhukumu mapungufu ya mtu mmoja kuhukumu dini au dhehebu la mtu mwingine, karibu kila sehemu wapo, msafara wa nzige na panzi wamo
 
Takata kabisaaa... sisi warombo tuliamua kubaki njia kuu. Watarudi wenyewe parokiani. Kuna ndugu zangu wamefunguaga kanisa miaka na miaka ni walokole tena sijui ndo wamekua wachungaji wa kusomea kbs ila ni wachafu na wazinzi wakubwaaa. Wakija mbele ya halaiki utasema ni malaika. Anyways, huwa hawaenjoy saana wakija kijijini... maana kila mtu anazungumzia Misa na siyo kwa nabii
Mkuu,
Hata huko Katioliki mbona wanafanya hayo mambo ya uovu?!!

Ndio maana hairuhusiwi kukaa jinsi mbili tofauti peke yenu.maana kinachofuata ni hicho .hapo lazima shetani awe katikati yenu.
Ubaya hauna kwao.
 
Kuna haja ya watumishi wa Mungu kuwekewa kigezo cha elimu japo wahuni kama huwa hawaishi makanisani kama walivyo mtaani. Huyo si mchungaji wa Mungu bali mchungaji wa shetani na ni mhuni kama wahuni wahovu walioko mtaani japo alijificha kwenye kivuli cha dini tu. Sheria imuadabishe kama funzo kwa watu wengine.
 
Kuna mstari umerukwa hapa , wale wataalam wakusoma between the line tutakubaliana kuwa Kuna mstari umerukwa hapa

1 Iliwezekanaje family nzima tena wake kwa waume yaani Baba Mama mjomba ,majirani hadi mzee wa ukoo wamuache mgonjwa teeena binti wa kike kwa mchungaji teena mchungaji wa kiume peeke yake

Inatuingia akilini hii?

anyway , ngoja niwasogeze kidogo .

Kwa wasiyofika wala kujua misingi ya Imani ya wa Rombo

99.9% ya Wa Rombo ni wakatoliki kindakindaki tuzingatie hilo ,kiasili wakatoliki huwa hawawaamini wala kuwabali kabisa wazee wa shika neno tenda neno

Swali la kuanzia ilizezekanaje jamii nzima niliyoieleza hapo juu ikawa na utayari wakumwaamini mtu imani nyingine kwa viwango hivyo?

Hebu tuweke nukta

Kwa mujibu wa mwandishi wa hiyo habari nikama anaonyesha anachuki na mchungaji , vinginevyo atusaidie kujua alijuaje kuwa tendo hilo lilifanywa nyakati mgonjwa akiwa amepoteza fahamu na siyo kabla hajafika kwa mchungaji?

Alimkagua kabla?

Taarifa yake ni kwa mujibu wa daktari? Ikiwa hapana ,na inaelezwa kuwa hakukuwepo na mtu zaidi ya mgonjwa na Baba mchungaji , yeye alijuaje?

Hii ni dhana hasi ya kutaka kutuchafulia viongozi wetu wakiimani ,, ifahamike kuwa makanisa yakiuamsho Rombo yanapigwa vita sana ,

Siku hizi dini ni biashara , na zina mbinu zote zakiushindani kama wafanyianazo washindani wakibiashara wengine .

neno langu ,wakuu tujihari, tusije tukajikuta tunajiingiza kwenye ugomvi usiyo tuhusu .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo katika Kijiji cha Manda Chini wilayani Rombo, Amani Upendo kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wakati akimfanyia maombi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema tukio hilo lilitokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo alipokwenda kwenye maombi, baada ya familia yake kuzunguka kwa muda mrefu kumtafutia tiba ya ugonjwa wa kuanguka uliokuwa ukimsumbua.

“Huyu mchungaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumbaka mwanafunzi, aliyekuwa na ugonjwa wa kuanguka, baada ya familia kujaribu kumtibu hospitalini pamoja na sehemu nyingine ikashindikana.

“Hivyo wakaamua kumpeleka kwenye maombi, kwa hiyo akiwa kwenye maombi ndipo mchungaji alipofanikiwa kumbaka," amesema Kanali Maiga.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, Mwenyekiti wa Kijiji Manda Chini, Ernest Mrosso amesema siku hiyo wakati tukio linatokea binti huyo alikuwa ametumwa kusaga mahindi aliporudi nyumbani alijiandaa kwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kwenda kuombewa.

"Alipofika nyumbani aliacha ule unga akawa amekwenda kwenye maombi na alikuwa na wenzake ikafika mahali mchungaji akawaambia wale aliokuwa nao waondoke yeye ataendelea kumwombea binti huyo.

"Wakati akimwombea huyu mtoto alidondoka chini ndipo mchungaji alipomchukua na kwenda kumfanyia unyama huo aliofanya, hatimaye mtoto alipokuja kuzinduka ndio akakuta tayari amefanyiwa unyama huo ndipo alipochukuliwa na kupelekwa hospitali," amesema Mrosso.

Mwenyekiti huyo amelaani kitendo hicho huku akisema ni unyama ambao haufai kabisa kwa kiongozi wa kiimani kufanya tukio la namna hiyo na kusema ni kitendo ambacho kimeichukiza jamii.

Chanzo: Mwananchi
wachungaji wapumbavu kama hawa wakomeshwe.Wanawaibiaga waumini kwa kuwambia walipe kiasi cha fedha wawaombee matatizo yaishe.Sasa maombi yananunuliwa kwa hela wizi mtupu na ufuska.
 
Mkuu,
Hata huko Katioliki mbona wanafanya hayo mambo ya uovu?!!

Umeona nilichojibu huko juu?
 
Back
Top Bottom