Robert Alai: Tanzania is Burying Covid-19 Victims at Night

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Tuambiane tu ukweli, kuna ongezeko kubwa la vifo ndani ya wiki hii, mara mbunge, mara mkuu wa wilaya, mara mstaafu wa CTI, mara mstaafu wa CUF

Halafu mazishi watu wasiozidi kumi? Je, wanafariki kwa magonjwa mengine au magonjwa mengine yanapelekea magonjwa mengine kuwaua?

Huko makaburini Ununio na pengine, raia wanazikwa usiku chap chap... Why? Tanzania is Burying Covid-19 Victims at Night-Robert Alai

Kwanini misiba ya siku hizi inazikwa na serikali?

Corona haikwepeki:


Mombasa Billionaire Who Escaped Quarantine Dies From Covid-19 in Tanzania
 
Watu wasiozidi kumi kuondoa misongamano, wanafariki kwa magonjwa yao ya zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Lini na wapi serikali ilitangaza kuwa kwa kipindi hiki ni serikali ndiyo itakuwa inazika misiba bila kujali mtu amekufa kwa ugonjwa upi?

Unataka kusema hivi sasa ndugu akifa hata kwa kugongwa gari watu tunatakiwa kwenda kuripoti serikalini ili wafuate maiti na wakaizike wao?

Ikiwa PM akizungumzia suala la misongamano; kwa issue ya kwenye mabaa amesema "watu wawe makini".

Hivi ikiwa hata Walevi wanaruhusiwa waendelee kula maji ya dhahabu but "wawe makini" hivi unaamini kabisa serikali imejitwisha jukumu la kuzika maiti, na wala sio wanazozika ni special cases?!

Acheni fix bhana
 
Ukitumia takwimu za chadema unaweza kudhani kuna watu laki 5 wanafariki kila siku, tumia commonsense hapo mtaani kwako kama kuna watu 10 wamefariki wiki hii jua hali ni mbaya lkn kama misiba ipo kawaida kama miaka 10 iliyopita basi na wewe jiongeze.

Tokea Januari misiba imetokea mitano hapa mtaani ambayo ni hali ya kawaida kwa mtaani kwangu
 
Ukitumia takwimu za chadema unaweza kudhani kuna watu laki 5 wanafariki kila siku, tumia commonsense hapo mtaani kwako kama kuna watu 10 wamefariki wiki hii jua hali ni mbaya lkn kama misiba ipo kawaida kama miaka 10 iliyopita basi na wewe jiongeze. Tokea Januari misiba imetokea mitano hapa mtaani ambayo ni hali ya kawaida kwa mtaani kwangu
Toeni takwimu sahihi, lumumba kafa mtu jirani pale? Mjipange!!!
 
Mimi jirani yangu amefariki jumamosi alfajiri bado hajazikwa na serikali kwa taratibu zao wanasema watampima majibu yatakuwa tayari ndani ya 72hrs nadhani mwisho nj leo.

Kweli siyo kila anaekufa anakufa kwa Corona wengine ni kwa maradhi zoeya but serikali kwa kukosa kwao vifaa nahisi inabidi watu wazikwe kiCorona kwa ruhusa ya ndugu hata kabla haijawa confirmed ili kuondoa misongamano mortuary, kwa aliyewahi kuingia vyumba vya kuhifadhia miili atanielewa unakuta sometimes kumejaa miili mingine ipo chini na kila saa watu tunakufa ukisema ndugu yako akae nje ya jokofu akisubiri vipimo saa 72 atavimba mpate shida bora azikwe tu wanavyotaka mamlaka japo hali hii inaumiza sana kwa ndugu wanaobaki.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom