Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Ukisema ivyo unakuwa unaweka ugumu mwenyewe man yaan nirud nianze kuisoma mpaka nikute iyo maali? Angalia ni episode ya ngap useme nikuwekee mkula
 
Ukisema ivyo unakuwa unaweka ugumu mwenyewe man yaan nirud nianze kuisoma mpaka nikute iyo maali? Angalia ni episode ya ngap useme nikuwekee mkula
Part2.. season 2.......anzia episode ya 9
 
Aya izo apo 8,9,&10, ivi kumbe kuweka story apa ni kazi kweli kweli, tuwe tunawashukuru sana na kuwavumilia wanaotuleteaga izi mambo asee ile mwanzo mwisho inaitaji moyo laana ukijumlishia na yale malawama yetu, big up to all'ya
 

Attachments

Aya izo apo 8,9,&10, ivi kumbe kuweka story apa ni kazi kweli kweli, tuwe tunawashukuru sana na kuwavumilia wanaotuleteaga izi mambo asee ile mwanzo mwisho inaitaji moyo laana ukijumlishia na yale malawama yetu, big up to all'ya

Asante mkuu na pole.
 
Aya izo apo 8,9,&10, ivi kumbe kuweka story apa ni kazi kweli kweli, tuwe tunawashukuru sana na kuwavumilia wanaotuleteaga izi mambo asee ile mwanzo mwisho inaitaji moyo laana ukijumlishia na yale malawama yetu, big up to all'ya
Shukrani mkuu
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 1
DAR ES SALAAM
Muziki uliofunguliwa
kwa sauti ndogo ulisikika
katika sebule kubwa
nyumbani kwa Mathew
Mulumbi ambamo Austin na
Gosu Gosu walikuwa kimya
na kila mmoja alionekana
kuzama mawazoni.Life goes
on wimbo wa mwanamuziki
marehemu Tupac Shakur
ndio uliokuwa ukichezwa mle
sebuleni.Huu ni wimbo
ambao Austin January
hupenda sana kuusikiliza
hasa pale anapokuwa na
mawazo mengi.Alifuatisha
mdundo kwa kichwa huku
akiimba mashairi ya wimbo
ule alioonekana kuufahamu
vizuri.Gosu Gosu alikuwa
amejilaza sofani na mbele
yake kulikuwa na meza
ndogo yenye chupa tatu za
bia.Hawakuwa
wakizungumza na kila
mmoja sura yake ilionekana
kujawa na mawazo.
Wimbo ulimalizika na
Austin akaendelea kusikiliza
nyimbo nyingine za
marehemu Tupac.Aliinuka
sofani akaenda katika friji
akafungua na kuchukua
chupa ya bia akaenda
kusimama dirishani
akanywa funda moja na
kuchungulia nje.Tayari
kulianza kupambazuka.Milio
ya ndege ilianza
kusikika,akageuka na
kumtazama Gosu Gosu
ambaye naye alionekana
kuwa mbali sana kimawazo
“Papaa
kumepambazuka.What are
we going to do?akauliza
Austin.Gosu Gosu akainuka
akakaa na kuchukua chupa
akanywa funda kubwa na
kusema
“Hatuna cha
kufanya.Umesikia
alichokisema mkuu wa nchi
kwamba tuachane na suala
hili.Hatuwezi kupingana na
kauli yake.We have to stop”
akasema Gosu Gosu.Austin
naye akanywa funda moja
halafu akaenda kuketi sofani
“Papaa una hakika kweli
unataka kukata tamaa?Kuna
jambo linaloendelea hapa na
tunapaswa kulifahamu”
akasema Austin
“Austin kaka
yangu,nadhani tuyaheshimu
mawazo ya Rais.It’s over !
Tukiendelea kutaka
kulazimisha jambo hili
tutaingia katika vita
ambavyo hatutashinda.Yule
ni mkuu wa nchi na lazima
tutii maelekezo
yake.Amesema tuachane na
hili suala hakuna namna
tunavyoweza kuendelea nalo”
akasema Gosu Gosu
“Unadhani Mathew
angekuwepo angekubali
suala hili liishie
hapa?akauliza
Austin.Ilimchukua muda
kidogo kwa Gosu Gosu kujibu
swali lile.
“We’re not Mathew.Yule
alikuwa ni mtu wa kipekee
kabisa hivyo basi hatuwezi
kujifananisha naye.Austin
hakuna unachoweza
kunieleza
kitakachonishawishi
niendelee na operesheni
hii”akasema Gosu Gosu
“C’mon Papaa.Kwa nini
unakuwa hivyo?Inakuingia
akilini kwa Rais kututaka
tuachane na operesheni hii?
Lazima kuna jambo hapa si
bure” akasema Austin
“Austin kama
nilivyosema,kuwe na jambo
kusiwe na jambo mimi
sihusiki tena.Kwa sasa
naendelea na maisha yangu
ya kawaida na sitaki tena
kujihusisha na masuala
haya.Tulikwisha jitoa
kumsaidia Rais katika
mapambano haya lakini ni
yeye mwenyewe aliyekuja
kutuzuia tusiendelee hivyo
basi hakuna haja ya
kuendelea tena.Rudi kambini
kwako endelea na majukumu
yako ya kawaida” akasema
Gosu Gosu
“I can’t believe this !!
akasema Austin kwa sauti
ndogo.Hakuamini kuyasikia
maneno yale ya Gosu Gosu
“Austin kapumzike
kaka.Umepata likizo hivyo
nenda mahala ukapumzishe
akili yako aidha Zanzibar au
sehemu nyingine mbali na
hapa”
“Natamani Mathew
Mulumbi angekuwepo
hapa.Asingeweza kukubali
kuliacha jambo hili likielea
hewani” akasema Austin na
Gosu Gosu akainuka kwa
hasira akagonga meza
iliyokuwa na chupa za bia
zikaanguka akamfuata
Austin akamkunja shati
“Usithubutu
kuzungumza kuhusu
Mathew wakati ni wewe
uliyemuacha porini.Usitake
kunipandisha hasira.Please
go ! akafoka Gosu
Gosu.Austin aligundua Gosu
Gosu hakuwa akitania tayari
sura yake ilikwisha badilika
akachukua begi lake na
kuondoka kimya kimya
MASAA MANNE
YALIYOPITA
MAKAO MAKUU YA IDARA
YA SIRI YA USALAMA WA
NDANI WA NCHI
Juhudi kubwa zilikuwa
zinafanywa na wataalamu
wa usalama wa mtandao
kudhibiti kirusi hatari
kilichopandikizwa katika
mfumo wa kompyuta wa
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi.Kwa saa mbili
sasa juhudi ziliendelea bila
mafanikio.Mkuu wa idara
hiyo Tamar Axon alikuwepo
ofisini kwake kuhakikisha
mambo yote yanakwenda
vizuri.Iligundulika kwamba
kirusi kile kiliingia katika
mfumo kupitia akaunti ya
Samson Mkuza ambaye
hakuwa akipatikana
hewani.Ilitumwa timu ya
watu watatu kwenda
kumfuatilia na kujua mahala
alipo lakini timu ile
ilirudisha majibu kwamba
Samson alijipiga risasi ya
kichwa baada ya kugundua
anataka kukamatwa.
“Huyu lazima atakuwa ni
Agatha ! Ninaapa kumtafuta
kwa namna yoyote ile hadi
apatikane.Nilimuamini sana
na kumfanya aishi maisha
mazuri ya kifahari lakini
ndiye aliyekuja
kunisaliti.Amenisikitisha
sana.Huko aliko muda wake
unahes…..” Tamar akatolewa
mawazoni baada ya mlio
Fulani kusikika katika simu
yake ya mkononi.Akaitazama
haraka haraka kuna picha
zilitumwa katika simu yake
akazifungua
kuzitazama.Kulikuwa na
watu nyumbani kwake
“Nani hawa wamevamia
nyumbani
kwangu?akajiuliza.Alihisi
kiubaridi kwa ndani.Alikuza
picha zile zilizotumwa katika
simu yake kutoka katika
kamera ya siri iliyofungwa
nyumbani kwake
akazitazama vyema
“Huyu mmoja
ninamfahamu.Ni Austin
January.Ni mkuu wa kikosi
cha jeshi cha operesheni
maalum.Anatafuta nini
nyumbani kwangu?akajiuliza
akiendelea kushuhudia
kupitia simu yake namna
akina Austin walivyokuwa
wanahangaika nyumbani
kwake.
“Wanatafuta nini hawa
jamaa? Akajiuliza
“Agatha ! akasema kwa
sauti ndogo iliyojaa hasira
“Lazima watakuwa
wanafanya kazi na Agatha
na ndiye aliyewaelekeza
nyumbani kwangu.Stupid !
akawaza na kutafuta namba
za Rais akampigia
“Hallow Tamar” akasema
Dr Fabian Kelelo
“Fabian ninakutumia
picha Fulani sasa hivi halafu
nitakupa maelekezo”
akasema Tamar na
kumtumia Rais picha zile za
Austin na Gosu Gosu wakiwa
nyumbani kwake
wakihangaika kuingi ndani
“Umewatambua hao
watu ?akauliza Tamar na Dr
Fabian akababaika kujibu
“Fabian umewatambua
hao watu?akauliza tena
Tamar
“H..N..Ndiyo.Ninamfaha
mu mmoja ni mkuu wa kikosi
cha operesheni maalum”
akasema Dr Fabian
“Good.Nilidhani
ungekana humjui.Hawa
watu wamevamia nyumbani
kwangu na sijui
wanachokitafuta hapo ni
nini.Nataka waondoke mara
moja kabla hayajawakuta
mambo makubwa” akasema
Tamar na kukata simu
“Austin na wenzake
wamekwenda kutafuta nini
nyumbani kwa Tamar?
Kama kuna kitu walitaka
kwenda kukichunguza kwa
nini hawakunijulisha kabla
ya kujiamulia wenyewe
kwenda kuvamia nyumbani
kwa Tamar? Ni kweli mimi
ndiye niliyewatuma kazi
lakini walipaswa kunijulisha
kama wanakwenda kuvamia
nyumbani kwa Tamar.Yule
ni mtu mkubwa sana na
hawakupaswa kuvamia
nyumbani kwake kama
mhalifu.Hii sijaipenda”
akawaza Dr Fabian na
kumpigia simu Austin
Austin na Gosu Gosu
wakiwa tayari wameingia
nyumbani kwa Tamar
wakikitafuta chumba cha
kulala cha Tamar mara simu
ya Austin ikatetema.Akaitoa
akatazama mpigaji alikuwa
ni Rais
“Rais ! Austin akastuka
akaiacha simu ile ikiita na
kukatika ikaanza kuita tena
akaamua kuipoea
“Mheshimiwa Rais !
akasema Austin
“Austin ninafahamu
mahala mlipo na ninaomba
muondoke hapo haraka sana!
akasema Dr Fabian kwa
ukali
“Mheshim………..”
“Austin sasa hivi nataka
muondoke hapo! Akafoka Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo la msingi sana
tunalifuatilia ndiyo maana
tuko hapa.Umefaham…”
Austin akakatishwa na Dr
Fabian
“Austin you have three
minutes to get out of
there.This is an order !
akasema Dr Fabian.Austin
alibaki ameduwaa asijue la
kufanya
“Austin C’mon ! akasema
Gosu Gosu baada ya
kumuona Austin amesimama
“Papaa we have to go !
“What?!! Gosu Gosu
akashangaa
“Tuondoke” akasema
Austin
“Austin acha
masihara.Tulikuja hapa
kufanya upekuzi kutafuta
kile kitakachoweza
kutusaidia kufahamu nani
waliomuua balozi
Benjamin.Tutaondoka vipi
kabla hatujafanya kazi
iliyotuleta?akauliza Gosu
Gosu
“It’s an order from
president”
“President?
“Ndiyo.Ametutaka
tuondoke haraka sana eneo
hili.Ametoa dakika tatu”
akasema Austin
“Rais amejuaje kama
tuko hapa?
“Sijui amefahamu vipi
lakini tayari anafahamu
kama tuko hapa na
ametutaka tuondoke haraka
sana.Hajaonekana
kufurahishwa na ujio wetu
hapa” akasema Austin kisha
akageukana kuanza
kuondoka
“Austin ! akaita Gosu
Gosu lakini Austin
hakugeuka akaendelea na
harakati zake za
kutoka.Nyumba ile likuwa
kimya kabisa hakukuwa na
mtu yeyote.Gosu Gosu
alisimama akimtazama
Austin akiondoka hakuwa na
la kufanya akapiga ngumi
ukuta kwa hasira naye
akaondoka.Walitoka nje ya
lile jumba la Tamar
wakaingia katika gari lao na
kuondoka eneo lile.
“Austin tafadhali nipe
jibu kwa nini Rais ametutaka
tuondoke pale wakati
tunafuatila jambo la muhimu
sana? Amefahamu vipi tuko
hapa?akauliza Gosu Gosu
“Nilimueleza kuwa tuko
pale kwa sababu
maalum,kuna jambo
tunalifuatilia la muhimu
lakini hakunielewa
akatutaka tuondoke haraka
sana”
“Nashindwa kuelewa
maamuzi haya ya
Rais.Kwanini hukumweleza
kama Tamar anadukua
mawasiliano yake na
anashirikiana na balozi
Benjamin?akauliza Gosu
Gosu
“Tulipanga tumueleze
jambo hili baada ya kuzipata
zile rekodi hata hivyo
hakunipa nafasi ya
kumueleza” akasema Austin
na ukimya ukapita
“Rais ndiye aliyetupa
kazi hii tuifanye
ninashindwa kuelewa kwa
nini basi aamue kuzuia
tusifanye uchunguzi wetu?
Tamar ni mtu muhimu mno
katika suala hili” akasema
GosuGosu
“Papaa hili jambo
linachanganya sana,kwanza
ni namna Rais alivyofahamu
kuhusu uwepo wetu
pale.Nani alimweleza tuko
nyumbani kwa
Tamar?akauliza Austin
“Austin jambo hili
haliwezi kuisha hivi hivi
lazima tumuulize Rais tujue
kwa nini ametuzuia
tusiendelee kumchunguza
Tamar? Ikiwezekana
tumweleze ukweli ili
aturuhusu kuitafuta
kompyuta hiyo yenye rekodi
zinazomuhusu yeye”akasema
Gosu Gosu
“Papaa sisi sote ni
wanajeshi na tunafundishwa
kutii amri za viongozi
wetu.Rais ni kiongozi wetu
na ametoa amri hivyo lazima
tuitekeleze bila kuhoji
chochote”
“Austin hii si operesheni
ya jeshi.Tumeyaweka maisha
yetu hatarini na kukubali
kufanya kazi ya Rais kwa
nini yeye mwenyewe aingilie
na kutuzia tusiendelee na
kazi aliyotupa?akauliza Gosu
Gosu na safari ikaendelea
kimya kimya.
Walifika katika makazi
ya Gosu Gosu wakakaa
sebuleni.
“Austin mpigie
Rais.Lazima atueleze kwa
nini ametuzuia
tusimchunguze
Tamar?Wakati anatupa kazi
hakutupa masharti kwamba
kuna watu ambao
hawapaswi kuguswa katika
uchunguzi wetu hivyo basi
tunahitaji kujua sababu za
kutomchunguza Tamar”
akasema Gosu Gosu.Austin
akafikiri kidogo na kuchukua
simu akampigia Dr
Fabian.Simu iliita bila
kupokelewa
“Hapokei simu” akasema
Austin
“Call him again”
akasema Gosu Gosu na
Austin akampigia tena simu
ikapokelewa
“Austin
unasemaje?akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais tayari
tumekwisha sitisha lile zoezi
letu kama ulivyoelekeza na
kuondoka mahala pale”
“Safi.Naomba msiendelee
tena na hili zoezi hadi pale
nitakapowapa maelekezo
zaidi”akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais !
akasema Austin kwa
mshangao
“Austin kwa sasa
operesheni yenu itasimama
hadi pale nitakapowaelekeza
tena.Waambie vijana wako
kila mmoja akaendelee na
shughuli zake za kawaida
hadi hapo utakapowajulisha
tena”akasema Dr Fabian na
kukata simu.Austin akaitupa
simu sofani kwa hasira
“Anasemaje Rais?
“Amesitisha tusiendelee
na chochote hadi hapo
atakapotoa maelekezo
mengine” akasema Austin na
Gosu Gosu akatoa kicheko
“Nashindwa kuelewa
kinachoendelea hapa Austin
hadi Rais atuzuie tusiendelee
na kazi aliyotupa” akasema
Gosu Gosu na kuinuka
akaenda katika friji
akachukua chupa tatu za bia
akaziweka katika meza
ndogo akakaa na kuanza
kunywa
“Upo msemo usemao
kuvuja kwa pakacha ni
nafuu ya mchukuzi.Pakacha
letu limevuja na ninafuu
kwetu.Hatujui tumeepushwa
na jambo gani huko mbele
kama
tungeendelea.Yawezekana
baada ya balozi Benjamin
kuuawa Rais anadhani
mambo yamekwisha kumbe
mambo ndiyo kwanza
yameanza.Austin mimi
nimekubali na kutii agizo
lake nitakaa pembeni lakini
nakuomba usinifuate tena
kunieleza eti kuna kazi ya
Rais” akasema Gosu Gosu
huku akiendelea kukata bia
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 2
Toka kulipopambazuka
Rais Dr Fabian amekuwa
akipokea simu kutoka wa
viongozi wa mataifa mbali
mbali wakimpa pole
kuhusiana na shambulio lile
lililotokea katika hoteli ya
Zimba na kusababisha vifo
vya watu sitini na
tatu.Shambulio lile ilikuwa
ni habari kubwa katika
vyombo mbali mbali vya
habari duniani.
Wakati akipata kifungua
kinywa Dr Fabian alikuwa
anapitia magazeti ya hapa
nchini ambayo nayo habari
kuu ilikuwa ni shambulio lile
kubwa
“Mauaji makubwa sana
haya na ya kikatili.”
Akasema Millen mke wa Dr
Fabian
“Haijawahi kutokea
nchini mwetu watu wengi
kiasi hiki wakauawa kikatili
namna hii.Wauaji hawa
lazima wasakwe kila kona na
wapatikane! Akasema Dr
Fabian kwa ukali
“Balozi wa umoja wa
Ulaya alikuwemo mle
ukumbini na ni mmoja wa
watu waliouawa unahisi
mauaji yale yanahusiana na
hiki kinachoendelea hivi sasa
baina ya nchi yetu na nchi za
Ulaya?akauliza Millen
“Siwezi kuhusisha moja
kwa moja tukio hili na hiki
kinachoendelea japo naamini
umoja wa Ulaya wataamini
kwamba mauaji haya ni
mpango wa serikali kulipiza
kisasi kwa balozi wao kwa
kuiandika vibaya Tanzania”
akasema Dr Fabian.
“Ni kweli lazima watahisi
hivyo kwa sababu balozi
Benjamin ndiye aliyekuwa
wa kwanza kuandika katika
ukurasa wake wa twitter
kwamba Tanzania si mahala
salama kutembelea.Picha
itakayojengewa ni kwamba
Tanzania wameamua
kumuua balozi huyu kufuatia
ujumbe ule alioutuma katika
akaunti yake ya
twitter.Kuna kazi kubwa
hapa ya kuwatafuta
waliomuua balozi huyu
kwani Tanzania inazidi
kuchafuka.Watu waliouawa
ni wengi sana na hii ina
athari kwetu kwani hivi sasa
dunia nzima wanaamini
Tanzania si mahala salama
tena” akasema Millen
“Lazima wauaji
wapatikane haraka sana kwa
namna yoyote ile.Lakini
pamoja na tukio hili usiache
kuendelea na mpango wa
maandalizi ya mkutano
mkubwa wa wake za marais
duniani.Kwa namna yoyote
ile mkutano huo lazima
ufanyike na utatusaidia
kuithibitishia dunia kwamba
Tanzania ni sehemu salama”
akasema Dr Fabian na baada
ya kupata kifungua kinywa
akaondoka kwenda kuanza
majukumu yake ya siku.
Dakika chache baada ya
kuingia ofisini
kwake,akataarifiwa kwamba
Rais wa Ufaransa alikuwa
katika laini ya simu akitaka
kuzungumza naye.
“Mambo yameanza.Huyu
ndiye aliyekuwa
akishirikiana na Benjamin
katika kushinikiza
uchunguzi ufanyike
kuhusiana na kifo cha
Laurent Muganza” akawaza
Dr Fabian na kuelekea
katika chumba cha
mawasiliano ya moja kwa
moja.Katika runinga
alionekana Rais wa
Ufaransa.
