Riwaya: Siri

SIRI

episode 18

Mtunzi.Patrick CK

sana hadi nikashindwa kujua kama
kuna mtu alikuja hapa
kunitazama.Najiuliza ni nani huyu
mtu sipati jibu.Hakuna
anayenifahamu huku Israel zaidi ya
Olivia na Judy.Au Olivia kuna tatizo
amelipata?akajiuliza Edger na
kubonyeza kitufe pembeni ya
kitanda chake na ndaniya sekunde
chache muuguzi akafika
“Edger kuna tatizo
lolote?akauliza mwanadada yule
muuguzi aliyekuwa na tabasamu
usoni
“Ndiyo nina tatizo.Nahitaji
kujua nani alikuja kunitembelea
jana usiku hapa chumbani?akauliza
Edger
“Sina hakika kwa sababu mimi
nimeingia asubuhi hii.Nitamuuliza
muuguzi aliyekuwepo usiku halafu
nitakupa jibu.Kwa nini umeuliza
hivyo Edger?akauliza yule muuguzi.
“Usijali dada.Kuna kitu kingine
naomba unisaidie.Nataka simu
kuna watu nahitaji kuwasiliana
nao” akasema Edger na muuguzi
akaenda kumletea simu
akaziandika zile akapiga lakini
hazikuwa zikipatikana
“Huyu ni nani anataka
nimpigie huku hapatikani
simuni?akajiuliza Edger.
“Nitajaribu tena
baadae,yawezekana akawa ni mtu
muhimu au anaweza kuwa ni balozi
: wetu hapa Israel anataka
kuzungumza nami ndiyo maana
akanitumia ujumbe huu kunitaka
niwasiliane naye” akawaza na mara
akapata wazo
“Yawezekana akawa ni Sayid
anataka kuzungumza nami.Naamini
atakuwa ni yeye kwani nilimjulisha
kuwa niko hapa.Lazima atakuwa ni
mwenyewe ngoja niwasiliane naye”
akawaza na kuchukua kompyuta
yake akampigia simu Sayid Omar
“Edger vipi maendeleo yako?
Akauliza Sayid ambaye alikuwa
anatumia simu yake ya mkononi
“Ninaendelea vyema
Sayid.Maendeleo yangu si mabaya”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Nimekuwa na mawasiliano
na madaktari wa hapo hospitali na
wamekuwa wakinijulisha kila
kinachoendelea kuhusiana na hali
yako”akasema Sayid
“Umekuwa unawasiliana na
madaktari?Edger akashangaa
“Ndiyo Edger.Nimekuwa
nikiwasiliana nao mara kwa mara
kujua maendeleo yako”
Edger akafikiri kidogo na
kuuliza
“Jana usiku ulikuja hapa
hospitali au kuna mtu yeyote
ulimtuma aniletee ujumbe
wowote?akauliza Edger
“Hapana sijafika huko ila
nimekuwa nawasiliana kwa karibu
sana na madaktari wa hapo.Ujumbe
gani huo?akauliza Sayid
“Nimekuta kuna bahasha
pembeni ya kitanda changu na
ndani yake kuna kadi yenye namba
za simu nikaelekezwa kwamba
nipige simu hiyo,nimepiga lakini
simu haipatikani nikahisi labda ni
wewe ulitaka kuwasiliana nami”
“Hapana si mimi Edger.Kama
ningehitaji kuwasiliana nawe
nisingekutumia ujumbe.Nitumie
hizo namba ambazo umeelekezwa
upige” akasema Sayid na Edger
akampatia zile namba
“Nitakupigia tena baadae”
akasema Sayid na kukata simu
“Nani ambaye aliniachia
ujumbe huu niwasiliane
naye?Nilitegemea angekuwa sayid
lakini amekana si yeye.Nadhani
Sayid atanisaidia kujua mtu huyo
ni nani” akaendelea kuwaza.
***************
Saa nne za asubuhi Dr Olivia
akiwa na Judy waliwasili hospitali
kumtazama Edger kama ilivyo
kawaida yake.Kabla hajaingia
katika chumba cha Edger Dr Olivia
akaamua kwenda kwanza kumuona
Chris.Aligonga mlango wa chumba
cha Christopher akaruhusiwa
kuingia.
“Christopher” Olivia akasema
huku akitabasamu
“Dr Olivia.Karibu sana habari
za toka jana? Chris akajibu uso
wake ukiwa katika tabasamu
kubwa.
“Habari za toka jana nzuri.Vipi
maendeleo yako?
“Ninaendelea vizuri Olivia”
Chris akajibu huku akitabasamu
“Chris nimekuja kumuona
mgonjwa wangu nikaona nipite
kwanza kukujulia hali kabla
sijaenda kumuona
Edger.Nashukuru unaendelea
vizuri” Dr Olivia akasema huku
akisimama na kujiandaa kutoka.
“Nashukuru sana Olivia kwa
kuja kunijulia hali” Chris akasema
huku akionekana kutaka kuuliza
kiuliza kitu.
“Kuna kitu unataka kuniambia
Christopher? Akauliza Olivia
“Naomba dakika zako chache
kuna kitu nataka kukuuliza kama
hutajali” akasema Dick
“Usijali Christopher uliza
chochote unachokitaka” akasema
Olivia
“Dr Olivia naomba usinielewe
vibaya kwa hili
nitakalokuuliza.Wewe ndiye
uliyemleta Edger hapa hospitali.Je
mtu huyu hana familia?Hana mke
au ndugu mwingine ambaye
angeweza kuambatana naye hapa
kuja kumuuguza na wewe ukapata
nafasi ya kuendelea na majukumu
yako mengine?akauliza Dick
“Nakumbuka nilikueleza jana
kwamba mimi na Edger hatukuwa
tukifahamiana.Aliletwa katika
hospitali ninakofanya kazi akiwa
hajitambui na baada ya kumpa
huduma tuliona kama angeendelea
kukaa pale angepoteza maisha
hivyo ikalazimu kufanya mpango
wa kumleta huku kwa matibabu ya
juu zaidi.Mimi ndiye niliyekuwa
daktari wake hivyo ikanibidi
nisafiri naye.Sifahamu chochote
kuhusu Edger ,sifahamu familia
yake wala sijui kama ana mke au
hana” akasema Olivia
“Hujawahi kumuuliza kuhusu
familia yake?
“Hapana sijawahi
kumuuliza.Edger mwenyewe
amekuwa mgumu sana kuongelea
chochote kuhusu familia yake”
akasema Olivia
“Sawa Olivia ahsante sana kwa
kuja kunitembelea” akasema Dick
na Olivia akatoka akaelekea katika
chumba cha Edger
Mara tu Olivia alipotoka,Dick
naye akatoka akiwa na simu
aliyopewa na Yair kwa ajili ya
matumizi kwa muda wote
atakaokuwepo nchini
Israel.Alikwenda kujitenga sehemu
iliyotulia akaandika namba za simu
za waziri mkuu akampigia
“Hallo” akasema waziri mkuu
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania baada ya kupokea simu
ya Dick
“Mheshimiwa waziri mkuu
shikamoo”
“Marahaba
Dickson,unaendeleaje
huko?akauliza waziri mkuu.
“Hukuninaendelea vyema
mzee wangu.Kila kitu kinakwenda
vyema”
“Nafurahi kusikia hivyo
Dickson.Vipi mgonjwa wetu
anaendeleaje?
“Maendeleo yake nimazuri
yanatia moyo.Anapata matibabu
mazuri na anaendelea vyema”
“Ashukuriwe Mungu sana kwa
maendeleo haya
mazuri.Tunamuhitaji sana huyo
kijana hivyo hakikisha anakuwa
salama kwani waliotaka kumuua
hawatafurahi wakisikia kwamba
anaendelea vyema.”
“Mzee kuna jambo nataka
kukuomba unisaidie”akasema
Dickson
“Omba chochote Dickson”
akasema waziri mkuu
“Mzee nataka kufahamu
kuhusu familia ya Edger
Kaka.Nataka kufahamu kuhusu
wazazi wake ni akina nani na wako
wapi,nataka kufahamu kama ana
watoto au hana na kama anao wako
wapi?Nani mke wake? Nisaidie
kupata taarifa hizo mheshimiw
waziri mkuu” akasema Dickson.
“Nitakusaidia kupata taarifa
hizo Dickson lakini nataka
kufahamu je kuna sababu yoyote ya
kutaka kupata taarifa hizo?akauliza
waziri mkuu
“Ndiyo mzee.Kuna mambo
yametokea ambayo yamenifanya
intake kupata taarifa hizo.Baada ya
kuzipata na kuzifanyia kazi
nitakujulisha ni kwa nini
ninazihitaji” akasema Dickson
“Sawa Dickson.Nitamuelekeza
spika wa bunge akutumie taarifa
hizo zote katika barua pepe yako na
kama kuna kitu chochote
unakihitaji usichelewe kunijulisha”
akasema waziri mkuu na kuagana
na Dickson.
*****************
Dr Olivia baada ya kutoka
chumbani kwa Dick alielekea katika
chumba cha Edger akaingia bila
hata kugonga hodi akamkuta Edger
akizungumza na Judy.
“Edger unaendeleaje? Dr Olivia
akamsalimia Edger ambaye
alimtazama na kwa sauti ya
unyonge akasema.
“Naendelea vizuri Olivia,habari
za toka jana?
“Habari nzuri.Vipi hali yako
kwa jumla?
“Kwa ujumle ninaendelea
vizuri na kama hali ikiendelea
namna hii,nitaomba kurejea
nyumbani haraka sana”akasema
Edger na kumstua Dr Olivia
“Kurejea nyumbani? Dr Olivia
akashangaa
“Ndiyo Olivia.Ninahitaji
kurejea nyumbani.Maendeleo
yangu ni mazuri na sina sababu ya
kuendelea kukaa hapa,nina mambo
mengi yanayonisubiri
nyumbani.Mbona
umeshangaa?hutaki kurudi
nyumbani? Hakuna shughuli
zinazokusubiri kule?” Edger
akauliza
“You must be kidding Edger”
Olivia akasema huku akicheka
“Sitanii Olivia.Nimeamua
kurudi nyumbani”
“Hujanipa bado sababu za
msingi za kuamua kurudi
nyumbani ukiwa bado haujapona
vizuri”akasema Dr Olivia
“Olivia ninaendelea vizuri kwa
sasa na ninaweza kurudi nyumbani
na kuendelea na matibabu katika
hospitali za serikali.Unaonaje wazo
hili? Edger akauliza
Dr Olivia akamtazama Edger
usoni halafu akasema
“Edger naomba
unisikilize.Suala la kurudi
nyumbani kwa sasa ni
gumu.Utarudi nyumbani pale
utakapokuwa umepona.Mimi ndiye
niliyekuleta huku na ndiye
nitakayekurudisha.Mimi ni daktari
na ninafahamu kwamba bado
hujapona” Dr Olivia akasema
“Olivia nashukuru sana kwa
kuyaokoa maisha yangu kwa
kunileta huku Israel.Najua
umetumia muda mwingi na
gharama kubwa lakini kwa hapa
nilipofika nadhani niko salama na
ninaweza kurudi nyumbani.Kwa
nini hutaki kurudi nyumbani? Kitu
gani kinakufanya upende kukaa
huku katika nchi za watu?
