Role of Indians in the Tanzanian Economy

williams king

Member
Dec 3, 2006
34
2
habari za leo wanaforum sasa katika hii THREAD tujaribu kumshauri Rais wetu MUH. JAKAYA M.KIKWETE, tuongelee yale ambayo hawezi kuyaona kwa sababu bunge liko hoi,

yanafanywa na watendaji wake,ataasipochukua hatua ,basi naye ajuwe kwamba tumefahamu mchezo wa wanasiasa wa tanzania wanavyo fanya, pia

mataifa mengine yajuwe ,basi nchi iwekewe mashari ya kusaidia wananchi na siyo ahadi hewa kama vile mwaka umeisha ni matatizo tu sasa serekali

inasubutu kusema wameridhi matatizo kutoka serekali ya awamu ya tatu,
huku wanafanya sherehe kubwa na kuwaalika marais wa nchi nyingine kuja

kusheherekea MIAKA 45 YA UHURU ,sasa nimeamini nyiye ni wazee wa kuvuta raha hamjali nyumbani kuni kilio watu mnapiga DISCO,hapo JK,NA LOWASSA mnapunguza kura zenu 2010 au mpepanga muongoze kipindi kimoja tu, mnatumaliza alafu muwape upinzani siyo watu ambao hawana address,

hii serekali ina mbunge MLEBANONI na ndiye mshauri wa rais jamani mimi sijui hawa ni wafanya biashara hawaangalii masikini bwana,

sasa kuhusu wahindi akuna sehemu duniani wahindi wanakubalika ukiangalia NIGERIA malesia,singapore,kenya,uganga IDDI AMINI aliwafukuza ,tanzania , dili zote za serekali ndiyo wanafanya kenya wamemchafua moi wame mpaka mavi,

tananzania tuna wakumbapatia sasa angalieni walivyo tuingiza mkenge viongozi hawajui kesho wanajua leo tu basi wahindi wana watumia vizuri sana ,

angalia kazi kidogo tu nita zitaja kama nitakuwa nimekosea mnirekebishe mimi siyo mtanzania kuanzai MIKATABA YA MADINI madalali ni wahindi nita wataja majina baadaye,RADA,NDEGE YA RAIS, ITPL-RAIA MALESIA,RICHMOND,na biashara nyingi za uwingizaji bidhaa chafu kama chakula,mchele,sukari ,mafuta ya kula ,dawa za dinadamu,,na za mifugo,kilimo, n.k.

KILA KITU WALICHO FANYA HAWA WAHINDI KINATUGARIMU SANA PESA ZA WALALA HOI,YAHANI JK NA LOWASSA HAMJAJIFUNZA TU AU MNAKULA NAO MTU YEYOTE,
MWENYE ''DATA'' ZAIDI ZA HAWA WAHINDI AZIWEKE KWENYE HII FORUM ,

NAOMBA KUTOA HOJA

BY KING
 
Hao Wahindi Nao Ni Watanzania Kama Sisi Na Wana Haki Zote Za Kufanya Chochote Kama Watanzania Lakini Wasivunje Sheria Tu, Mimi Sioni Ubaya Wao Wala Longolongo Zao , Mimi Nimesoma Na Wahindi Maisha Yangu Yote Na Kwa Habati Mbaya Au Nzuri Kuna Shule Niliwahi Kwenda Ambapo Mswahili Nilikuwa Ni Mimi Mwenyewe Darasani Mpaka Katika Dom Ya Wanafunzi Nikaishi Kule Kwa Miaka 3 Sijaona Ubaya Wao Wala Uhuni Wao Na Mpaka Sasa Hivi Bado Niko Nao Tunakutana Mitaani Tunasalimiana Na Katika Mambo Mengine Ya Kibiashara Na Familia Yangu Sijaona Kosa Lao

Ila Wahindi Wanachotaka Ni Equal Oppotunities Kwa Mwafrika Hakuna Equal Oppotunity Ndio Maana Wanagombana Mara Kwa Mara
 