“Mr Michael Weren”
akasema Dr Fabian bila
kupoteza wakati
“Mheshimiwa Rais Dr
Fabian.Poleni sana kwa
tukio baya la usiku wa
jana.Kwa niaba ya nchi
yangu na kwa niaba ya ya
umoja wa Ulaya ninatoa
salamu nyingi za pole kwa
madhira haya yaliyotokea”
akasema Rais Michael
“Kwa niaba ya wananchi
wa Tanzania ninasema
ahsante sana” akasema Dr
Fabian
“Naweza kusema
kwamba hili ni tukio baya
zaidi kuwahi kutokea nchini
Tanzania.Hili ni tukio la
ugaidi.Kuna mtu yeyote
ambaye amekamatwa hadi
sasa kuhusika katika mauaji
hayo?akauliza Rais Michael
“Mheshimiwa Rais
Michael,tayari vyombo vyetu
vimekwisha anza
kulichunguza jambo hili na
tutatoa taarifa nani
waliohusika katika mauaji
yale”
“Mheshimiwa Rais,balozi
wa umoja wa Ulaya na mke
wake ni miongoni mwa
waliouawa katika shambulio
hilo na hili si tukio la kwanza
kwa watu wanaohusiana na
umoja wa Ulaya kuuawa
nchini Tanzania.Siku chache
zilizopita aliuawa Laurent
Muganza hapo hapo Dar es
salaam na jana kauawa
balozi wa Umoja wa
Ulaya.Sitaki kusema moja
kwa moja kwamba
yawezekana shambulio hilo
la jana lilimlenga balozi
Benjamin kwani sina
ushahidi wa kutosha lakini
ninakuomba kwa mara
nyingine tena waruhusu
wachunguzi wa umoja wa
Ulaya waje wasaidie
kuchunguza suala
hili.Ninakuhakikishia
mheshimiwa Rais kwamba
wachunguzi hao
hawatahusika na mambo
mengine zaidi ya kusaidia
katika uchunguzi” akasema
Rais Michael
“Mheshimiwa
Rais,yalipotokea mauaji ya
Lucy na Laurent Muganza
uliniomba jambo hilo
nikakataa kwani suala lile
bado linachunguzwa na
vyombo vya ndani.Katika
suala hili pia hatutaruhusu
wachunguzi wowote kutoka
nje ya nchi kwani
linashughulikiwa na vyombo
vyetu vya ndani lakini pale
tutakapohitaji msaada wa
kutoka nje hatutasita
kuomba.Kwa hiyo ninasema
hapana kwa ombi lako”
akasema Dr Fabian
“Mheshimwia Rais
kitendo cha Tanzania
kuendelea kukataa kuruhusu
wachunguzi wa kutoka nje ya
nchi kusaidia katika
kuchunguza kuhusu mauaji
haya kinatia shaka sana na
kuwafanya watu wahisi
yawezekana kuna mambo
serikali yako haitaki
yajulikane ndiyo maana
kumekuwa na ugumu
mkubwa katika kuruhusu
wachunguzi wa
kimataifa.Hili ni doa kwa
serikali yako na kuliondoa
doa hili ni kuruhusu timu ya
wachunguzi iweze kuja
kusaidia uchunguzi”
akasema Rais Michael
“Hatuna chochote cha
kuficha mheshimiwa Rais
baada ya uchunguzi
kukamilika kila kitu
kitawekwa wazi na kama
hakuna lingine mheshimiwa
Rais,nina majukumu
mengine pia ya kufanya”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nakuomba ulitafakari suala
hilo kwani athari zake
zitakuwa ni kubwa kwa nchi
yako”akasema Rais Michael
“Jibu nililolitoa
mheshimiwa Rais
halitabadilika.Hakuna
mchunguzi wa kimataifa
atakayeruhusiwa kuingia
nchini.Ahsante kwa kupiga
simu mheshimiwa Rais”
akasema Dr Fabian na
kuzima kamera,akashusha
pumzi.Akatoka katika kile
chumba na kurejea ofisini
kwake akaketi na kuvuta
pumzi ndefu wakati
akitafakari simu yake ya
mkononi ikaita alikuwa ni
Tamar.
“Habari yako Tamar”
“Nzuri kabisa habari
yako Fabian?
“Nzuri.Unaendeleaje
Tamar?
“Ninaendelea
vizuri.Nimekupigia
kukujulisha kwamba
tumepata tatizo.Mfumo wetu
wote wa kompyuta
umeingiliwa na kirusi hatari”
akasema Tamar
“Mfumo umeingiliwa na
kirusi?akashangaa Dr
Fabian
“Ndiyo Fabian mfumo
wetu umeingiliwa na kirusi
hatari hivyo kila kitu hapa
kimesimama.Nimekesha
hapa na wataalamu
wakijaribu kutafuta kila njia
ya kudhibiti kirusi hicho”
“Lini limetokea hilo
tatizo?akauliza Dr Fabian
“Limeanza jana usiku”
“Imewezekanaje
mkashambuliwa na kirusi
wakati mfumo wenu wa
kompyuta hapo una ulinzi wa
hali ya juu sana?akauliza Dr
Fabian
“Kuna mmoja wa
mfanyakazi wetu hapa
anaitwa Agatha ambaye
tuligundua kwamba alikuwa
anaiba siri za idara na
hatujui alikokuwa
anazipeleka.Baada ya kujua
tumemgundua alitoweka na
mpaka sasa
hajapatikana.Tunaamini
huyo ndiye aliyepandikiza
kirusi hicho katika mfumo
wetu kwa kupitia katika
akaunti ya mfanyakazi
mwingine aliyekuwa na
ukaribu naye.Picha za
kamera zinaonyesha kwamba
kijana huyo aitwaye Samson
alimaliza majukumu yake
akaondoka lakini baadae
akarejea tena na moja kwa
moja akaelekea katika
chumba cha
seva.Tumefuatilia chanzo cha
kirusi hicho tukagundua
kilianzia katika akaunti yake
na kilitumwa kutoka katika
kompyuta ambayo mpaka
sasa bado hatujaweza
kutambua ni ya nani na yuko
wapi.Baada ya kugundua
hilo tulimfuata Samson ili
atueleze chanzo cha kirusi
kile lakini alijipiga risasi na
kujiua kabla watu wetu
hawajamkamata.Tulibahatik
a kuipata simu yake na
tulipoipekua tumegundua
jana usiku aliwasiliana na
Austin January na muda
waliowasiliana ndio muda
huo ambao kirusi kiliingia
katika mfumo wetu”akasema
Tamar
“Austin Janury?! Dr
Fabian akashangaa
“Ndiyo Fabian.Simu
iliyotumika kuwasilina na
huyo kijana ni ya Austin
January.Hata hivyo
aliyekuwa anaitumia simu
hiyo kuwasiliana na Samson
ni mwanamke ambaye baada
ya kuihakiki sauti yake
tumegundua ni Agatha
ambaye tunamtafuta kwa
kuiba siri za
idara.Tunaamini Austin na
Agatha wanafanya kazi
pamoja na Austin anafahamu
mahala alipo
Agatha.Sifahamu nini hasa
wanachokitafuta katika
idara yetu au wamepewa
taarifa gani na Agatha hadi
wakafikia kufanya kitendo
hiki walichokifanya.Kama
haitoshi walijaribu kuvamia
nyumbani kwangu na kwa
bahati nzuri nina mfumo wa
ulinzi ambao ulinitumia
picha za wavamizi hao katika
simu yangu ndipo
nikawasiliana
nawe.Ningeweza kuwafanya
chochote kibaya watu wale
waliovamia nyumbani
kwangu lakini tunamuhitaji
Austin.Tunahitaji kufahamu
alipo Agatha” akasema
Tamar na Dr Fabian akavuta
pumzi ndefu
“Tamar kuna jambo
ambalo nataka
ulifahamu.”akasema na
kunyamaza kidogo
“Austin nilimtuma kazi
maalum ya kuwatafuta
wauaji wa balozi Benjamin
Hudson sasa nashangaa
amefikaje fikaje hadi katika
idara yako na kuleta
uharibifu mkubwa namna
hiyo” akasema Dr Fabian na
Tamar akatoa kicheko kidogo
“Fabian toka lini
ukaanza kuwatumiwa
wanajeshi katika operesheni
kama hizi wakati idara
yangu ipo na ndiyo
inayoshughulika na masuala
hayo? Ukiacha sisi kuna
polisi na vyombo vingine kwa
nini ukaviacha hivyo vyote
na kuamua kumpa jukumu
Austin January?Don’t you
trust us anymore?Hatufanyi
kazi vizuri? Akauliza Tamar
“Tamar si hivyo.Kuamua
kumtumia Austin
hakumaanishi kwamba
nimepoteza imani na idara
yako au idara nyingine lakini
nilikuwa na sababu zangu
binafsi kufanya hivyo
,naomba usinielewe
vibaya.Mmekuwa mkifanya
kazi nzuri siku zote na nina
imani kubwa na ninyi”
akasema Dr Fabian
“Fabian sitaki kufahamu
sababu zako za kuamua
kumtumia Austin katika
kuwatafuta wauaji wa balozi
Benjamin lakini
ninachokihitaji kwa sasa ni
kufahamu mahala alipo
Agatha na anayefahamu
mahala alipo ni
Austin.Ninahitaji kumpata
Austin nimuhoji na
kufahamu alipo Agatha hivyo
naomba msaada wako”
akasema Tamar na Dr
Fabian akawa kimya
“Fabian najua jambo hili
limekustua kidogo lakini
kumpata Austin ni lazima
kwetu ili atuonyeshe mahala
alipo Agatha na vile vile
tujue ni siri zipi za idara
ambazo amekuwa akipewa
na Agatha.Fabian hawa watu
wawili lazima watakuwa na
mpango mkubwa sana wa
kuhujumu idara yetu na
lazima tuwadhibiti haraka”
akasema Tamar.Dr Fabian
akavuta pumzi ndefu
alishindwa aseme nini.
“Fabian say something !
akasema Tamar
“Tamar nashindwa
niseme nini kwani Austin ni
mtu wangu wa muhimu sana
na amekuwa akinisaidia
katika shughuli zangu mbali
mbali hivyo inaniwia ugumu
kusaidia kumteka.Niachie
suala hilo nitazungumza
naye mimi mwenyewe na
kumuhoji alipo Agatha
halafu nitakujulisha”
akasema Dr Fabian
“Fabian you don’t
understand.Huyu mtu
amekuwa anashirikiana na
Agatha mfanyakazi wetu
humu kuiba siri za idara na
sielewi kwa madhumuni
yapi.Huyu mtu ni hatari
lazima kuna mahala
anazipeleka siri hizo ambazo
nyingi zinahusiana na
usalama wa nchi hivyo hata
ukizungumza naye
hatakueleza
chochote.Tusaidie sisi
tumpate tutamfungua kwa
mateso” akasema
Tamar.Picha ya Austin
ikazunguka katika kichwa
cha Dr Fabian halafu
akasema
“Tamar hapana,siwezi
kuruhusu Austin akafanyiwa
chochote kabla sijamuhoji
kujua kwa nini alifanya
hivyo alivyofanya na kwa
nini anashirikiana na
Agatha” akasema Dr Fabian
“Fabian unanifanya
niamini kwamba yawezekana
wewe ndiye uliyemtuma
Austin afanye haya
aliyoyafanya” akasema
Tamar
“Mimi nilimpa kazi
nyingine kabisa ambayo
haihusiani na idara
yako.Kama kuna taarifa
yoyote ninaitaka katika
idaya yako ningeweza
kuagiza niletewe hivyo basi
siwezi kumtuma mtu aibe
siri za idara”akasema Dr
Fabian
“Kama hukumtuma
alikuwa anatafuta nini
nyumbani kwangu? You sent
him to spy on me? Tamar
akauliza
“I didn’t send him to spy
on you.Kwa nini nifanye
hivyo?akauliza Dr Fabian
“Kama hukumtuma kwa
nini unamkingia kifua?Nina
uhakika mkubwa huyu
jamaa kuna kitu anakifanya
katika idara yetu,nina
uhakika mkubwa
ananichunguza kwa nini
hutaki nijue
kinachoendelea?akauliza
Tamar
“Tamar nina mambo
mengi ya kufanya leo hivyo
naomba tulimalize hili
suala.Sitaki Austin
aguswe.Nitazungumza naye
mimi mwenyewe na
atanieleza kile
anachokitafuta katika idara
yako” akasema Dr Fabian
“Fabian sasa unanifanya
niamini kwamba unamtumia
Austin
kunichunguza.Umeniudhi
sana na sasa naomba
unisikilize vyema.Utake
usitake nitamchukua Austin
nimuhoji nifahamu kile
anachokitafuta katika idara
yetu,nijue sababu ya kwenda
kuvamia nyumbani kwangu
na vile vile nijue mahala
alipo Agatha.Please don’t try
to stop me” akasema
Tamar.Kauli ile ya Tamar
ilionyesha kumchukiza sana
Dr Fabian
“Tamar nakuonya
usinijaribu ! Mimi si mtu wa
kujaribu.Mimi ni Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzan……” akasema Dr
Fabian na simu ikakatwa
“Huyu mwanamke
mshenzi sana anataka
kunipanda kichwani na
kunitawala.Nimempa cheo
kikubwa na sasa anataka
kukitumia
vibaya.Nitamuondoa haraka
sana asifanye mchezo na
mimi.Akithubutu kumgusa
Austin nitammaliza”
akawaza Dr Fabian na mara
ukasikika mlio wa ujumbe
mfupi wa simu.Akaufungua
ulikuwa ni ujumbe kutoka
kwa Tamar.Ilikuwa ni video
fupi.Dr Fabian alipoitazama
video ile akahisi jasho
likimtoka usoni na muda huo
huo simu yake ikaita
akaipokea
“Tamar what’s the
meaning of this?akauliza Dr
Fabian kwa ukali
“Nimekutumia
kukukumbusha tu kwamba
wewe ni Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
lakini mimi nina nguvu zaidi
yako ninaweza kukuondoa
katika nafasi yako uliyo nayo
hivyo unapaswa
kuniheshimu sana na
kunisikiliza kila
ninachokitaka.Tusifike
huko.I need Austin” akasema
Tamar.Dr Fabian alihisi joto
akalegeza tai na kushusha
pumzi
“Mnataka nifanye
nini?akauliza
“Mpigie simu mwambie
saa mbili usiku leo aende
Dino’s hotel ambako kuna
mtu utamtuma ampelekee
taarifa Fulani ya
siri.Akishafika pale sisi
tutajua namna
tutakavyomchukua”akasema
Tamar
“Sawa nitafanya hivyo”
akasema Dr Fabian
“Thank you Mr
President.I’m reminding you
don’t try to warn him or let
him escape” akasema Tamar
“Tamar this will be the
last warning to you stop
blackmailing me !.Please
destroy this
video.Sintakuonya tena
kuhusu jambo hili ! akafoka
Dr Fabian na simu ikakatwa
Dr Fabian alihisi
kuchanganyikiwa akaendelea
kuzunguka mle ofisini
akitoka pembe moja hadi
nyingine
“Nilifanya makosa
makubwa sana kumuweka
Tamar katika ile nafasi na
tayari amekwisha nibana
kwenye kona kwa kuwa
anajua anayo ile video !
akawaza Dr Fabian na
kugonganisha mikono kwa
hasira
“Austin ni mtu muhimu
sana kwangu kwa wakati
huu.Ni yeye ndie
aliyefanikisha mauaji ya
Lucy Muganza na ni mtu
ambaye nimechagua
kumuamini na kumtumia
katika operesheni mbali
mbali za siri.Kwa nini nimtoe
kafara mtu muhimu kama
huyu?Kuna nini kinaendelea
hapa hadi akavamia
nyumbani kwa Tamar?Kuna
swsali la kujiuliza pia nini
kilimpelekea Austin kwenda
nyumbani kwa Tamar? Ni
kweli anashirikiana na
mmoja wa wananyakazi wa
SNSA kuiba siri za
idara?Kama ni kweli kwa
madhumuni gani? Nilifanya
makosa makubwa kukubali
agizo la Tamar la kuwaondoa
Austin na wenzake
nyumbani kwa Tamar
walikokuwa wamevamia bila
kumuhoji na kujua
kinachoendelea” akawaza Dr
Fabian na kuegemea meza.
“Naanza kuamini
yawezekana ni kweli Austin
anashirikiana na huyo
Agatha mfanyakazi wa SNSA
kuiba siri za idara na kuna
taarifa walikwenda kuitafuta
pale nyumbani kwa
Tamar.Kwa nini lakini
Austin afanye hivi? Kama
kuna taarifa anaihitaji
kutoka SNSA angenieleza ili
nimsaidie kuipata kuliko
kushirkiana na mmoja wa
wafanyakazi kuiba siri kitu
ambacho ni kibaya
sana.Ninaanza kuwa na wasi
wasi yawezekana hata
mauaji yale ya jana Austin
anahusika kwa sababu ni
yeye niliyempa jukumu la
kumfuatilia balozi Benjamin
na kuna uwezekano walisuka
mpango wa kumuua balozi
Benjamin kimya kimya”
akawaza Dr Fabian
“Naanza kuiona pointi ya
msingi ya Tamar.Kuna
mambo mengi ambayo
hatuyajui kuhusu Austin na
anapaswa kuhojiwa aeleze
kila kitu.Mambo kama haya
ndiyo yanayonifanya niwe
muoga wa kuwaamini
watu.Kila unayemuamini
anakuwa na kasoro
zake.Tayari nilikwisha anza
kumuamini Austin lakini
kwa kitendo cha kuanza
kuiba siri za idara nyeti ya
usalama wa ndani wa nchi
inaonyesha wazi hapaswi
kuaminiwa” akaendelea
kuwaza Dr Fabian na
kuishika simu yake mara
akaikumbuka ile video
aliyotumiwa na
Tamar.Akaifuta haraka
haraka na kushusha pumzi
akaegemea kiti
“Mpaka lini Tamar
ataendelea kunilazimisha
nifanye kila akitakacho kwa
sababu ya video hii?Hapo
mwanzo nilichukulia rahisi
lakini kwa sasa naona hili
jambo linaanza kuwa kubwa
na ameanza kuvuka mipaka
yake.Anataka anitawale na
nimtimizie kila
anachokihitaji hata ambacho
hakiwezekani.Natakiwa
haraka sana kutafuta namna
ya kuweza kumdhibiti kwani
bila kufanya hivyo ataniletea
matatizo makubwa sana
huko tuendako kwani
anaweza akanitaka hata
niachie ngazi.Ningeweza
kumuondoa but …oh my God
I can’t ! akawaza Dr Fabian
na baada ya muda
akachukua simu na
kumpigia Austin
“Mheshimiwa Rais”
akasema Austin baada ya
kuipokea simu
“Austin nina shughuli
nyingi sana leo sintaweza
kuonana nawe ila kuna
jambo la muhimu ambalo
nilitaka nikuonyeshe lakini
nitamtuma mtu wangu.Fika
Dino’s hotel saa mbili za
usiku utakutana naye na
atakupa hizo
nyaraka.Ukishazipitia
utanipa mrejesho”
“Sawa mheshimiwa Rais”
“Ahsante Austin”
“Mhesh…….” Austin
akataka kusema kitu lakini
tayari simu ilikwisha katwa.
“I have no choice
Austin.I’m so sorry” akasema
Dr Fabian baadaya kukata
simu
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 3
“Gosu Gosu” Sauti laini
ya mwanamke ilimstua Gosu
Gos kutoka katika usingizi
mzito.Alifumbua macho na
kujikuta akiwa amelala
sofani.Mezani kulikuwa na
chupa kadhaa za
bia.Akafikicha macho na
kuinuka akakaa
“Agatha” akasema
“Mlirudi saa ngapi
kutoka kwa Tamar?akauliza
Agatha
“Ahsante kwa
kuniamsha.Ninahisi kichwa
kizito sana.I need to take a
bath” akasema Gosu Gosu na
kuchukua bastora yake
akaelekea chumbani kwake
akajimwagia maji baridi
“Nimelala usingizi mzito
sana halafu mbaya zaidi
niliweka bastora mezani.Hii
ni hatari,angeweza kuingia
mtu mbaya na kunimaliza”
akawaza Gosu Gosu
“Lakini usingizi huu
umesababishwa na bia
nilizokunywa jana.Si
kawaida yangu kulala
namna hii” akaendelea
kuwaza
“Sitaki kushiriki tena
kazi yoyote ile
atakayoniomba Austin.Jana
Rais ametufanyia kitu kibaya
sana na mpaka sasa bado
sifahamu kwa nini alifanya
vile.Kwa nini hakutuacha
tukaendelea na zoezi letu na
badala yake akaamuru
tuondoke haraka nyumbani
kwa Tamar tulikofuata
jambo muhimu tena kwa
faida yake yeye mwenyewe?
Anyway, I’m done.Sitaki tena
kushiriki katika operesheni
yoyote ya serikali.Toka
wakati wa Mathew mambo
kama haya yalikuwa
yanatokea.Viongozi ndani ya
serikali hawaeleweki na
hawaaminiki.Ninaweka
nukta katika mambo haya na
ninataka kujikita zaidi
katika kusimamia biashara
za Mathew” akawaza Gosu
Gosu na kuitazama picha
kubwa ya Mathew ukutani
“What happened to you
Mathew Mulumbi? Are you
real dead ?If not where are
you brother?akajiuliza Gosu
Gosu na mlango wake
ukagongwa akaufungua
alikuwa ni mtumishi wake
wa ndani aliyemjulisha
kwamba kifungua kinywa
tayari.Kabla ya kwenda
katika chumba cha chakula
Gosu Gosu akaenda katika
chumba cha wageni
walimolala akina
Agatha.Mlango
ukafunguliwa akatoka
Agatha
“Gosu Gosu” akasema
Agatha
“Watoto
wanaendeleaje?akauliza
“Bado wako katika
mstuko.Bado wanaogopa”
akajibu Agatha
“Ni kweli lilikuwa tukio
baya.Itachukua muda tukio
lile kuwatoka vichwani
mwao” akasema Gosu Gosu
“It’s breakfast time”
akasema Gosu Gosu
“Sina hakika kama
watakubali kutoka humu
chumbani.Bado wanaogopa
sana”
“It’s okay.Mtumishi
atawaandalia kifungua
kinywa humo humo
chumbani” akasema Gosu
Gosu na kuelekea katika
chumba cha chakula kupata
kifungua kinywa.
“Lazima nitafute namna
ya kuwasaidia Agatha na
familia yake waweze kuwa
salama.Nina uhakika
mkubwa lazima Tamar na
idara yake wataelekeza
nguvu zao nyingi kumsaka
na kuhakikisha
anapatikana” akawaza akiwa
mezani.Alipomaliza akaenda
tena katika chumba cha
Agatha akagonga mlango na
kumtaka Agatha
wazungumze wakaelekea
katika bwawa kubwa la
kuogelea
“Usiwe na hofu Agatha
hapa uko sehemu salama na
nitahakikisha wewe na
familia yako mnakuwa
salama,naomba uniamini”
“Ahsante nashukuru”
“Kwa sasa mtaendelea
kukaa hapa kwangu hadi
pale tutakapopata sehemu
salama zaidi mtakapoishi
kwa amani bila
bughudha.Kitu chochote
mtakachokihitaji usisite
kunijulisha”
“Nakushukuru sana
Gosu Gosu kwanza kwa
kutuokoa jana na pili kwa
kuhakikisha tunaendelea
kuwa salama.Bila wewe hivi
sasa mimi na familia yangu
tungekwisha
uawa.Nashukuru vile vile
kwa huduma nzuri
tunazopatiwa hapa.Ukiacha
mstuko ambao bado watoto
wanao lakini tunajihisi tuko
nyumbani”akasema Agatha
huku akitabasamu
“Msiwe na hofu jisikieni
nyumbani.Jumba hili ni
kubwa na mko huru
kuzunguka sehemu mbali
mbali.Kuna bustani nzuri na
sehemu za michezo ya
watoto.Unaweza ukawatoa
ndani ukawaleta hapa kuja
kupumzika” akasema Gosu
Gosu
“Hujanieleza kuhusu
jana.Mlifanikiwa kupata
chochote nyumbani kwa
Tamar?akauliza Agatha.