Edger akasema huku uso wake
ukiwa umeanza kuonyesha dalili
Fulani za hasira.
“Hapana Edger hautarudi
Tanzania hadi pale utakapokuwa
umepona kabisa.Lakini kama
umeamua kwa hiari yako kurudi
Tanzania sikukatazi.Unaweza
kurudi lakini mimi bado
nitaendelea kubaki hapa hapa hadi
hapo nitakapoamua kurudi
nyumbani.” Dr Olivia akasema huku
naye uso wake ukionyesha hakuwa
na masihara tena.
“Nitarudi nyumbani
Olivia.Utake usitake ni lazima
nirudi nyumbani.You can’t control
me..” Edger akafoka.Dr Olivia
akabaki akimshangaa.Judy aliona
hali ile iliyoanza kujitokeza mle chumbani akatoka nje na kuwaacha
Edger na Olivia
“Whats going on Edger ? Dr
Olivia akauliza
“I want to go home,that’s all”
Edger akajibu
“I’m tired of being alone in
here” Akasema tena
“Alone? Dr Olivia akauliza kwa
mshangao
“Yes alone.No body cares for
me here.Kila mtu yuko hapa kwa
mambo yake!! Akasema Edger na
kumfanya Dr Olivia kucheka
kidogo.
“Edger Please stop.Don’t ever
say that again.Hakukuwa na mtu
yeyote aliyeyajali maisha yako zaidi
yangu mimi ndiyo maana
nikajitolea kufa na kupona ili
kuhakikisha ninakufikisha hapa.
Ninakujali na ndiyo maana
nimeacha shughuli zangu zote kwa
ajili ya kukuhudumia wewe tu. I’m
here for you.”
Edger hakujibu kitu
akaendelea kutazama chini.
“Edger nieleze nikufanyie kitu
gani ili ujue kwamba ninakujali? Dr
Olivia akauliza tena
“Ulikuwa wapi jana usiku?
Edger akauliza
“Jana usiku? Dr Olivia akauliza
kwa hamaki
“Ndiyo jana usiku ulikuwa
wapi?”
“Kwa nini unauliza hivyo? Dr
Olivia akauliza
“Judy alinipigia simu na
kuniuliza kama niko na wewe kwa
sababu ulimuaga unakuja hospitali
kuonana nami lakini sikukuona
kabisa jana usiku hapa
hospitali.Ulikwenda wapi?
“Nilikuwa hotelini” Dr Olivia
akajibu kwa haraka na kwa ufupi
“Usinidanganye Olivia.Kama
ungekuwepo hotelini Judy
asingepiga simu
kukuulizia.Ninafahamu kwamba
jana ulikuja hapa hospitali ulikuwa
na Christopher” Edger akasema .Dr
Olivia akamuangalia kwa jicho kali.
“Ulikuwa
unanifuatilia?akauliza Dr Olivia
“Nilitaka tu kufahamu uko
wapi na ndiyo maana nikauliza
mapokezi kama umeonekana
maeneo haya wakasema kwamba
ulikuwa bustanini na Christopher”
Edger akasema
“Edger masuala yangu binafsi
yanakuhusu nini? Dr Olivia akauliza
kwa ukali.
“Ni kwa sababu ninakujali
Olivia.Nilipatwa na wasiwasi kama
uko salama”
“Edger please ! Don’t ever try
again to do that.Who am I to you?
Am I your wife or girlfriend?
Sikutegemea Edger kama unaweza
ukafanya kitu kama hiki.For the
records I don’t like
this.……”akasema Dr Olivia kwa
ukali
“Dr Olivia let me explain”
Edger akasema
“You have nothing to explain
Edger.Niliona toka jana
tulipotambulishwa kwa
Christopher,ulimchukia ghafla.Kwa
nini humpendi Chris? Olivia
akauliza kwa ukali
“He’s good for nothing
Olivia.Don’t fall for that man from
nowhere,he’s not good for you!!
Edger naye akajibu kwa sauti yenye
ukali ndani yake
“Good for nothing? Akauliza Dr
Olivia
“A good for nothing is you
Edger !! Huwezi kujilinganisha na
Chris.He is a gentleman” Dr Olivia
akajibu kwa sauti kali
“I am a gentleman Olivia.I care
about you! Edger akasema
“You care about me? Olivia
akauliza
“And why do you care? Dr
Olivia akauliza tena
“Because I love you…….!!”
Edger akajikuta akitamka kwa
nguvu.
Dr Olivia akashika kiuno huku
akimshangaa Edger.Hakuamini
alichokuwa amekisikia toka kwa
Edger.
“Stupid……………!!” Akasema
Olivia akanyakua mkoba wake na
kutoka kwa kasi mle chumbani.
“Olivia..I’m sorry” Edger
akasema baada ya kuona Dr Olivia
akiondoka mle chumbani akiwa
amekasirika.Dr Olivia hakugeuka
nyuma akaufunga mlango na
kuondoka.Edger akajishika kichwa
na kujilaumu
“Its true..I’m a stupid..How
could I do something like that?
Edger akajilaumu akiwa ameweka
mikono kichwani.
“Wivu umepelekea haya yote
kutokea.Nilipaswa kuwa mvumilivu
lakini sasa nimemkasirisha
Olivia.Badala ya kumuweka Olivia
karibu sasa nimemsogeza mbali
zaidi.Itanigharimu kumrejesha
karibu zaidi kwani tayari nimempa
tiketi ya kuwa karibu zaidi na
Christopher.I hate this guy!!
Akawaza Edger na kwenda
kuchungulia dirishani
“Sikupaswa kufokeana na
Olivia ambaye ndiye aliyeyaokoa
maisha yangu. Kama kweli
ninampenda na ninataka kuwa
naye maishani ninapaswa
kumuomba msamaha haraka
iwezekanavyo.” Edger akawaza.
“Hapana hili si wazo zuri kwa
sasa kwani bado ana
hasira.Nitazungumza naye hasira
zikipungua” Akawaza Edger Dr
Olivia alipoondoka pale hospitali
alielekea moja kwa moja hotelini
“Kumbe Edger ametokea
kumchukia Chris kwa sababu
ananipenda,so stupid.!!.Siwezi
kuwa na mahusiano na
mwanasiasa.Uhusiano wangu naye
utabaki wa mgonjwa na
daktari.Hajafanya vibaya kuweka
wazi hisia zake kwangu lakini
hakutumia busara.Alitakiwa atafute
njia nyingine ya kuelezea hisia zake
kwangu na si kwa kuanza
kunifuatilia nyendo
zangu.Ameniudhi sana kwa hili
alilolifanya” Dr Olivia akawaza
“Wanaume!!..yaani
kumuonyesha kumjali katika
kipindi hiki kifupi tayari
ananitaka.!!! Dr Olivia akawaza na
kwa mara ya kwanza toka ametoka
hospitalini akatabasamu.
“Edger ni kijana
mzuri,mwenye sura
nzuri,anapendwa na watu wengi
lakini kwangu mimi atabaki kuwa
rafiki yangu na si zaidi ya hapo.Sijui
kwa nini moyo wangu unastuka
kila nikimfikiria Chris.Ni mapema
sana kusema lakini nahisi kuna kitu
Fulani kati yetu ndiyo maana
namuwaza namna hii.Toka
nimeonana naye hazipiti dakika
bila kuiwaza sura yake yenye
tabasamu la kupendeza.Is he the
one I’ve been looking for? Anaweza
kuyatibu majeraha ya mapenzi
moyo wangu uliyoyapata toka kwa
Nickson? Siwezi kumsahau
baradhuli yule kwa jinsi
alivyonitenda.Alinilaghai na mimi
nikaridhika kwamba ananipenda
kumbe hana lolote.Niliumia sana
.This time I don’t want to get hurt.I
need someone special for me
only.Kwa funzo nililolipata toka
kwa Nickson sitakiwi kuwa na
haraka na Chris.Nahitaji muda
mwingi wa kumfahamu vizuri
zaidi” Dr Olivia akawaza
Akiwa bado katika mawazo
mengi juu ya kilichotokea muda
mfupi uliopita aliamua kumpigia
simu Stanley.Akawasha kompyuta
na kumtafuta Stanley akampigi
simu
“Edger habari yako? Akasema
Stanley
“Habari si nzuri Stanley”
akasema Edger
“Kuna matatizo gani tena ?
Stanley akauliza akionekana kuwa
na wasi wasi
“Nimekwaruzana na Olivia
asubuhi hii alipokuja
kunitazama.Nilipomuona
nilishindwa kujizuia nikajikuta
nikisema maneno mabaya ambayo
yamemuudhi sana .Ameondoka
kwa hasira nyingi .Hapa nilipo
nimechanganyikiwa sijui hata
nifanye kitu gani” akasema Edger
“Edger ndugu
yangu,nimekwisha kuonya mara
nyingi kuhusu huyo Olivia.Ukitaka
kufanikiwa katika mambo yako
achana naye kabisa.Uhusiano wako
naye ubaki wa mgonjwa na daktari
na si vinginevyo.Hebu tulia akili
Edger na ufikirie mambo ya
msingi.Una mambo ya muhimu
sana yanakukabili ambayo
inakubidi uelekeze nguvu zako
huko na si kupoteza muda mwingi
kumuwaza Olivia ambaye hana
msaada wowote kwako”Stanley
akasema
“Olivia ni mtu muhimu sana
katika maisha yangu.Hata kama
nikifanikiwa ndoto zangu lakini
sintakuwa na furaha kamwe kama
sintakuwa naye.Tuachane na hayo
nipe habari za huko” Akasema
Edger
“Habari za huku nzuri.Jana
usiku nimezungumza na Mathew
Lazaro ambaye mwenyekiti wa
chama cha Democratic,nimeongea
naye kwa kirefu sana kuhusu
mpango wako na amefurahi kupita
kiasi.Ameniambia kwamba nimpe
siku ya leo na kesho ili aitishe
mkutano wa dharura wa kamati
kuu walijadili suala hili halafu
watatoa jibu.Lakini uwezekano wa
kukubali ugombee urais kupita
chama chao ni mkubwa sana kwa
sababu walikuwa wakikuna vichwa
katika kutafuta mgombea mwenye
sifa anayeweza kupeperusha
bendera ya chama chao katika
uchaguzi huu.Kwa hiyo tusubiri
majibu yao halafu tuone tutafanya
nini.” Stanley akasema
“Stanley umefanya vyema japo
umekwenda haraka sana.Lengo
langu kubwa lilikuwa ni
kukifahamau vyema hicho chama
kama kinaweza kunifaa”
“Edger hatuna muda wa
kusubiri.Ngoja ngoja unaweza
ukajikuta umebadili
mawazo.Mambo lazima yaanze
haraka sana na moto huu ulioanza
hautazimika” akasema Stanley
“Vema Stanley utanijulisha jibu
watakalokupa lakini hata mimi
ninataka kuonana na daktari
niombe ruhusa ya kurejea
nyumbani nikaendelee na matibabu
katika hospitali za serikali.Sitaki
kuendelea kukaa huku.Maendeleo
yangu ni mazuri sasa hivi.” Edger
akasema.