Hawa WTZ wenye asili ya Asia hususan India wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Viongozi wa serikali katika kuendelea kutafuna keki ya taifa bila aibu na wanaendelea kutesa tu. Tuliona jinsi Chavda alivyotunyoa, Tunaye mwingine Chande ambaye amekuwa akisifiwa sana na serikali ya UK, hivi sasa ameibuka Manji na mwingine ambaye ndio chimbuka la uuzaji wa Radar na vifaa kama magari Jeshini n.k. Sailesh Vithlani. Wote hawa wanajulikana na ndio wanasukuma dili zote kutoka serikalini kupitia mikononi mwao kwa wahindi wenzao na wageni kuendelea kuwakandamiza WTZ.

Hata waziri mkuu hivi juzi juzi tu alikuwa na sherehe kule Arusha ambapo wanaomsaidia kuiba keki ya taifa ndio walikuwa waalikwa mahsusi. Bila kusahau wachimbaji wa madini ambao wanashirikiana na viongozi wa taifa kutufilisi.

Je, ni jukumu la nani kuwafanya hawa WTZ waache mara moja kuiba keki ya Taifa wakati Serikali iliyopewa hiyo dhamana inasuasua? Je watakubali kushambuliwa binafsi kama vile vibaka wanavyouawa hadharani ambao wao huiba kuku tu? Je sisi walalahoi tuendelee kuwaangalia tu wakati tunaumia?
 
Mimi nadhani watu wa kuwashambulia ni JK na wanamtandao wenzake.

Manji, Chavda, Chande au yoyote ajaye huko mbeleni asipopata USHIRIKIANO wa WATUMISHI WETU Serikalini kamwe wasingeweza kula keki yetu ya Taifa.

Hivyo leo ukimfukuza Manji na kumuacha JK kesho atakjwa Chavda mwingine na kuendeleza alipoishia Manji. Tumuondoe JK na Manji...kisha tuweke SHERIA kali na watu waadilifu kulinda keki ya Taifa dhidi ya hawa wadokozi.
 
Hawa wadosi ni watoaji rushwa na wachukuaji wakubwa sana, lakini wanachotoa ni kidogo sana ukilinganisha na wanachochukua. Wameshakumbatiwa na "wasanii" isomeke viongozi, na hao wasanii wameshawekwa mifukoni mwa hao wadosi. Huyu manji inasemekana ndiye aliyekuwa "bank" ya baadhi wagombea wa juu kabisa wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005.

Angalia scandal alizonazo lakini anapeta tu maana wasanii wameshaahidi kumkingia kifua kwa lolote, lakini wananchi wanayaona mabaya yanayofanywa kama kilio cha walala hoi hakitasikilizwa na wasanii na kurekebisha kasoro mbali mbali ndani ya siri kali kuhusiana na utendaji wake, basi Tanzania inaelekea pabaya. Mwenyezi Mungu apishilie mbali. Hatuihitaji miaka mitano kutathmini utendaji wa wasanii wa awamu ya nne, maana "nyota njema huonekana asubuhi."
 
tumeanza na wachagga.. lets keep going..! hadi tujue ni mtanzania gani, ni kabila gani, ni watu wenye asili ya wapi watatuokoa! keep breaking the principle.. the "principle will find a way of breaking you" (Mwalimu)!
 
Wahalifu wooote washughulikiwe na sheria bila ya kujali asili au siasa zao.

Tatizo ninaloliona, na ambalo utanisuta nalo ni kuwa sheria hazifanyi kazi. Hapo nitakubaliana nawe moja kwa moja. Kwa hiyo kazi yetu sote kama taifa, iwe kuhakikisha kuwa sheria madhubuti zipo na zinaonekana kufanya kazi ipasavyo. Tutafanikisha vipi lengo hili? Hilo ndilo tatizo.
 
Mzee Mwanakijiji

tumeanza na wachagga.. lets keep going..! hadi tujue ni mtanzania gani, ni kabila gani, ni watu wenye asili ya wapi watatuokoa! keep breaking the principle.. the "principle will find a way of breaking you" (Mwalimu)!