“It was complicated”
“Complicated?
How?akauliza Agatha
“Tulifanikiwa kuingia
nyumbani kwa Tamar na
wakati tukielekea katika
chumba chake cha kulala
Austin akapigiwa simu na
Rais akamtaka tuondoke
haraka sana mahala pale”
“Rais? Akauliza Agatha
“Ndiyo.Rais alipiga simu
na kututaka tuachane na
zoezi lile na tuondoke haraka
sana mahala pale”
“Kwa nini akafanya vile?
Si yeye aliyewapa kazi hii
kwa nini basi awazuie
msitekeleze kazi
aliyowapa?akauliza Agatha
akionyesha mshangao
mkubwa
“Hilo ndilo swali ambalo
hata sisi tumekuwa
tunajiuliza.Imetokea nini
hadi Rais akafanya maamuzi
kama haya?Tulikwenda pale
kwa nia ya kumsaidia yeye
mwenyewe ili rekodi za
mawasiliano yake zisiwafikie
wabaya wake lakini dah !
Gosu Gosu akashindwa
kuendelea akainamisha
kichwa
“Alifahamuje kama mko
pale?akauliza Agatha
“Agatha sisi hatufahamu
chochote.Anyway naomba
tuachane na suala hilo kwani
hata sisi tumeamua
kuachana nalo.Kwa vile
aliyetupa kazi ambaye ni
Rais ameamua kutuingilia
katika kazi aliyotupa hatuna
haja ya kuendelea na hili
jambo.Kipaumbele changu
kwa sasa ni kuhakikisha
wewe na familia yako
mnakuwa salama” akasema
Gosu Gosu na ukmya
ukatanda mahala pale.Baada
ya kama dakika tano hivi
Agatha akasema
“Gosu Gosu hampaswi
kuliacha jambo hili
hewani.Rais yuko katika
hatari kubwa.Zile rekodi
kama zikitoka katika
kompyuta ya Tamar basi
Rais atakuwa katika hatari
kubwa.Je mlijaribu
kumweleza jambo hilo na
hatari inayomkabili?akauliza
Agatha
“Hapana hatujamweleza
bado.Tulitaka tuipate
kwanza kompyuta ya Tamar
tuhakikishe tunazo rekodi
ndipo tumueleze Rais
kilichokuwa kinaendelea”
“That’s a mistake.Rais
anapaswa kuambiwa nini
kinaendelea.Yawezekana
hajui kuna bomu
linalokaribia kumlipukia”
akasema Agatha
“Agatha tuachane na
hayo mambo.Wanasiasa wa
aina yake ambao ni vigeu geu
dawa yao ni kuwaacha wafe
na misalaba yao.Hakuna
haja ya kupoteza muda na
kuhatarisha maisha
kumsaidia mtu ambaye
haoni thamani ya msaada
wetu.Let him be.Hilo bomu
likimlipukia atajua
mwenyewe” akasema Gosu
Gosu.
Ukimya ukapita tena
halafu Agatha akasema
“Gosu Gosu nafahamu
umeshafanya mengi kwangu
lakini kuna msaada nina
uhitaji”
“Sema unahitaji nini
Agatha?
“Nahitaji kuzungumza na
Samson”
“I’m sorry Agatha
hutakiwi kuzungumza na
mtu yeyote kwa sasa.Watu
wako wanaweza wakafuatilia
simu na kujua mahala ulipo”
“Nalifahamu hilo ndiyo
maana nataka tukawasiliane
naye mbali kidogo na hapa ili
hata kama wakinifuatilia
wasigundue kwamba niko
hapa.Nakuomba sana Gosu
Gosu nisaidie kwa hilo”
akasema Agatha
“Sauti yako ina
ushawishi mkubwa na
hakuna anayeweza kusema
hapana.Jiandae twende
ukawasiliane na huyo mtu
wako” akasema Gosu Gosu
na Agatha akainuka
kuelekea chumbani kwake
kujiandaa.Gosu Gosu
akabaki kwenye kiti
akimtazama
“Mtoto ameumbwa
kiafrika haswaa.Sura yake
nzuri ya upole,sauti yake
tamu laini,macho yake
malegevu dah naona taratibu
anaanza kuingia katika
ubongo wangu” akawaza
Gosu Gosu huku
akitabasamu naye akainuka
na kuelekea chumbani
kwake kuchukua bastora
Agatha alivaa suruali ya
jeans rangi ya bluu na shati
jeusi kichwani akavaa kofia
na miwani mikubwa myeusi
ili isiwe rahisi
kutambulika.Wakaingia
garini na kuondoka
“Do you mind if I
ask?akauliza Gosu Gosu
“Uliza chochote Gosu
Gosu”
“Mumeo yuko
wapi?akauliza
“Alikwisha fariki kwa
ajali.Alifariki wakati
mwanangu akiwa na mwaka
mmoja”
“Pole sana.Nini kilifuata
baada ya hapo?
“Una maanisha
nini?Agatha akauliza
“Uliolewa tena au bado
uko peke yako?
“Sikutaka kuolewa tena
kwani uwezo wa kumtunza
mwanangu ninao hivyo
sikuona sababu ya kutafuta
mwanaume
mwingine”akasema Agatha
na Gosu Gosu akatoa kicheko
“Nini
kimekufurahisha?akauliza
Agatha
“Wanawake
mnanifurahisha
sana.Hukutaka kuolewa kwa
vile uwezo wa kumsomesha
mwanao unao.Lakini kama
usingekuwa nao
ungeolewa?Why you always
thinking of ..” akanyamaza
“Say it” akasema Agatha
“Tuachane na hilo
jambo”akasema GosuGosu
“Sema tu we always
thinking of money?
“I didn’t mean that.But
isn’t it true? akasema Gosu
Gosu
“Umewaza nini hadi
ukauliza hivyo? Agatha
akauliza
“Zama hivi fedha na mali
vimepewa kipambele sana
katika mahusiano kuliko
upendo alio nao mtu na hii
iko sana kwa upande wa
wanawake.Wengi
wanamkubali mtu kutokana
na uwezo wake wa kifedha
bila kujali kama mtu huyo
ana mapenzi ya kweli kwake
au hapana.Ninazungumza
kitu ambacho nina uzoefu
nacho.Hapo kabla sikuwa
hivi nilivyo,sikuwa na fedha
wala mali,I was no
body.Ilikuwa kazi ngumu
sana kumtongoza
mwanamke akanikubali
kutokana na hali yangu ya
wakati huo lakini kwa sasa
baada ya kuwa mtu
ninauona usumbufu mwingi
sana kutoka kwa
wanawake.They call me
handsome,baby na majina
yote ya kimahaba.Wengine
kwa sura hii hii
wananiambia eti nimefanana
na P didy.Nyie wanawake
Mungu anawaona” akasema
Gosu Gosu na wote
wakaangua kicheko
“Mkeo yuko
wapi?akauliza Agatha
“Sina mke”
“Kwa nini mtu mwenye
mafanikio makubwa kama
haya usiwe na mke mpaka
leo?Utaruka ruka hadi lini?
Au unasubiri ufungue shirika
la ndege ndipo uamue kuwa
na familia?akauliza Agatha
“Ngoja nikueleze ukweli
Agatha mali hizi
unazoziona,jumba lile
kubwa,magari si
vyangu.Mimi ni msimamizi
tu.Mali hii ina mwenyewe
hivyo usione kama
nimefanikiwa” akasema
Gosu Gosu na sura ya
Agatha ikaonyesha
mshangao kidogo
“Nimeona nikwambie
ukweli mapema ujue kwani
wanaume wengi hawapendi
kusema ukweli.Sipendi
kumdanganya malaika kama
wewe kwamba mali hizi ni
zangu.Mimi ni msimamizi tu
yupo mwenyewe” akasema
Gosu Gosu na Agatha
akacheka
“Nimekuwa malaika
tena”
“Hujioni katika kioo
ulivyo Agatha?Mungu
amekupendelea na kukupa
ile sura ya
kimalaika.Wanawake
wachache sana waliojaliwa
uzuri wa aina yako” akasema
GosuGosu na Agatha
akatabasamu
“Una maneno mengi sana
Gosu Gosu.By the way what’s
your real name?akauliza
Agatha
“Jina langu mimi ni hilo
hilo Gosu Gosu sina jina
lingine”
“Una lafudhi ya
kikongo.Umewahi kuishi
kule?
“Ndiyo mimi asili yangu
ni jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo lakini kwa sasa ni
mtanzania.Ninafurahi sana
kuwa mtanzania” akasema
Gosu Gosu
Walifika kati kati ya jiji
Gosu Gosu akaegesha gari
katika mgahawa Fulani
wakashuka na kuingia ndani
wakaagiza supu.Agatha
akaiwasha simu yake na
kumpigia Samson.
Katika idara ya siri ya
usalama wa ndani wa
nchi,simu ya Samson ilikuwa
imewekwa katika kifaa
maalum na mara tu ilipoita
jina la Agatha
likaonekana.Lucas ambaye
alikuwa amekabidhiwa
jukumu la kuifuatilia simu
ile haraka haraka akainua
simu na kumpigia Tamar
akamjulisha kwamba Agatha
anapiga.Haraka haraka
Tamar akatoka ofisini kwake
na kumfuata Lucas katika
meza yake.
“Umefuatilia kujua
anapiga kutokea
wapi?akauliza Tamar.Lucas
akabonyeza kompyuta yake
kisha ramani ikatokea katika
runinga kubwa.
“Yuko mtaa wa Ali
Mzawa”
“Good job.Alex chukua
kikosi cha watu watano
mumfuate Agatha haraka
sana.Yuko mtaa wa Ali
Mzawa tutakuwa tunawapa
maelekezo kila mahala
atakakoenda” akasema
Tamar
“Nitakupata
Agatha.Hutaweza
kunikimbia.Huna sehemu ya
kujificha kahaba wewe nchi
hii yote ninaiona katika
kiganja changu!
Nitakapokutia mikononi
nitakuonyesha raha ya
usaliti” akawaza Tamar na
kurejea ofisini kwake
Agatha alipiga simu
mara ya kwanza lakini
haikupokelewa,akapiga mara
ya pili lakini haikupokelewa.
“Something is not
right.Samson huwa ana kifaa
cha kupokelea simu sikioni
na haijawahi kutokea hata
mara moja nikapiga simu
mara mbili bila
kupokelewa”akasema Agatha
na kunyamaza kidogo
wakatazamana
“He must be in trouble”
akasema Akasema Agatha na
kuizima simu yake
akachomoa betri.
“Twende tuondoke hapa
haraka sana.Lazima
watakuwa wanaifuatilia
simu yangu na watajua niko
hapa” akasema Agatha
GosuGosu akamrushia
muhudumu noti mbili za elfu
kumi kumi kulipia supu ile
ambayo ilikwisha letwa
mezani wakaondoka
“Tunaelekea wapi?
Akauliza Gosu Gosu
“Nataka twende
nyumbani kwake tukajue
kama ana tatizo lolote.Nina
wasi wasi yawezekana
wakawa wamegundua
kwamba kirusi kile
nilichokipandikiza katika
mfumo wao kilipitia katika
akaunti yake.Kama
wakiligundua hilo nitakuwa
nimemuweka katika wakati
mgumu sana” akasema
Agatha na kumuelekeza
GosuGosu anakoishi Samson
Iliwachukua zaidi ya
dakika hamsini kuwasili
katika mtaa anakoishi
Samson.Mara tu
walipokaribia katika nyumba
ya Samson walikutana na
umati mkubwa wa watu na
magari ya polisi.
“Nini kimetokea pale?Ni
karibu sana na nyumbani
kwa Samson” akasema
Agatha kwa woga.Gosu Gosu
akaegesha gari pembeni
“Stay in the
car.Ninakwenda kuangalia
nini kimetokea”akasema
Gosu Gosu na kushuka
garini akaenda kuungana na
umati ule mkubwa wa watu
“Kuna nini hapa”
akamuuliza kijana mmoja
aliyekuwa karibu yake
“Kuna kijana mmoja
amejipiga risasi asubuhi ya
leo”
“Unamfahamu kijana
huyo?
“Ndiyo ninamfahamu
kwa sura lakini nimesikia
watu wanaomfahamu vyema
wanamuita Samson”
“Wanadai nini sababu ya
kujipiga risasi?akauliza
GosuGosu
“Hakuna anayefahamu
hadi sasa chanzo cha
kujipiga risasi lakini wengine
wanadai ni sababu za
kimapenzi ila hakuna
mwenye uhakika” akajibu
Yule kijana.Gosu Gosu
hakutaka kuendelea
kupoteza muda akarejea
garini
“He’s dead.Samson is
dead.Amejiua kwa kujipiga
risasi leo asubuhi” akasema
Gosu Gosu.Agatha akainama
na kuangua kilio.Gosu Gosu
akawasha gari wakaondoka
“Agatha usilie tafadhali
huu ni wakati wa kuwa
imara sana.Mambo ndiyo
kwanza yameanza” akasema
Gosu Gosu
“Samson asingeweza
kujiua na hakuwa na sababu
ya kujiua lazima watakuwa
wamegundua kile
nilichokifanya kupita
akaunti yake na ili
kujiepusha na matatizo
akaamua kujiua.Moyo
unaniuma sana ni mimi
ambaye nimesababisha kifo
chake”akasema Agatha
akiendelea kulia
“Agatha usijilaumu
tafadhali kwa kile
ulichokifanya”
“I did that to protect
President but…….” Agatha
akanyamaza na kufuta
machozi
“Inauma kwani juhudi
zote hizi za kumsaidia Rais
lakini yeye ndiye amekuwa
mstari wa mbele kuturudisha
nyuma.Gosu Gosu please
help me to get out of the
country.Kama nikiendelea
kukaa hapa Tanzania mimi
na familia yangu
tutauawa.Hakuna mahala
ndani ya Tanzania ambako
tunaweza kujificha na
kuamini tuko salama”
akasema Agatha
“Agatha
usihofu.Nitakulinda na
utakuwa salama”
“Gosu Gosu you don’t
know these people they’re
powerfull.Wana uwezo wa
kufika kokote kule” akasema
Agatha
“Naomba uniamini
tafadhali.Nitakulinda kama
nilivyokuahidi” akasema
Gosu Gosu na mara ukaingia
ujumbe katika simu
yake.Mwendo wa gari
ulikuwa wa taratibu sana
kutokana na
foleni.Akaufungua ujumbe
ujumbe ule akausoma
“Tukutane sasa hivi
Msanzi hotel.Kuna jambo la
muhimu sana.Austin”
Ndivyo ulivyosomeka
ujumbe ule
“Austin kwa nini
ameamua kutumia namba
nyingine kunitumia
ujumbe?Kwa nini hajatumia
namba yake ya
kawaida?akajiuliza Gosu
Gosu na kuamua kumpigia
kupitia namba ile
aliyotumiwa ujumbe.
“Hallow”akasema Gosu
Gosu
“Papaa najua
umeshangaa lakini hiyo ni
namba yangu nyingine
ambayo huwa ninaitumia
kwa dharura.Naomba
tafadhali tukutane mahala
nilipokuelekeza”akasema
Austin
“Kuna nini
Austin?akauliza Gosu Gosu
“Nitakueleza utakapofika
Papaa lakini ni jambo la
muhimu sana” akasema
Austin
“Sawa ninampeleka
Agatha nyumbani halafu
nitakuja hapo”akajibu Gosu
Gosu
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 4
Gosu Gosu aliwasili
Msanzi Pub ambako Austin
alikuwa anamsubiri
“Karibu Papaa ahsante
sana kwa kufika” akasema
Austin muhudumu akafika
kwa haraka Gosu Gosu
akaagiza bia.
“Nimeshangaa sana kwa
nini hukutumia ile namba
yako ya kawaida
niliyoizoea?akauliza Gosu
Gosu
“Gosu Gosu kuna kitu
nimekuitia hapa.Najua
umekwisha kata tamaa
kabisa na hutaki kusikia
chochote kutoka kwangu
lakini lazima nikushirikishe
jambo hili”
“Usijali Austin.Kuna
nini?
“Tulipoachana asubuhi
nilikwenda nyumbani
kambini kupumzika.Nikiwa
napumzika natafakari kile
kilichotokea jana usiku Rais
akanipigia simu” akasema
Austin na kunyamaza baada
ya kuona sura ya Gosu Gosu
imebadilika
“Usikasirike Papaa najua
hutaki kusikia chochote
kuhusu Rais”akasema
Austin.
“Austin umenichafua
kabisa kusikia kuwa Rais
alikupigia simu.Naomba
nikuweke wazi kabisa kama
kuna kazi amekupa mimi
usinihusishe! Akasema Gosu
Gosu
“tafadhali nisikilize
kwanza Papaa”akasema
Austin
“Rais aliniambia kwamba
kuna nyaraka muhimu
atamtuma mtu aniletee jioni
ya leo hivyo natakiwa
kwenda Dino’s hotel
kukutana na huyo mtu na
nikisha zipitia nyaraka hizo
nitakazoletewa nimjulishe”
akasema Austin.Gosu Gosu
akainuia chupa ya bia
akanywa funda kubwa
“Tatizo liko wapi
Austin?Kama anataka
kukupa nyaraka nenda
kazichukue uzifanyie
kazi”akasema Gosu Gosu
“Hapo ndipo kuna tatizo
Papaa.Huoni kama jambo
hili lina ukakasi?
“Ukakasi kivipi Austin?
“Kwanza kabisa Rais Dr
Fabian ni msiri sana na
hapendi mambo yake ya siri
yajulikane.Alinihakikishia
kwamba mpaka sasa hana
mtu anayemuamini
kumshirikisha katika mambo
yake ya siri na ndiyo maana
rais aliyepita Dr Evans
akamuelekeza kwangu
kwamba anaweza
akaniamini na nikafanya
naye kazi za siri.Kitendo cha
kutaka kumtuma mtu
kwangu kuniletea nyaraka
za siri tena hotelini
kinanishangaza kidogo kwa
sababu hana utaratibu
huo.Kama kuna jambo lolote
la siri anataka kunieleza
huwa ananiita ikulu
tunazungumza ana kwa ana
lakini leo hii anataka
kumtuma mtu kwangu
kuniletea taarifa ya
siri.Hainiingii akilini
Papaa.Tukiliweka hilo
pembeni turejee katika suala
la usiku wa jana.Rais
alifahamuje kama
tumekwenda nyumbani kwa
Tamar?Baada ya kufahamu
kwa nini hakutuacha
tuendelee na kile
kilichotupeleka pale na
badala yake akatutaka
tuondoke?Kama haitoshi
akapiga tena simu na
kututaka tuachane na
uchunguzi tuliokuwa
tunaufanya hadi hapo
atakapotueleza.Ukilitazama
vizuri jambo hili utagundua
kwamba kuna mawasiliano
kati ya Rais na SNSA na
unapozungumzia SNSA
unamzungumzia
Tamar.Ninaamini Rais
alipata taarifa zetu jana
kutoka kwa Tamar.Ninahisi
pale nyumbani kwa Tamar
kuna kamera za siri ambazo
zimeunganishwa na mtambo
maalum ambao humjulisha
Tamar kama kuna mtu
ameingia nyumbani kwake
wakati hayupo.Baada ya
kupewa taarifa hizo ndipo
akamjulisha Rais” akasema
Austin.Ukimya ukapita kila
mmoja akipiga mafunda
kadhaa ya kinywaji halafu
Austin akaendelea
“Kama ni hivyo linaibuka
swali.Baada ya kujua
tumevamia kwake Tamar
angeweza kupiga simu polisi
akawajulisha kwamba kuna
watu wamevamia nyumbani
kwake,angeweza kutuma
vijana wake mahiri kutoka
SNSA wakatufuata pale na
kutuweka chini ya ulinzi au
angeweza kutufanya
chochote lakini alimjulisha
moja kwa moja Rais ambaye
naye alitutaka tuondoke pale
haraka sana na akatutaka
tusiendelee tena na
uchunguzi wowote.Kwa nini
Tamar alimjulisha Rais
kuhusu sisi kuvamia
nyumbani kwake? Kabla
hatujapata jibu turejee
katika lile suala letu la
kwanza.Rais ananitaka
nikaonane na mtu
atakayemtuma jioni ya leo
hotelini hudhani kama huo
ni mtego
nimetegewa?akauliza
Austin.Gosu Gosu akatikisa
kichwa
“Austin umenifumbua
macho na kuna kitu
ninakiona katika hayo
uliyonieleza.Kweli hapa
kunaonekana kuna jambo
halijakaa
vyema.Nakubaliana nawe
kwamba yawezekana huu
ukawa ni mtego.Kuna kitu
nimekumbuka.Jana usiku
tukiwa nyumbani ulimpa
simu yako Agatha
kuwasiliana na Samson
ambaye alimsaidia katika
kuingiza kirusi kwenye
mfumo wa kompyuta wa
SNSA.Kabla ya kuja hapa
Agatha aliniomba nimpeleke
mahala akawasiliane na
Samson,alimpigia simu
lakini simu yake
haikupokelewa.Tukaenda
nyumbani kwake na kukuta
amejipiga risasi.Yawezekana
SNSA walikuta namba yako
ya simu katika simu ya
Samson na wanaamini
kwamba lazima utakuwa
unafahamu mahala alipo
Agatha ambaye anafahamu
siri nyingi za SNSA hivyo
wanataka kutengeneza
mtego wakukamate kwa
lengo la kufahamu alipo
Agatha” akasema Gosu Gosu
“Kama ni hivyo kwa nini
basi wamtumie Rais?
Akauliza Austin
“SNSA iko chini ya
Rais.Malengo ya kuanzishwa
kwa taasisi hii ya siri ni
kumsaidia Rais katika
kutawala hivyo kila
wanachokifanya lazima Rais
ajue hivyo watakuwa
wamemtumia yeye ambaye
ni mtu wa karibu kwako ili
kukupeleka katika mtego”
akasema Gosu Gosu
“Lakini idara hiyo hiyo
ambayo iko chini ya Rais
ndiyo inayotumiwa kutaka
kumuhujumu Rais.Kwa nini
anashindwa kuliona hilo?
