Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Leo ni siku 7 tangu post ya mwisho mkuu barige. Ebu jaribu kukumbuka uzi wako huu.
 
Hizi nyakati ni mbaya kuna jamaa wa "msako wa hayawani" tuliambiwa kafariki ati
 
barige 22:16 13th July 2015
SURA YA NANE
III
Jasho jembamba .....

barige angalia muda huo toka post yako y mwisho. wiki zima limekatika mkuu wangu.
 
TUTARUDI NA RHO ZETU?
SURA YA TISA
Binadamu hajapata kuwa na adui
mwingine, mkubwa na mkatili katika
maisha yake zaidi ya kifo. Ni kifo
pekee ambacho kimeishinda akili ya
binadamu. Hakukosea yule
mwanamuziki aliyeimba "kifo hakina
huruma, kifo ni kiboko yao".
Hutokea binadamu akawa na
shughuli zote, siku nenda rudi bila
kukipa kifo wazo lolote hadi
kinapotokea bila kutegemewa. Ni
hiyo sababu pekee inalomfanya
mwanadamu asitokwe na jasho la
hofu siku zote za maisha yake kwa
kuogopa kifo. Kwa vile hutokea bila
ya kutegemewa.
Hivyo hakuna kifo kibaya kama kifo
cha kusubiri siku na saa. Hasa kifo
cha kinyama na cha kikatili kama
hiki ambacho kilikuwa kikitegemewa
na watu kadha wa kadha katika nchi
kadha wa kadha za Kiafrika. Leo
ilikuwa imewadia siku ile. Siku
ambayo Afrika ya Kusini ilikuwa
imetoa kuwa ingekuwa ya mwisho
kabla ya kuachia pigo la mwisho
ambalo lingeiteketeza miji yote ya
nchi zilizoko mstari wa mbele.
Pamoja na ukweli kwamba tukio hili
lilikuwa limeamriwa kuwa siri kubwa
sana miongoni mwa wahusika, kama
yale mengine ambayo huishia katika
masikio ya wachache na hutoweka
bila ya raia wa kawaida kuyapata,
lakini hili kwa njia moja ama
nyingine lilikuwa limevuja na
kusambaa mitaani. Jambo ambalo
lilisababisha mashaka na hofu kubwa
mitaani. Wananchi waumini wa dini
walitoroka makazini na kukimbilia
kwenye makanisa na misikiti ili
kutubu dhambi zao zote na
kumbembeleza Muumba awanasuwe
awanasuwe katika janga hili. Wale
ambao hawakumwamini Mungu
walitulia katika vikundi vikundi
wakizungumza kwa utulivu.
Wachache sana waliamua
kuyamalizia maisha yao huku
wakinywa pombe katika baa ambazo
hazikufunguliwa milango.
Viongozi wa Chama na Serikali
walikuwa katika vikao vya dharura
wakijaribu kujadiliana hili na lile.
Lolote la haja halikupatikana,
japokuwa yalitokea mapendekezo
mengi. Jambo ambalo kila mmoja
alitamani kutamka ingawa ulimi
ulishindwa kutamka hadharani kwa
aibu, ni ambalo lingewahakikishia
wananchi uhai na usalama wao.
Lakini maadamu ungekuwa uhai usio
na uhuru, na usalama usio na
uhakika na hakuna aliyethubutu
kupendekeza hivyo. Iliyonaki ilikuwa
kupeana moyo tu kuwa haiweze
kutokea, na endapo itatokea cha
kufanya ni kujaribu kuepuka
majengo ambayo yanaweza kuelekea
kuyavuta macho ya muuaji. Ilielezwa
pia kuwa kote nchini wananchi
walikuwa wakichimba mahandaki
kwa ajili ya kujificha.
Ikulu, Rais na baraza lake la
mawaziri walikuwa katika kikao cha
muda mrefu. Kikao ambacho
kilichukua siku nzima, hata usiku
ukaanza kukaribia. Inangawa
kilikuwa kikao cha siri sana, lakini
ilikuwa dhahiri kuwa chochote
ambacho kilikuwa kikijadiliwa ndani
hakikupata ufumbuzi ya tatizo.
Mmoja alikuwa amependekeza kwa
mara nyingine kuwa nafasi hiyo
itumike kuivamia Afrika Kusini
kijeshi, "Ili tukomeshe kabisa suala
hili la kutishiwa na kuonewa mara
kwa mara. Tutumie majeshi yetu yote
ya nchi za mstari wa mbele kuingia
nchini humo na kuanzisha
mapambano ili kuunda utawala
halali. Najua, adui ana jeshi imara na
silaha kali sana. Lakini wingi witu
wetu utasaidia tutashinda..."
Mapendekezo hayo yalijadiliwa lakini
hayakuonekana kama yangekuwa jibu
la kuziokoa nchi za Afrika na
kumaliza tatizo ambalo lilikuwa
mbele likisubiri saa chache ili litokee.
mwingine akatoa wazo. "Si rahisi
kutumia masaa manane yaliyobaki
kukusanya majeshi na kuyaongoza
katika nchi nyingine na kuanzisha
vita. Zaidi yote, hatari au mkasa
ambao uliokuwa ukisubiriwa ulikuwa
ukitokea angani, hivyo uvamizi huo
usingesaidia au kuzuia maafa
hayo...". Baraza la mawaziri
liliendelea kujadiliana kwa utulivu
katika ukumbi huo wa Ikulu. Jengo
hilo likiwa miongoni katika majengo
kadhaa yaliyokuwa katika orodha ya
kulipuliwa ilikuwa kana kwamba Rais
na mawaziri wake walikuwa
wameamua kikisubiri kifo hicho kwa
pamoja; kufa kiofisa...
Binadamu aliyekuwa na hali mbaya
kuliko wote nyumbani nchini
Tanzania aliitwa Inspekta Mkwaju
Kombora. Yeye alikuwa akitaabika
kimwili na kiakili. Juhudi zake zote,
pamoja na wenzake wa kutoka nchi
mbalimbali, zilikuwa kama upuuzi.
Upelelezi ulikuwa haukuzaa matunda
yoyote yale. Na hasa upelelezi huo
ulikuwa kama umewafanya wazidi
kujipalia mkaa wa moto; kwani
ilikuwa dhahiri kuwa kila jambo
linaloafikiwa hapa wakati huo huo
utawala wa makaburu unakuwa na
taarifa nalo. Hayo yalithibitika
alipoarifiwa kuwa wapelelezi wote
waliotumwa kuingia Afrika Kusini
walikuwa mikononi mwa makaburu.
Ilikuwa kama waliopelekwa kufa
makusudi kabisa. Jambo ambalo
lilimfanya ashuku mara moja
kwamba miongoni mwao alikuwemo
chui aliyejivika ngozi ya kondoo.
Hivyo Insipekta Kombora aliugeuza
upelelezi wake kutoka mstari wa
mbele na kuanza kuchunguza mstari
wa nyuma. Na haukupita muda kabla
dalili hazijajitokeza kuwa huyu mgeni
aliyedhaniwa kuwa msamaria
mwema, ambaye alileta fununu
nyingi kutoka Afrika Kusini
angehitaji kuchunguzwa zaidi.
Uchunguzi ukaanza katika vikosi
vyote vya wapigania uhuru duniani,
katika vyuo na hospitali ambazo
alidai amepitia na hata Afrika Kusini.
Taarifa zilizidi kuongeza haja ya
kutazamwa kwa makini. Na
haukupita muda kabla kabla ya watu
waliokabidhiwa jukumu la
kumwangalia hawajatoa taarifa kuwa
alikuwa mtu wa BOSS. Habari hiyo
ilimuumiza sana Kombora. Alitoa
amri kuwa mtu huyo aliyejiita Clay
achunguzwe kwa makini sana, kwani
kwa vyovyote leo ilikuwa siku ya
mwisho iliyotolewa na utawala huo
haramu na lazima angekuwa na
jambo la kuarifu kwa mabwana zake.
Baada ya hayo Insipekta Kombora
aliendelea na shughuli katika ofisi
yake. Alipokea na kujibu simu na
walkie talkie nyingi ambazo hakuona
kama zilikuwa zikimsaidia chochote.
Aliwasiliana na maofisa wenzake
katika nchi za Zambia, Zimbabwe,
Angola, Msumbiji, Naijeria na
kwingineko kujaribu kuona
wamefikia wapi. Hakuna alichopata
zaidi zaidi ya yale aliyotegemea.
Kwamba wananchi walikuwa
wakitaabika na kulalamika mitaani
katika hali ya hofu kubwa. Kwamba
hata makazini hawakuwa
wamekwenda. Ilikuwa kama
walikuwa wakisubiri kifo na maafa
hayo. Kwamba watu wengi walikuwa
wamefungulia radio zao na
televisheni zao wakisubiri kusikia
habari mbaya kokote Afrika.
Kwamba ingawa vyombo vya habari
vya dunia nzima vilikuwa vikiendelea
na ratiba zao kama kawaida lakini
ilikuwa dhahiri kuwa kuna jambo,
zito na la kutisha, ambalo lilikuwa
likisubiliwa na kila mtangazaji.
Kombora aliachana na taarifa hizo
na kuulizia maendeleo ya maofisa
ambao aliwakabidhi jukumu la
kumchunguza Clay na yote
anayofanya. Haikumpendeza
aliposikia kuwa alikuwa katika hali
ya kawaida, kama ambaye hakuna na
lolote la kufanya.
"Endeleeni kumchunguza kwa
umakini", Kombora aliagiza.
Ofisi ilikuwa haikaliki. Inspekta
Kombora kila alipojaribu kutulia juu
ya kiti chake, kiti hakikuafikiana
naye. Kila alipoinuka ili atoke,
hakujua angeelekea wapi. Unawezaje
kutulia wakati unahesabu masaa ya
kuishi ukisubiri kifo, au maafa ya
kusikitisha ambayo ni aibu kwako,
kwa taifa lako na bara lako zima la
Afrika? Aliendelea kutaabika kimwili
na kimawazo, akipokea na kusikiliza
habari kutoka sehemu mbalimbali.
Mara zilimfikia habari za Joram na
Nuru kuwa walikuwa wameingia
Afrika Kusini na kuomba hifadhi ya
kisiasa. Kwa Kombora ilikuwa habari
ya kushangaza sana. Habari ya
kusikitisha. Habari inatotia aibu.
"Joram Afrika Kusini!" Kombora
alishangaa.
Hata hivyo Kombora alikwisha choka
kushangazwa na habari za kijana
huyu anayeitwa Joram. Mambo yote
aliyokuwa akiyafanya, ambayo
yalikuwa yakiwafikia watu wa habari,
Kombora alikuwa ameyasikia au
kuyaona katika vyombo vya habari.
Angeweza kumsifu Joram kwa
mbwembwe zake ambazo zilikuwa
zimewafanya polisi wote wa miji
mbalimbali ya nchi zilizoendelea
washindwe kumtia mikononi. Lakini
kila alipokumbuka kuwa mbio hizo za
Joram zilikuwa za kukimbiza akiba
pakee ya pesa za kigeni alizoiibia
nchi yake Kombora alikuwa akijisikia
vibaya. Hayo yakifuatwa na tishio
lililokuwa likizidi kusogea vilimfanya
ajilazimishe kuliondoa jina hilo
akilini mwake.
"...Inspekta Kombomba anaongea.
Namba ngapi hiyo?..."alijibu sauti
katikam walkie talkie iliyokuwa
mikononi mwake. Alipotajiwa namba
alijikuta akiisikiliza kwa makini
zaidi. Ilitoka kwa kiongozi wa
makachero ambao walikuwa
wakifuatilia nienendo ya Clay.
"...Inaelekea kama tutamkamata red
handed mzee. Sasa hivi anaunganisha
mitambo yake ya mawasiliano..."
"Nisubiri nakuja mara moja".
Dakika mbili tatu baadaye, Kombora
alikuwa miongoni mwa polisi wanne
ambao walikuwa katika chumba
fulani katika hoteli ya Kilimanjaro.
Chumba hiki kilikuwa cha nne kutoka
chumba cha Clay. Hata hivyo
kutokana na mitambo waliyotega
kitaalamu, japokuwa hawakuwa
wakimwona, waliweza kumsikia Clay
akiongea kupitia chombo fulani cha
kijasusi.
"Sikiliza mzee...sikia..." askari
mmoja alimwambia Insipekta
Kombora akitweta.
"...Ndiyo. Ndiyo...nimefanikiwa
kupanda katika majumba ya kutosha.
Moja Ikulu... Hapa Kilimanjaro
moja... Jengo la IPS moja...
Kitegauchumi... Muhimbili... Benki
Kuu ya muda... Tipper... Kiwanda cha
Urafiki na sehemu mbalimbali
muhimu. Tunachosubiri ni saa tu.
Ikifika kwa jinsi nilivyotega inaelekea
jiji zima litalipuka. Mimi nitaondoka
hapa wakati wowote..."
"Unasikia mzee? Unasikia?"
Kombora hakusubiri kumsikiliza
afisa huyo. Aliwaamuru kumfuata
kukiendea chumba cha Clay.
Kinyume na mategemeo yao
waliukuta mlango ukiwa wazi. Naye
akiwa kaketi kwa utulivu juu ya
kochi, gazeti mkononi. Yeyote
ambaye angeingia bila kufahamu
kinachotokea angemdhania kuwa
alikuwa akisoma gazeti.
Aliwalaki Kombora na wenzake kwa
utulivu wa kushangaza. "Karibuni.
Vipi, mbona ghafla hivyo? Kuna
habari mpya?" aliuliza Clay.
"Inuka na uweke mikono yako juu",
Kombora alifoka, tayari akiwa
ameitoa bastola yake na kuishika
mkononi na kufanya bastola
zilizomwelekea zikiwa nne.
"Vipi Inspekta mbona sikuelewi..."
"Mikono yako juu!" Kombora
aliunguruma.
Clay aliinuka na kuweka mikono yake
angani.
"Achia gazeti".
Aliachia. Ndipo kilipoonekana
kikasha kidogo chenye ukubwa wa
kibiriti ambacho Clay alikuwa nacho
mikononi. Kombora alimsogelea na
kuiweka bastola kifuani mwake huku
akimwuliza kwa ukali, "Nini hicho?".
"Kwanini Inspekta?... Hiki
sikifahamu. Nimekiona sasa hivi tu".
Jibu hilo lilimchukiza Kombora
kupita kiasi. alijibu kwa pigo zito
ambalo lilitua barabara katika uso
wake. Clay alipepesuka lakini
hakuanguka, jambo ambalo
lilimshangaza na kuzidi kumchukiza
Kombora. Pamoja na umri wake
mkubwa hakumbuki lini alipata
kumpiga mtu ngumi nzito kama hiyo
na mtu huyo akaendelea kusimama.
Inspekta Kombora akarudi nyuma
hatua mbili na kumwamuru askari
mmoja amkague. Ni hapo lilipotokea
jambo ambalo halikutegemewa. Clay
kwa wepesi usiokadirika alikuwa
amechomoa kisu na kumchoma
askari huyo. Kisu cha pili
kilimkwaruza Kombora mikononi.
Papo hapo alikuwa amechupa
mlangoni akienda zake. Lakini
hakuwa mwepesi zaidi ya risasi za
polisi ambazo zilimfanya aanguke
mkangoni kifudifudi. Wakamvutia
chumbani na kumlaza kitandani bila
kujali damu ambayo iliendelea
kumtiririka kutokana na majeraha
makubwa ya risasi hizo.
Wakamkagua na kumpokonya bastola
kadhaa na visu sita zaidi.
"Sema haraka; ulikuwa ukiwataarifu
nini hao mabwana zako?" Kombora
alimwuliza.
"Itakusaidia nini Inspekta?" Clay
alihoji kwa udhaifu na maumivu
makali. "Hakuna unaloweza kufanya.
Bado saa chache sana.
"Kama utapenda kufahamu nilikuwa
nikitoa taarifa ya mafanikio ya kazi
yangu. Nimefanikiwa kutega vifaa
katika majengo mbalimbali. Wakati
utakapowadia mlipuko utakaotokea
utakuwa wa kupendeza sana. Laiti
ningekuwa hai nione na kusikia vilio
vyenu".
Kombora hakujua aseme nini.
Hakujua kama alipaswa kumtisha au
kumbembeleza mtu huyo ambaye kila
dalili zilionyesha kuwa angekata roho
mapema.
"Mpelekeni hospitali", Kombora
aliamuru.
"Ya nini Inspekta? Sipendi kufa kwa
moto... Naweza kufa kwa njia
nyingine nzuri zaidi..."
Kombora hakumsikiliza. Akamgeukia
askari wake aliyekuwa mahututi.
Yeye pia hakuwa na dalili za kuishi
sana. Kisu kilikuwa kimemwingia
vizuri kifuani upande wa moyo.
Kitendo hicho kilipandisha hasira za
Kombora dhidi ya Clay. Akamgeikia
akamtazama usoni kwa hasira.
Alimwona Clay akitafuna kitu.
Akakumbuka kuwa majasusi wengi
wa utawala wa makaburu
walivyokuwa wakiishi na sumu kali
mdomoni. Matumaini ya Kombora
kupata habari zozote za kusaidia
yakawa yameyeyuka. Akamsogelea na
kumwuliza taratibu.
"Sema tafadhali... tunaweza
kuuzuiaje mkasa huu ulio mbele
yetu?"
Clay alicheka kwa maumivu huku
akijikongoja kusema, "Labda
uchukue furushi moja katika mfuko
wangu uangalie unachoweza
kufanya". Moyoni Clay alifahamu
kuwa mfuko huo ulikuwa na akiba
nyingine ya vile vigololi, ambavyo
alikuwa bado hajamaliza kuvitega
kwenye majengo aliyokusudia. Hivyo
aliamini kuwa Kombora
angevichukua na kuvifikisha kituo
kikuu cha polisi na kulifanya jengo
lao liwe moja kati ya majengo
mengine yatakayopigwa na radi hii
iliyoundwa na binadamu. Hilo
likamfanya ajitahidi kucheka tena
kifedhuli huku akisema kwa taabu,
"Usijali Inspekta... muda si mrefu
tutakutana kuzimu...tutakuwa wengi
sana...mimi natangulia".
Kombora hakuona kama mtu mwenye
roho ya kinyama kama huyo alistahili
kufa kifo cha kiungwana kiasi hicho.
Hivyo akaichomoa bastola yake na
kumsindikiza ahera kwa risasi ya
kichwa ambayo ilifumua kabisa fuvu
lake la kichwa.
ITAENDELEA 0784296253
Share
 
asante barige, usikawie sana kuleta nyingine, tufikishie shukrani zetu kwa mpigansji blog na kumsihi awe anaweka angalau twice per week.
 
Sasa MKUU hayo masaa yalobaki mambo yaharibike situendelee bhana
 
hii kitu haijaisha tu? mimi mpaka nikutane na neno mwisho ndipo nitaanza kuisoma. period
 
barige vipi mkuu, kwema huko? utatokea tena 22+7= 29/7/15?
 
tarehe 29 leo ni Jumatano nyingine, siku saba zimekamilika, barige ukumbuke uzi huu tafadhali.
 
hii kitu haijaisha tu? mimi mpaka nikutane na neno mwisho ndipo nitaanza kuisoma. period

mwanzoni tulikulaumu kwa kututesa kumbe na wewe unateseka mkuu?

nadhani Nyakasagani ametia nia huko kwao bunda hivyo yuko extra busy kuiandaa
 
Back
Top Bottom