Rombo: Mchungaji ashikiliwa kwa kumbaka muumini

Rombo: Mchungaji ashikiliwa kwa kumbaka muumini

Takata kabisaaa... sisi warombo tuliamua kubaki njia kuu. Watarudi wenyewe parokiani. Kuna ndugu zangu wamefunguaga kanisa miaka na miaka ni walokole tena sijui ndo wamekua wachungaji wa kusomea kbs ila ni wachafu na wazinzi wakubwaaa. Wakija mbele ya halaiki utasema ni malaika. Anyways, huwa hawaenjoy saana wakija kijijini... maana kila mtu anazungumzia Misa na siyo kwa nabii

Mbona hata huko kuna baadhi ya mapadre, maparoko ambao wamekuwa wakikutwa na tuhuma kama hizi, na wakati mwingine hadi kulawiti watoto wa kiume...

Huu ushetani kwa sasa hauna cha dhehebu wala dini, tuwalinde watoto zetu...
 
Mbona hata kuna mapadre, maparoki wamekuwa wakikutwa na tuhuma kama hizi, na wakati mwingine hadi kulawiti watoto wa kiume...

Huu ushetani kwa sasa hauna cha dhehebu wala dini, tuwalinde watoto zetu...
We Jamaa we unatafuta matatizo kwa hio unamsapoti jamaa kwa ujinga alioufanya?

Kweli wahuni sio watu
😬
 
Mbona hata huko kuna baadhi ya mapadre, maparoko ambao wamekuwa wakikutwa na tuhuma kama hizi, na wakati mwingine hadi kulawiti watoto wa kiume...

Huu ushetani kwa sasa hauna cha dhehebu wala dini, tuwalinde watoto zetu...
Hawakua na wito. Ila si hawa makanjanja wanaamka tu anakuambia ameoteshwa kuwa yeye ana maono na anafungua kanisa
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo katika Kijiji cha Manda Chini wilayani Rombo, Amani Upendo kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wakati akimfanyia maombi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema tukio hilo lilitokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo alipokwenda kwenye maombi, baada ya familia yake kuzunguka kwa muda mrefu kumtafutia tiba ya ugonjwa wa kuanguka uliokuwa ukimsumbua.

“Huyu mchungaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumbaka mwanafunzi, aliyekuwa na ugonjwa wa kuanguka, baada ya familia kujaribu kumtibu hospitalini pamoja na sehemu nyingine ikashindikana.

“Hivyo wakaamua kumpeleka kwenye maombi, kwa hiyo akiwa kwenye maombi ndipo mchungaji alipofanikiwa kumbaka," amesema Kanali Maiga.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, Mwenyekiti wa Kijiji Manda Chini, Ernest Mrosso amesema siku hiyo wakati tukio linatokea binti huyo alikuwa ametumwa kusaga mahindi aliporudi nyumbani alijiandaa kwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kwenda kuombewa.

"Alipofika nyumbani aliacha ule unga akawa amekwenda kwenye maombi na alikuwa na wenzake ikafika mahali mchungaji akawaambia wale aliokuwa nao waondoke yeye ataendelea kumwombea binti huyo.

"Wakati akimwombea huyu mtoto alidondoka chini ndipo mchungaji alipomchukua na kwenda kumfanyia unyama huo aliofanya, hatimaye mtoto alipokuja kuzinduka ndio akakuta tayari amefanyiwa unyama huo ndipo alipochukuliwa na kupelekwa hospitali," amesema Mrosso.

Mwenyekiti huyo amelaani kitendo hicho huku akisema ni unyama ambao haufai kabisa kwa kiongozi wa kiimani kufanya tukio la namna hiyo na kusema ni kitendo ambacho kimeichukiza jamii.

Chanzo: Mwananchi

Yaani kila sehemu imekuwa majanga kwa watoto wetu
 
Takata kabisaaa... sisi warombo tuliamua kubaki njia kuu. Watarudi wenyewe parokiani. Kuna ndugu zangu wamefunguaga kanisa miaka na miaka ni walokole tena sijui ndo wamekua wachungaji wa kusomea kbs ila ni wachafu na wazinzi wakubwaaa. Wakija mbele ya halaiki utasema ni malaika. Anyways, huwa hawaenjoy saana wakija kijijini... maana kila mtu anazungumzia Misa na siyo kwa nabii
Wewe mrombo wa wapi nisije nikatongoza mshiki...
 
Wachungaji wanawabandua sana wake,madem za watu

Ova
 
Back
Top Bottom