Akauliza Austin na baada ya
tafakari Gosu Gosu akasema
“Austin kuna kitu
kinaendelea hapa ambacho
hatukifahamu.Rais
amebadilika ghafla sana na
kuleta wasiwasi mkubwa”
akasema Gosu Gosu
“NIkweli mabadiliko ya
Rais yanashangaza na
anatulazimisha tuhisi kuna
jambo linaloendelea”
akasema Austin
“What’s the
plan?akauliza Gosu Gosu
“Papaa naomba
nikuweke wazi kwamba
mimi sina mke,sina mtoto
sina familia.Sina kitu
chochote cha kupoteza hivyo
basi nimeamua kuondoka
zangu.Siwezi kushindana na
Rais yeye ana mtandao
mrefu.Nimefikiria sana na
hayo ndiyo maamuzi
yangu”akasema
Austin.Gopsu Gosu
akamtazama kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
“Are you sure Austin that
you want to run away?
“I’m sure.I’m done
here”akasema Austin na
kuchukua chupa yake
akanywa funda kadhaa za
bia.
“Austin siwezi kupingana
na maamuzi yako ya kutaka
kuondoka kuepukana na
matatizo lakini naomba
nikukumbushe kitu kimoja
kwamba kukimbia si
suluhisho la hili jambo.Hata
ukikimbia hawa watu wana
mashirikiano na nchi mbali
mbali hivyo unaweza
ukakamatwa au ukamalizwa
kimya kimya”akasema Gosu
Gosu na kunyamaza
“Nini ushauri wako?
Austin akauliza
“Sikushauri
ukimbie.Nashauri tulikabili
hili jambo hadi mwisho
wake.Tuchimbe zaidi na
kuufahamu ukweli wa
mabadiliko haya ya ghafla ya
Rais” akasema Gosu Gosu
“Papaa unaposema
tukabiliane na hili suala
unamaanisha kwamba
tupambane na SNSA na
Rais?Hatuna uwezo wa
kupambana na hawa
watu.SNSA wana uwezo wa
kumpata mtu yeyote
wanayemtaka hapa nchini
hivyo sidhani kama
tunaweza kup……..”
“Austin remember we’re
soldiers.Hatuogopi chochote
na kazi yetu sisi ni
kupambana.Mimi
nitakuunga mkono katika
mapambano haya ili tuweze
kujua kile kinachoendelea
nyuma ya pazia” akasema
Gosu Gosu kisha
wakaendelea na majadiliano
mengine
RAMALLAH – PALESTINA
Soko kubwa la samaki
liliendelea kujaa watu.Ndani
ya gari moja lililokuwa
pembeni kidogo ya lile soko
Habib, msaidizi wa Ammar
Nazari alikuwa na watu
wengine watatu wakiwa
wameyaelekeza macho yao
katika kompyuta.Walikuwa
wanamuangalia Mathew
Mulumbi aliyekuwa ndani ya
gari ambalo kuliwekwa
kamera za siri
zilizounganishwa na
kompyuta ile waliyokuwa
wakiitazama.
Mathew alifumba macho
baada ya muda kufika halafu
akabonyeza kitufe
alichoelekezwa na Habib
lakini hakukutokea
mlipuko.Habib na wenzake
wakatazamana na
kutabasamu
“Huyu kweli ni
mpiganaji.Atatufaa sana”
akasema Habib
Ndani ya gari alimo
Mathew Mulumbi jasho
lilimtiririka usoni kama mtu
aliyesimama kwenye matone
ya mvua.
“Nini kimetokea?Mbona
bomu halijalipuka?akajiuliza
na kufumbua
macho.Akatazama kama
kuna kitu amekosea lakini
kila kitu kiko vile vile
kilivyoachwa na Habib.Mara
mlango ukafunguliwa
akaingia Habib
“Nimefanya kila
ulichonielekeza
lak……….”akasema Mathew
Habib akamkatisha
“Hongera sana Abu.Huu
ulikuwa ni mtihani kwako na
umeushinda vizuri.Hili bomu
halikuwa limeunganishwa
hivyo usishangae kwa nini
halikulipuka.” akasema
Habib na kuwasha gari
wakaondoka
“Kila mtu ambaye
anajiunga na sisi lazima
apewe mitihani kumpima
kama kweli ana nia ya dhati
ya kujiunga nasi na moja ya
mtihani ambao hupewa ni
kama wanaweza wakajitoa
mhanga kujilipua na
bomu.Wengi wamekuwa
wanakwama kila
wanapopewa mtihani kama
huu na wengine hutoka
ndani ya gari wakakimbia.Si
kazi nyepesi kujitoa mhanga
hivyo ni moja kati ya mtihani
mgumu sana ambao ili
ukubaliwe kujiunga nasi
lazima uupitie.Hongera Abu
wewe ni jasiri na unafaa
kuwa mmoja wetu” akasema
Habib lakini Mathew
hakujibu kitu bado
aliendelea kutokwa na jasho.
“Naomba Mungu
anisaidie niweze kutoka
salama kwa hawa
wauaji.Mimi ni mtu jasiri
sana lakini leo ujasiri wangu
wote umeingia
mfukoni.Nimetetemeka.Ni
vipi kama lile bomu
lingekuwa la kweli?Hivi sasa
ningekwisha kuwa
marehemu.Nimezoea kuua
watu lakini leo nimenusa
kifo.Nimeogopa sana”
akawaza Mathew bado mwili
uliendelea kumtetemeka.
“Nashukuru kwamba
sasa wananiamini na hili ni
jambo zuri kwani lengo langu
la kuelekea kuonana na
Habiba Jawad linakwenda
kutimia.Naomba Mungu
aendelee kunikinga na hawa
jamaa ili niweze kumfikia
Habiba Jawad” akaendelea
kuwaza Mathew.
“Abu naomba usiwe na
wasiwasi wowote kuhusu
sisi.Hizi ni taratibu zetu za
kawaida kwa kila ambaye
anataka kujiunga nasi na
katika wote ambao nimewahi
kuwafanyia usaili wewe
umeshinda kwa kiwango cha
juu sana.Nini mipango
yako?akauliza Habib
“Mipango yangu kama
nilivyomueleza Ammar ni
kwamba nataka kuendelea
kupambana na Israel.Ni hilo
pekee ndilo lililopelekea
kuamua kujiunga na
Ammar” akasema Mathew
“Ulikutana vipi na
Ammar gerezani?akauliza
Ammar
“Ni hadithi ndefu lakini
ninamshukuru sana Ammar
kwani ni mtu aliyenisaidia
sana tukiwa
gerezani.Nilipokutana naye
nilikuwa katika hali
mbaya.Nilikuwa nimeteswa
mno na nilikuwa nimekata
tamaa.Ni Ammar ambaye
alikuwa karibu nami
akanisaidia hadi nikawa tena
binadamu.Kwa bahati nzuri
tukakutana mimi na yeye
sote tuna malengo sawa na
akanishauri
tutakapofanikiwa kutoroka
gerezani basi nijiunge naye”
akasema Mathew
“Gereza mlilokuwa
mmefungwa ni gereza
linalosifika kwa ulinzi mkali
sana.Mliwezaje kutoroka
gerezani? Akauliza Habib
“Ni hadithi ndefu sana
hiyo.Nitakueleza siku
tukipata nafasi.Kwa sasa
nahitaji kupumzika”
akasema Mathew na
kujiegemeza kitini akafumba
macho akajifanya amelala
“Natakiwa haraka sana
kuanza kutafuta njia ya
kujinasua kutoka kwa hawa
watu.Sitaki kutumia muda
mrefu sana nikiwa na mgaidi
hawa” akawaza Mathew na
kusinzia
Walirejea katika makazi
ya Ammar wakashuka na
kuingia ndani ya jumba
kubwa la Ammar
“Karibuni sana” akasema
Ammar aliyekuwa amejilaza
katika godoro pale sebuleni
“Ahsante sana
Ammar.Vipi maendeleo
yako?akauliza Mathew
“Ninaendelea vyema
kabisa” akasema Ammar na
kumgeukia Habib
“Habib nataka unieleze
mlikuwa wapi?Ulimpeleka
wapi Abu?akauliza Ammar
huku akiinuka na kukaa.
“Kama tulivyokuwa
tumekubaliana jana Ammar
nimetoka kumpa Abu
mtihani kidogo”akasema
Habib
“Amefuzu?akauliza
Ammar
“Ndiyo amefuzu vyema
kabisa.Ni mtu jasiri na
ninaweza kusema kwamba ni
mtu ambaye tunamuhitaji
sana” akasema Habib
“Nashukuru kusikia
hivyo” akasema Ammar na
kumfanyia ishara mmoja wa
wasaidizi wake asogee karibu
halafu akamtuma aende
akawaite watu wote
waliokuwa nje waiingie
ndani.Sebule ilikuwa ndogo
kwani watu waliokuwa nje
walikuwa wengi wengine
wakabaki nje.Walikuwa na
hamu sana ya kutaka
kusikiliza kile ambacho
mkuu wao alitaka
kukisema.Ammar akamtaka
msaidizi wake amsaidie
kusimama na kujitegemeza
kwa kutumia fimbo
“Naombeni mnisikilize
ninyi nyote ! akasema
Ammar
“Ninamshukuru Mungu
baada ya miaka kadhaa ya
kufungwa gerezani hatimaye
nimeweza kutoka gerezani
na sasa nimekuja kuungana
nanyi tena.Ninawashukuru
sana kwa kuendeleza
mapambano hata wakati
ambao sikuwepo.Kwa hiki
mlichokifanya nina uhakika
mkubwa sana kwamba hata
nikifa leo hautakuwa mwisho
wa mapambano.Bado
mapambano
yataendelea.Ninawahakikish
ia kwamba jeshi letu
litakuwa imara sana na
damu nyingi inakwenda
kumwagika Israel” akasema
na kunyamaza
“Jambo la pili ambapo
nataka kuzungumza nanyi ni
kwamba mimi ndiye kiongozi
wa kundi hili la Ammar
Nazari brigades na hata
nitakapokuwa kaburini bado
kundi hili litaendelea kubeba
jina langu.Nikiwa kama
kiongozi ninahitaji heshima
na kauli yangu mimi ni ya
mwisho.Nitakachokisema
lazima wote mkitii” akasema
na kunyamaza kidogo
“Nimetoka gerezani kwa
msaada mkubwa wa Abu”
akasema akimnyooshea
kidole Mathew
“Mimi na yeye tulikuwa
tumefungwa gereza moja na
yeye ndiye aliyenisaidia
mimi hadi
nikatoroka.Mpango wa
kutoroka ulikuwa wa kwake
lakini hakutaka kuniacha
akaondoka nami.Nimepigwa
risasi mara mbili angeweza
kuniacha gerezani lakini kwa
ujasiri mkubwa hakuweza
kufanya hivyo alinibeba na
kuhakikisha anaondoka
nami.Narudia tena ni kwa
sababu yake niko nanyi hapa
leo” akasema Ammar na
kunyamaza kidogo
“Sisi tunazo taratibu zetu
kwa mtu ambaye anataka
kujiunga nasi na ninyi nyote
mmepitia huko kila mmoja
kwa namna yake.Tunafanya
hivyo ili kupata uhakika
kwamba ni kweli mna nia ya
dhati ya kujiunga nasi.Abu
ni mtu ambaye kwa kile
alichokifanya cha kunisaidia
nikatoka gerezani tayari
amekwisha onyesha
uaminifu kwetu kwani
aliyaweka maisha yake
hatarini kwa ajili
yangu.Baada ya kufika hapa
kuna baadhi ya wenzangu
ambao hawakutaka
kumuamini na walitaka
kumfanyia majaribio.Licha
ya kuwaeleza kwamba Abu
ni mtu mwaminifu kwetu na
hakuna haja ya kumsumbua
kwa kumfanyia majaribio
lakini bado wameendelea
kusisitiza kutaka kumfanyia
majaribio.Sijapendezwa na
hiki walichokifanya hawa
wenzangu wakiongozwa na
Habib.Kitendo cha
kushindwa kuniamini hata
mimi kiongozi wenu ni
kitendo cha dharau na
kimenisikitisha sana.Leo
nataka kutoa fundisho
kwamba nimerudi
mwenyewe na sitaki
dharau.Nitakachokisema
nataka kitekelezwe.Kauli
yangu mimi ni ya mwisho !
akasema Ammar kwa ukali
akamfanyia ishara mmoja wa
wasaidizi wake ampatie
bastora na akafanya kitendo
ambacho wote hawakuwa
wamekitegemea.
Alimnyooshea bastora
Habib na kumpiga risasi ya
kichwa akaanguka chini
akafa palepale.
“Hili ni onyo kwenu
nyote kwamba sitaki
dharau.Nitakachokisema
mimi ni amri na kila mtu
lazima akitekeleze” akasema
Ammar na kuwataka watu
wote watoke mle
ndani.Akamgeukia Mathew
“Abu samahani sana kwa
yote yaliyotokea.Wewe ni
mtu muhimu sana kwetu
hukupaswa kufanyiwa hivi
walivyokufanyia.Huwa
tunawafanyia hivi wale
ambao ni wageni kabisa
katika mapambano haya
lakini wewe si mgeni.Wewe
ni mpiganaji mkubwa na
unapaswa kuwa kiongozi wa
ngazi za juu kabisa katika
kundi letu.Habib ni mtu
wangu wa karibu sana
nimetoka naye mbali lakini
nimemuua kwa heshima
yako.Mimi kama kiongozi
wao sina mashaka yoyote
nawe na ninakuamini kwa
asilimia mia moja lakini yeye
ameonyesha dharau kwangu
kwa kuamua kwenda
kukufanyia majaribio.Ni vipi
kama huko mlikoenda
mngekamatwa na majasusi
wa Israel waliotapakaa kila
sehemu?Naomba usinione
mkatili sana nilichokifanya
ni kudumisha nidhamu
katika kundi langu.Pole sana
na samahani kwa yote
Abu.Sasa nenda
ukapumzike” akasema
Ammar na Mathew
akaelekea katika chumba
chake kujipumzisha.
“Mambo ndiyo kwanza
yameanza.Bado nitakutana
na mambo mengi makubwa
yaliyojaa ukatili mkubwa
lakini sipaswi kukata
tamaa.Nimekuja hapa
kupambana na lazima
nipambane.Lazima nifikie
lengo langu la kumfikia
Habiba Jawad.Natakiwa
kuwa karibu sana na Ammar
ambaye naamini ndiye
atakayeniongoza kufika kwa
Habiba.Haitakuwa rahisi
kufika kwa Habiba lakini
nitajitahidi hadi nifike na
nimuondoe kwani utakuwa
ni ukombozi mkubwa kwa
dunia.Huyu ndiye uti wa
mgongo wa ugaidi duniani
kama huyu akiondoka basi
ugaidi utakosa nguvu”
akawaza Mathew akavua
nguo na kuingia bafuni
kuoga
“Nilitaarifiwa mapema
kwamba Ammar ni mtu
mbaya sana na leo
nimelithibitisha hilo kwa
kitendo chake cha kumuua
mshirika wake wa karibu
Habib.Hakuna aliyetegema
kitu kama kile
kutokea.Umakini mkubwa
unatakiwa huyu jamaa hana
rafiki” akawaza Mathew na
kutoka bafuni baada ya
kumaliza kuoga akabadili
nguo na kujilaza kitandani.
“Natamani kupata nafasi
ya kuwajulisha Mossad
kwamba tayari nimekwisha
fika na niko salama lakini
sina simu na sijui nitapata
wapi simu.Lazima nitafute
njia ya kuwasiliana nao”
akawaza Mathew na
kutolewa mawazoni baada ya
mlango wa chumba chake
kugongwa.Akamruhusu
mgongaji kuingia
ndani.Alikuwa ni Nawal mke
mdogo wa Ammar aliyekuwa
amebeba birika la chai na
sinia la vitafunwa
akamuandalia Mathew
mezani
“Karibu chai” akasema
Nawal Mathew akainuka na
kushika kikombe akanywa
chai kidogo halafu akasema
“Nashukuru sana Nawal”
Nawal aliendelea
kusimama akimtazama
Mathew
“Kwa nini umemsaidia
Ammar?Kwa nini umemtoa
gerezani?akauliza Nawal
kwa sauti ndogo na Mathew
akatabasamu
“Nakuuliza Abu kwa nini
umemsaidia
Ammar?Unamfahamu
vyema?akauliza Nawal
“Ammar ni rafiki yangu
na nisingeweza kumuacha
katika mpango wangu wa
kutoroka gerezani” akasema
Mathew
“Ulifanya kosa kubwa
sana Abu.Hukupaswa
kumtoa Ammar
gerezani”akasema Nawal
“Kwa nini
Nawal.Hujafurahi kwa
mumeo kurejea
nyumbani?akauliza Mathew
“Sijafurahi na wala
siwezi kufurahi.Humfahamu
vizuri Ammar ni mtu katili
sana” akasema Nawal na
sura yake ilionyesha
alimaanisha
alichokisema.Mathew
akaweka kikombe chini na
kumtazama Nawal
“Nawal uko sahihi ni
kweli simfahamu vyema
mumeo nimekutana naye
gerezani tukawa marafiki”
akasema Mathew
“tafadhali ondoka.Hapa
si sehemu sahihi kwako”
akasema Nawal
“Kwa nini unasema hivyo
Nawal?
“Nikikutazama macho
yako hayaonyeshi ukatili
hauonekani kama ni
gaidi.Mahala hapa wamejaa
magaidi ambao ni watu
makatili sana na wanaweza
wakakuua.Tafadhali ondoka”
akasema Nawal
“Nawal sina sehemu
nyingine ya kwenda,hapa
nimefika nyumbani.Ninataka
kufanya kazi na Ammar na
kundi lake” akasema
Mathew na Nawal
akaondoka kwa hasira
“Huyu mwanamke
inawezekana ametumwa
kuja kunichunguza na
kuniwekea mtego.Siamini
kabisa hawa watu kwani
wataniwekea mitego mbali
mbali ili kunipima kama
kweli nina nia ya dhati ya
kujiunga nao.Bado nina
safari ndefu kidogo lakini
lazima nifanyue kila juhudi
kuwafanya
waniamini.Haiwezekani mke
wake asifurahi mumewe
kutoka gerezani.Nimekwisha
utambua mtego wao
wanataka kumtumia Nawal
kunichimba kwa
undani.Hapa
wamekwama,hawatapata
chochote” akawaza Mathew
PARIS – UFARANSA
Katika jumba la bilionea
Peniela hali ilikuwa ya
ukimya japo shughuli za
hapa na pale ziliendelea
kama kawaida.Maafisa wa
usalama walikuwa
wanaingia na kutoka katika
jumba hili la kifahari
wakitaka kupata taarifa za
kina kuhusiana na tukio la
mauaji ya walinzi wanne wa
Peniela pamoja na mpenzi
wake Nahum baada ya
kushambuliwa na watu
wasiojulikana.Waandishi wa
habari nao walipiga kambi
nje ya jengo la Peniela
wakitafuta habari za kile
kilichojiri.
Saa tano za asubuhi
Peniela akiwa amevaa
mavazi meusi aliingia katika
gari lake la kifahari na
msafara wake ukaondoka
kuelekea hospitali.Ulinzi
wake uliimarishwa sana siku
hii.
“Siamini kama leo
ninakwenda kumuaga
mpenzi wangu Nahum.Jana
nimeshinda naye kutwa
nzima tukifurahi na kupeana
raha lakini leo hii siko naye
tena na ninakwenda
kumuaga.Kweli dunia haina
usawa kabisa.Kwa nini kila
pale ninapoipata furaha ya
maisha yangu dunia
inanikatili?Kwanza alikuwa
ni Mathew ambaye alitoweka
na mpaka leo hii hata kucha
zake sikuwahi
kuziona.Baada ya Mathew
amekuja Nahum ambaye
kidogo alinivutia na
nikaanzisha mahusiano naye
akanisaidia kuyapunguza
machungu ya kuondokewa
na Mathew lakini naye
amenyakuliwa kama
upepo.Mimi nina mkosi
gani?Kwa nini dunia
inaniadhibu kiasi hiki?
Sipaswi kupenda au kuwa na
mpenzi? Akajiuliza Peniela
akiwa garini.Picha mbali
mbali akiwa na Nahum
wakifurahi zikaendelea
kupita kichwani kwake
“Ni vigumu kuamini
lakini ni kweli ninakwenda
kumuaga Nahum.Siku nzima
ya jana alikuwa
anazungumza masuala ya
kufa hadi nikamtaka
asiendelee tena kutamka
maneno yale yanayohusiana
na kifo.Ni kama vile alijua
atakufa.Nani lakini
waliomuua Nahum?
Akawaza Peniela akachukua
kitambaa na kujifuta
machozi
“Kuna kitu kinaniumiza
kichwa sana kuhusu mauaji
haya ya Nahum.Alikuwa na
mabadiliko ya ghafla na
hakutaka tena kuendelea na
mambo yoyote ya kibiashara
na badala yake akataka
tutumie muda mwingi
kustarehe.Kutwa nzima ya
jana hakuonekana kuwa na
raha na alikuwa
anazungumzia sana masuala
ya kufa hadi nilipomtaka
asiendelee kuongelea mambo
hayo.Je alijua atakufa ndiyo
maana akawa katika hali
ile?akajiuliza Peniela na
kuanza kukumbuka namna
tukio lile lilivyotokea.
“Peniela nisikilize.Watu
hawa wananitafuta mimi
wamekuja kuniua hivyo
kama nikifa nakuomba
umtafute Mathew
Mulumbi.Yuko hai” Peniela
akayakumbuka maneno
aliyoambiwa na Nahum
dakika chache kabla ya
kuuawa.Akafuta machozi
“Alijuaje kama watu wale
wamekuja kumfuata yeye
kumuua ? akawaza na
kuendelea kufuta machozi
“Kuna maneno Nahum
aliyasema ambayo
yananichanganya zaidi !
akawaza na kuikumbuka
sauti ya Nahum
“Nisikilize
Peniela.Mathew Mulumbi
yuko hai.Tafadhali mtafute”
“Alimaanisha nini kwa
kauli hii? Akajiuliza
“Nahum aliirudia kauli
hii mara mbili tena kwa
msisitizo mkubwa kwamba
Mathew yuko hai akinitaka
nimtafute.Oh my God what’s
going on?Who was he?