“Edger wazo la kurejea
nyumbani si wazo baya kama
madaktari wataona inawezekana
litakuwa jambo jema” Stanley
akasema.
“Nitakujulisha itakavyokuwa
Stanley” akasema Edger na kukata
simu

TANZANIA
Saa sita za mchana Damian
Mwamba akiwa ameongozana na
dereva wake waliwasili mjini
Morogoro.Moja kwa moja
wakaelekea City 5 stars hotel moja
kati ya hoteli kubwa na nzuri
ambako alipatiwa chumba na kwa
kuwa hakuwa na mizunguko
mingine hapo Morogoro yoyote
akaamua kujipumzisha chumbani
kwake.Alijitupa katika kitanda
kikubwa kilichokuwemo mle
chumbani na mara sura ya Sintah
ikamjia akilini na kumfanya
atabasamu.
“This girl is driving me
crazy.Nina mipango mikubwa sana
na mizuri juu yake pindi
akishamaliza masomo yake ya
kidato cha sita.Binti kama yule
anatakiwa kuwekwa katika sehemu
nyeti kama benki kuu au sehemu
yoyote ile yenye hadhi
kubwa.Ngoja nimpigie simu
nimtaarifu kuwa nimeshafika
Morogoro” Akawaza Damian
Mwamba huku akizitafuta namba
za Sintah katika simu yake akapiga
“Hallo darling” Ikasikika sauti
tamu ya Sintah.
“My baby,how are you?
Akasema Damian Mwamba huku
akitabasamu.
“I’m fine baby.How are you?
Akasema Sintah kwa sauti nyororo
iliyomsisimua Damian.
“Wewe mtoto hiyo sauti yako
kila nikiisikia inanitoa jasho”
Akasema Damian huku akicheka
“Ouh Darling I love
you.Umefika wapi sasa hivi?
Akauliza Sintah
“Mimi tayari niko
Morogoro.Niko hapa City 5 stars
hotel chumba namba 127.”
“wow..kumbe umeshafika?
“tayari nimefika malaika
wangu.Ninakusubiri,saa ngapi
utakuja? Kumbuka nimevuruga
ratiba zangu na kuamua kulala
hapa Morogoro kwa ajili yako.”
“Nashukuru sana darling kwa
kunijali.Kila kitu tayari nimekiweka
sawa hapa shuleni.Nitaondoka
hapa saa moja na nusu wakati
tayari kuna giza nitafika hapo
kuanzia saa mbili za usiku.”
“Usikose kuja kwa sababu nina
hamu sana na wewe.Unanipa vitu
adimu na kunifanya kijana kila
ninapokuwa nawe.” Akasema Mr
mwamba huku akicheka.
“Usijali Darling,mimi ni wako
leo hadi asubuhi.Mwaaaahh.”
Sintah akamalizia na busu zito
halafu akakata simu.
Damian Mwamba aliendelea
kutabasamu ,akainua simu ya mle
chumbani na kuomba aletewe
mvinyo.
*****************
Paul alikuwa makini akifuatilia
maongezi kati ya Damian Mr
Mwamba na Sintah kupitia
mitambo yake iliyoyanasa
maongezi yale moja kwa moja
kupitia chombo kidogo
kilichowekwa katika simu ya
Damian.Baada ya simu kukatwa
akavua spika za masikioni
alizokuwa amevaa ,akatabasamu.
“Finaly Damian Mwamba is
going down” Akasema huku
akitabasamu.
Akiwa bado anatabasamu
akainua simu yake na kumpigia
Donald Nkebo
“Hallo Paul habari yako?
“Habari yangu nzuri Mr
Nkebo.Nimekupigia nina taarifa
muhimu kwamba leo ni siku ya
historia kubwa kwani mmoja kati
ya wanasisasa wakubwa wa nchi hii
Damian Mwamba anakwenda
kupotea kabisa katika medani za
siasa.” Paul akasema na kumfanya
Mr Nkebo kutoa kicheko kikubwa.
“Niambie Paul nini
kinaendelea?akauliza Donald
Nkebo
“Damian Mwamba yuko
Morogoro tayari amefikia City 5
star hotel chumba namba
127.Ametoka kuwasiliana na Sintah
muda mfupi uliopita na
wamepanga kukutana saa mbili
usiku wa leo ambapo Sintah atalala
na Damian hotelini hapo hasi
asubuhi ya kesho.Kwa kuwa
tulikiwisha fahamu kuhusu mpango
huu,tayari vijana wangu
wanakaribia kufika Morogoro
ambako watakutana na wazazi wa
Sintah na kuwaeleza kila kitu
anachokifanya Damian Mwamba
halafu wataambatana hadi katika
hoteli alikofikia Damian
Mwamba.Vijana wangu
wamefuatana pia na waandishi wa
vyombo vikubwa vya habari hapa
nchini ambao wataripoti tukio hilo
la Damian mwamba kufumaniwa na
mwanafunzi wa sekondari.Kuanzia
usiku wa leo habari kubwa
itakayokuwa ikitawala anga za
habari ni kuhusu fumanizi la Mr
Mwamba.Nitakupigia tena simu saa
nne za usiku baada ya mambo
kukamilika” Paul akasema.Huku
akicheka Donald Nkebo akasema
“Paul una akili sana.Vipi
kuhusu Edger mipango
inakwendaje?
“Kuhusu Edger tunaendelea
kusubiri taarifa kutoka kwa Judy.
Nitakutaarifu nitakapopata kitu
chochote kutoka kwake” Paul
akasema
“Ahsante sana Paul.Tuendelee
kuwasiliana.Nimepanga kuonana
na mheshimiwa rais baadae. leo,naamini atafurahi sana kusikia
hatua mliyofikia.Kazi njema Paul”
akasema Donald Nkebo na kukata
simu.
HAIFA – ISRAEL

Dickson Kipuma alipokea
barua pepe kutoka kwa spika wa
bunge ambayo ilikuwa na taarifa
zote za mbunge Edger kaka.Taarifa
ile ilieleza Edger ni mtoto yatima
ambaye wazazi wake wote
walikwisha fariki.Taarifa ile bado
iliendelea kuonyehsa mpaka wakati
ule mbunge Edger alikuwa bado
hajaoa na hana familia.
“Hii inazidisha ukakasi.taarifa
zinaonyesha Edger kaka hana
wazazi,wote wamekwisha fariki
lakini usiku wa jana nilipompigia
simu yule mwanamke Habiba alijua
anazungumza na Edger na
akamuita “mwanangu”.Alikuwa na
maana gani kumuita Edger
mwanae?Ni mwanae
kivipi?akajiuliza Dickson.
“Naanza kupata picha kuna
mambo ambayo hatuyafahamu
bado kuhusiana na Edger
kaka.Kuna mambo yamejificha sana
ambayo lazima
tuyafahamu.Anafahamiana na
Habiba ambaye ana mafungamano
na mtandao wa IS.Who is this
guy?akajiuliza Dick
“Nimemuona anatumia sana
kompyuta yake kuwasiliana.kwa
bahati mbaya nilikosea kutega
kamera hivyo nashindwa kupata
sauti kujua anazungumza na nani
na anazungumza nini.Nitalazimika
kuipata kompyuta ile niweze
kuchunguza mawasiliano yake”
akawaza Edger na kumpigia simu
Yair
“Yair kuna msaada wako
ninautaka wa haraka sana”
“Sema unachokitaka Dickson”
“Nimepokea barua pepe
kutoka Dar es salaam yenye
maelezo yote ya kuhusina na Edger
kaka.Maelezo yanaonyesha Edger
hana wazazi.Wote wamekwisha
fariki.Vile vile mpaka sasa hana
mke wala mtoto.Nikiunganisha
taarifa hii na kile kilichotokea jana
Habiba kumuita Edger mwanae
ninazidi kupata hamu ya kuendelea
kumchunguza huyu jamaa kwani
inaonekana kuna mambo mengi ya
siri ambayo hatuyafahamu kuhusu
huyu mtu”
“Unataka kufanya nini
Dickson?Yair akauliza
“Nataka Edger atolewe
chumbani kwake ili nikaichukue
kompyuta yake ambayo ndiyo
anaitumia sana katika
mawasiliano.Nataka kujua
anawasiliana na akina nani.Fanya
mpango daktari aje amchukue na
kumtoa chumbani” akasema Dick
“Sawa Dick naomba unipe
muda mfupi nilishughulikie hilo
suala” akasema Yair
Baada ya dakika kumi Yair
akampigia simu na kumtaka aende
katika chumba cha Edger kwani
tayari amekwisha chukuliwa
amepelekwa kwa daktari.Bila
kupoteza muda Dickson akaingia
katika chumba cha Edger na
kuikuta kompyuta juu ya meza
akaifungua na haraka haraka
akaanza kutafuta rekodi za
mawasiliano yote ya Edger katika
kompyuta ile.Akazipata na
kuzihifadhi katika kifaa chake
kidogo cha kuhifadhia kumbu
kumbu halafu akatoka na kurejea
chumbani kwake akamjulisha Yair
kwamba tayari amekwisha toka
chumbani kwa Edger na
amefanikiwa kupata kile
alichokuwa anakitafuta.
Dick akachomeka kifaa kile cha
kuhifadhi kumbu kumbu katika
kompyuta yake na kuanza kupitia
kumbu kumbu zote za mawasiliano
ya Edger.Kwa kutumia kompyuta
yake Edger alikuwa amewasiliana
na watu wawili tu mmoja ni Stanley
na mwingine ni Sayid Omar ambaye
amewasiliana naye mara mbili.
“Sayid Omar hili si jina geni
kulisikia” akawaza Dickson na
kujaribu kuvuta kumbu kumbu ni
wapi amewahi kulisikia jina lile
lakini akashindwa kukumbuka
“Kumbu kumbu haziji lakini
jina hili si geni masikioni mwangu”
akawaza na kumpigia Yair
“Yair huyu jamaa
amewasiliana na watu wawili tu
ambao ni mtu anaitwa Stanley
ambaye naamini atakuwa
mtanzania na mwingine anaitwa
Sayid Omar ambaye amewasiliana
naye mara mbili” akasema Dickson
“Umesema Sayid
Omar?akauliza Yair akionekana
kustuka
“Ndiyo.Inaonyesha amempigia
simu kwa kutumia mtandao wa
skype mtu anaitwa Sayid Omar” “Dickson kama utakumbuka
jana nilikueleza kwa kirefu kuhusu
Habiba mwanamke tajiri sana
ambaye alikuja kumuona Edger
Kaka hapo hospitali,nikakueleza pia
kwamba mshirika mkubwa wa
Habiba anaitwa Sayid Omar na
huyu ndiye ambaye amekuwa
mfadhili mkubwa wa kikundi cha IS
kwa sasa.Kama Edger kaka
anafahamiana na anawasiliana na
Sayid Omar ni wazi atakuwa
anafahamiana pia na Habiba Jawad
na hii inazidi kuongeza kigugumizi
kuhusu Edger.Je naye ana
mahusiano na kikundi cha
IS?Ninauliza hivyo kwa sababu
hainiingii akilini amefahamiana vipi
 
SIRI

Episode 19

Mtunzi.Patrick CK
na hawa jamaa? Je ni wao ndio
wanaofadhili harakati zake za
siasa?Kama wao ndio wafadhili
wake wakubwa wana malengo gani
naye? Akauliza Yair
“Yair umenipa mwelekeo
mzuri.Nadhani kuna ulazima wa
kumchunguza kiundani sana
namna anavyoendesha siasa
zake,tuchunguze vyanzo vyake vya
mapato,mali zake na kila kitu
kuhusu yeye.Kuna siri kubwa
anayo huyu jamaa” akasema
Dickson
“Endelea na uchunguzi
Dickson na kama kuna kitu
chochote unakihitaji nieleze
nitakusaidia” akasema Yair
akaagana na Dickson
Baada ya kutoka kuonana na
daktari Edger kaka alirejea
chumbani kwake akionekana kuwa
na furaha kubwa.Moja kwa moja
akaichukua kompyuta yake na
kumtafuta Stanley akampigia simu
“Hallo Stanley” akasema Edger
“Edger mbona sauti yako
inaonyesha furaha sana tofauti na
ulivyokuwa asubuhi? Akauliza
Stanley
“Stanley nina furaha kubwa
sana” akasema Edger
“Furaha ya nini ndugu yangu?
Akauliza Stanley
“Nimetoka kuonana na
daktari.Amekubali kuwa ninaweza
kurudi nyumbani na kuendelea na
matibabu ya kawaida katika
hospitali zetu za nyumbani lakini
ninatakiwa kila baada ya siku tisini
nije huku kwa uangalizi wa
maendeleo ya afya
yangu.Nimefurahi sana Stanley.I’m
coming home soon” akasema
Edger kwa furaha kubwa
“Hizo ni habari njema sana
Edger.Nafurahi kusikia unarudi
nyumbani.Huku nako mambo
yamekwenda vizuri.Nimepokea
simu muda si mrefu toka kwa
mwenyekiti wa chama cha
Democratic Bw Mathew Lazaro
kuwa baada ya kikao cha dharura
kamati kuu ya chama hicho
imekubaliana na nia yako ya
kugombea urais kupitia chama
chao cha Democratic.Hivi
nikwambiavyo wanaandaa ujumbe
mzito kuja kukuona huko huko
Israel kwa sababu hawakuwa na
uhakika ni lini utarejea
nyumbani.Kwa kuwa kwa sasa una
uhakika wa kurejea nyumbani basi
nitawataarifu kuwa hakuna haja ya
kuutuma ujumbe huo nchini Israel
bali wakusubiri hadi hapo
utakapokuwa umerejea nyumbani”
akasema Stanley.
“Hizo ni taarifa za kufurahisha
sana Stanley.Waambie hawana
sababu ya kuja huku tena kwani
muda si mrefu nitarejea nyumbani
tutakuja kuzungumza” akasema
Edger.
“Vipi kuhusu Olivia?
Umekwisha mpa taarifa ya daktari?
Stanley akauliza
“Olivia bado sijamtaarifu lakini
naamini hatalipokea vizuri suala
hili kwani yeye bado anataka
kuendelea kukaa hapa Israel ili awe
karibu na huyu kobe Christopher”
Edger akasema.
“Sawa Edger ngoja niwasiliane
na viongozi wa chama niwajulishe
kuhusu kurejea kwako
nyumbani.”akasema Stanley
“Stanley nashukuru sana kwa
msaada wako” Edger akajibu na
kukata simu “Safari ya kuelekea ikulu
inaanza kuiva.Sintarudi nyuma
katika azma yangu ya kuwania
urais wa Tanzania.Ni urais peke
utakaonipa nguvu ya kupambana
na wabaya wangu na hasa wale
wanaotafuna rasilimali za umma
kwa manufaa yao binafsi.Ni urais
huo huo ndio utakaonipa
mwanamke wa ndoto zangu
Olivia”Edger akawaza

******************
Edger akiwa amejipumzisha
chumbani kwake watu watatu
waliovalia suti nadhifu
wakaingia.Hakuwafahamu watu wale.Aliyekuwa wa kwanza kuingia
mle ndani akampungia mkono
huku akitabasamu kwa mbali
halafu akamtaka Edger asiwe na
wasi wasi kuna kazi wanataka
kuifanya mle ndani.Edger akapatw
ana wasi wasi mkubwa kuhusu
watu wale ambao kwa muonekano
wao hawakuonekana kama
madaktari.Mmoja wao alikuwa na
sanduku dogo akaliweka mezani na
kulifungua akatoa kompyuta na
kuiowasha halafu mmoja wao
akachukua kifaa Fulani akakiwasha
na kuanza kukipitisha kile sehemu
ya kile chumba na mara kikatoa
mlio.Akasimama na kisha akaanza
kwenda taratibu sana kufuatilia
mlio ule na mara akafika katika saa
ya ukutani na kuitungua saa ile
akaiweka mezani akaifungua na
ndani yake akatoa kamera
ndogo.Mwingine akaendelea
kuzunguka mle chumbani akiwa na
kifaa na mara akasikia mlio karibu
na kitanda cha Edger.Akamtaka
asimame na baada ya kuchunguza
akakuta kuna kitu kimenasishwa
chini ya kitanda akakitoa na
kuendelea kuzungusha kifaa kile
ndani ya chumba akasikia mlio
mwingine katika dirisha na kutoka
nyuma ya dirisha lililokuwa wazi
akakuta kuna kifaa kingine kidogo
akakibandua.Kutoka ndani ya kile
chumba walikuta kuna kamera tatu
za siri zimefungwa pamoja na vifaa
vingine vya kunasa mawasiliano
yote yanayofanywa na
Edger.Walijadiliana kwa lugha
ambayo haikuwa kiingereza
ambayo Edger hakuifahamu.
Dickson Kipuma akiwa
chumbani kwake amepumzika
alisikia mlio kutoka katika
kompyuta yake na baada ya
kuifungua hakuweza kuona
chochote kutoka katika kamera zile
alizozifunga katika chumba cha
Edger.Alipatwa na mstuko
mkubwa.
“Nini kimetokea?Mbona picha
zimekata ghafla?akajiuliza na
kujaribu kubofya kompyuta yake ili kurejesha picha lakini ghafla wakati
akiendelea na zoezi lile mlango
ukafunguliwa wakaingia watu
wawili waliovalia suti
nyeusi.Dickson haraka haraka
akaifunika kompyuta yake na
kuiweka kitandani.Wale jamaa
hawakumsemesha kitu.Dick
akasimama
“Karibuni” akasema kwa
kiingereza lakini wale jamaa
hawakujibu walionekana kana
kwamba kuna kitu wanakitafuta
mle chumbani.Mara ghafla mmoja
wao akamvaa Dick na kumtandika
ngumi nzito iliyomuangusha Dick
kitandani na kabla hajainuka
akachomwa sindano shingoni halafuakashikiliwa kwa nguvu
huku amefumbwa mdomo.Taratibu
macho yalianza kuisha nguvu.Wale
jamaa wakamlaza vizuri kitandani
na kuichukua kompyuta ya Dick
pamoja na simu aliyokuwa
anaitumia wakatoka na kurejea
katika chumba cha Edger
wakachukua vifaa vyao na kabla
yakuondoka mmoja wa wale jamaa
akamuandikia Edger katika
karatasi
“Call Sayid” akamuonyesha
Edger ujumbe ule kisha
wakaondoka
Edger jasho lilimtoka kwa kile
kilichotokea.kwanza alistuka sana
baada ya kushuhudia vifaa vile
vilivyokuwa vimetegwa chumbani
kwake.Aliogopa sana.Hakuwa na
wazo lolote kama kuna vifaa
vimetegwa katika chumba chake
“Nani wametega vifaa vile
katika chumba changu na kwa
madhumuni yapi?NImeshuhudia
vifaa vikitolewa sehemu mbali
mbali kama vile chini ya kitanda
kwenye dirisha na kwenye saa
mahala ambako huwezi kudhani
kumetegwa kifaa.Dah ! nimeogopa
sana kumbe hawa jamaa
wanaendelea kunifuatilia hadi huku
!! akawaza huku bado akiendelea
kutetemeka
“Hawa jamaa waliokuja hapa
ni akina nani?Wamejuaje kama
kuna vifaa vimetegwa humu ndani?
Sayid ndiye aliyewatuma?
Akajiuliza Edger na kukumbuka
kwamba aliambiwa ampigie Sayid
“Ngoja nimpigie sayid nijue
kama ni yeye aliyewatuma watu
hawa” akawaza na kuchukua
kompyuta yake na kumtafuta Sayid
akampigia
“Edger samahani kwa ugeni
wa ghafla ambao haukuutarajia”
akasema Sayid baada ya kupokea
simu aliyopigiwa na Edger
“Sayid hapa nilipo
ninatetemeka mwili
wote.Mmefahamuje kama kuna
vifaa vimetegwa katika chumba
changu?akauliza Edger
“Mama yako alikuja jana usiku
hapo hospitali kukujulia hali lakini
akakukuta ukiwa katika usingizi
mzito akakuachia ujumbe ule
kwamba umpigie”akasema Sayid
“Mama alikuja hapa jana?Kwa
nini hakuniamsha?Amewezaje
kuingia Israel bila
kujulikana?akauliza Edger
“usihofu kuhusu hilo lakini
ameweza kufanya kila
lililowezekana hadi akafika kuja
kukuona hata hivyo hamkuweza
kuonana.Kilichotokea ni kwamba
kuna mtu ambaye alikuwa
amefunga kamera za siri ndani ya
chumba chako na alikuwa
anafuatilia kila kinachoendelea na
baada ya mama yako kutoka
akachukua namba zile na kupiga
ndipo mama yako akastuka
kwamba haukuwa wewe akakata
simu na kuizima kabisa.Mimi
sikuwa nikilifahamu hilo uliponipa
zile namba ndipo nikagundua ni
namba za mama yako nikampigia
akanieleza kila kitu kilichotokea
ndipo nilipowatuma watu wangu
kuja kufanya uchunguzi katika
chumba chako na wakagundua
kwamba kuna kamera zilikuwa
zimefungwa katika chumba chako
pamoja na vifaa vingine vya kunasa
mawasiliano yote.Walikuwa
wanakufuatilia kwa kila
unachokifanya na mawasiliano
yako yote walikuwa wanayanasa”
akasema Sayid na kumstua sana
Edger
“Nani hao wanaonifuatilia
namna hiyo?Mmekwisha
wafahamu?akauliza Edger
“Usihofu kuhusu hilo
tumekwisha wafahamu ni akina
nani na tunawashughulikia mmoja
baada ya mwingine.Wapoambao
wako hapa Israel na wengine wako
Tanzania lakini nakuhakikishia
kwamba hakuna atakayebaki
salama wote lazima
washughulikiwe.Ondoa hofu sasa
uko salama” akasema Sayid
“Sayid nashukuru sana kwa
hili mlilolifanya.Nilikuwa kwenye
hatari kubwa bila
kufahamu.Ahsante sana nifikishie
salamu nyingi kwa mama” akasema
Edger
“Edger umefikia wapi katika
lile suala nililokutaka ufikirie?
“La kugombea urais?akauliza
Edger
“Ndiyo.Hiyo ndiyo njia pekee
ya kuweza kupambana na mtandao
huu.Edger umeandaliwa uwe mtu
mwenye nguvu kubwa na
tumekujenga ili uje uongoze nchi na
wakati wa kushika madaraka
makubwa ni huu.Tunataka kusikia
jibu lakokama uko tayari ili tuanze
mikakati mara moja ya kukuingiza
ikulu”
“Sayid sikuwa nimekujulisha
jambo hili lakini nimetafakari na
nimeamua kugombea urais.Lakini
sintagombea kwa kupitia chama
changu itanilazimu kuhama
chama.Nitagombea kwa kupitia
chama pinzani”
“Edger umenifurahisha sana
kwa maamuzi hayo na nina imani
hata mama yako atafurahi sana
akipata taarifa hizi.Umefanya
maamuzi mazuri na haijalishi
unagombea kupitia chama gani
kwani lazima utaingia
ikulu.Tutafanya kila
linalowezekana hadi kuhakikisha
kwamba unashinda uchaguzi.Edger
endelea kupumzika nitawasiliana
nawe baadae.Kwa sasa usiwe na
hofu uko salama” akasema Sayid
“Sayid kuna suala lingine
ambalo sikuwa nimekujulisha
pia.Kwa kuwa hali yangu
inaendelea vyema nimezungumza
na madaktari na wamesema
kwamba ninaweza kurejea
nyumbani nikaendelea kutibiwa
katika hospitali za nyumbani.Muda
wowote ninaweza nikarejea
nyumbani”akasema Edger
“Hapana Edger muda wa
kurejea nyumbani bado.Lazima
tuhakiki kwanza usalama wako
ndipo tukuruhusu urejee
nyumbani.Kwa sasa utaendelea
kukaa hapo hospitali hadi
tutakapokuelekeza” akasema Sayid
“Lini nitaonana na mama?
“Siwezi kukwambia lini
utaonana naye kwani tunazingatia
kwanza usalama wake.Muda
wowote anaweza akafika
hapo”akasema Sayid na kuagana na
Edger
“Jasho linazidi kunitoka.Watu
hawa wanazidi
kuniogopesha.Wamenikosa kuniua
kwa sumu lakini bado wanaendelea
kuniandama hadi huku.Hakuna
mahala ninakoweza kwenda
duniani bila watu hawa kuacha
kuniandama.Wanachokihitaji ni
roho yangu na kama alivyosema
Sayid kwamba njia pekee ya
kuweza kupambana na hawa jamaa
ni kushika nafasi ya
urais.Nikifanikiwa kushika nafasi
hii kubwa kabisa nitakuwa na
nguvu ya kupambana nao.Uhakika
wa kuingia ikulu ni mkubwa
sana,ninao mtaji mkubwa wa
wafuasi na nguvu ya mamana Sayid
ni kubwa na nikiunganisha na
nguvu yangu pia uhakika wa
kuingia ikulu ni mkubwa sana”
akawaza Edger
TANZANIA
Ni saa moja za jioni,jua
limekwisha zama na kiza tayari
kimekwisa tanda.Nje ya nyumba
moja iliyokuwa na rangi nyeupe
gari ndogo tatu zilisimama na watu
wanne waliovalia nadhifu sana
wakashuka toka katika gari
lililokuwa limetangulia mbele
wakaelekea getini na kubonyeza
kengele.Muda wa dakika mbili
mlango mdogo wa geti
ukafunguliwa na watu wale
wakakaribishwa.Ndani ya sebule
kubwa Mchungaji Apolo Leonard
na mkewe walikuwa wamepumzika
huku nyimbo za dini zikisikika kwa
mbali.Mchungaji Apolo alikuwa
ameishika biblia yake mkononi
akipitia maandiko huku mke wake
akitazama muziki wa kwaya katika
runinga kubwa.Mara tu wageni
wale walipoingia mle sebuleni
mama mchungaji akasimama na
kuwapokea.Mchungaji Apolo
akawapa mikono na kuwakaribisha
waketi.Wakahudumiwa vinywaji
halafu Mchungaji akaanzisha
maongezi.
“Ndugu zanguni karibuni sana”
“Tunashukuru sana baba
mchungaji” Mmoja wa jamaa wale
akasema.
“Naona kama wenzangu
mnanifahamu lakini mimi
siwafahamu” Mchungaji Apolo
akasema
“Kweli baba mchungaji,nina
imani hutufahamu japo sisi
tunakufahamu.Tumetokea jijini Dar es salaam.Ni waandishi wa
habari.Mimi naitwa ndugu Maiko
hastoni,mwenzangu pale anaitwa
Benard nyangeta,yule bwana pale
anaitwa Ezekiel stanslaus na yule
wa mwisho anaitwa bw Salvatory
Kelvin.” Akatoa utambulisho mfupi
Maiko ambaye alionekana kama
kiongozi wa msafara ule.
“Nimefurahi sana kuwaona
ndugu zangu karibuni sana.Mimi
naitwa Mchungaji Apolo Leonard
na yule pale ni mke wangu.Karibuni
sana” akasema mchungaji Apolo
“Baba mchungaji,safari yetu
imetufikisha kwako kwa masuala
mawili makubwa.Kwanza
tungependa kufahamu kama Sintah
Leonard ni mwanao” Maiko
akauliza.Mchungaji apolo akastuka
kidogo halafu akasema
“Kuna nini mbona mmenistua
sana” akasema mchungaji Apolo
“Usiogope mchungaji hakuna
jambo baya”
“Kama mnamzungumzia
Sintah Lenard anayesoma shule ya
Forest girls high school huyo ni
mwanangu”
“Tunashukuru kwa hilo baba
Mchungaji.Nadhani mwanao
anasoma shule ya bweni”
“Kweli kabisa,mwanangu
anasoma shule ya bweni”
Mchungaji Apolo akajibu huku
akiwa na wasi wasi
“Kwa siku za hivi karibuni
hujawahi kupata taarifa au hata
kusikia fununu zozote za mwanao
kuwa na mahusiano yoyote ya
kimapenzi na mwanaume yoyote?
“Hapana ndugu
mwandishi.Muda mwingi huwa
niko katika kazi zangu za
kichungaji,ninakwenda huku na
huko kwa ajili ya kutoa huduma ya
neno la Mungu na hata Sintah
anapokuwa amerudi likizo mara
nyingi huwa anakuwa na mama
yake.Kwa hiyo siwezi kufahamu
kama mwanangu ana mahusiano
yoyote ya kimapenzi.Siku zote
nimekuwa nikimuonya kwamba
asijiingize katika mambo yoyote
yanayohusiana na mapenzi hadi
hapo atakapokuwa amemaliza
masomo yake ya juu.Nataka
mwanangu awe msomi mkubwa
hata kunizidi mimi baba yake.Hiyo
ndiyo sababu niliamua
kumuhamishia katika shule ya
bweni ili aweze kusoma kwa uhuru
bila bughudha toka kwa vijana
wasumbufu” Mchungaji Apolo
akasema
Kimya kidogo kikatanda mle
ndani halafu Maiko akasema
“Baba mchungaji,tunajua una
nia ya dhati ya mwanao kupata
elimu iliyo bora kwa ajili ya maisha
yake ya baadae.Pamoja na nia hiyo
nzuri lakini vijana wengi siku hizi
wamekuwa wakienda kinyume na
matakwa ya wazazi wao.Kwa ufupi
tu baba Mchungaji ni kwamba
tumepata taarifa zenye uhakika
toka katika vyanzo vyetu vya
habari vikisema kwamba mwanao
Sintah ana mahusiano ya kimapenzi
na mmoja kati ya vigogo wakubwa
serikalini”
“Jesus christ!!! …” Mchungaji
Apolo akastuka.
“Ndugu mwandishi hiki
unachonieleza ni cha kweli?
“Baba mchungaji mwanao ana
mahusiano ya kimapenzi na mmoja
kati ya wanasiasa wakubwa wa
nchi hii.Tunao ushahidi wa kutosha
wa kuthibitisha mahusiano yao
kukuthibitishia hilo usiku wa leo
Sintah na kigogo huyo watakuwa
pamoja hotelini alikofikia kigogo
huyu ambaye alikuwa katika safari
ya kuelekea Dodoma lakini
ameahirisha safari yake kwa ajili ya
kuwa na Sintah usiku wa leo.Sisi
kama waandishi w a habari tuna
kazi ya kukomesha vitendo kama
hivi na ndiyo maana tumekuja hapa
kwako kukupa taarifa hii ili
kukuomba nawe uwe shuhuda wa
matendo machafu yanayofanywa
na wanasiasa wetu kuwarubuni
watoto wetu wa kike na kuwatumia
kimapenzi”
Mchungaji Apolo jasho lilianza
kumtoka.Alikuwa ameinama huku
akifanya maombi kwa sauti ndogo
na alipomaliza akawageukia akina
Maiko.
“Vijana imenibidi nifanye
maombi ili kuomba nguvu na roho
wa bwana aniangazie katika suala
hili kubwa ambalo
mmenieleza.Sikuwahi kuota kama
mwanangu niliyemlea kimaadili
angeweza kufanya kitendo kama
hiki tena na mtu mkubwa kama
mnavyodai.Mimi niko tayari vijana
wangu kwenda pamoja nanyi hadi
huko aliko huyo kigogo ambaye
anasababisha mwanangu ashindwe
kusoma.” Mchungaji akasema
“Baba mchungaji ahsante sana
kwa kushiriki.Katika tukio hili pia
tutaambatana na maafisa wa polisi
ambao watamtia nguvuni kigogo
huyo na kumfikisha katika vyombo
vya sheria ambako atafunguliwa
kesi na kama ikithibitishwa na
mahakama kwamba mtuhumiwa
alitenda kosa basi atahukumiwa
kwa mujibu wa sheria za nchi”
Maiko akasema.
“Sawa vjanaa,hakuna haja ya
kusubiri twendeni haraka sana
tukamtie nguvuni huyo shetani
mwenye kuharibu watoto wa watu”
akasema mchungaji Apolo kwa
hasira..
Walitoka pale chumbani
,wakaelekea hadi katika kituo kikuu
cha polisi ambako walichukua
askari polisi sita wenye silaha kwa
ajili ya kumtia nguvuni Mr
mwamba halafu wakaelekea city 5
star hotel
*******************
Saa moja za jioni Donald
Nkebo aliwasili Ikulu kwa ajili ya
kuonana na Rais.Dr Evans alikuwa
ameketi sofani akipata kahawa
huku akitazama kikao cha bunge
kilichokuwa kikiendelea katika
runinga.Akasimama na
kumkaribisha Donald
“Donald karibu sana” akasema
kwa furaha Dr Evans
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais.Habari za siku mbili tatu?
“Habari nzuri Mr Donald.Vipi
mambo yako yanakwendaje?
Akauliza Dr Evans
“Mambo yanakwenda vizuri
mheshimiwa rais” akasema Donald
“Donald nadhani tungeenda
moja kwa moja katika maongezi
kwa sababu ninategemea kuwa na
wageni nusu saa ijayo” akasema Dr
Evans huku akiongoza njia
kuelekea katika chumba cha
maongezi ya faragha.
“Donald nipe ripoti mambo
yanakwendaje? Akaanzisha
maongezi Dr Evans
“Mheshimiwa rais mambo
yanakwenda vizuri.Vijana wetu
wanafanya kazi nzuri
sana”akasema Donald na Dr Evans
akatoa kicheko kidogo
“Donald unanipa furaha kabla
hata sijajua ni kitu gani
kinaendelea” Dr Evans akasema
huku akicheka
“Mheshimiwa rais nilikuahidi
kwamba ni lazima utachaguliwa
tena kwa mara nyingine kuiongoza
Tanzania na ndivyo
itakavyokuwa.Mpaka sasa
tumeshathibitisha kwamba kuna
watu wawili ambao ni hatari wa
kwanza ni Damian Mwamba na wa
pili ni Edger kaka.Mheshimiwa rais
kwa upande wa Damian kama
ujuavyo ni mtu mwenye nguvu
kubwa ndani na nje ya
chama.Mtandao wake ni mkubwa
hivyo ni mtu tishio sana kwetu
kwani tayari amekwisha anza
harakati za kuhakikisha anateuliwa
na chama kupeperusha bendera
katika uchaguzi mkuu ujao.Pamoja
na umaarufu na nguvu alizo nazo
vijana wamefanya kazi kubwa
kuhakikisha anaangushwa na usiku
wa leo utakuwa wa kihistoria
kwake kwa sababu ni usiku
utakaomuondoa kabisa katika
uwanja wa siasa” akasema Donald
na kunyamaza kidogo.Dr Evans
alikuwa anamtazama Donald kwa
makini sana.
“Are they going to kill
him?akauliza Dr Evans akionekana
kuwa na wasiwasi
“Vijana wamefanikiwa
kugundua kwamba Damian
Mwamba ana mahusiano ya
kimapenzi na msichana wa shule
moja huko Mororgoro.Hivi
tunavyoongea vijana wetu
wakifuatana na baba wa
msichana,polisi na waandishi wa
habari wako njiani wakielekea
katika hoteli ambayo Damian
mwamba yuko na huyo msichana
anakutana na msichana huyo usiku
wa leo.Damian Mwamba atatiwa
nguvuni na kufunguliwa mashitaka
ambayo kutokana na sheria mpya
ya mwaka 2011 ni lazima atapatikana na hatia na kufungwa jela.Kwa hili
ninaamini kabisa kwamba
umaarufu wote wa Damian
Mwamba utapotea ndani ya masaa
machache yajayo.Ninasubiri ripoti
ya vijana usiku wa leo muda
wowote nikiipata nitakutaarifu”
akasema Donald na Dr Evans
akatabasamu
“Donald ama kweli
umenifurahisha sana kwa namna
unavyolipeleka hili suala”
“Wa pili ambaye alionekana ni
hatari kwetu ni huyu kijana Edger
kaka.Kama nilivyokutumia
maongezi yaliyonaswa na vijana
wetu ni kwamba Edger ana mpango
wa kurudi nchini Tanzania na kuna
uhakika mkubwa wa kugombea
urais kupitia chama cha
upinzani.Mpaka sasa hivi tayari
msaidizi wake mkubwa Stanley
amekwisha fanya mawasilianao na
chama cha democratic ili Edger
aweze kuhamia huko na kugombea
urais kupitia chama hicho.Tayari
wamekwisha mkubali na
kinachosubiriwa ni kumkaribisha
rasmi katika chama pindi
atakaporejea toka nchini
Israel.Muda wowote kuanzia sasa
Edger atarejea nchini kwa sababu
tayari amekwisha pewa ruhusa ya
kurudi nyumbani kutokana na hali
yake kuendelea vizuri.Mheshimiwa
rais kijana huyu akirudi na
akajiunga na chama cha upinzani
basi nina hakika ataugeuza upepo
wa kisiasa hapa nchini.Kijana huyu
ana maelfu ya wafuasi na hasa
vijana ambao ndio wapiga kura
wengi.Uungwaji wake mkono
katika jamii ni wa kushangaza
sana.Sisemi uongo kijana huyu
anapendwa mno hapa nchini.Ni
suala hili ndilo limenifanya nitake
kuonana nawe usiku huu ili tuweze
kusikia kutoka kwako una ushauri
gani” Akasema Donald Nkebo.Dr
Evans akamtazama huku
akitabasamu.
“Kwanza kabisa napenda
nichukue nafasi hii kukupongeza
Donald kwa kazi nzuri
uliyoifanya.Nimefurahi sana kutoka
moyoni.Mtu niliyekuwa namuhofia
sana ni Mwamba.Ninamfahamu
vizuri,amekuwa rafiki yangu wa
muda mrefu.Ninazifahamu mbinu
zake na uwezo wake.Huyu ndiye
aliyekuwa akininyima
usingizi.Lakini iwapo usiku wa leo
atatiwa nguvuni na vyombo vya
usalama basi hakuna mtu
mwingine ninayemuhofia.Labda
utokee muujiza atoroke kabla
hajatiwa nguvuni usiku wa
leo,lakini iwapo atakamatwa na
ushahidi wa kutosha basi mwisho
wake katika siasa za Tanzania
utakuwa umewadia.Nimefurahi
kupitiliza Donald”Dr Evans
akasema kwa furaha na kumpa
mkono wa pongezi Donald Nkebo
aliyekuwa akitabasamu na kucheka
kichini chini kama kawaida yake
“Kuhusu huyu kijana Edger
nimeona nikubaliane na ushauri
wako uliosema kwamba tunaweza
kumtumia Olivia katika
kummaliza.Hatuna sababu ya
kumuua bali tunaweza kumtumia
Olivia akamuondoa katika
siasa.Nilikupinga uliponieleza
jambo hili lakini baada ya
kutafakari kwa kina nimeona kuna
umuhimu wa kumtumia Olivia
katika kumuondoa huyu kijana
kwenye siasa”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais kuna jambo
sikuwa nimekufahamisha kwamba
uhusiano wa Olivia na Edger
umekuwa si mzuri kutokana na
Olivia kuwa karibu sana na kijana
mmoja toka Zimbabwe ambaye
naye kama Edger amelazwa katika
hospitali ile ile kwa maradhi ya
moyo.Kumetokea mtafaruku baina
yao na hii ndiyo sababu kubwa ya
Edger kutaka kurudi nyumbani
haraka.Pamoja namtafarukuhuo
uliojitokeza lakini bado Edgfer
anampenda sana Olivia na yuko
tayarikufanya chochote kwa ajili ya
kumpata”akasema Donald
“Nitazungumza na baba yake
Olivia ambaye ni rafiki yangu
mkubwa sana na kumtaka amuombe Olivia amkubali Edger ili
tuweze kumtumia katika mpango
huu wa kummaliza kabisa
Edger.Ninaamini atakubaliana
nami” akasema Dr Evans
“Wazo lako zuri mheshimiwa
rais,lakini tukiwa Dodoma
nilikueleza kwamba huyu kijana
Edger amekuwa anatufuatilia sana
mimi na wenzangu kuhusiana na ile
benki ya taifa ya vijana.Nilikueleza
kwamba kuna vijisenti tulivichota
na huyu kijana anao ushahidi
kwamba sisi ndio tuliosababisha
benki ile kufilisika.Utatusaidiaje
kwa hilo mheshimiwa rais? Huoni
kama akirejea atatuanika
hadharani na tukichafuka sisi ambao ni watu wako wa karibu na
wewe utachafuka pia” akaseam
Donald
“Unashauri nini Donald
kuhusu suala hilo?