Tatizo ni jinsi ambavyo unaweza kuendelea KUTAKA KUPOTOSHA HOJA NILIYOLETA, wizi wao sio wa kuiba kuku bali wa kulihujumu taifa, sielewi ni lini uliondoka Tanzania lakini ukweli ni kwamba kama huna pesa Tanzania wengi wao watakwambia inabidi waende kwa wahindi (gabacholi) wao/mhindi wangu, na sio niende kwa benki manager kujaribu kupata over draft au kukopa. Mkandara atarudi karibuni muulize akwambie.


A NATIONAL survey conducted last year has revealed that 89 per cent of the people do not have a formal bank account. According to a study conducted in July and August last year, 89 per cent of Tanzanians did not have a formal bank account. This is not a very healthy situation taking into account that banking is an important sector of the economy of any country.


Hii ni tabia ambayo inaendekezwa na wale ambao kwa njia moja au nyingine wanafaidi keki ya taifa bila kutoa jasho. Maneno ya mwalimu yalitolewa wakati tofauti na sasa na yalikuwa na malengo fulani ambayo ni lazima uyatafakari sio copy and paste business hapa. Hata kama unakumbuka vizuri mwalimu aliwakemea CCM na kuwaambia kuwa ingawa yeye alianzisha hicho chama wasifikirie kuwa CCM ni mzazi wake? Kama huna cha kuchangia soma kama wengine huna sababu ya kuleta hiyo topic ambayo wewe mwenyewe umeikimbia. VIPI UNATAKA KURUDI KWA MLANGO WA NYUMA? Kama una issue ya ukabila rudi kule utoe mawazo yako.
 
Tatizo sio wa asia, sheria zetu na viongozi wabovu. Hii ni hatari watu wanaanza kukata tamaa na kukimbilia njia za mkato.

Azimio la Arusha lilitaifisha majumba na mali kadhaa wa kadhaa za wahindi. Tukawa na NHC na msajiri. Kisutu tukaenda kukaa wazawa. Njaa zetu tukawarudisha wenyewe wahindi.

Wengi wa waasia ni wafanyabiashara, hakuna mfanyabiashara anaependa kulipa kodi nk. Dawa ni kuwabana sio kuwafukuza. Amin aliwafukuza wote, wat happen after that? Tusikimbilie majibu rahisi kwa maswali magumu
 
.....
Je, ni jukumu la nani kuwafanya hawa WTZ waache mara moja kuiba keki ya Taifa wakati Serikali iliyopewa hiyo dhamana inasuasua? Je watakubali kushambuliwa binafsi kama vile vibaka wanavyouawa hadharani ambao wao huiba kuku tu? Je sisi walalahoi tuendelee kuwaangalia tu wakati tunaumia?

Mwanakijiji... whistling!
 
Ebana wacha watukamue!

Nasema hivyo kwa sababu nyingi ambazo ni vigumu kuzianika zote lakini baadhi nijaribu kama hivi:

Watanzania wenye asili ya Asia:

1. Ni 'wasanii' na ndo waliowafundisha usanii watanzania kiasi watanzania wakawa 'wasanii' kwelikweli! Hata kumwamini mwenzio inakuwa shida lakini huu 'usanii' wao walau umetufumbua macho. Angalia mfano huu chini na utaelewa namaanisha nini:

A contractor from Bongo Land

Three contractors . . . one from Tanzania, another from Germany and the third from England are bidding to repair the White House fence. They go with a White House official to examine the fence.

The England contractor takes out a tape measure and does some measuring, then works some figures with a pencil. "Well," he says. "I figure the job will run $90,000 . . . $40,000 for materials, $40,000 for labour and $10,000 profit for me."

The Germany contractor also does some measuring and figuring, then says, "I can do this job for $70,000 . . . $30,000 for materials, $30,000 for my crew and $10,000 profit for me."

