Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 2,398
- 3,071
"LIMI BUPE ISANA:
"Bhanhu bhakatongela bupe.
"Bakaja lushiku lumo ku Ban'igulu n'itandala lya Lububi. Lububi lwali giti 'giligilita' yabo.
"Aliyo ban'igulu bakabi na wisu: bakabis'Isana nu tusandiko twa bubhi twalekanile na twa wiza.
"-Huna lulu, bhakashoka mu Si. Aho balugula ikundikikijo ly'isandiko limo likafuma Limi!
"Hangi bakalugula isandiko lya kabili, Ngweji! gwafuma!
"Nose lya kadatu likalugulwa, angu Nsonda ningi jikapumuka!"
Kutoka -Pr. Jan Hendriks Chenya WF. Imani za jadi za kisukuma katika hadithi, methali na desturi za maisha -1988
Tafsiri isiyo rasmi:
"Watu walitangulia kuwepo duniani kabla ya mwangaza.
"Siku moja wakaenda kuwatembelea wana wa mbinguni kwa kutumia kitu kama tawi la mmea fulani. Hilo tawi ndio lilikuwa kama gari au trekta yao.
"Wana wa mbinguni walikuwa na kama kaujanja au namna fulani: maana eti walilificha jua katika sanduku bayabaya hivi wamelitenganisha na visanduku vingine vizuuuri sana.
"- Basi bwana watu wale wakarudi kwenye ardhi.
"Walipofungua mfuniko wa sanduku mojawapo likatokamo Jua.
"Tena wakafungua sanduku la pili huooo! Mwezi ukatokamo!
"Mwishowe la tatu likafunguliwa, basi ati Nyota nyiingi zikalipuka!"
Kila jamii ina vihadithi vyake. Vizuri na vya mafunzo na burudani. Je stori ya kuanza kwa mwanga duniani ipoje kulingana na jamii yako.
Wenzetu wajanja. Stori zao walianza kuziweka kwenye vitabu. Sasa hivi wanaziweka kwenye muvi kabisa zisipotee. Wape watoto stori zote za kiarabu, kiyahudi, kichina, kidenmark. Lakini pia usisahau za kikwenu.
Peace ✌🏽