“Ushauri wangu mimi kwa nini
huyu kijana tusimuondoe huko
huko Israel ili tujihakikishie
usalama?Tunavyoendelea
kumuacha hai anaendelea
kujipanga upya.Ushauri wangu
mimi ni kumuondoa haraka sana
akiwa hapo hapo hospitalini Israel”
akasema Donald
“Donald suala la kumuua huyu
kijana linaweza kuleta matatizo
kidogo kwa nionavyo mimi.Huyu
tummalize taratibu sana kiasi
kwamba hakuna ambaye atahisi
kwamba kuna mkono wa serikali
lakini kwa sasa akiuawa kila mtu
ataitupia lawama serikali na wakati
huu ambao tunaelekea katika
uchaguzi mkuu si wakati wa
kuzusha matukio ambayo
yanaweza yakaamsha hasiar kwa
wapiga kura.Tunatakiwa
kummaliza kama itakavyotokea
kwa Damian mwamba kila mtu
atajua amefanya kosa kutembea na
mwanafunzi na kila mtu atalaani
kitendo hicho hivyo basi na huyu
naye tunatakiwa kutafuta namna ya
kuweza kummaliza kwa njia
hiyo.Kuhusu suala la vijisenti
kutoka kwenye ile benki lisikupe
taabu nitajua nini cha
kufanya”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais wazo lako ni
zuri na nitawaelekeza vijana wangu
hasa yule aliyeko kule Israel
kumchimba zaidi Edger na
kumfahamu kiundani tuone namna
ya kummaliza kabla ya kipenga cha
uchaguzi kupulizwa”akasema
Donald na kunyamaza baada ya
mlango kugongwa
“Donald mlango huo
unagongwa nadhani ni wageni
niliokuwa nawategemea usiku huu
watakuwa wamefika.Tunaupenda
urais lakini si kazi nyepesi.Hakuna
muda wa kupumzika.Vikao kila
mara.Nashukuru sana kwa kazi
nzuri uliyoifanya Donald ila
endeleeni kumchimba zaidi
Edger.Nifikishie salamu zangu kwa
vijana na waambie kwamba
ninawaandalia jambo zuri ambalo
litakuwa na faida kwao na kwa
vizazi vyao”
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais kwa muda wako. Nakuahidi
kuyafanyia kazi maelekezo yako na
tutapata namna bora ya kummaliza
Edger Kaka.Nitazidi kukutaarifu
kila hatua tunayopiga”akasema
Donald na kuagana na rais akatoka
na kuingia katik agari lake
akaondoka.Usiku huu hakuwa na
dereva wale alikuwa anaendesha
gari mwenyewe.Mara tu alipotoka eneo la ikulu akampigia simu Paul
“Paul nipe mrejesho nini
kinaendelea Morogoro?Nimetoka
kuzungumza na mheshimiwa rais
sasa hivi na nimemuhakikishia
kwamba mbuyu utaanguka usiku
wa leo”
“Usiwe na shaka Donald kila
kitu kinakwenda vyema kabisa.Hivi
tuongeavyo tayari timu imekwisha
jikusanya na wanasubiri isife saa
tano au saa sita ndipo wamvamie
Damian wanataka wamkute akiwa
anafanya mapenzi na
Sintah.Nitakujulisha kila kitu
kitakavyokwenda”
“Paul hakikisha hakuna tatizo
lolote linatokea.Hakikisha kjila kitu
kinakwenda kama kilivyopangwa
kwani tayari rais ana uhakika
kwamba usiku wa leo ni wa
mwisho kwa Damian mwamba
katika siasa”akasisitiza Donald
“Itakuwa hivyo Donald”
akasema Paul
“Paul kuna jambo lingine pia
ambalo mheshimiwa rais ametoa
maelekezo.Anataka tumchimbe
zaidi Edger Kaka na kufahamu
mambo yake mengi ili tuweze
kummaliza kama tutakavyofanya
kwa Damian Mwamba.Ameshauri
kwamba kwa sasa haitakuwa
vyema kumuua bali tutafute namna
yoyote nyingine ya
kummaliza.Nataka nguvu kubwa
kwa sasa iwekezwe kwa Edger
ambaye atarejea nyumbani hivi
karibuni.Mheshimiwa rais
amenituma niwashukuru sana kwa
kazi kubwa mliyoifanya na
ameahidi kuwa mara tu kazi hii
itakapokamilika basi mtafurahi
wenyewe.Huu ni wakati wenu wa
kuuaga umasikini.Anasema
anawaandalia jambo zuri ambalo
litakuwa na faida kwenu na kwa
vizazi vyenu”akasema Donald
“Donald ninashukuru sana
kwa maneno hayo kutoka kwa
mhesimiwa rais.Kwa niaba ya
wenzangu ninasema ahsante
sana.Mr Donald….” Akasema Paul
na kusita kidogo
“Unasemaje Paul?
“Kuna jambo ambalo sikuwa
nimekueleza”
“Jambo gani Paul.Nieleze
tafadhali” akasema Donald
“Katika uchunguzi wetu
tumegundua kwamba Edger
amekuwa na mawasiliano na mtu
anaitwa Sayid Omar huyu ni mmoja
wa watu wanaodaiwa kufadhili
mtandao wa kigaidi wa IS”
“What ?! Donald akastuka
“Tulinasa mazungumzo ya
Edger na sayid na baada ya
kumchunguza sayid ni nani
tukagundua kwamba ni mmoja wa
watu wanaodaiwa kuwa wafadhili
wakubwa wa mtandao wa IS”
“Oh my God!
“Sikuwa nimekueleza hili kwa
sababu nilitaka kwanza kufanya
uchunguzi kuhusu mahusiano yao
lakini kwa kuwa mheshimiwa rais
ameelekeza kwamba tutafute
namna nyingine ya kummaliza
Edger kisiasa nimeona nikueleze
jambo hili.Edger kuna siri anazo
ambazo tukifanikiwa kuzifahamu
basi tutammaliza vizuri sana”
“Edger umenistua sana kwa
taarifa hiyo.IS ni kikundi hatari
sana kwa sasa na kama Edger ana
mahusiano na mmoja wa wafadhili
wa kikundi hicho basi huyu ni mtu
hatari sana.Naamini kama
mkiendelea kumchimba zaidi kuna
mambo mengi mtayagundua
ambayo tutayatumia
kummaliza”akasema Donald
“Ndiyo maana nililiweka suala
hili pembeni kwanza ili tuendelee
kuchunguza.Mpaka sasa Edger
amekwisha wasiliana na Sayid
mara mbiliakiwa hapo hapo
hospitali na mara ya mwisho
wamewasiliana leo.Nitakutumia
rekodi za mazungumzo yao
uyasikilize lakini tunaendelea
kumchimba zaidi huyo Edger”
akasema Paul
“Nitumie sasa hivi nisikilize
wanachokizungumza”akasema
Donald na haukupita muda mrefu
Paul akamtumia rekodi mbili za mazungumzo ya Edger na Sayid
Omar.Donald Nkebo akalazimika
kusimamisha gari pembeni akaaza
kuyasikiliza mazungumzo
yale.Alipomaliza kuyasikiliza
akampigia simu Paul
“Paul hili suala limenifanya
nihisi baridi.Kwa mujibu wa
mazungumzo yao Sayid
anamshawishi Edger agombee
urais.Sayid anatamka wazi kwamba
wamemuandaa Edger aje kushika
nafasi ya urais.Akina nani wako
nyuma ya Edger?Ni akina Sayid?I’m
confused” akasema Donald Nkebo
“Mr Donald unapomzungumza
Sayid Omar unazungumzia IS.Sayid
anadai kwamba wamemuandaa
Edger kwa muda mrefu hii ina
maana kwamba IS ndio walioko
nyuma ya Edger na wamekuwa
wanamuandaa kushika nafasi
kubwa ya urais”akasema paul
“Jesus !! akasema Donald
ambaye aliogopa sana
“Mr Donald nimeona ni vyema
nikujulishe kuhusu jambo hili lakini
bado ninaendelea na uchunguzi
zaidi kuhusiana na Edger.Nataka
nipate taarifa zake za kifedha
nataka niyafahamu maisha
yake.Nataka kuyafahamu maisha
yake kwa ujumla” akasema Paul
“Paul nakuomba fanya kila
uwezalo kumchimba Edger.Hiki
ulichokigundua kimenistua sana”
“Mr Donald ninakuomba kitu
kimoja.Usimweleze rais kuhusu
suala hili hadi hapo tutakapokuwa
tumekamilishja uchunguzi
wetu.Nataka tumueleze rais tukiwa
tayari na ushahidi wa kutosha
kwamba Edger ana mahusiano na
watu walio katika mtandao wa IS”
“Sawa paul sintamweleza rais
kuhusu jambo hili lakini tafadhali
fanya haraka katika uchunguzi”
“Nitajitahidi Mr Damian”
akasema Paul na kuagana na
Damian mwamba.
HAIFA – ISRAEL
Mlio wa simu iliyokuwamo
chumbani ilimstua Dr Olivia
ambaye tayari alikuwa amepitiwa
na usingizi.Akainuka na kwenda
kuipokea
“Hallo” akasema Olivia kwa
sauti ya uchovu
“Mapokezi hapa.Samahani
Olivia kuna mtu anahitaji
kuzungumza nawe anapiga kutoka
Rambam hospital anaitwa Edger
kaka.Uko tayari kuzungumza
naye?akauliza mtu wa
mapokezi.Olivia akafikiri kwa
sekunde chache halafu akasema
“Niunganishe naye”
Kikapita kimya cha sekunde
kadhaa halafu sauti ya Edger
ikasikika
“Hallow Olivia”
Olivia akavuta pumzi ndefu na
kusema
“What do you want Edger ?
“Olivia samahani kwa
kukusumbua lakini kuna mambo
mawili ninataka nikujulishe.Jambo
la kwanza la muhimu naomba
samahani kwa yote yaliyotokea leo
hospitali.Sikupaswa kukukwaza
Olivia.Naomba unisamehe
tafadhali” Edger akasema
Olivia akawaza halafu akasema
“Nimeshakusamehe Edger
lakini naomba nikiri kwamba
uliniudhi sana leo.”
“Nalifahamu hilo ndiyo maana
nimeamua kukuomba msamaha”
Edger akasema
“Nimeshakusamehe Edger ila
usirudie tena.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Olivia.Uko
wapi saa hizi? Edger akauliza
“Niko hotelini,kwani vipi?
Olivia akajibu
“Olivia nilitaka kufahamu uko
wapi kwa sababu kuna suala la
muhimu nataka nikueleze”
“Suala gani hilo Edger ?
“Nataka nikujulishe Yule
mwenzetu Christopher kutokea
Zimbabwe amefariki
dunia”akasema Edger
Taarifa ile ilimstua sana Olivia
akabaki kimya hakujua ajibu nini
“Olivia ! akaita Edger
“Edger umenistua sana na
taarifa hii.Tafadhali naomba huu si
wakati wa kufanya utani”
“Si utani Olivia ni kweli kabisa
Christopher amefariki dunia”
“Mungu wangu ! akasema
Olivia
‘Nini kimemuua?
“Mpaka sasa bado haijasemwa
nini kimemuua lakini madaktari
wanahisi ni kupanda kwa shinikizo
la damu kumepeleka kifo chake”
akasema Edger.Baada ya tafakari ya
muda Olivia akasema
“Edger ninakuja hapo hospitali
sasa hivi.Nataka nithibitishe kama
taarifa hizi ni za kweli” akasema
Olivia na kwa haraka akajiandaa ili
kwenda hospitali kuthibitisha
taarifa ile aliyopewa na
Edger.Alipomaliza kujiandaa
akaenda katika chumba cha Olivia
akamgongea mlango ili kumjulisha
kwamba anakwenda
hospitali.Aligonga mara tatu lakini
hakujibiwa akaamua kuondoka
Olivia alifika hospitali na
taarifa alizozikuta ni kweli
Christopher alikuwa amefariki
dunia.Olivia alimwaga machozi
mengi.Taarifa ile ya kufariki
Christopher ilikuwa nitaarifa njema
sana kwa Edger kaka kwani
alikuwa ni mtu aliyemnyima amani
sana katika mpango wake wa
kuanzisha mahusiano na Dr Olivia.
“Pole sana Olivia najua
umeumia kwa kifo hiki cha ghafla
cha Christopher.Najua ukaribu
wenu ulikuwa mkubwa lakini
nakusihi usiwe na hofu mimi nipo
hapa muda wowote ukihitaji mtu
wa kuongea naye” akasema Edger
akimbembeleza Olivia aliyekuwa
anamwaga machozi kwa kifo kile
cha ghafla cha Christopher au Dick.
Olivia alirejea hotelini kwake
akaenda moja kwa moja katika
chumba cha Judy kwa lengo la
kumjulisha kuhusu kifo cha
Dick.Aligonga mlango wa chumba
cha Judy mara tatu na kusubiri
lakini hakujibiwa.Akagonga tena
safari hii kwa nguvu zaidi lakini
hakujibiwa.Akakiminya kitasa
lakini mlango ulikuwa
umefungwa.Akaenda chumbani
kwake akapiga simu mapokezina
kuwauliza kama Judy ametoka
lakini jibu alilopewa ni kwamba
mapokezi hawakuwa na taarifa
zozote za Judy kutoka nje ya
hoteli.Akaenda tena katikamlango
wa Judy akagonga lakini hakukuwa
na majibu.Chumba kilikuwa kimya
kabisa.Akapatwa na wasi wasi
akaenda chumbani kwake akapiga
simu mapokezi na kuomba
muhudumu aje afungue chumba
cha Judy ili wahakikishe kama
ametoka.Dakika mbili muhudumu
akafika akiwa na kadi ya akiba na
kufungua chumba cha Judy.
Judy alikuwa amelala
kitandani na kulikuwa na michirizi
ya damu katika pua zake na
mdomoni.Olivia akahisi miguu
inaisha nguvu.Akamsogelea na
kumtikisa
“Judy !! Judy!! Akaita lakini
Judy hakufumbua hata ukope.Dr
Olivia akamshika kifuani lakini
hakuhisi mapigo ya moyo.Machozi
yaakanza kumtoka
“Oh my God she’s
gone”akasema kwa sauti ndogo
akamjulisha yule muhudumu
kwamba Judy tayari amekwisha
fariki.Haraka haraka taarifa
ikatolewa kwa uongozi wa hoteli
ambao walitoa taarifa kwa vyombo
husika wakafika kwa ajili ya
kushughulikia tukio lile.Kompyuta
ya Judy wala sanduku lake la nguo
havikuwemo mle chumbani na hii
ikazidi kumpa wasiwasi mkubwa
Dr Olivia
TANZANIA
Saa tatu na dakika nne za
usiku gari nne ziliingia katika hoteli
ya City 5 stars moja kati ya hoteli ya
hadhi ya juu mjini Morogoro.Watu
kadhaa wakashuka kutoka katika
gari wakiwa wameambatana na
polisi wenye silaha.Baada ya
kushuka wakaelekea moja kwa
moja mapokezi ambako waliomba
kuonana na meneja wa
hoteli.Wahudumu wa hoteli ile
walistuka sana baada ya kuuona
msafara ule wa watu ukiwa
umeongozana na askari wenye
silaha.Meneja wa hoteli
akawakaribisha ofisini kwake huku
akiwa na wasi wasi mwingi.
“Karibuni ndugu zangu”
akasema meneja ambaye kibao
kilichokuwa mezani kwake
kiliandikwa Justin.k. Mbwambo.
“Ahsante sana
bw.Justin.Tumefika hapa tuna
tatizo.Kuna mgeni mmoja
amepanga hapa hotelini kwako
anaitwa Mr Damiani Mwamba
amepanga chumba namba 127.”
“Mheshimiwa mbunge ni kweli
yuko hapa hotelini kwa mapumziko
ya sikumoja”
“Mheshimiwa huyu ndiye
aliyetuleta hapa.Tunao ushahidi wa
kutosha kabisa kwamba
mheshimiwa huyu yuko na
mwanafunzi wa sekondari
chumbani kwake sasa
hivi.Tumefuatana na mzazi wa
msichana huyo ambaye ni yule pale
baba mchungaji,wanausalama na
mashahidi mbali mbali ili
kuthibitisha kama ni kweli hilo
linalosemwa lipo ili hatua stahili
ziweze kuchukuliwa dhidi
yake.Kwa hiyo bwana Justin bila
kupoteza wakati tunaomba
utupeleke chumba namba 127 kwa
mheshimiwa Damian Mwamba”
Bila ubishi huku akiwa na wasi
wasi mwingi Justin meneja wa
hoteli ile akainuka kuongoza
msafara ule wa watu kuelekea
kilipo chumba namba
127.Walipofika wakauzunguka
mlango halafu Justin akagonga
mlango mara tatu.
“Nani? Ikauliza sauti ya kiume
kutokea ndani
“Huduma za hoteli” akasema
Justin
“Sihitaji huduma zozote kwa
sasa” ikasema sauti ile
“Samahani ndugu mteja kuna
mambo nataka
nikuelekeze.Naomba dakika mbili
tu” akasema Justin na baada ya
muda mfupi mlango ukafunguliwa
na Damian mwamba aliyekuwa
amejifunga taulo huku akiwa
akijifuta jasho akajitokeza na
kujikuta taulo alilokuwa amelishika
likianguka baada ya kushuhudia
kundi lile la watu na huku
akimulikwa kwa mianga ya
kamera.Haraka haraka akaubamiza
mlango kurudi ndani lakini askari
walikwisha muwahi na kuusukuma
mlango wakaingia ndani.Kitandani
alikuwepo binti mdogo akiwa
amejifunika shuka baada ya kundi
lile la watu kuingia mle
chumbani.Waandishi wa habari
kama kawaida yao waliifanyakazi
yao kwa haraka ya kuchukua picha
za haraka harak za hali waliyoikuta
mle chumbani.Nguo za msichana
yule aliyekuwa na Damian
mwamba zilikuwa sofani zikapigwa
picha.Damian Mwamba alikuwa
alianguka na kupoteza fahamu.
Justin aliita gari la wagonjwa
ambalo lilifika haraka na Damian
akapakiwa garini kukimbizwa
hospitali huku akisindikizwa na
gari la polisi lililokuwa na polisi
watatu na waandishi wa habari
ambao walitaka kwenda kuchukua
habari za hospitali.
“Binti hebu tafadhali jifunike shuka haraka.” Akaamuru askari
mmoja.Sintah hakuweza kujifunua
shuka kutokana na aibu.
“Nisameheni jamani” alisema
huku akilia.
“Tafadhali inuka na uvae nguo
zako haraka sana” Akaamuru tena
askari yule.Mchungaji Apollo
alikuwa amesimama huku akifanya
maombi ya kimya
kimya.Alipomaliza huku akiwa na
sura iliyokunjamana akasogelea
pale kitandani.
“Sintah ni mimi baba
yako.Nasema inuka haraka sana
hapo kitandani” Sintah aliposikia
sauti ya baba yake kwa haraka
akajifunua shuka kichwani.Uso
wote ulikuwa umejaa machozi.
“baba naomba unisamehe”
“Inuka haraka sana uvae nguo”
akasema mchungaji Apollo huku
uso wake ukionyesha hasira
kali.Sintah kwa aibu akaanza
kuinuka pale kitandani na ghafla
bila kutazamia mchungaji apolo
akamvamia mwanae na kuanza
kumvurumishia makofi
“Tunahangaika usiku na
mchana kuhakikisha unasoma uwe
na maisha mazuri kumbe huu ndio
upuuzi unaofanya !!! Alisema kwa
hasira mchungaji Apollo huku
akiendelea kuvurumisha makofi
makali usoni mwa mwanae.Askari
waliokuwa wamebaki mle
chumbani wakamshika na kumzuia
asiendelee kumuadhibu mwanae.
“Mwanangu huyu sijawahi
kumpiga hata kofi moja lakini kwa
alivyoniudhi leo imenibidi
nimtandike makofi.Nimemlea
katika maadili mema lakini kumbe
amevaa ngozi ya kondoo.Akinipa
mgongo huu ndio uchafu
aufanyao…” Aliendelea kulalama
mchungaji Apollo.Sintah huku
akilia akavaa nguo zake huku
waandishi wa habari wakiendelea
kumpiga picha.Mchungaji Apollo
alikuwa ameuficha uso wake kwa
viganja vya mikono yake.
“Nitauficha wapi uso wangu
mimi kwa aibu hii kubwa uliyonipa
Sintah? Akasema mchungaji kwa
hasira huku akitikisa kichwa.
Baada ya kuvaa nguo zake
akakalishwa kitandani akaanza
kuhojiwa huku akilia.Sintah
alishindwa kujibu maswali
aliyokuwa akiulizwa akainama
chini na kuuficha uso wake mikono.
“Baba mchungaji huyu
mwanao itabidi tuondoke naye kwa
ajili ya mahojiano zaidi.” Akasema
askari mmoja mwenye cheo cha
sajenti
“Ina maana anaenda kulala
polisi? Akauliza mchungaji Apollo
“Ndiyo mzee.Inatubidi
tuondoke naye hadi kituoni ili
akahojiwe halafu ataachiwa kwani kawaida mzee ni lazima afikishwe
kwanza kituoni kwa mahojiano
kabla mhusika hajafunguliwa
kesi.Halafu inabidi tumpeleke
akafanyiwe uchunguzi kama ana
maambukizi yoyote ya magonjwa
ya zinaa,ukimwi au kama ana
mimba”Akasema afisa wa polisi
Mchungaji Apollo akainama
akafikiri halafu akasema
“Afisa mimi kama mzazi
nimeumia mno na kitendo
alichokifanya huyu
mhesimiwa.bado siamini kama
mheshimiwa kama huyu anaweza
akawa ndiye mfano mbaya wa
kuharibu watoto wa wenzake.Ni
hatua gani atachukuliwa ?
Mchungaji akauliza kwa ukali
“taratibu ziko wazi,utafanyika
uchunguzi na ukikamilika
atafikishwa mahakamani
akikabiliwa na makosa ya kufanya
mapenzi na mwanafunzi.Ushahidi
tulioupata ni mkubwa na lazima
atapata adhabu kali sana” Akasema
afisa yule wa polisi
“Naombeni mhakikishe
anapata adhabu stahiki hata kama
yeye ni mtu mkubwa
serikalini.Hakuna mzazi anayeweza
akavumilia uchafu kama huu
anaoufanya wa kuharibu watoto wa
wenzake” Mchungaji akasema kwa
hasira.
Sintah akatolewa mle
chumbani akapakiwa katika gari na
wote wakaondoka kuelekea kituo
cha polisi kwa ajili ya mahojiano.
 
Siasa isikie tu Ila ni kuamua kuwa mkweli siasani ni sawa na kujitoa mhanga
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…