The Tanzanian "a.k.a Mbongo Asilia" contractor doesn't measure or figure, but leans over to the White House official and whispers: "$270,000."

The official, incredulous, says, "You didn't even measure like the other guys! How did you come up with such a high figure?"

"Easy," the Tanzanian contractor explains, "$100,000 for you, $100,000 for me and we hire the guy from Germany to do the work."


Source:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=31954#post31954

'Usanii' wa aina hii ni mbaya sana lakini ndo hivyo tena; we're in!

Kuna jambo serikali yetu inatakiwa kulijua; hawa wanakwepa sana ulipaji wa kodi kwa kulipa mishahara midogo kwenye salary slips huku wakikupa vijisenti vya ziada pembeni na kutokana na njaa za watanzania wengi wanalazimika kukubali kudaka chao pembeni ili mradi life goes on!

2. Waajiri wengi wa watanzania katika makampuni binafsi ni watanzania wenye asili ya Asia. China, India, Indonesia, Japan, UAE, Oman etc wote hawa wamejazana Bongo na wanaendelea kurundikana hadi kazi ambazo watanzania kibao wanaweza kuzifanya zinafanywa na watu hawa. Just imagine mtu kuweka marumaru kwenye nyumba analetwa tokea India! What a joke? Tena serikali hii hii inawapa uraia hawa walioletwa kwa ajili hiyo. Au fikiria mtu anatoka Malaysia kuja kusimamia vibarua kwenye kiwanda cha nguo au kiwanda cha miwa wakati tumewasomesha vijana wetu Management... Labda ndo maana tunawatimua ovyo vyuoni ili kuharibu jina la vyuo vikuu vyetu mbele ya waajiri hawa 'wenye asili ya kiasia'.

Binafsi nawapenda sana kwani hata wakiona una jitihada katika kazi yako wanaweza kukupa support kubwa kuliko hata kuajiriwa na mtanzania mwenzako. Katika hili seriously nasema wako mbele (hasa ukiwa na shule kubwa si ile ya Form IV au VI).

NOTE: Kuwafukuza si jambo jema na halina manufaa kwetu; jambo la msingi kabisa ni kuongea na wafanyakazi wa waajiri hawa na kujua ukweli wa mambo na kuwabana accordingly ikiwa ni pamoja na kudhibiti ukwepaji kodi. Lakini hapo lazima na TRA waache kamchezo kao wanakofanya ka kuongea kwa herufi kubwa na kumalizana nao juu kwa juu!

Mfano hai:
Asilimia zaidi ya 80 (not researched but anyone in Dar can confirm this!) ya watanzania walioajiriwa na waasia ni vibarua hata kama wana miaka 3 katika vibarua vyenyewe! Haijalishi una degree ama Diploma. Kuna viwanda (naviweka kapuni) ukipita asubuhi unakuta umati wa watu wakiwa magetini huku wakiwa wanaonekana kama wanashangilia jambo flani. Hawa ukiongea nao wanachokwambia ni kuwa wanasubiri kuona kama walau wataitwa wafanye kibarua kwa siku hiyo.

KINACHONIUDHI:

Serikali imewakumbatia hawa watu wanaoendekeza tabia hii chafu kwakuwa wanawapa % flani hivyo hawana uchungu nasi wananchi bali wao wenye nchi ndio wanaonufaika na waasia hawa. Hili halipo Tanzania peke yake; I met the same in Kenya & Uganda! Mwasia anakwambia 'live' kuwa anakutimua kazi na anajua wazi huna pa kwenda na hata ukienda utachemsha kwakuwa 'ana network kubwa'.

Kumbukeni: Hata viongozi wa juu wakati wanagombea na wanatafuta wadhamini, wengi wa waliowadhamini ni waasia! Pingeni hilo lakini ukweli unabaki palepale! Tumeshaamua kuwaita 'watanzania wenye asili ya Asia' kwakuwa utanzania wanapewa kirahisi tu!

Oh, I love Tanzania!
 
Matajiri weusi...