Akajiuliza Peniela
“Ngoja kwanza niachane
na hili jambo litaniumiza
kichwa change,nimalize
kwanza misiba hii
iliyonikuta niwazike walinzi
wangu halafu nitakaa na
kutafakari kwa kina hiki
kilichotokea.Kwa sasa akili
yangu imechoka kabisa na
kuendelea kutafakari jambo
kubwa kama hili ni
kuendelea kujichosha zaidi
na sintapata muafaka
wowote.Naliweka jambo hili
pembeni kwa muda”
akawaza Peniela.
DAR ES SALAAM
Saa kumi na moja za
jioni Gosu Gosu alirejea
katika makazi yake akiwa na
mwanaserere
mkubwa.Alipoingia ndani
akawakuta Agatha na
mwanae Teddy pamoja na
Nancy wakiwa katika
chumba cha mapumziko
wakitazama filamu.
“Hallo” akasema Gosu
Gosu akitabasamu.
“Karibu Gosu Gosu”
akasema Agatha na Gosu
Gosu akamfuata Teddy
akapiga magoti na kumpatia
Yule mwanasesere.
“Sweetheart this is the
gift from your uncle”
akasema Gosu Gosu na
Teddy akamchukua Yule
mwanasesere
“Thank you uncle”
akasema Teddy
“Mmeshindaje
hapa?akauliza Gosu Gosu
“Tumeshinda
salama.Tunaendelea
vizuri.Any news?akauliza
Agatha
“Hakuna habari yoyote”
“Uncle what’s your
name?akauliza Teddy
“My name?akauliza Gosu
Gosu huku akitabasamu
“Yes”
“My name is uncle Gosu
Gosu”
“Uncle Gosu Gosu do you
have children? I want
someone to play
with”akasema Teddy
“Do you want to play?
“Yes I want to play”
akajibu Teddy na Gosu Gosu
akawataka watoke mle ndani
wakaeleka bustanini ambako
kulikuwa na bembea na
michezo mbali mbali ya
watoto.Mathew alikuwa
ameitengeneza bustani hii
maalum kwa ajili ya wanae
kila wanapokuja kutembea.
Gosu Gosu akaenda na
Teddy kwenye bembea
akaanza kumsukuma
taratibu.Teddy alifurahi
sana.Baada ya muda Gosu
Gosu akamuacha Teddy na
Nacy akamfuata Agatha
“Thank you so much
Gosu Gosu”akasema Agatha
na Gosu Gosu akatabasamu
“Kwa mara ya kwanza
toka nimepatwa na matatizo
nimejikuta
nikitabasamu.Nilikuwa na
mawazo mengi sana kuhusu
Teddy kama angeweza hata
kucheza kutokana na hali
aliyokuwa nayo leo
asubuhi.Hakutaka hata
kutoka nje.Ahsante kwa
kumfanya atabasamu tena”
akasema Agatha huku
akilengwa na machozi
“Usijali
Agatha,nilikuahidi kwamba
nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha mnakuwa
salama na wenye furaha
tena”
“Alikuuliza swali kuhusu
watoto wako hukumjibu”
akasema Agatha na wote
wakacheka
“Lilikuwa swali gumu
sana.Mwanao ana akili
nyingi anasoma shule gani?
“Anasoma shule moja ya
kimataifa ndiyo maana hata
lugha anayozungumza muda
mwingi ni kiingereza zaidi”
“Jitahidi sana
kumuwekea misingi mizuri
ya kielimu.Tukiachana na
hayo kuna jambo limetokea
leo ambalo limetushangaza
kidogo kuhusu Rais”
akasema Gosu Gosu na
kumueleza Agatha
kuhusiana na hofu yao kwa
mambo anayoyafanya Rais
“Mwenendo huu wa Rais
unatufanya tujiulize maswali
mengi hasa kuhusu
mahusiano yake na Tamar
Axon.Anaonekana
anamsikiliza mno Tamar na
ndiyo maana baada tu ya
kufahamishwa kwamba tuko
katika nyumba ya Tamar
akatuamuru tuondoke
haraka sana na kama
haitoshi akatutaka
tusiendelee na kazi ile
aliyotupatia.Tamar
anashirikiana na watu
ambao tunaamini hawana
malengo mazuri na nchi yetu
na afrika mashariki kwa
ujumla.Tamar ana malengo
mabaya sana na Rais na
tunajiuliza kwa nini Rais
anamsikiliza Tamar kiasi
hiki?Kuna chochote
unachokifahamu kuhusu
Tamar na Rais? Akauliza
Gosu Gosu
“Kama nilivyokueleza
jana kwamba Tamar ni msiri
sana na mambo yake mengi
hapendi
yajulikane.Ninachokifahamu
mimi ni kwamba SNSA iko
chini ya Rais na hakuna
jambo linalofanyika bila Rais
kujulishwa.Tamar yuko chini
ya Rais na hawezi
akamuamuru kitu chochote”
“Tamar alikupa kazi ya
kudukua mawasiliano ya
rais.Katika udukuzi wako
uliwahi kupata mawasiliano
ya Rais na Tamar?akauliza
Gosu Gosu na Agatha
akababaika kidogo
“Mawasiliano ya Rais na
Tamar?
“Ndiyo.Uliwahi
kuyanasa?
“Hapana sijawahi kunasa
mawasiliano ya Rais na
Tamar”
“SNSA iko chini ya Rais
na uliniambia kwamba kila
kinachofanyika katika idara
ile lazima Rais awe na
taarifa.Wanawasiliana vipi
kumpa rais taarifa?Nani
mwenye jukumu la kumpa
Rais taarifa za kila siku za
idara ya SNSA?
“Jukumu la kumjulisha
Rais kuhusu shughuli za
SNSA ni za mkurugenzi
mkuu ambaye ni Tamar
lakini sifahamu
wanawasiliana vipi”akasema
Agatha
“Agatha umekuwa karibu
na Tamar na unayafahamu
mambo yake mengi tafadhali
tusaidie tuweze kumfahamu
vyema huyu mwanamke
hatari”
“Nimekueleza yote
ninayoyafahamu kuhusu
Tamar.Ni mwanamke msiri
sana ambaye hapendi mambo
yake mengi yajulikane”
akasema Agatha
“Sawa Agatha
ninashukuru hata kwa
taarifa hizi chache
ulizotusaidia” akasema Gosu
Gosu na kuelekea ndani
akawaacha akina Agatha
bustanini akaenda kujiandaa
kwa ajili ya mpango
waliokuwa wameupanga na
Austin jioni hiyo.
OFISI KUU SNSA
“Listen to me everyone!
Sauti kali ya Tamar
ikawafanya wote waliokuwa
katika meza zao wakiendelea
na shughuli katika ukumbi
mkubwa,waache kila
walichokuwa wanakifanya
wakageuka kumtazama
mkuu wao.
“Kama mnavyofahamu
kwamba mfumo wetu
umeingiliwa na kirusi
ambacho tunaamini
kilipandikizwa na mmoja wa
watu wetu Agatha
akimtumia mwenzetu
mwingine Samson ambaye
amejiua leo asubuhi
tulipokwenda
kumkamata.Kirusi hicho
hatari kimeharibu kabisa
mfumo wetu.Kwa bahati
nzuri tulikuwa tumejiandaa
kwa mfumo wa akiba bila
hivyo hali ingekuwa mbaya
sana.Bado hatujajua nini
hasa malengo ya Agatha
kupandikiza kirusi katika
mfumo wetu lakini
tunachokifahamu ni kwamba
Agatha anashirikiana na
kikundi cha watu na mmoja
wa watu ambao
anashirikiana nao ni huyu
hapa” akasema Tamar na
kubonyeza kiunga mbali na
picha ya Austin January
ikatokea katika runinga
kubwa
“Huyu anaitwa Austi
January.Ni mkuu wa kikosi
cha jeshi kinachohusika na
operesheni maalum.Austin
amewahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi
Tanzania na baadae akaenda
kuishi nchini Afrika kusini
akifanya biashara lakini
alirejea nchini baada ya
kutokea vurugu kubwa
zilizopelekea familia yake
kuuawa.Baada ya kurejea
nchini akajiunga na kikosi
hicho cha operesheni
maalum.He’s someone very
dangerous.Huyu ndiye
ambaye amekuwa
akishirikiana na Agatha na
tukifanikiwa kumpata huyu
tutafahamu mahala alipo
Agatha,hivyo basi jioni ya leo
tunakwenda kumchukua
hoteli Dino’s.Tayari mpango
umekwisha andaliwa na
Sandra ndiye atakayeongoza
operesheni hiyo.Austin tayari
amekwisha elekezwa afike
Dino’s hotel tayari kukutana
na Sandra.Chumba namba
109 kimeandaliwa kwa ajili
ya Sandra na Austin
kukutana na tayari Sandra
amekwisha pewa maelekezo
yote na atakapofika hapo
hotelini atamfuata Austin na
kumchukua kuelekea
chumba hicho
kilichoandaliwa.Akiwa humo
chumbani Sandra anajua
nini atafanya na sisi
tutavamia na kumchukua
Austin.Operesheni hii ni ya
kimya kimya na hakuna
mauaji yoyote labda kama
ikilazimika lakini timu
itakayokwenda huko
tujitahidi sana kujizuia
kuua.Tunayemuhitaji ni
Austin peke yake hivyo basi
tujielekeze katika lengo hilo
moja.Lakini tukumbuke
kwamba Austin hayuko peke
yake kuna watu
anashirikiana nao kwa siri
hivyo basi umakini mkubwa
unatakiwa.Justin utaongoza
timu hiyo itakayokwenda
kumchukua Austin hapo
hotelini.Wengine wote kazi
yetu itakuwa ni kuwasaidia
wenzetu waweze kufanikisha
shughuli yao” akasema
Tamar na kuondoka
akaelekea katika chumba
kimoja alimokuwamo Sandra
msichana mwembamba
mrefu mwenye weusi wa
kung’aa.
“Are you ready?akauliza
“Yes I’m ready” akajibu
Sandra.Taar akamtazama
halafu akasema
“Sandra,Austin is very
dangerous.Are you sure you
want to do this?akauliza
Tamar
“Yes I want to do
this.Nataka nianze na mimi
kujifundisha taratibu na
kupata uzoefu” akajibu
Sandra
“Good. Justin na timu
yake watakuwepo karibu
kuhakikisha unakuwa
salama.Jitahidi usionyeshe
woga wowote utakapokutana
na Austin” akasema Tamar
“Usihofu Tamar
nitajitahidi” akasema
Sandra.Wakaagana Sandra
akatoka akaingia katika gari
lake na kuondoka.Tamar
akarejea katika ukumbi ule
mkubwa akamfuata Hamisa
“Austin amepiga simu
yoyote kwa kutumi namba ile
ya simu tunayotumia
kumfuatilia?akauliza Tamar
“Hapana hajapiga simu
yoyote kutwa nzima ya leo
kwa kutumia namba ile ya
simu tunayoifuatilia”
akasema Hamisa
“Good.Keep following
him” akasema Tamar na
kuelekea ofisini
kwake.Akachukua simu na
kumpigia Dr Fabian
“Tamar” akasema Dr
Fabian baada ya kupokea
simu
“Fabian muda
umefika.Mwambie Austin
aanze kuelekea eneo la tukio”
akasema Tamar
“Sawa Tamar.Lakini
mmejipanga vizuri?akauliza
Dr Fabian
“Ndiyo tumejipanga
vyema.Tayari timu yetu
imeelekea huko.Mwambie
aanze safari sasa hivi and
Fabian don’t try to do
anything stupid ! Akasema
Tamar na kukata
simu.Baada ya dakika
chache akapigiwa simu na
Hamisa kwamba tayari
Austin amepigiwa simu na
Rais na amekwisha anza
safari kuelekea Dino’s hotel.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 5
Austin alifika Dino’s
hoteli.Akaegesha gari halafu
akachukua simu nyingine
akampigia Gosu Gosu
“Papaa tayari nimefika
hapa Dino’s hotel.Uko
wapi?akauliza Austin
“Ninakaribia kufika
hapo”
“Ok good.Kila kitu kama
tulivyopanga” akasema
Austin
“Usihofu Austin.Niko
nyuma yako” akasema Gosu
Gosu.
“Just to remind you
Papaa kama mtego huu
unawekwa kati ya Rais na
SNSA basi huyo mtu
atakayetumwa hatakuwa
peke yake lazima kutakuwa
na timu ya watu hivyo
tusitegemee urahisi”
akasema Austin
“Usihofu Austin.Mimi
peke yangu ni kikosi cha
watu kumi na
mbili.Hujawahi
kunishuhudia katika
mapambano” akasema Gosu
Gosu.
Austin akaichukua ile
simu aliyoitumia
kuwasiliana na Gosu Gosu
akaiweka katika mfuko wa
ndani wa koti bila kuikata ili
kumuwezesha Gosu Gosu
aweze kusikia kila
kinachoendelea.Taratibu
akafungua mlango na
kushuka akaangaza angaza
kwa sekunde kadhaa halafu
akaanza kutembea kuelekea
ndani
“Tayari ameshuka garini
anaelekea ndani” mmoja wa
watu wa SNSA aliyekuwa
katika timu ya Justin
akawajulisha
wenzake.Austin akaingia
ndani ya hoteli akaelekea
upande wa baa akaenda
kukaa kaunta akaagiza glasi
ya mvinyo akaanza kunywa
taratibu.
Gosu Gosu naye akafika
pale hotelini akaegesha
gari.Sikioni alikuwa
ameweka kifaa cha
kumuwezesha kufuatilia kile
simu ile ya Austin ambayo
hakuizima.Akachukua begi
lake la mgongoni akavaa
kofia kichwani halafu
akashuka na kutembea
taratibu kuelekea upande wa
baa kwani tayari Austin
alikwisha mpa maelekezo
yote.Alipoingia ndani ya baa
akamuona Austin amekaa
kaunta akipata kinywaji
taratibu akaenda kukaa
katika meza ambayo
haikuwa na mtu akaagiza
kinywaji.
Baada ya dakika kama
kumi hivi,akatokea
mwanamke mmoja mrefu
mwembamba mwenye weusi
wa kung’aa.Usiku huu alivaa
sketi nyeusi iliyombana na
juu akavaa blauzi nyeusi
ambayo ilifunguliwa vifungo
maeneo ya kifua hivyo
kuonyesha sidiria yake
nyeusi iliyoyabeba matiti
yaliyojaa.Shingoni alivaa
mkufu wenye madini ya
kung’aa.Nywele zake ndefu
alizibana kwa nyuma kwa
ujumla alikuwa
amependeza.Mwanamke
Yule akamfuata Austin na
kukaa karibu yake
“Hello handsome”
akasema huku akitabasamu
na kukaa katika stuli ndefu
iliyokuwa pembeni mwa
Austin
“Hi” akasema Austin
naye akitabasamu
“Naitwa Sandra.Mgeni
wako uliyekuwa
unanisubiria” akasema
Sandra
“Ouh kumbe ni
wewe.Nimefurahi
kukuona.Karibu sana”
akasema Austin na kumtaka
muhudumu amsikilize
Sandra kinywaji
anachotumia
“Ahsante sana Austin
kwa kinywaji lakini
ingependeza zaidi kama
tungeburudika baada ya
kumaliza kwanza
mazungumzo ya muhimu”
akasema Sandra
“Ni jambo zuri
pia.Mheshimiwa amekupa
ujumbe gani?akauliza Austin
“Hatuwezi kuzungumza
hapa mambo
nyeti.Nimechukua chumba”
akasema Sandra
“I’m not comfortable in
the room.Hatuwezi kutafuta
sehemu tukakaa na
kuzungumza?Kuna sehemu
nyingi hapa hotelini
zinazofaa kwa mazungumzo
ya faragha” akasema Austin
na Sandra akatabasamu na
kumsogelea Austin
“Mazungumzo nyeti
yanazungumzwa sehemu
maalum.Nimeandaa chumba
maalum ambako tutakuwa
huru bila kuingiliwa na mtu
yeyote.Usiogope kuwa na
amani” akasema Sandra
huku akiichezea tai ya
Austin
“Okay.Tunakwenda
chumba namba
ngapi?Nataka utangulie
mimi nitakufuata nyuma
haitapendeza
tukiongozana.Hii ni kwa ajili
ya usalama wetu” akasema
Austin
“Chumba namna 109”
akasema Sandra na kuanza
kuondoka kuelekea katika
kikwezi (lifti)
“Ninaelekea chumbani”
Sandra akawajulisha
wenzake akielekea upande
kilipo kikwezi.
Mazungumzo yote ya
Sandra na Austin,Gosu Gosu
aliyasikia kupitia kifaa cha
kupokelea simu alichokiweka
sikioni kwani simu ya Austin
haikuwa imezimwa.Mara tu
Sandra alipoanza kuondoka
pale kaunta Gosu Gosu naye
akainuka na kuelekea katika
kikwezi.Milango ilifunguka
wakashuka watu sita.Ndani
ya kikwezi waliingia watu
wanne,Gosu Gosu,Sandra na
watu wengine wawili
walioonekana kuwa ni
wapenzi.Sandra akabonyeza
kitufe namba nne
akimaanisha anashuka
ghorofa ya nne Gosu Gosu
akamuomba ambonyezee
kitufe namba tano.Mara tu
kikwezi kilipoanza kuondoka
Ghafla Gosu Gosu akatoa
kifaa chenye chaji ya umeme
na kuwapitishia wale
wapenzi wawili kwa haraka
na wote wakaanguka na
upoteza fahamu halafu kwa
kasi ya aina yake akatoa
bastora na kumnyooshea
Sandra kisha akaweka kidole
mdomoni ishara ya kumtaka
akae kimya.Sandra
alitetemeka Gosu Gosu
alipomsogelea
“Don’t try to move or
scream.You are going to do
what I tell you to do !
akasema Gosu Gosu kwa
sauti ndogo.
“Give me your phone”
akasema na kuichukua simu
ile ya Sandra.Milango ya
kikwezi ilifunguka walipofika
ghorofa ya nne lakini
hawakushuka.Gosu Gosu
akauvuta mkufu wa Sandra
na kuurusha nje milango
ikajifunga wakaendelea juu
hadi ghorofa ya saba ambayo
ni ya mwisho wakashuka na
kupanda juu kabisa ya
ghorofa.Gosu Gosu
akachukua simu ya Sandra
na kuandika namba ya simu
ya Austin ambayo
inafuatiliwa na SNSA.
“Mwambie Austin
kwamba tayari” akasema
Gosu Gosu na kumnyooshea
Sandra bastora.
Austin aliitoa simu
mfukoni akaipokea
“Hallow” akasema
“Austin tayari” akasema
Sandra na Gosu Gosu
akachukua simu ile akaikata
na kuikanyaga kanyaga
halafu akachukua simu yake
na kumuandikia Austin
ujumbe
“Done”
Gosu Gosu akafungua
begi lake na kutoa mavazi
meusi ya wanawake
akamrushia Sandra avae na
yeye akavaa kanzu.Sandra
akajifunika hadi usoni
akaacha macho
pekee.Haikuwa rahisi
kumtambua.
Simu ya Austin ilipoita
makao makuu ya SNSA
waliona
“Simu ya Austin inaita”
akasema Hamisa
“Unaweza ukajua nani
anampigia?akauliza Tamar
aliyekuwa na timu ya
wataalamu wakifuatilia zoezi
lile
“Ni Sandra anapiga”
akasema Hamisa
“Justin,Sandra
anampigia simu Austin”
akasema Tamar akiwajulisha
timu yake walioko pale
hotelini lakini ghafla
akastuka
“Something is strange !
akasema Tamar
“Mpango ulikuwa Sandra
amchukue Austin na
ampeleke katika chumba
kilichoandaliwa.Nini
kimetokea hadi Sandra
aamue kumpigia simu
Austin?Something is not
right.Call Sandra now !
akasema Tamar na Hamisa
akampigia simu Sandra
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana.
“Oh my God ! Can you
see the tracker?akauliza
Tamar
“Yes.I can see it but it’s
not moving” akasema
Hamisa.
“Justin we have a
problem” akasema Tamar
“Kuna tatizo
gani?akauliza Justin
“Austin bado yuko baa?
“Ndiyo bado ninamuona
hapa baa anakunywa”
“Good.Tuma mtu haraka
sana aende chumba 109
akamtazame Sandra.Kuna
kitu kimetokea hapa kinaleta
mashaka kidogo” akasema
Tamar na Justine akamtuma
mtu haraka kwenda chumba
109 kumtazama
Sandra.Baada ya dakika
mbili mtu aliyetumwa na
Justin kwenda kumtazama
Sandra chumbani akarejea
na kumnong’oneza
“Sandra is not there ! I
repeat Sandra is not in the
room ! Justin akamjulisha
Tamar
“Oh my God ! Find her
!akasema Tamar
“Justin hakikisha
humpotezi Austin ! Tamar
akaendelea kutoa maelekezo.
“Everyone get
inside.Sandra is missing!
Justin akawajulisha watu wa
timu yake
Wakati akiendelea kutoa
maelekezo kwa timu yake
kumtafuta Sandra Justin
mara katika runinga kubwa
ukutani katika ofisi za SNSA
ule mduara mwekundu
uliokuwa unaonekana
ambayo ilikuwa ni simu ya
Austin ukatoweka.
“We’ve lost the
signal.Austin amezima simu”
akasema Hamisa
“Justin simu ya Austin
imezimwa.Bado unamuona
hapo baa?akauliza Tamar na
kumfanya Justin apatwe na
mstuko mkubwa sana baada
ya kugeuka na kutomuona
tena Austin
“Oh my God ! He’s gone”
akasema Justin
“Justin make sure you
find him ! akafoka Tamar na
kuvua spika za masikioni
akazitupa mezani kwa
hasira.
Katika eneo la maegesho
gari ziliendelea kuingia na
kutoka.Miongoi mwa gari
zilizokuwa zinatoka ni gari la
Gosu Gosu.Ndani ya gari
hakuwa peke yake alikuwa
na Sandra aliyekuwa amevaa
mavazi meusi ya kufunika
hadi uso na kuacha macho
akiwa na pingu
mkononi.Taratibu gari
lilitoka katika geti la hoteli
na kuingia barabara
kuu.Mita kadhaa Gosu Gosu
akapunguza mwendo na
kusimamisha gari.
“C’mon Austin where are
you?akajiuliza Gosu Gosu
akiwa anaangaza angaza nje
huku bastora yake ikiwa
mkononi.Mara mlango wa
nyuma ukafunguliwa na
Austin akaingia ndani.
