"In the Name of Uzalendo"

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Tangu JPM alipongia madarakani kuna mambo mengi sana yasiyofaa yamefanyika in the name of uzalendo.

Mauzauza yote waliyofanyiwa wenye pesa yalipewa baraka za in the name ofa uzalendo.

Mishahara ya watumishi haikupandishwa in the name of uzalendo.

Ajira zilisitishwa in the name of uzalendo.

Maiti ziliokotwa ufukweni in the name of uzalendo.

Tundu Lissu akashambuliwa in the name "Amekosa Uzalendo".

Wapinzani wakaporwa nafasi zao walizoshinda in the name "Siyo Wazalendo".

Mambo mengi sana yalifanyika kwa kupakwa mafuta ya in the name of uzalendo.

Sasa amekuja Mama, mchezo ule ule unaendelea, in the name of uzalendo.

Kwamba jambo letu likawa 20k in the name of uzalendo.

Kubwa kuliko yote Tozo nazo zimeletwa in the pretty name of uzalendo.

Uzalendo unatumika vibaya sana, na kuna siku mtaanzisha vitu vinavyohitaji uzalendo kweli lakini hamtaeleweka sababu tayari watu wanaamini uzalendo unatumika kama njia ya kuwanyonya.

Wanasiasa inabidi muende mkajifunze maana ya uzalendo katika mataifa yenye raia wazalendo kama Marekani. Wale watu inapokuja suala fulani nyeti linalohusu taifa, basi wana uzalendo usiopomika.

Lakini pamoja na uzalendo wao, huwa hawana masihara kabisa na vitu visivyo vya kizalendo, mfano ukiwa waziri au Rais kisha uanzishe/ufanye kitu ambacho kiko kinyume na katiba au sheria basi wanakuchomoa siku moja tuu, watakupiga spana mpaka utajiuzulu mwenyewe.

Ukitaka kujua wale watu ni wazalendo kwa nchi yao ngoja niwape mfano wa muvi moja ya mwaka huu inaitwa Top Gun: Maverick.

Kile muvi imeshika namba moja kwenye mauzo, lakini siyo kwamba ni nzuri sana kushinda muvi zilizotoka hivi karibuni. Kuna muvi nzuri sana kuishinda hiyo lakini jiulize kwa nini yenyewe inaongoza kwa mauzo?

Jibu ni theme au ujumbe iliyobeba, ujumbe wenyewe ni "Uzalendo kwa Nchi Yako". Muvi inamuonesha mwanajeshi, rubani wa ndege za kivita aliyeacha kazi katika umri mdogo kutokana na kumpoteza rafiki yake kipenzi walipoenda kwenye mission moja ya kijeshi. Baada ya hapo alipata trauma iliyomfanya astaafu.


Hiyo ni miaka 30 iliyopita, ila mwaka husika kulikuwa na hatari ya shambulio kutoka kwa maadui, dhambulio ambalo lilikuwa linahusisha silaha za nyukilia. Ilihitajika wapatikane marubani wa kijeshi walioiva hasa ili wakalipue mahali hiyo nyuklia ilipohifadhiwa kabla haijafikia hatua ya kutumika kama silaha.

Kwa sababu ya uzalendo kwa nchi yake, huyu rubani alikubali kuongoza ile mission, akiwa na vijana 4, kwa sababu tuu ya uzalendo wake kwa nchi yake.

Na hiyo ndiyo sababu kuu iliyoifanya hiyo muvi iongoze kwa mauzo huko Marekani, kwao uzalendo ni kitu kikubwa sana. Muvi zinazoonesha maudhui ya uzalendo zinapata mauzo makubwa sana. Siyo sawa na huku kwetu, ambako ili muvi ifanye vizuri basi lazima ijae mambo ya ngono ngono na ujinga jinga mwingine mwingi.

Hivyo wanasiasa acheni kubatiza maovu yenu "Jina la Uzalendo" kwani mnazidi kuharibu mindset za raia wa nchi hii. Neno uzalendo linaonekana kama adui wa maisha ya wananchi, kila wanapolisikia wanashikwa na kichefuchefu.
 
Back
Top Bottom