Reference ya kwanza ni Mengi. Huyu siwezi kuongea as kuna topic ilikuwa inaongelea na watu wameandika mengi.

Wengine weusi:

Kama unakumbuka kuna mada ile inaongelea ukabila ikulu, TRA n.k. Hiyo inawagusa wengi japo imeongelewa TRA pekee. Hilo suala linaenda zaidi hadi kwenye wenye makampuni yao binafsi ajira zinatolewa ki-upendeleo. Hilo nalo ushahidi kutoa inakuwa ngumu sana lakini wengi tunajua hiyo.

Mfano: Ukiitembelea Law Chamber kama ni ya mhaya (kumradhi simaanishi wote), basi unakuta Lawyers wote ni kina Rwa... au Ruta... Hii inakuwa applicable kwa makabila mengine.

Aidha, tajiri mweusi wanaendekeza ngono! Si wote lakini asilimia kubwa. Mabinti na wanawake wanaweza kukiri hili na wengine nawajua waliochemsha kwa mtanzania mwenye utajiri flani akaanzisha Kampuni ya kutoa mikopo na akamlazimisha kuvua chu... japo dada wa watu ana degree yake! Huyu akachemsha na kuamua kurejea serikalini. Watanzania wachache walio tayari kuajiriwa na weusi kwakuwa ajira pia huwa subject to kufukuzwa anytime kwakuwa nao walishatengeneza 'network' na wenye nchi. Utajiri wao wengi hata kama wamesomea unaambatana na uganga sana (wengine wanakufa wakiwa njiani kuelekea Bagamoyo!) ili mradi fweza!

Imani za kishirikina badala ya profession zetu weusi zimetawala kiasi ambacho hata kuacha naona inawawia ngumu wengi.

KINACHONIFURAHISHA:

Mweusi kuajiriwa anaona raha sana na hata ushirikiano na wenzake ili waanzishe chao anabana sana hata kama akiiona business proposal. Tuna roho za korosho (za kwanini) hasa kushirikiana na wenzetu wenye upeo zaidi yetu! Si watanzania tu lakini waafrika tulio wengi ushirikiano wa kuwezeshana unatushinda (labda muwe wa familia moja). Wengi ukiwauliza wanakwambia ni kwa sababu usanii mwingi. Kutoaminiana kumetawala!

More qns?

MFANO: Mwanakijiji, hakuna business opportunities zinazopatikana uliko ambazo unaamini kwa ushirikiano na wenzako mnaweza ku-earn zaidi na zaidi? Au nawe unaamini wataalam wanapatikana Norway tu? (Just kidding)
 
Tatizo si wahindi bali ni ufisadi..

ndugu zetu wahindi kitu kinacho wasahidia ni networking na uaminifu
Networking
Hawa jamaa wana mtandao karibu dunia nzima, zaidi ya hapo lobing inawasaidia sana kupata 'inside information' kuhusu tender na kazi yoyote ya serkali, na taarifa huwasishwa kenye vikao vyao vya siri kwenye nyumba zao za ibada au wanapakuwa ufukweni bahari ya hindi, wakati huo sisi wenzangu na mie tukishindana kunya pombe baa na kuangika na milupo.

uaminifu
Wakishapewa kazi wahindi, si dhulumati, watawakilisha kwa kadri ya makubaliano, na kamwe hawawezi kutuo siri kwa wasio husika, kwa upande wa waswahili uaminifu ni kitu kigumu, wanaweza kukudhulumu au kusaliti pale pombe zinapowazidi uwezo, kila siku tunawasikia baa ' unanijua mimi nani' mara ohhh.. jana nilikuwa na Kigogo abc.....

Ila kuna kitu kimoja ambacho wahindi wameshindwa kificha, nacho ni picha wanazopiga na wanasiasa[loabing] tembelea maduka ya wahindi, kila duka utakuta wamepiga picha na kikwete, kabla ya kampeni ya urais, wakati wa kampeni na baada ya kampeni.

Tusiwachukie wahindi, tupambane na ufisadi
 
Back
Top Bottom