“Let’s go ! akasema
Austin na Gosu Gosu
akaondoa gari.
Justin na timu yake
walizunguka hoteli nzima
wakiwatafuta Austin na
Sandra bila
mafanikio.Katika ghorofa ya
sita waliweza kuupata mkufu
wa Sandra ambao ulikuwa
na kifaa maalum cha
kuwawezesha kujua mahala
alipo na juu kabisa ya hoteli
walikuta mavazi ya Sandra
na viatu vyake
“We’ve lost them !
Ninarudia tena
tumewapoteza.Austin
ametoweka na Sandra
haonekani.Tunahisi atakuwa
ameondoka naye” akasema
Justin
“Justin hii
imetokeaje?Una timu kubwa
ambayo mngeweza kujipanga
vyema na kuhakikisha kila
kitu kinakwenda kama
kinavyotakiwa.Kwa nini
mkashindwa kumpata
Austin? ! akauliza Tamar
kwa ukali
“Tulijipanga vizuri
madam Tamar lakini sijui
nini kimetokea hapa hadi
tukampoteza Austin na
Sandra.I’m sorry madam !
akasema Justin
“Rudini hapa haraka
sana tuanze mchakato upya
wa kuwatafuta Austin na
Sandra.” akasema Tamar na
kuelekea ofisini kwake alihisi
kichwa kizito.Akachukua
simu na kumpigia Rais.
“Hallow Tamar” akasema
Dr Fabian
“Fabian we have a
problem”
“Kuna tatizo gani
Tamar?akauliza Dr Fabian
“Tumeshindwa kumpata
Austin”
“Hamjampata
Austin?Kwa nini? akauliza
Dr Fabian
“Timu niliyoituma
kumfuatilia Austin
wamememfuatilia hadi
dakika za mwisho lakini
amepotea katika mazingira
ya kutatanisha sana.Si yeye
tu bali hata Yule msichana
ambaye tulimtumia naye
ametoweka na hatujui yuko
wapi.Tunahisi Austin lazima
atakuwa ameondoka naye”
akasema Tamar
“Tamar huu ni uzembe
mkubwa sana
umefanyika.Kwa nini watu
wako wakamuacha Austin
akatoweka?Hamuoni sasa
mambo yanazidi kuwa
magumu?akauliza Dr Fabian
“Fabian huu si muda wa
kuanza kutoleana
lawama.Ninachokuomba
tusaidie tuweze kumpata
Austin”akasema Tamar
“It’s too late.Mpaka sasa
tayari atakuwa amekwisha
fahamu kwamba nilitumika
kuandaa ule mtego na hii
itakuwa mbaya sana
kwangu.Oh my God !
akasema Dr Fabian
“Fabian do something !
Call him.Mwambie chochote
akuelewe.Mwambie kwamba
mpango ule ulivuja…ouh
gosh I don’t know ! akasema
Tamar na kushika
kiuno.Alichanganyikiwa.
“Tamar listen to
me.Tayari tumeharibu.Kama
Austin anaye huyo msichana
uliyemtumia basi muda huu
tayari atakuwa amekwisha
jua kwamba ule ulikuwa ni
mtego na baada ya
kulifahamu hilo mimi
nitakuwa adui yake mkubwa
hivyo siwezi kumpigia simu
kumueleza
chochote”akasema Dr Fabian
“Tutafanya nini Fabian
kumpata Austin?akauliza
Tamar
“Njoo ikulu.We need to
discuss something important”
akasema Dr Fabin
“Sawa ninakuja”
akasema Tamar na kukata
simu
“Aaagghhh ! akasema
Tamar kwa hasira na
kutawanya mafaili
yaliyokuwa mezani.
“Huyu Austin kwa nini
anacheza na akili yangu
nana hii? Lakini nitampata
tu na kumuonyesha mimi ni
nani.Hawezi
akanikimbia.Ngoja kwanza
nikaonane na Fabian nijue
ana jambo gani anataka
kuniambia” akawaza Tamar
na kufunga ofisi yake
akaondoka bila kuaga mtu
yeyote
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 6
Geti la mojawapo ya
bohari linalomilikiwa na
makampuni ya Mathew
Mulumbi,likafunguliwa na
gari la akina Gosu Gosu
likaingia ndani.Sandra
akashushwa na kuingizwa
katika kijichumba kimoja
kidogo ndani ya lile bohari
lililokuwa na bidhaa mbali
mbali.Akakalishwa katika
kiti kisha akatolewa gundi
aliyokuwa amezibwa
mdomoni. “Jamani
naombeni msiniue! Akasema
Sandra kwa woga
“Binti naomba
nikufahamishe kwamba sasa
umeingia katika mikono ya
ziraili ambaye muda wowote
anaweza akaitoa roho
yako.Kitakachokuokoa ni
ukweli ! akasema Gosu Gosu
na kumtazama Sandra kwa
macho makali.
“Narudia tena kwamba
kitakachokuokoa ni
ukweli.Kuna mambo ambayo
tunataka kuyafahamu
kutoka kwako na kila
tutakachokuuliza tafadhali
kuwa mkweli.Ukithubutu
kutudanganya hautatoka
salama humu
ndani.Umenisikia?akauliza
“Nimekusikia kaka”
akajibu Sandra huku
akitetemeka
“Jina lako nani?akauliza
Austin
“Naitwa Sandra Benard”
akajibu Sandra bado alikuwa
anatetemeka
“Sandra relax.Take a
deep breath ! akasema
Austin na Sandra akavuta
pumzi ndefu
“Good.Sandra nataka
kufahamu wewe ni
nani?Unafanya kazi gani?
Akauliza Austin lakini
Sandra akasita kujibu.Gosu
Gosu aliyekuwa karibu yake
akamnasa kofi zito
akaanguka chini
“Easy papaa.We don’t
need to hurt her yet”akasema
Austin.GosuGosu akamuinua
Sandra na kumketisha kitini.
“Ukiulizswa swali
unajibu mara moja bila
kujishauri” akasema Gosu
Gosu kwa ukali
“Narudia tena kukuuliza
Sandra unafanya kazi gani?
akauliza Austin
“Ninafanya kazi katika
idara ya serikali”
“Zipo idara nyingi za
serikali.Idara ipi unafanya
kazi?akauliza Austin
“Idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi.SNSA”
akasema Sandra
“Nani aliyekutuma
kwangu?Ni Rais?akauliza
Austin
“Hapana si
Rais.Nimetumwa kwako na
Tamar ambaye nndiye
mkurugenzi wa SNSA”
akajibu Sandra.Austin na
Gosu Gosu wakatazamana
“Sema ukweli wako
Sandra vinginevyo utakuwa
katika matatizo makubwa
sana” akasema GosuGosu
“Nasema kweli
kabisa.Nimetumwa na
Tamar”
“Hujatumwa na Rais?
“Hapana.Sijatumwa na
Rais nimetumwa na Tamar”
“Tamar alikutuma nini
kwangu?akauliza
Austin.Sandra akabaki
kimya.Gosu Gosu akainua
mkono wake
“Nitajibu msiniumize”
akasema Sandra
“Jibu haraka ! akafoka
Gosu Gosu
“Nilitumwa kwako
nijifanye nimetumwa na Rais
halafu nikuchukue
nikupeleke chumba 109 ili
nikakupe maagizo
yake.Tukiwa chumbani
nilitakiwa kukushawishi
tufanye mapenzi na wakati
tukiendelea na kitendo hicho
iliandaliwa timu kwa ajili ya
kuja kuvamia na kukuteka”
akasema Sandra.Austin
akavuta pumzi ndefu na
kuuliza
“Kwa nini ninatafutwa
na idara yenu?
“Tamar ametueleza
kwamba unashirikiana na
Agatha kuiba siri mbali
mbali za idara na vile vile
unahusika katika
kupandikiza kirusi katika
mfumo wetu wa kompyuta”
akasema Sandra.
“Ahsante kwa kunieleza
ukweli.Sasa nataka
kufahamu kuhusu
Tamar.Anatumia njia gani
kuwasiliana na Rais?
Akauliza Austin
“Sina ukaribu mkubwa
na Tamar na mambo yake
mengi siyajui lakini kuna
mtu mmoja ambaye nina
uhakika mkubwa atakuwa
anafahamu mambo yake
mengi kutokana na ukaribu
wao mkubwa na ambaye
tumeambiwa kwamba
mnashirikiana naye”
akasema Sandra
“Ni nani huyo?
“Agatha”
“Agatha?
“Ndiyo.Agatha ni mtu wa
karibu sana na Tamar kwani
wanashiriki mapenzi ya
jinsia moja”
“Real ? akauliza Gosu
Gosu kwa mshangao
“Ndiyo.Tamar na Agatha
ni wapenzi japo wamekuwa
wakifanya jambo hilo kwa
siri”
“Wewe umefahamu vipi
hilo suala?akauliza Austin
“Tamar aliwahi kuniita
nyumbani kwake siku moja
usiku alikuwa na tatizo
katika kompyuta yake na
nilipofika nikawakuta yeye
na Agatha na alinionya
nilichokiona iwe ni siri yangu
nisithubutu kumweleza
mtu.Agatha ni mtu
anayemfahamu sana Tamar”
akasema Sandra.
“Unafanya kazi gani
SNSA?akauliza Austin
“Mimi ni mtaalamu wa
kutengeneza program za
kompyuta pale SNSA”
“Unafahamu chochote
kuhusu udukuzi unaofanywa
na idara yenu katika simu za
watu na mitandao ya
mawasiliano?akauliza Austin
na Sandra akawa kimya
“Jibu ! akasema Gosu
Gosu
“Ndiyo ninafahamu”
“Unafahamu kama simu
ya Rais nayo inadukuliwa?
“Hapana sifahamu
hilo.Ninachofahamu mimi
tumekuwa tukidukua simu
za watu mbali mbali ambao
tunawafuatailia kuhusiana
na usalama wa nchi lakini
sifahamu kama simu ya Rais
inadukuliwa”akasema
Sandra.Austin na Gosu Gosu
wakatazamana na kupeana
ishara kisha Gosu Gosu
akachukua kitambaa na
kumfunga Sandra usoni
“Ahsante Sandra kwa
ushirikiano uliotupa but you
are coming with us” akasema
Gosu Gosu na kumbeba
Sandra akamuingiza katika
gari wakaondoka pale katika
bohari
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 7
Tamar Axon mkurugenzi
wa idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi aliwasili
ikulu alikoitwa na Rais Dr
Fabian.Baada ya kupokelewa
waliekea sehemu ya
mazungumzo ya faragha.
“Tamar nini kimetokea
hadi mkashindwa kumpata
Austin?akauliza Dr Fabian
“I real don’t know what
happened lakini nilituma
timu ya vijana mahiri kabisa
na tulikuwa tumejipanga
vyema.Wote tumeshangazwa
na hiki kilichotokea namna
Austin alivyotoweka”
“Vipi kuhusu huyo
msichana ambaye
ulimtumia?Kuna taarifa zake
zozote umezipata hadi
sasa?akauliza Dr Fabian
“Mpaka sasa hatujapata
chochote na tuna uhakika
yawezekana Austin ndiye
amemteka”akasema Tamar
Dr Fabian akavuta pumzi
ndefu
“Kushindwa kumpata
Austin ni mgogoro mwingine
mkubwa mmeutengeneza na
mimi ndiye ambaye
ninajiweka katika wakati
mgumu zaidi” akasema Dar
Fabian
“Nalielewa hilo Fabian..”
“No you don’t understand
Tamar.You real don’t.Kama
ungekuwa unafahamu ni
madhara gani yatanipata
kama mngemkosa Austin
usingekubali vijana
wakampoteza ! akasema Dr
Fabian kwa sauti kali kidogo
“Fabina kwa nini na
wewe hutaki kunielewa
ninapokwambia kwamba
haikuwa dhamira yetu
kushindwa kumpata Austin?
Tunamsaka kwa udi na
uvumba kwa kuwa ni mtu
ambaye anashirikiana na
Agatha kuiba siri zetu
ambazo ni siri za nchi.Mimi
na idara yangu tusingekubali
kumpoteza hivi hivi.Nakiri
kuna makosa madogo
yanaweza kuwa yalifanyika
hivyo naomba unielewe na
mimi” akasema Tamar
“Tamar sikurushii wewe
lawama lakini
ninazungumzia uhalisia
uliopo.Mimi ndiye
niliyempigia simu Austin na
kumtaka aende pale hotelini
na kumdanganya kwamba
kuna mtu ninamtuma
akampelekee ujumbe.Kama
amefanikiwa kutoroka basi
lazima atakuwa amegundua
kwamba ule ulikuwa ni
mtego na kama atakuwa
amemteka huyo msichana
uliyemtumia basi lazima
atafahamu kwamba
sikumtuma Yule msichana
bali ametumwa na
SNSA.Nilikubali kufanya
vile kwa kuamini kwamba
baada ya kutekwa ungekuwa
ni mwisho wake lakini
imekuwa tofauti” akasema
Dr Fabian
“We’ll get him” akasema
Tamar
“Muda huo ambao
mtampata tayari tutakuwa
tumechelewa sana kwani
tayari anajua mambo mengi ”
akasema Dr Fabian
“Fabian hatuwezi
kuumiza vichwa vyetu na
mtu mmoja.Niachie mimi
jukumu hilo na
nitahakikisha ninampata
Austin” akasema Tamar
“Tamar kuna jambo
ambalo unapaswa
kulifahamu kuhusu
Austin”akasema Dr Fabian
na kunyamaza akavuta
pumzi ndefu
“Jambo gani Fabian?
Akauliza Tamar
“I used him to kill Lucy
Muganza”
“You did what ?akauliza
Tamar kwa mshangao
“I killed Lucy
Muganza.Austin January
ndiye aliyetekeleza misheni
hiyo” akasema Dr Fabian na
Tamar akashusha pumzi
“Najua umestuka lakini
..”
“Ni kweli nimestuka
Fabian.Kwanza sikutegemea
kabisa kama ungeweza
kufanya jambo la hatari
kama hili lakini pili
sikutegemea kama ungeweza
kuviacha vyombo vyote
vilivyo chini yako ambavyo
vingeweza kulifanya jambo
hili kwa umakini mkubwa
sana na ukaamua kumtumia
Austin.Tatu kwanini Lucy
Muganza? Why you killed
her? Akauliza Tamar.Dr
Fabian akamtazama Tamar
kwa muda halafu akasema
“Lucy Muganza alikuwa
ni hatari kwa taifa letu na
jumuiya nzima ya afrika
mashariki.Alikuwa
anatumiwa na mataifa
makubwa ya nje katika
mpango wao mkubwa wa
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki.Mimi kama
mwenyekiti wa jumuiya hiyo
sikuwa tayari jambo hilo
litokee na suluhu pekee
ilikuwa ni kumuondoa Lucy
Muganza” akasema Dr
Fabian
“Fabian taarifa hizo za
kiintelijensia kwamba Lucy
anatumiwa na mataifa
makubwa katika mpango wa
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki umezipata
wapi? Halafu siku zote
unapopata taarifa nyeti kwa
usalama wa nchi kama hizo
umekuwa ukiziwasilisha kwa
idara yetu au idara nyingine
za serikali kwa ajili ya
kufanyiwa kazi kwanini
safari hii ulipozipata taarifa
hizo za Lucy Muganza
ukaamua kuchukua hatua
kimyakimya bila
kutushirikisha?akauliza
Tamar
“Sikiliza Tamar,jambo
hili ni la siri kubwa na
sikutaka kuzihusisha taasisi
za serikali ili hata kama
ukifanyika uchunguzi basi
serikali isihusishwe bali
kikundi kidogo cha watu
ndiyo maana nikaamua
kumtumia Austin ambaye
alitekeleza misheni hiyo
akishirikiana na watu
wachache” akasema Dr
Fabian
“Fabian umenisikitisha
sana kwa kushindwa
kuniamini na kunishirikisha
katika suala hili”
“Si kwamba sikuamii
Tamar lakini nilitaka jambo
hili lifanyike kwa siri”
“Why are you telling me
now?akauliza Tamar
“Because it’s
complicated”
“Complicated ?How?
“Austin na wenzake
walifanikiwa kumuua Lucy
Muganza kama
nilivyowaelekeza lakini kuna
kosa dogo walilifanya ambalo
limezua utata mkubwa.Miili
ya Lucy na mumewe
ilifanyiwa uchunguzi na
kukutwa na risasi ambazo ni
za bunduki kubwa za
wadunguaji ambazo
majambazi wanaodaiwa
kutekeleza shambulio lile
hawakuwa nazo.Laurent
Muganza mume wa Lucy
alikuwa ni mfanyakazi
katika ofisi za umoja wa
Ulaya hivyo umoja huo
unataka wachunguzi kutoka
umoja wa Ulaya waruhusiwe
kuingia nchini kuja kufanya
uchunguzi wa suala
hilo.Nilikataa jambo hilo na
kuwaeleza kwamba
uchunguzi unafanywa na
vyombo vya ndani na hapo
ndipo mgogoro
ulipoanzia.Aliyekuwa balozi
wa umoja wa Ulaya hapa
nchini Benjamin aliandika
katika ukurasa wake wa
twitter kwamba Tanzania si
mahala salama kutembelea
halikadhalika rais wa
Ufaransa naye alifanya hivyo
kwa kuandika katika
ukurasa wake akiwaonya
raia wa Ufaransa na wa nchi
nyingine za Ulaya kuwa
waangalifu wanapotembelea
Afika Mashariki na hasa
Tanzania” akanyamaza
akameza mate kulainisha
koo halafu akaendelea
“Balozi Benjamin
alinishangaza kwa kuwa na
taarifa nyeti kabisa za
nchi.Niliamini lazima kuna
watu anashirikiana nao
ndipo nikawataka Austin na
timu yake waanze
kumchunguza lakini jana
nikapewa taarifa kwamba
watu wasiojulikana
wamevamia ukumbi
alimokuwamo balozi
Benjamin na kumuua kwa
risasi.Kifo cha Benjamin
kimezidi kuiweka pabaya
Tanzania kwani dunia nzima
hivi sasa wanaamini serikali
ya Tanzania wanahusika
katika kifo hicho.Nimekuwa
na malumbano makubwa
siku ya leo na viongozi wa
umoja wa ulaya wakitaka
wachunguzi wa kimataifa
waruhusiwe kuingia nchini
kuchunguza kifo hiki cha
Benjamin na kile cha
Laurent Muganza lakini
nimeendelea kushikilia
msimamo wangu kwamba
hakuna mchunguzi yeyote
wa kimataifa ambaye
ataruhusiwa kuingia hapa
nchini kuchunguza.Austin
anafahamu siri hii na kwa
hiki kilichotokea leo siri hii
haiko salama tena,hivyo basi
kwa namna yoyote ile lazima
tuhakikishe Austin
anapatikana” akasema Dr
Fabian.Ulipita ukimya
halafu Tamar akauliza
“You are so stupid
Fabian” akasema Tamar
“Stupid ! akahamaki Dr
Fabian
“Tamar iwe ni mwanzo
na mwisho kunidharau kiasi
hicho.Unaponidharau mimi
unawadharau watanzania
walioniweka hapa.Mimi ni
rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania na
unapaswa
kuniheshimu.Kama huwezi
kuniheshimu mimi kama
Fabian basi heshimu nafasi
niliyo nayo.Ukiingia ndani ya
jumba hili tukufu kabisa
unapaswa uwe na heshima !
akasema kwa ukali Dr
Fabian
“Fabian sijakudharau
kwamba huna akili lakini
nimekudharau kwa sababu
umeyatafuta matatizo wewe
mwenyewe halafu
yanakushinda
kuyatatua.Kwa nini
ulishindwa kuniita
ukanieleza na mimi
nikakushauri namna bora ya
kulishughulikia suala hili
lakini badala yake ukaamua
kutumia magenge ya wahuni
kwa misheni kubwa kama
hii.Hujiamini?Huniamini
hata mimi?Fabian unatakiwa
ubadilike vinginevyo
utashindwa kuongoza nchi
hii” akasema Tamar na
ukimya ukapita
“Fabian tuyaweke
pembeni yote
yaliyotokea.Makosa
yamekwisha fanyika na
jukumu letu ni kujisahihisha
na kusonga mbele.Nataka
kujua nini kinafuata baada
ya hapa?akauliza Tamar
“Kinachofuata hapa ni
kuhakikisha siri hii haivuji
na ili kuizuia siri hii ni
kuhakikisha Austin
anapatikana”akasema Dr
Fabian
“Fabian kuna jambo
nataka nikuulize na
ninaomba uwe muwazi
kwangu.Je unahusika na
mauaji ya Benjamin?
“Hapana
sihusiki.Sikutaka Benjamin
auawe kwani nilikuwa
naendelea kumchunguza
kujua mtandao wake”
“Ahsante kwa kunieleza
ukweli Fabian lakini swali
lingine ni namna gani
tutaweza kumpata Austin?
Nimeuliza hivyo kwa kuwa
wewe ndiye unayemfahamu
zaidi kuliko mimi”akasema
Tamar
“Kuna mtu ambaye
nitamuuliza kuhusu Austin
ambaye anamfahamu
vizuri.Usiwe na hofu Tamar
uhakika wa kumpata Austin
ni mkubwa”
“Fabian naomba
nikukumbushe kwamba
suala hili ni zito kwani
Austin kwa sasa atakuwa na
watu wawili kutoka katika
idara yetu na wote hao ni
watu muhimu.Agatha ni mtu
muhimu sana katika udukuzi
na Sandra ni mtu
tunayemtegemea sana katika
kutengeneza program mbali
mbali za kompyuta
tunazozitumia.Wote hawa
wawili wanafahau siri nyingi
za idara yetu na nina
wasiwasi kwamba Austin
akizipata siri hizo, nchi
inaweza ikaingia katika
kitisho cha usalama kwani
hatujui dhumuni lake ni
nini” akasema Tamar
“Tamar ninahisi akili
yangu imechoka na haifikiri
sawa sawa.Ninahitaji
mapumziko.Hadi kesho saa
nne za asubuhi nitakuwa
nimepata taarifa za kutosha
kuhusiana na huyu mtu
Austin
January.Ninachokuomba
Tamar nimekushirikisha
katika siri hii kubwa naomba
tuungane tuwe kitukimoja
kwa manufaa ya nchi.Tofauti
zetu tuziweke pembeni”
“Usihofu Fabian.Mimi
ninashukuru kwa
kunishirikisha siri hii
kubwa.Naomba kuanzia sasa
kusiwe na usiri
tushirikishane katika
masuala yote nyeti ya
taifa.Mimi na watu wangu
tunakwenda kujipanga
kuhakikisha tunafahamu
alipo Austin.Nawe pia
ukipata taarifa zozote
zinazoweza kutusaidia kujua
mahala alipo nijulishe mara
moja” akasema Tamar
akaagana na Dr Fabian
akaondoka
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 8
Katika makazi ya
Mathew Mulumbi kulikuwa
na nyumba mbili ndogo
ambazo hutumika kama
nyumba za wageni.Austin na
Gosu Gosu wakamuingiza
Sandra katika mojawapo ya
nyumba hizo halafu Gosu
Gosu akaenda katika
chumba alimo Agatha
akagonga mlango
“Gosu Gosu” akasema
Agatha
“Agatha wanaendeleaje
watoto?akauliza Gosu Gosu
“Wanaendelea
vizuri.Tayari wamepumzika”
“Good.Tunaweza
kuzungumza kidogo?akauliza
Gosu Gosu
“Hakuna tatizo” akasema
Agatha na kutoka akamfuata
Gosu Gosu hadi katika ile
nyumba walikompeleka
Sandra.
