SURA YA TISA
IV
Watu hao Joram Kiango na Nuru,
waliokuwa wakitafutwa kwa udi na
uvumba, alfajiri iliwakuta wakiwa
wamesimama mbele ya hoteli moja
ndogo, katika mtaa ambao ulikuwa
umejaa watu waliokuwa wakijadiliana.
Macho yao yaliwatazama raia hao wa
makaburu waliojaa wasiwasi kwa
dhihaka. Kadhalika waliwakebehi na
kuwadhihaki askari wa polisi waliokuwa
wakipita huku na huku katika mitaa na
vichochoro wakiwasaka huku wakiwapita
Joram na Nuru bila hata kuwatupia
macho. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote
kuwashuku. Pamoja na kukesha
wakifanya kazi ya kwenda hapa na pale,
huku wakilazimika kuua na kuua tena,
bado walijitahidi kuwa katika hali yao ya
kawaida kama raia yeyote wa kawaida
katika nchi hiyo. Hali ambayo ilitokana na
mavazi waliyovaa pamoja na rangi yao.
Yeyote aliyewaona Joram na Nuru
aliamini kuwa hao walikuwa vijana
wengine kabisa tena kutoka katika jamii
ya makaburu. Hayo yalikuwa moja ya
matokeo ya shughuli nyingi ambazo
Joram alikuwa amezifanya kwa gharama
kubwa sana alipokuwa akisafiri hapa na
pale katika miji mbalimbali. Alikuwa
amempata mwalimu ambaye alikuwa
amewatengenezea ngozi za bandia
zilizovaliwa usoni, mikononi na kufunika
vichwa vyao kwa nywele za kizungu. Vitu
hivyo ni miongoni mwa mali zake ambazo
Joram alikuwa amezisafirisha kwa hila
akimtumia yule mfanyabiashara wa
Mmarekani More.
Kwa ujumla Joram aliona kuwa mambo
yote yalikwenda vizuri kama
yalivyopangwa, ingawa kiasi yalianza
ghafla kuliko alivyotegemea. Joram
alikuwa amesitushwa sana na taarifa ya
jana alipomsikia kiongozi wa BOSS
akisema kwamba leo saa nne wangeilipua
Dar es Salaam na miji mbalimbali ya nchi
za Kiafrika wakitumia ile silaha ya hatari
iliyofungwa angani. Hivyo Joram hakuwa
na simile tena moyoni. Ndipo alipoamua
kufanya mapenzi ya hali ya juu na Nuru,
akiwa na uhakika kuwa anatazamwa
kupitia mtambo wao ambao alikwisha
uona mapema. Alifanya vile ili
kuwapumbaza watazamaji hao.
Baada ya hapo ndipo alipofanya hila
kuukorofisha mtambo huo. Katika kipindi
hicho cha kutoonekana kupitia mtambo
huo, Joram aliondoka kwa kupenyapenya
kwa hila katika vichochoro hadi nyumbani
kwa More ambako alibisha mlango na
kufunguliwa na Moore mwenyewe. Joram
alipoomba mzigo wake Moore alikanusha
kabisa kuwa hakuwa amechukua mzigo
wa mtu kama huyo. Lakini ngumi mbili
tatu nzito kutoka kwa Joram zilimfanya
Moore amuongoze ghalani ambako
Joram alimfunga mikono na miguu kwa
kamba maalumu, kisha akachukua vitu
vile vya muhimu tu. Akarudi haraka hadi
chumbani kwake ambako alisaidiwa na
Nuru, walipekuapekua na kupata ramani
walizokuwa wameziandaa, pesa na vitu
vingine vingine. Ni wakati Joram
alipomaliza kujivika kozi hizo za bandia
zilizomfanya aonekane kama alivyo sasa,
yule kachero wa kwanza alipoingia, hila
aliyotumia Nuru ya kujifanya kwamba
alikuwa akipambana na 'Mzungu'
aliyetaka kumnajisi ilimsaidia sana.
Ndipo kachero huyo alipopata kile
alichostahili kupata. Nae akafanya haraka
kumsaidia Nuru kuvaa 'Uzungu' wake na
alipokamilika walivichukua vitu vyao
muhimu na kuingia mitaani.
Wakiwa wameikariri vizuri ile ramani
kikamilifu, kazi waliyoifanya mitaani
humo ilikuwa ya kuyafuata yale majengo
waliyoyakusudia na kutega vile vigololi
vilivyopatikana kwa Chonde na
kuvitegesha katika kipindi cha saa tatu
kamili. Walikuwa wameifanya kazi hiyo
kwa ukamilifu kuliko walivyokuwa
wametegemea wenyewe. Watu wachache
waliolazimika kupoteza maisha ni wale
ambao waliwashuku ama kuwazuia
kufanya kazi yao kwa makini. Wakiwa
hawajui kuwa wanapambana na nani
watu hao walikufa kwa utulivu kabisa,
isipokuwa yule ambaye kifo
kilimtetemesha hata akaamu kuruka
dirishani kutoka ghorofa ya nne akiwa na
kisu kifuani.
Sasa kazi ya kutega vigololi ikawa
imekwisha. Joram alimtazama Nuru na
kumnong'oneza. "Awamu iliyobaki ni
ngumu sana, itakuwa kazi yangu peke
yangu. Ni lazima niingie katika mtambo
wao na kuulipua. Nikiweza kuulipua kabla
ya madhala tuliyoyaandaa katika jiji hili
kutokea litakuwa jambo jema sana.
Nikishindwa, mioto itakapoanza nenda
pale ambapo nimekuonyesha katika
ramani unisubiri".
"Hatuwezi kwenda wote?", Nuru akahoji.
"Haiwezekani, tumelijadili hilo mara nyingi
sana", Joram akamwambia.
Wakakubaliana.
Kisha Joram akajiingiza kuwa miongoni
mwa watu waliokuwa wakipita katika
mitaa hiyo akaelekea ilikomwelekeza
ramani yake. Mwendo wake ulikuwa wa
haraka na uhakika, ingawa aliufahamu
kikamilifu ulinzi mkali uliokuwa
umeuzunguka mtambo huo. Matumaini ya
kurudi ilikuwa ndoto isiyo na uhakika.
Hata hivyo hakujali. Asingejali kufa
endapo kifo hicho kingemtokea baada ya
kufanikiwa kutega mabomu yake katika
mtambo huo. Aliamini kuwa ikitokea
amekufa katika dhoruba hiyo, Nuru
asingeshindwa kurudi Tanzania baada ya
msukosuko mkubwa utakaoutokea mji
huo saa mbili na nusu baadaye.
Nuru alikuwa amemwacha Joram
aondoke kwa hatua chache. Mara Joram
alipoondoka na kuamini kuwa hawezi
kugeuka tena kumtazama, Nuru nae
alianza kumfuata nyuma. Hakujua kuwa
yeye pia alikuwa akifuatwa na watu
wengine wanne wenye silaha kali
mikononi na mioyo yenye hofu na hasira
dhdi yake...
ITAENDELEA 0784296253