Rombo: Mchungaji ashikiliwa kwa kumbaka muumini

Rombo: Mchungaji ashikiliwa kwa kumbaka muumini

Ukweli kanisa la leo limevamiwa na wahuni,, kwa nnje ni watumishi lakini ndani yao wamejaa ushetani wash kutisha mathayo 24:24
 
Hizi mambo za sijui maombi ya mtu moja moja na wakati mwingine maombi hayo yanafanyikia Hotelini alikofikia mtumishi, kuna siku utakuja tolewa ushuhuda wa kutisha.

Yana anza, MAOMBI, Kisha MAOMBEZI Mwishoni UNA OMBWA
 
Tatizo udini na ukatoliki umemjah

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Weweee rudi shule mkuu kichwa chako kina matatizo wapi umeona nmeegemea kwenye dini ya mtu hapo ?

Usidhani kila anaesemea Jambo fulani baya kwenye ishu ya dini basi ni dini fulani

Acha kukaririri

Umekisoma alichokiandika huyo mtu hapo huoni km ana sapoti una watoto wa kike na wa kiume wewe?

Utajisikiaje mtoto wako wa kiume akilawitiwa na baba mchungaji wako alafu anatoka mwehu mmoja bila aibu anakuja kusema mboni huko Zanzibar mashekhe wanawalawiti watoto?

Wewe ukiwa na akili timamu utamchukuliaje km sio kwamba anasapoti huo ujinga?

Tumia akili zako vizuri sio kupingapinga kila kitu

Jitafakari mara tatu mkuu
 
Kwa mamlaka niliyo nayo natangaza rasmi nyege ni janga namba la 4 la taifa.
Huyo mchungaji uchwara naye ainamishwe hakuna namna ya kukomesha wahuni wanaobaka zaidi wao nao kubakwa kavu kavu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo katika Kijiji cha Manda Chini wilayani Rombo, Amani Upendo kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wakati akimfanyia maombi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema tukio hilo lilitokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo alipokwenda kwenye maombi, baada ya familia yake kuzunguka kwa muda mrefu kumtafutia tiba ya ugonjwa wa kuanguka uliokuwa ukimsumbua.

“Huyu mchungaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumbaka mwanafunzi, aliyekuwa na ugonjwa wa kuanguka, baada ya familia kujaribu kumtibu hospitalini pamoja na sehemu nyingine ikashindikana.

“Hivyo wakaamua kumpeleka kwenye maombi, kwa hiyo akiwa kwenye maombi ndipo mchungaji alipofanikiwa kumbaka," amesema Kanali Maiga.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, Mwenyekiti wa Kijiji Manda Chini, Ernest Mrosso amesema siku hiyo wakati tukio linatokea binti huyo alikuwa ametumwa kusaga mahindi aliporudi nyumbani alijiandaa kwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kwenda kuombewa.

"Alipofika nyumbani aliacha ule unga akawa amekwenda kwenye maombi na alikuwa na wenzake ikafika mahali mchungaji akawaambia wale aliokuwa nao waondoke yeye ataendelea kumwombea binti huyo.

"Wakati akimwombea huyu mtoto alidondoka chini ndipo mchungaji alipomchukua na kwenda kumfanyia unyama huo aliofanya, hatimaye mtoto alipokuja kuzinduka ndio akakuta tayari amefanyiwa unyama huo ndipo alipochukuliwa na kupelekwa hospitali," amesema Mrosso.

Mwenyekiti huyo amelaani kitendo hicho huku akisema ni unyama ambao haufai kabisa kwa kiongozi wa kiimani kufanya tukio la namna hiyo na kusema ni kitendo ambacho kimeichukiza jamii.

Chanzo: Mwananchi
MUNGU hadhihakiwi
 
Mkuu au Mimi kipofu
Emu soma hio sentensi vizuri sio kwa mhemuko inaashiria nini?

Sasa yeye ana maanisha nini hapo baada ya kupinga yeye ananasibisha na kile kinachofanyika kwa mlengo wa kwamba mboni wengine wanafanya sasa hio inamaanisha nini km sio kusapoti kinachofanyika?

Inamaana kwamba km wengine wanafanya kwa hio haitakiwi kupinga pale mwingine anatokea na kufanya Jambo km hilo au Mimi ni kipofu sioni?

Au wewe umeelewa nini hapo mkuu?

Nilimnukuu na kumkumbusha mtu aliyejielekeza kupeleka lawama kwa viongozi wa makanisa yasiyo ya kikatoliki pekee, kwamba hata katika kanisa hilo kongwe kuna viongozi wapumbavu wanaovuka mipaka ya uadilifu...(kuna jamaa ktk uzi huu wamefanya citations ya matukio husika kwa kuweka links unaweza ukapitia).

Unapohadaa umma kwa kuaminisha kwamba katika kanisa kongwe hakuna hayo matukio, ina maana wazazi wanaweza hadaika na kudhani watoto wao hawapo hatarini wakiwa kwenye kanisa kongwe.

Ndio maana nikahitimisha kwa kuandika, yatupasa watu wote kama wazazi/walezi, kuwalinda watoto wetu dhidi ya ukatili huu.

Natumai hadi hapa utakuwa umeelewa mantiki ya post ile...
 
Okay mkuu hapo sasa nimekuelewa vizuri labda uwasilishaji wako wa mwanzo ulipelekea Mimi kuelewa tofauti ila sasa nmekuelewa mkuu

Peace be upon you
Shalom!
 
Okay mkuu hapo sasa nimekuelewa vizuri labda uwasilishaji wako wa mwanzo ulipelekea Mimi kuelewa tofauti ila sasa nmekuelewa mkuu

Peace be upon you
Shalom!

Aleichem shalom
 
Back
Top Bottom