“Agatha sitaki kuchukua
muda mrefu kuna jambo
nataka kukuuliza na
ninaomba unipe jibu la
kweli” akasema Gosu Gosu
na Agatha akaonyesha
wasiwasi kidogo
“Jambo gani Gosu
Gosu?Uliza tu kama nina
jibu nitakupa”
“Nataka kufahamu
namna Tamar
anavyowasiliana na Rais”
“Uliniuliza swali hili na
nikakujibu kwamba
sifahamu chochote kuhusu
mawasiliano ya Tamar”
akajibu Agatha
“Are you sure Agatha?
“Yes I’m sure.Kwani
kuna nini Gosu
Gosu?akauliza Agatha
“Agatha nimegundua
kwamba unanidanganya na
kwamba wewe na Sandra
mna ukaribu mkubwa sana
kwa kuwa ninyi wawili mna
mahusiano ya
kimapenzi.Mnashiriki
mapenzi ya jinsia moja”
akasema GosuGosu kwa
ukali.Midomo Agatha
ikamtetemeka akakosa cha
kusema.Alistuka sana.
“Kwa nini
ukanidanganya Agatha? I
saved your life,nimeweka
maisha yangu mbele
kukulinda wewe na wanao
kwa nini ukanidanganya?
Gosu Gosu akauliza
“Gosu Gosu nani kakupa
taarifa hizo? Agatha akauliza
“Haijalishi nani kanipa h
izo taarifa ninachohitaji ni
kufahamu je ni kweli ama si
kweli?
“Hapana si kweli.Hizo ni
taarifa za uongo” akajibu
Agatha.
“Agatha sipendi
kudanganywa.Utanifanya
nikuchukie.Niambie ukweli
tafadhali” akasema
GosuGosu
“Gosu Gosu aliyekupa
taarifa hizi amekudanganya
mimi sifanyi hayo
mambo.Ukaribu wangu na
Tamar ni wa mtu na kiongozi
wake wa kazi,hakuna zaidi
ya hapo” akasema
Agatha.GosuGosu akapiga
makofi na mlango wa
chumba ukafunguliwa
akatokea Austin akiwa
ameongozana na
Sandra.Agatha akasimama
kwa mshangao.Hakuamini
kile alichokiona mbele yake
“Sandra ?!! akauliza kwa
mshangao
“Sit ! akaamuru Gosu
Gosu
“Ladies we don’t have
much time.Sandra nataka
unithibitishe mbele ya
Agatha zile taarifa
ulizotueleza” akasema Austin
“Ni kweli kama
nilivyowaeleza huyu ndiye
mtu wa karibu na
Tamar.Mambo yake yote
huyu ndiye anayeyafahamu
kwa kuwa ni mpenzi
wake.Agatha naomba ukatae
mbele yangu halafu
nionyeshe vithibitisho”
akasema Sandra.Agatha
akainama alikosa jibu
“Agatha ! akaita Gosu
Gosu
“Usiiname chini
tunahitaji majibu !
“I’m so sorry guys.It’s
true.Nimekuwa nikishiriki
mapenzi ya jinsia moja na
Tamar”akasema Agatha na
kuanza kulia
“Oh my God ! akasema
Gosu Gosu akiwa ameshika
kiuno
“Watu kama hawa ndiyo
wanaosababisha Mungu
atupunguzie umri wa kuishi
duniani.Hili ni chukizo
kubwa sana kwake.Amekosa
mwanaume mtoto mzuri
kama huyu hadi akashiriki
mapenzi na mwanamke
mwenzake?Mwanamke
mzuri ana kila sifa nzuri ya
kike lakini kasoro yake ni
hiyo moj….” Gosu Gosu
akatolewa mawazoni na
Austin
“Nyamaza kulia
Agatha.Naamini machozi
hayo ni ishara ya kwamba
unajutia kile ulichokuwa
unakifanya.Nadhani
umegundua si kitu sahihi na
hakikubaliki katika jamii
yetu.Yawezekana tumesoma
nje ya nchi au tumekaa sana
huko lakini tusiige pia na
tamaduni zao na kuzileta
huku kwetu.Tazama
GosuGosu anavyokutazama
kwa macho makali
anakushangaa.Hakutegemea
mwanamke mzuri kama
wewe ungeweza kushiriki
katika mambo kama
hayo.Anyway hatuko hapa
kukuhukumu bali
tunakushauri uachane na
hayo mambo” akasema
Austin na Agatha akafuta
machozi
“Sandra mimi naitwa
Austin January nadhani
tayari
unanifahamu,mwenzangu
pale anaitwa Gosu Gosu.Sisi
kwa pamoja tunashughulika
na operesheni mbali mbali za
siri hapa ndani ya nchi na
nyingi ya operesheni zetu
zinakuwa ni za
serikali.Kama mtakumbuka
miaka mitatu iliyopita
kulitokea tukio la kigaidi
hapa nchini ambapo magaidi
waliteka watoto na sisi ndio
tuliofanikisha kuwakomboa
watoto wale.Maisha yetu
tumeyatoa kwa ajili ya
kuhakikisha nchi inakuwa
salama” akasema Austin na
kuwatazama akina Sandra
“Siku chache zilizopita
Rais Dr Fabian alipata
taarifa za kiintelijensia
kwamba kuna mtu ambaye
anaandaliwa na mataifa
makubwa kuwa Rais wa
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo na mtu huyo anataka
kutumiwa katika
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika Mashariki.Mtu huyo
ni Lucy Muganza.Baada ya
kupata taarifa hiyo Rais
aliinita akanipa kazi mimi na
wenzangu ya kumuondoa
Lucy Muganza.Naomba
mfahamu kwamba mimi na
huyu mwenzangu hapa ndio
tuliomuua Lucy Muganza na
mumewe Laurent lakini
tulifanya hivyo kwa amri ya
Rais na kwa maslahi mapana
ya nchi yetu,jumuiya ya
Afrika Mashariki na jamhuri
ya kidemokrasia ya
Congo.Baada ya kumuondoa
Lucy Muganza mambo ndipo
yalipoanza.Kwanza umoja
wa Ulaya ulitaka kuleta
wachunguzi wake hapa
nchini na Rais
akakataa.Nyote mnajua kile
alichokiandika balozi
Benjamin katika ukurasa
wake wa twitter.Balozi
Benjamin alikuwa na taarifa
kuhusiana na silaha
zetu.Hizi ni taarifa nyeti
sana za nchi na Rais akatupa
maelekezo
tumfuatilie.Katika
kumfuatilia ndipo
tulipokutana na Agatha”
akasema Austin na
kunyamaza kidogo.
“Agatha alipewa kazi na
Tamar ya kudukua simu ya
Rais.Kila siku alikusanya
rekodi zote za mawasiliano
ya Rais na kuzihifadhi katika
faili aliloelekezwa na kwa
mujibu wa maelezo yake ni
kwamba kila siku alikuwa
akipewa kitita cha fedha kwa
kazi ile.Katika harakati zake
za udukuzi Agatha alinasa
mawasiliano ya Rais Dr
Fabian na Rais Patrice
Eyenga wa Congo ambayo
yalizungumzia mauaji yale
ya Lucy Muganza.Alinasa
rekodi zaidi ya moja lakini
hakuzijumisha katika zile
rekodi alizokuwa
anazihifadhi.Kwa maelezo
aliyotupa anadai kwamba
hakujua rekodi zile Tamar
alikuwa anazipeleka
wapi.Jana Tamar alimtuma
Agatha apeleke bahasha kwa
balozi Benjamin.Akiwa njiani
Agatha aliifungua bahasha
aliyopewa akakuta kuna
diski
mweko(flashdisc).Alipoifungu
a akakuta kuna rekodi mbili
za mazungumzo ya Rais Dr
Fabian na Patrice
Eyenga.Alizifuta rekodi zile
na kuweka kirusi katika hiyo
diski mweko.Sisi pia
tulikuwa tunamfuatilia
balozi Benjamin na ndipo
tulipogundua kwamba
alipewa bahasha na Agatha
tukaanza kumuandama
tukafanikiwa kumpata na
kumuokoa kutoka katika
jaribio la kuuawa.Toka jana
tuko naye hapa
tunamuhifadhi na
kumlinda.Kitendo cha Tamar
kumpatia balozi Benjamin
rekodi zile za Rais ambazo ni
wazi zinazungumzia mauaji
ya Lucy Muganza
kinaashiria malengo mabaya
kwa Rais.Usiku wa jana
Balozi Benjamin aliuawa na
watu
wasiojulikana.Tuliamua
kuanza uchunguzi wetu
nyumbani kwa
Tamar.Tulifanikiwa kuingia
lakini kabla hatujafanya
chochote nilipigiwa simu na
Rais akatutaka tuondoke
mahala pale haraka
sana.Kama haitoshi Rais
akatutaka tusiendelee tena
na zoezi lile alilotupa la
kuchunguza watu
wanaoshirikiana na
Benjamin.Mchana wa leo
nimepigiwa simu na Rais
akanieleza kwamba jioni
niende Dino’s hotel pale kuna
mtu nitakutana naye atanipa
ujumbe muhimu.Kumbe
ulikuwa ni mtego
nimetegewa ili nikamatwe
lakini kwa bahati nzuri mimi
na mwenzangu Gosu Gosu
tuliweza kung’amua mapema
mtego huo na tukajipanga
tukautegua na kumchukua
Sandra”akanyamaza tena
kwa sekunde kadhaa halafu
akaendelea
“Nimewapa maelezo haya
marefu ili kuwapa picha
halisi ya kile kinachoendelea
hivi sasa.Rais yuko katika
hatari kubwa sana.Rekodi
zile za mazungumzo yake na
Patrice Eyenga bado ziko
katika kompyuta ya Tamar
ambaye alikuwa na
mahusiano na balozi
Benjamin kutoka umoja wa
Ulaya ambao walikuwa
wanamuandaa Lucy
Muganza awe Rais wa Congo
na vile vile kuisambaratisha
jumuiya ya Afrika
Mashariki.Kitu
kinachonishangaza ni
kwamba Rais anaonekana
kumsikiliza sana Tamar
ndiyo maana nilimuuliza
swali Agatha kwamba kwa
nini katika rekodi zote
alizokuwa anadukua za Rais
hakuwahi kupata
mazungumzo ya Rais na
Tamar? Au Tamar alikuzuia
kufuatilia mawasiliano yake
na Rais? Nataka kujua
Tamar na Rais
wanazungumza nini
wanapowasiliana kwani
kuna kitu nakiona hakiko
sawa” akasema Austin
“Austin na Gosu Gosu
naombeni mnisamehe
sana.Jana sikuwaeleza
ukweli wote kuna mambo
niliyaficha kuhusu Tamar”
akasema Agatha
“Endelea” akasema
Austin
“Mazungumzo ya Tamar
na Rais si rahisi kupatikana
kwa sababu Tamar anatumia
progamu Fulani ambayo kila
amalizapo kuzungumza na
mtu simuni basi program
hiyo hufuta kumbukumbu
zote za maongezi hayo
haraka sana hivyo ni vigumu
kupata rekodu zozote za
mazungumzo ya Tamar sin a
rais tu bali na mtu
yeyote.Programu hiyo
alimtengenezea
Sandra”Akasema
Agatha.Gosu Gosu na Austin
wakamgeukia Sandra
“Ni kweli
Sandra?akauliza Austin
“Ni kweli.Tamar
alinitaka nimtengenezee
progamu hiyo hivyo hakuna
kumbu kumbu yoyote ya
simu za Tamar inayobaki
ndiyo maana inakuwa
vigumu kupata rekodi za
mazungumzo yake na Rais”
akasema Sandra
“She’s very
smart”akasema Austin
“Ni muangalifu sana kwa
kila anachokifanya” akasema
Sandra
“Sandra na
Agatha,naomba mfahamu
kwamba kwa sasa nchi iko
vitani na mataifa makubwa
ambayo yanatafuta kila njia
iliwaweze kuingia katika
nchi zetu na kuchta
rasilimali zetu.Kiongozi
mkuu katika mapambano
haya ni Rais wetu ambaye
ameendelea kuwa na
misimamo isyiyumba kuhusu
rasilimali za nchi na hili
linamfanya awe ni mlengwa
namna moja.Mabeberu hawa
watatafuta kila namna ya
kuweza kumdhoofisha Rais
wetu na kama ikiwezekana
hata wamundoe madarakani
na kuweka mtu
wanayemtaka
wao.Wanachokitafuta sasa ni
kupata ushahidi wa kutosha
kumuhusisha Rais na mauaji
ya Lucy Muganza na
wanawatumia watu wa
karibu na Rais kama
Tamar.Nadhani mnaweza
kuona hatari aliyonayo Rais
wetu.Hivyo basi jukumu letu
sisi ni kumlinda Rais kwani
inaonekana wazi hajui
kinachoendelea nyuma ya
pazia.Tusiwaache
wafanikishe lengo
lao.Tunawahitaji sana ninyi
wawili katika mapambano
haya.Je mko tayari
kuungana nasi kumlinda
Rais? Akauliza Austin
“Mimi niko tayari ndiyo
maana nilizifua rekodi za
Rais ambazo zingeweza
kumuhusisha na mauaji yale
ya Lucy Muganza” akasema
Agatha
“Good ! Vipi kuhusu
wewe Sandra uko tayari?
“Let me honest with you
guys” akasema Sandra
“Baba yangu alikuwa ni
rafiki wa Dr Fabian na hata
alipofariki miezi mitano
iliyopita Dr Fabian
aligharamia mazishi yake.Ni
mtu ninayemuheshimu
sana.Mwili umenisisimka
baada ya kusikia maelezo
yako na hatari aliyonayo Dr
Fabian.Mimi siwezi kusema
hapana katika mpango huu
kwani Dr Fabian ni mtu
muhimu kwangu.Naamini
hata kufika kwangu hapa ni
kwa mpango wa Mungu
kwani nilisikia wanatafuta
mtu wa kwenda kukutana na
Austin nikajikuta
najitolea.Mimi sina utaalamu
sana na mambo hayo ya
kiuchunguzi bali nimebobea
katika mambo ya
kompyuta.Kama kuna
chochote kitahitajika kwa
upande huo mimi
nitashughulikia” akasema
Sandra
“Ahsante sana
Sandra.Tunahitaji mno
msaada wako.Tunahitaji mtu
ndani ya SNSA wa
kumchunguza
Tamar.Tunahitaji pia
kuzifuta rekodi zote za
mazungumzo ya Rais na
Patrice Eyenga zilizopo
katika kompyuta ya Tamar
haraka na kazi hiyi Sandra
utakwenda
kuifanya.Tunataka vile vile
kupata mawasiliano ya
Tamar tujue anaowasiliana
nao na wanawasiliana
nini.Can you help us with
that?akauliza Austin
“It’s a tough job but I can
do it to save president”
akasema Sandra
“Mpango utakuwa
namna hii.Tutakutelekeza
mtaa wa Chambo pale kuna
makahaba wengi.Utakuwa
umesawajika na utawaeleza
makahaba wale kwamba
ulitekwa na watu
usiowafahamu
wakakupeleka mahala
wakakufanyisha mapenzi
kwa nguvu kisha wakaenda
kukutupa pale.Makahaba
wale watakuhurumia
utawaomba simu umpigie
Tamar na kumtaka aje
kukuchukua na utakuwa
umerejea tena
SNSA.Utamweleza kwamba
nimekuachia huru baada ya
kugundua kwamba hujui
chochote na hauna taarifa
zozote za kunisaidia.Kesho
asubuhi utarejea ofisini
tunataka haraka sana
utafute kila njia ili uweze
kufuta zile rekodi zote za
maongezi ya Rais zilizopo
katika kompyuta ya
Tamar.Vile vile nataka
uondoe programu
uliyoitengeneza ya kufuta
kumbukmbuzote za
mawasiliano ya Tamar”
akasema Austin
“Guys” akasema Agatha
na wote wakamgeukia
“I think you all don’t
know madhara ya zile
rekodi.Nawahakikishia
kwamba rekodi zile ni mbaya
na hatupaswi kuchukua
muda mrefu kuziondoa
katika kompyuta ya
Tamar.Tukisema tumtumie
Sandra hataweza kuipata
kompyuta ya Tamar kwa
wakati na kadiri tunavyozidi
kuchelewa ndivyo Tamar
anavyopata muda wa
kutekeleza mipango
yake.Kama ni kuzifuta
rekodi basi iwe ni
leo”akasema Agatha
“Nini wazo lako?akauliza
Gosu Gosu
“Nataka nijitolee mimi
niende” akasema
“No you can’t.! akasema
GosuGosu
“Tamar anakujua wewe
ni msaliti na unashirikiana
na Austin akiuona tu lazima
atakuua”
“She won’t kill
me.Ninamfahamu Tamar
vizuri kuliko mtu yeyote I
know how I can handle her.I
know how I can make her
believe me.Ninawahakikishia
kwamba ataniamini na
nitapata nafasi ya kuingia
katika kompyuta yake na
kufuta rekodi zote za Rais”
akasema Agatha
“Agatha nakubaliana na
Gosu Gosu kwamba huo
mpango ni wa hatari kubwa
sana.Tamar hatakuamini
hata kidogo kwani anajua
unashirikiana na Austin na
kwa sasa katika idara nguvu
kubwa imeelekezwa katika
kukutafuta wewe na
Austin.Hakuna ambaye
atakuamini.Niache mimi
niende na nitafanya kila
niwezalo kuhakikisha
kwamba ninaipata kompyuta
ya Tamar”akasema Sandra
“Naombeni mniamini
ndugu zangu kwamba Tamar
ataniamini.Ninajua namna
ya kumfanya aniamini”
Agatha akaendelea kusisitiza
“Utafanya nini kumfanya
Tamar akuamini
tena?akauliza Austin
“Nitamwambia
niligundua kwamba balozi
Benjamin anafuatiliwa ndiyo
maana nikafuta zile rekodi
zilizokuwamo katika diski
mweko aliyonipa
nikapandikiza kirusi na
nilipofika nyumbani
nikavamiwa na mtu
aliyeniteka na kunipeleka
mahala nisipopajua na ndipo
nilipokutan na Austin
ambaye alikuwa ana uwezo
wa kuingia katika kompyuta
zetu na kuchukua siri mbali
mbali.Alinitaka nimsaidie
kudukua kompyuta yako
ndipo nilipomdanganya na
kuingiza kirusi katika
mtandao wetu ambacho
kimeweza kuharibu pia hata
kompyuta zake na kufuta siri
zote ambazo amekwisha ziiba
kutoka kwetu.Mpaka hapo
Tamar atakuwa ameniamini
na ntaweza kuichukua
kompyuta yake na kufuta
zile rekodi” akasema Agatha.
“Unaonekana ni mpango
mzuri lakini Tamar anaweza
akakuuliza umewezaje
kutoroka kutoka kwetu?
Lazima kutafuta maelezo ya
kutosha ili kumthibitishia
Tamar kwamba kweli
umefanikiwa
kutoroka”akasema Austin
“You’ll shoot me !
akasema Agatha
“Shoot you?akauliza
Gosu Gosu kwa mshangao
“Ili kumfanya aniamini
kwamba nilitoroka lazima
nipigwe risasi.Tamar akijua
nimepigwa risasi hatakubali
nikatibiwe hospitali
atanipeleka kwake na mimi
lengo langu kubwa ni
kwenda nyumbani kwake ili
nikafute zile rekodi pia
kufanya uchunguzi wa
mambo mengine
yanayomuhusu Tamar”
akasema Agatha
“Vipi kuhusu familia
yako?Akikuuliza wanao wako
wapi utampa jibu
gani?GosuGosu akauliza
Agatha akabaki
kimya.Alikosa jibu
“Guys,Tamar is very
smart.Tukifanya kosa hata
dogo anaweza akagundua
kwamba ni mchezo
tumeucheza hivyo tutakosa
kila kitu na kuwaweka ninyi
hatarini.Ninao ushauri kama
mtaona unafaa” akasema
Gosu Gosu
“Go ahead” akasema
Austin
“Mpango wa kumtumia
Sandra ulikuwa mzuri sana
na hauwezi kuwa na
mashaka kwani ni rahisi
kuaminiwa na Tamar hivyo
nashauri tuendelee na
mpango huo lakini kutokana
na unyeti wa rekodi hizo
nashauri tusichukue muda
mrefu sana kwani Tamar
anaweza akazihamisha au
akazituma mahali hivyo
hatuna njia nyingine zaidi ya
kumvamia na kumchukua
Tamar na hiyo kompyuta
usiku wa leo.” akasema Gosu
Gosu.Walikaa kimya
wakitafakari halafu Austin
akasema
“I think that’s the best
option right now” akasema
Austin
“Sawa kama mmeamua
hivyo” akasema Agatha
“Agatha si kwamba
mpango wako ulikuwa
mbaya lakini ulikuwa na
hatari.Tamar yuko makini
sana na anaweza akagundua
kwamba ni mchezo
umechezwa hivyo kukuweka
katika hatari ya kuuawa”
akasema Austin
Baada ya majadiliano
marefu wakakubaliana
watumie njia ile
aliyoipendekeza Gosu Gosu.
“Baada ya wote
kukubaliana na njia hii kuna
jambo la mwisho ambalo
lazima tulifanye ambalo ni
kumfanya Sandra aonekane
kweli alikuwa katika mateso
makali.Utatusamehe Sandra
kwani hakuna namna ya
kuepuka maumivu” akasema
Austin
“Hakuna tatizo” akasema
Sandra.Gosu Gosu akaenda
ndani na kuja na vifaa mbali
mbali vya kutesea
akamchoma sindano Fulani
“Hii sindano itakusaidia
usihisi maumivu makali”
akasema Gosu Gosu na
kusubiri kwa dakika chache
halafu akamtaka Sandra
avue lile gauni alilovaa
akabakiwa na nguo za ndani
akamfunga katika kiti na
kuanza kumchapa.Mwili wa
wa Sandra ulianza kuvimba
na kuanza kuonyesha alama
huku damu ikichuruzika.
“Imetosha” akasema
Sandra akilia.GosuGosu
akamfungua na kisha
akalichana chana lile gauni
lake likapakwa damu halafu
akalivaa.Sandra
alitengenezwa kama
walivyotaka yaani aonekane
mtu aliyetoka katika mateso
makali.
“Nadhani kila kitu tayari
sasa tuendelee na mpango
wetu” akasema Austin baada
ya maandalizi yote
kukamilika na Sandra
akapelekwa garini.Alihisi
maumivu makali.Kabla ya
kuingia garini Gosu Gosu
akamuita pembeni Agatha
“Agatha tutampata
Tamar usiku wa
leo.Tukimpata tutamleta
hapa.Will that be a problem
to you?akauliza Gosu Gosu
“Hakuna tatizo lolote”
“Good” akasema Gosu
Gosu na kuingia garini
wakaondoka
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 9
Mtaa wa Chambo
unasifika sana kwa kuwa na
wanawake wengi
wanaofanya biashara ya
ukahaba hasa ifikapo
nyakati za usiku.Austin
alisimamisha gari na baadhi
ya makahaba wakaanza
kulisogelea wakidhani ni
mteja mara wakashuhudia
mlango ukifunguliwa na
mwanamke mmoja
akasukumwa nje kisha gari
lile likaondoka kwa
kasi.Makahaba wale
wakamfuata Yule
mwanamke aliyesukumwa
kutoka ndani ya gari,alikuwa
ameeumizwa sana.
“Naombeni mnisaidie
jamani wale jamaa walitaka
kuniua” akasema Sandra na
kutaka kunyanyuka
akaanguka.Wanawake
wawili wakamsaidia
kunyanyuka wakampeleka
katika kijichumba Fulani
ambacho huwa wanakitumia
kwa shughuli zao za
ukahaba.
“Nini
kimekupata?akauliza mmoja
wao
“Nilikuwa klabu mimi na
wenzangu nikakutana na
wale wanaume wakataka
niondoke nao.Walikuwa na
fedha tukanywa pombe kisha
tukaondoka.Nilipoingia
katika gari lao wakanifunga
kitambaa usoni
wakanipeleka mahaa
nisipopajua wakanibaka na
kutishia kuniua.Hawajanipa
chochote wamenipora kila
kitu hadi nguo zangu
wakanivisha hili gauni na
kuja kunitupa hapa”
“Pole sana
shoga.Wanaume wa siku hizi
unapaswa kuwa mwangalifu
sana.Tena wewe una bahati
kubwa wamekuacha hao
wengine huwa wanabakwa
na kuuawa au hata kutupwa
porini”
“Unaishi wapi
kwani?akauliza mwingine
“Naombeni mnisaidie
simu niwasiliane na dada
yangu aje anichukue siwezi
kutembea katika hali hii”
akasema Sandra na mmoja
wa wale makahaba akampa
simu,akaandika namba za
Tamar na kupiga.Simu ikaita
bila kupokelewa.Akapiga
mara ya pili simu
haikupokelewa akapiga mara
ya tatu ikapokelewa
“Hallow” akasema Tamar
“Sandra hapa
ninaongea”akasema Sandra
akiwa katika maumivu
“Sandra ! akasema
Tamar kwa mshangao.
“Is that real you?akauliza
Tamar
“Tamar it’s me Sandra”
“Oh my God ! where are
you?
“Tamar naomba uje
unichukue.Nimekutwa na
matatizo makubwa”
“Uko wapi Sandra?
Akauliza Tamar na Sandra
akamueleza mahala alipo.
“Endelea kukaa hapo
hapo usiondoke” akasema
Tamar na kukata simu
Mita chache kutoka
mahala pale alipokuwapo
Sandra,Austin na Gosu Gosu
walikuwa ndani ya gari
wakifuatilia kila
kinachoendelea.Sandra
alikuwa amepewa kifaa
Fulani kidogo akibonyeze
pale tu atakapoona na Tamar
ambacho kitawapa ishara
mahala alipo.
“Papaa nina wasi wasi
kidogo kuhusu huu mpango”
akasema Austin
“Usiwe na wasi wasi
wowote Austin.Nina uhakika
mkubwa wa kumpata Tamar
usiku wa Leo na lazima
tumpate” akasema Gosu
Gosu
“Kuna wakati
ninavunjika moyo kwani mtu
ambaye tunapambana na
kuhatarisha maisha kwa ajili
yake hajui chochote na wala
hatuthamini” akasema
Austin
“Austin usifanye ili
uthaminiwe fanya kwa
sababu ni jambo sahihi
kulifanya.Rais alifanya
jambo la busara kumuondoa
Lucy na ni kwa maslahi ya
nchi zetu hivyo lazima
tuhakikishe tunamlinda
dhidi ya hatari yoyote ile
hata kama yeye mwenyewe
hataki tumlinde.It’s our job !
akasema Gosu Gosu
“Sawa ngoja
tuendelee.Lakini pata picha
kama tusingeung’amua
mapema mtego ule na
ningekamatwa na SNSA
nani sasa hivi angekuwa
anahangaika kwa ajili ya
usalama wake? Akauliza
Austin
“Austn we have a job to
do.Hayo mambo mengine
siku nafasi ikipatikana
utamuuliza” akasema Gosu
Gosu
Sandra akiwa bado ndani
ya kile chumba kidogo
alichohifadhiwa,mara
akaingia Yule mwanamke
aliyetumia simu yake
kuwasiliana na Tamar
“Kuna mtu wako
anakupigia simu” akasema
Yule mwanamke na kumpa
simu Sandra
“Hallow” akasema
Sandra
“Kuna gari iko hapo nje
nenda ingia uondoke mahala
hapo haraka sana” akasema
Tamar na kukata
simu.Sandra akawashukuru
wale wanawake halafu
akatembea kwa
kuchechemea akatoka nje
akaliona gari moja jeusi
limeegeshwa pembeni ya
barabara.Taa za gari lile
zikawaka na kuzima
akaitambua ishara ile na
kufungua mlango wa gari
akaingia na gari
likaondoka.Gosu Gosu na
Austin ambao hawakuwa
mbali na eneo lile
walimshuhudia Sandra
akitoka ndani ya kile
kijichumba na kuingia katika
gari akaondoka
“Papaa tumeliwa.Mbona
hajabonyeza kitufe kutupa
taarifa?akauliza Austin
“Usihofu
Austin.Kumbuka
tulimwambia hadi
atakapohakikisha amemuona
Tamar ndipo atupe
taarifa.Usiogope Austin
Sandra atatufikisha kwa
Tamar” akasema Gosu Gosu
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 3: EPISODE 10
Gari lililombeba Sandra
lilifika karibu na jengo la
biashara la Mawingu
tower.Sandra akashuka
kutoka ndani ya lile gari
akaelekezwa kuingia katika
gari lingine lenye rangi
nyeusi.Kitendo kile
kilifanyika haraka haraka
sana na magari yale
yakaondoka kila moja njia
yake.Wakati kitendo kile
kinafanyika Austin na Gosu
Gosu walikuwa wameegesha
gari umbali wa mita kadhaa
na walishuhudia kila
kilichofanyika kwa kutumia
kiona mbali.Pamoja na
kuingia katika gari lingine
bado Sandra hakuwa
amebonyeza kile kidude
alichopewa.
“These people are very
smart.Wanachukua
tahadhari kwa kila
wanachokifanya” akasema
Gosu Gosu
“Lazima wachukue
tahadhari kuhakikisha
kwamba
hawafuatiliwi.Lakini sina
amani kabisa na Sandra”
akasema Austin
“Kuwa na amani
Austin.Nina uhakika
mkubwa kwamba tutampata
Tamar usiku wa leo”
akasema Gosu Gosu
wakaendelea kulifuatilia lile
gari alimopanda Sandra
Gari lile lilifika hadi nje
ya klabu moja gari lile
likasimama mlango
ukafunguliwa na haraka
haraka Sandra akashuka
akaenda katika gari lingine
jeupe aina ya Range rover e
vogue akaingia na kufunga
mlango.Mara katika simu ya
Gosu Gosu ukasikika mlio
kutoka katika kile kidude
alichokuwa nacho Sandra
“Thank you
Lord.Tumempata
Tamar.Sandra amebonyeza
kile kitufe.Kumbe
mbadilishano wote huu wa
magari mwisho wake
ulikuwa kwa Tamar”
akasema Gosu Gosu
Sandra alipoingia katika
gari aliloelekezwa aingie
akamkuta Tamar.Kwa
haraka akabonyeza kile
kidude kuwapa taarifa akina
Austin
“Funga mkanda”
akasema Tamar mara
Sandra akaweka mkono
mdomoni akitaka kutapika
akafungua mlango na
kushuka chini akainama
katika mtaro wa
karibu.Lengo lake lilikuwa ni
kukitupa kile kifaa
alichokuwa nacho.Akakitupa
katika mtaro na kurejea
garini
“Are you okay?akauliza
Tamar
“I’m okay” akajibu
Sandra na Tamar akaondoa
gari.Austin na Gosu Gosu
ambao walikuwa
wanafuatilia kila kitu
wakiwa umbali wa mita
kadhaa nao wakaendelea na
zoezi lao la kumfuatilia
Tamar kwani walikwisha
liona gari lake
“Ahsante kwa kunipa
moyo Papaa.Mimi tayari
nilikwisha kata tamaa
kabisa na Sandra”akasema
Austin
Ndani ya gari la Tamar
kulikuwa na ukimya
mkubwa Tamar akiwa
makini katika usukani
“Unajisikiaje hali yako
Sandra? Umeumizwa?
akauliza
“Nimepigwa sana.Mwili
umevimba”
“Umeumizwa sana
nikupeleke
hospitali?akauliza Tamar
“Hapana nipeleke
sehemu salama” akajibu
Sandra na safari ikaendelea
kimya kimya.Baada ya muda
Tamar akasema
“Sandra I’m real
sorry.Sikupaswa kukuruhusu
uende ukafanye kazi hii ya
hatari wakati hauna uzoefu
na mambo yale.Yote
yaliyokupata ni kwa sababu
yangu” akasema Tamar
“Usijali Tamar.I wanted
to learn the field work”
akasema Sandra na kufumba
macho kwa maumivu
“I’m sorry Sandra”
akasema Tamar akimuonea
huruma Sandra kwa
maumivu aliyokuwa nayo
Hakukuwa na
mazungumzo mengine garini
hadi walipofika katika jumba
la Tamar na kwa kutumia
kiunga mbali akafungua geti
wakaingia ndani.Tamar
akashuka haraka haraka
akamfungulia mlango
Sandra akamsaidia
kushuka.Sandra alikuwa
anachechemea Tamar
akasaidia wakaingia sebuleni
“Sandra pole sana”
akasema Tamar huku
akimvua Sandra lile gauni
alilokuwa amevaa na kuona
namna mwili wake
ulivyovimba kwa kipigo.
“Mashetani hawa
wamekuumiza sana
Sandra.Pole”
“Ahsante sana” akasema
Tamar
“Tamar I’m sorry I failed
you! Akasema Sandra
“Shhhhh !! akasema
Tamar akimtaka Sandra
anyamaze
“Usiseme chochote
tafadhali.You did great.Kitu
kikubwa nashukuru u mzima
japo wamekuumiza.Twende
bafuni nikakusafishe
majeraha.Utalala hapa
kwangu na kesho daktari
atakuchunguza kujua kama
umeumizwa kwa ndani”
“Ahsante
Tamar”akasema Sandra
wakainuka na kuelekea
katika bafu lililomo
chumbani kwa Tamar
akachemsha maji na kuanza
kumkanda Sandra aliyekuwa
akitoa kelele za maumivu.
“Wamemuumiza sana
huyu mtoto.Hili ni kosa
langu kwani nilimruhusu
aende katika kazi ya hatari
wakati hana uzoefu wowote
na mambo haya.Ninaapa
lazima nimpate Austin na
wenzake” akawaza Tamar.
Akiwa bafuni akiendelea
kumkanda Sandra mara
akasikia mlio Fulani ukitoka
chumbani
kwake.Akamtazama Sandra
kwa macho makali
“What have you
done?akauliza Tamar kwa
ukali
“Sijafanya chochote !
akasema Sandra
“Wait for me
here.Usitoke tafad…..”
akasema Tamar na kabla
hajapiga hatua moja mlango
wa bafuni ukapigwa teke zito
ukafunguka mtu mmoja
akaingia mle bafuni akiwa
na bunduki.Alikuwa ni Gosu
Gosu
“Tamar Axon ! akasema
Gosu Gosu kwa sauti kali
“Piga magoti tafadhali
kisha weka mikono yako
kichwani !! akasema Gosu
Gosu
Taratibu Tamar akaanza
kupiga magoti lakini ghafla
akajigeuza kwa kasi ya ajabu
na kuinyakua chupa
iliyokuwa katika meza ndogo
akamrushia Gosu Gosu
ambaye alipinda ili kuikwepa
na hicho ndicho Tamar
alichokuwa
anakitafuta.Kabla Gosu Gosu
hajakaa sawa akakatwa
mtama na kuanguka chini
kama furushi akasindikizwa
na teke kali la mbavuni
lililomfanya Gosu Gosu atoe
mguno wa maumivu kisha
Tamar akainyakua bunduki
ndogo aliyokuwa nayo Gosu
Gosu.
“Simama ju……” Kabla
Tamar hajamlizia
kumuamuru Gosu Gosu
asimame akapigwa chupa ya
kichwani na Sandra
akapepesuka kisha Gosu
Gosu akamsindikiza na teke
zito lililomsukuma akaenda
kuangukia kioo kikubwa
kilichotenganisha bafu na
choo kikavunjika huku
Tamar akitoa ukulele wa
maumivu.
“Gosu Gosu are you
okay?akauliza Sandra
“Thank you Sandra.I’m
okay.Mshenzi huyu
ameniumiza mbavu
zangu”akasema Gosu Gosu
na kunyanyuka akaichukua
bunduki yake na kumfuata
Tamar aliyekuwa
anagugumia kwa maumivu
“Help me ! Help me !
akalia Tamar.Alikuwa
amekatwa na kioo tumboni
na utumbo ulianza kutoka
nje.
“Sandra tafadhali tafuta
kitambaa kisafi leta haraka
sana”akasema Gosu Gosu na
kumfuata Tamar pale chini
“Tamar ! Tamar !
akasema Gosu Gosu na
kugeuka kumtazama Sandra
aliyemtuma
kitambaa.Akaamua kuinuka
yeye mwenyewe kwenda
kutafuta kitambaa.Gosu
Gosu alifanya kosa kuacha
bastora yake pale chini
Tamar akanyoosha mkono na
kuishika akajilenga kichwani
na kuachia risasi.
Gosu Gosu alikipata
kitambaa na kurejea haraka
bafuni lakini akapatwa na
mstuko mkubwa kwa kile
alichokiona mle ndani.Tamar
alikuwa amejipiga risasi
kichwani.
“Nooooooo !! akasema
Gosu Gosu na kumfuata
akamtazama tayari Tamar
alikwisha kufa.Akasimama
na kushika kiuno huku
akihema kwa kasi.
“She’s gone.Tulimuhitaji
akiwa mzima” akasema Gosu
Gosu akimtazama Sandra
aliyekuwa nyuma yake
“Anastahili kifo cha
namna hii shetani huyu”
akasema Sandra
“Jiandae tunaondoka
hapa sasa hivi.Pekua tafuta
kama kuna kitu chochote
humu ndani ambacho
unadhani kinaweza
kutusaidia” akasema Gosu
Gosu na kutoka akaelekea
katika ofisi ya Tamar
alikokuwa Austin.
“She’s gone”akasema
Gosu Gosu
“You killed her? Austin
akauliza
“Hapana amejiua
mwenyewe.Umepata nini?
“Nimepata kompyuta
mbili,kadi za benki na hati
ya kusafiria.Bado naendelea
kupekua mafaili yake kuona
kama kuna kitu cha muhimu
kwetu” akasema Austin
“Austin we need to
go.Tulichokuwa tunakitafuta
ni kompyuta yake na tayari
tumeipata.Nina uhakika
ndani ya hiyo kompyuta
kuna mengi tutayapata”
Walifanya upekuzi wa
haraka haraka wakachukua
kila walichoona kina
umuhimu kwao na kujiandaa
kuondoka.
“Austin kabla
hatujaondoka nataka
nikukumbushe kwamba
nyumba hii ina kamera za
siri hivyo basi hatutakuwa
salama kama tutaondoka
hapa bila kuharibu kamera
hizo ambazo naamini
zimeturekodi wakati
tukiingia hapa.Tuichome
nyumba” akasema Gosu
Gosu
“Tuichome nyumba?
“Ndiyo.Hatuna muda wa
kuanza kuzitafuta hizo
kamera mahala
zilipo.Tukichoma nyumba
kila kitu kitateketea na
hakutakuwa tena na
ushahidi wowote” akasema
Gosu Gosu
“Guys kabla
hatujaondoka kuna kitu
ambacho lazima
mkifahamu.Tumefanikiwa
kuipata kompyuta ya Tamar
lakini kompyuta hii ili
ifunguke nywila yake ni jicho
la kulia la
Tamar.Tutafanyaje
kuifungua?akauliza
Sandra.Gosu Gosu
hakupoteza muda akachomoa
kisu na kuondoa jicho la
kulia la Tamar akalifunga
katika kitambaa.Sandra
alitetemeka kwa
woga.Hakuwahi kushuhudia
jambo kama lile
Baada ya kila kitu
kukamilika Tamar akatolewa
ndani ya nyumba akaingizwa
ndani ya gari lake nyumba
ikawashwa moto kisha
waondoka
*****************
“Guys poleni
sana.Mambo yamekwendaje
huko?akauliza Agatha baada
ya akina Gosu Gosu kurejea
“Mambo yamekwenda
vizuri.Tumepata
tulichokihitaji,tumeipata
kompyuta ya Tamar na vitu
vingine kadhaa” akasema
Gosu Gosu
“Where is she?akauliza
Agatha
“She’s gone” akajibu
Gosu Gosu na sura ya
Agatha ikabadilika
akalengwa na machozi
“Agatha utalia baadae
right now we still have job to
do” akasema Gosu Gosu
wakaingia ndani katika ofisi
yao.
“Jamani usiku wa leo
umekuwa mfupi sana lakini
wenye mafanikio kwa
upande wetu.Kikubwa
tulichokuwa tunakitafuta
tumefanikiwa kukipata
ambacho ni kompyuta hii ya
Tamar.Kitu cha kwanza
ambacho tunatakiwa
kukifanya ni kuzitafuta
rekodi zile za Rais na
kuzifuta kabisa halafu
tutaanza kumchunguza
mahusiano yake na balozi
Benjamin wa umoja wa
Ulaya aliyeuawa” akasema
Austin
Agatha akaitambua
kompyuta ile ya Tamar
ambayo huhifadhi zile rekodi
ikawashwa na kutakiwa
kuingiza nywila.Gosu Gosu
akalifungua lile jicho la
Tamar kutoka katika
kitambaa na kulielekeza
katika kompyuta ile
ikafunguka.
“Mlimuondoa jicho
lake?akauliza Agatha kwa
mshangao
“Agatha jielekeze katika
kazi ! akasema Gosu Gosu
Agatha akalitafuta faili
lile linalohifadhi rekodi za
Rais akalipata
“Nimelipata” akasema
Agatha na kuwaonyesha
wenzake
“Hatuna haja ya
kusikiliza mazungumzo ya
rais lifute moja kwa moja”
akasema Austin
“Kwa nini tusihifadhi
katika diski na kumuonyesha
Rais kitu
tulichokifanya?Lazima ajue
kwamba hayuko salama na
ili atuamini lazima
tumuonyeshe kile
kilichokuwa kimefanywa na
Tamar” akasema Gosu Gosu
“That’s a good
idea.Tufanye hivyo” akasema
Austin na faili lile
likahifadhiwa katika diski
mweko na kufutwa kabisa
katika kompyuta ya Tamar
huku wote wakishuhudia
“Congraturations
guys.Our president is safe
now” akasema Austin
“Tujipongeze kwa hatua
hii kubwa tuliyopiga lakini
kazi ndiyo kwanza
imeanza.Tamar alikuwa na
mahusiano na balozi
Benjamin na ndiye aliyempa
rekodi zile za mazungumzo
ya Rais.Tunatakiwa kujua
nini mipango yao? Je ni
Tamar ndiye aliyekuwa
akimpatia balozi Benjamin
siri mbali mbali za
nchi?Kama ndiyo kwa nini?
Swali lingine tunalohitaji
kulitafutia majawabu nani
waliomuua balozi Benjamin
Hudson?Bado tunayo kazi
kubwa mbele yetu” akasema
Gosu Gosu
“Ni kweli tunayo kazi
kubwa ya kufanya lakini kwa
muda huu uliobaki kabla ya
mapambazuko tupumzishe
miili yetu halafu kesho
tutajua wapi pa
kuanzia”akasema Austin
“Mimi sintalala,nataka
nizipitie kompyuta hizi kila
faili nifanyie uchunguzi kila
kitu ili tujue kila kilichomo”
akasema Sandra
“I’ll stay here with her”
akasema Gosu Gosu
“Thank you” akasema
Sandra.Agatha na Austin
kila mmoja akaenda
chumbani kwake kupumzika
wakawaacha Gosu Gosu na
Sandra sebuleni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom